Utulivu Wa Nafsi (Sakiynatun-Nafs) - 2

 

 

Utulivu wa Nafsi (Sakiynatun-Nafs)  2

 

Imekusanywa na Ukht Haliymah ‘Abdullaah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Ikiachwa maumbile (fitwrah) ya mwanaadamu na nafsi yake bila ya chenye kumuathiri cha nje anaishia kwenye UislaAm. Imekuja katika Hadiyth Swahiyh:

 

“Kila kiumbe anazaliwa katika umbile (fitwrah/Uislaam), wazazi wake ndio wanaomfanya (kumbadilisha kuwa) Yahudi au Naswara au Majusi” [Al-Bukhaariy].

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

أَمْ خُلِقُوا مِنْ غَيْرِ شَيْءٍ أَمْ هُمُ الْخَالِقُونَ ﴿٣٥﴾ أَمْ خَلَقُوا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۚ بَل لَّا يُوقِنُونَ ﴿٣٦﴾

“Au! wameumbwa pasipo na kitu chochote au wao ndio waliojiumba? Au wameumba mbingu na ardhi? Bali hawana yakini.” [Atw-Twuwr: 35-36]

 

 

Hapana budi hivyo kuwa kuna Aliyemuumba mwanaadamu na ulimwengu huu mpana na hapana budi Awe Muumbaji Huyu ni Mwenye elimu pana, hikma iliyotimia, Anatekeleza Anayotaka, Mwenye uwezo mkubwa. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

 

ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ﴿٦٢﴾ كَذَٰلِكَ يُؤْفَكُ الَّذِينَ كَانُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ يَجْحَدُونَ﴿٦٣﴾ اللَّـهُ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ قَرَارًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَصَوَّرَكُمْ فَأَحْسَنَ صُوَرَكُمْ وَرَزَقَكُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ ۖ فَتَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ﴿٦٤﴾

Huyo ndiye Allaah Rabb wenu, Muumba wa kila kitu, hakuna Muabudiwa kwa haki ila Yeye; basi vipi mnaghilibiwa? Hivyo ndivyo wanavyoghilibiwa wale waliokuwa wakizikanusha Aayaat (na ishara) za Allaah. Allaah Ambaye Amekufanyieni ardhi kuwa mahali pa makazi, na mbingu kama ni paa na Akakutieni sura, Akazifanya nzuri zaidi sura zenu, na Akakuruzukuni katika vizuri. Huyo Ndiye Allaah Rabb wenu. Basi Tabaaraka-Allaah, Amebarikika Allaah Rabb wa walimwengu.  [Ghaafir: 62-64]

 

 

3. Kuokoka Muumini Na Adhabu Ya Shaka Na Hayra

 

 

Kutokana na imani iliyokuja nayo wahyi na kuungwa mkono na akili na maumbile akasalimika Muumin na shaka na ikamtatulia kitendawili cha kuwepo, kujua chanzo chake mwisho wake na lengo. Akaelewa kwamba ana Rabb naye ni Rabb wa kila kitu Aliyemuumba na kumuwepesishia yaliyomo mbinguni na ardhini, akapata matumaini kwa Rabb wake na kuhisi raha kuwa jirani naye. Akaelewa kwamba maisha haya mafupi wanayoishi watu yamechanganyika kheri na shari. Uadilifu kwa batili, haki kwa batili, ladha kwa uchungu, hii si lengo. Ni shamba la maisha mengine. Kila nafsi italipwa iliyochuma, atadumu kwa aliyoyatenda. Akastarehe Muumin kwa maswali mapana ya maisha na mauti kupata jibu kwamba ameumbwa kwa ajili ya maisha ya milele, mauti yatamuhamisha kutoka sehemu kwenda sehemu nyengine. Akaelewa hakuumbwa bure katika maisha haya wala hakuachwa bure bali Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) alituma Manabii wenye kuelimisha ili waongoke watu katika kheri wajue yanayomridhisha wafuate, na yanayomuudhi wayaepuke.

 

Muumin kwa imani yake anaelewa hayuko peke yake katika huu ulimwengu vyote vilivyomo vinamtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).

 

تُسَبِّحُ لَهُ السَّمَاوَاتُ السَّبْعُ وَالْأَرْضُ وَمَن فِيهِنَّ ۚ وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلَّا يُسَبِّحُ بِحَمْدِهِ وَلَـٰكِن لَّا تَفْقَهُونَ تَسْبِيحَهُمْ ۗ إِنَّهُ كَانَ حَلِيمًا غَفُورًا ﴿٤٤﴾

Zinamsabihi mbingu saba na ardhi na waliomo humo. Na hakuna kitu chochote isipokuwa kinasabihi kwa Himidi Zake, lakini hamzifahamu tasbiyh zao. Hakika Yeye ni Mvumilivu, Mwingi wa kughufuria. [Al-Israa: 44]

 

 

Wanaomkanusha Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) wanaishi maisha yasiyokuwa na ladha wamejawa na wasiwasi hawana matumaini hata kuwepo kwao duniani hawana jibu nani kawaleta.

 

 

4. Uwazi Wa Lengo, Njia Kwa Muumin

 

Asiye Muumin anaishi duniani katika matatizo ya aina mbalimbali yanamsumbua malengo mengi, daima ana ugomvi ndani ya moyo wake, ajiridhishe nafsi yake au airidhishe jamii kama kilivyo kisa mashuhuri cha baba na mwanae na punda wao.

 

 

Muumini amesalimika na yote haya ana lengo moja tu la kumridhisha Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) hajali watu waridhike au wakasirike. Kama alivyojaalia Muumin matatizo yake (humuum) ni tatizo moja, nayo ni kufuata njia inayomfikisha katika kumridhisha Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) njia ambayo anamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) katika kila Swalaah:

 

اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ ﴿٦﴾

Tuongoze njia iliyonyooka. [Al-Faatihah: 6]

 

 

Ni njia moja isiyopinda. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

 

 وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٥٣﴾

Na kwamba hii njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Na wala msifuate njia nyinginezo zitakufarikisheni na njia Yake. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni (Allaah) kwayo mpate kuwa na taqwa. [Al-An’aam: 153]

 

 

Ni tofauti kubwa baina ya watu hawa wawili mmoja wao amejua lengo na njia akapata matumaini akastarehe, mwenzie kupotea anatenda bila lengo.

 

أَفَمَن يَمْشِي مُكِبًّا عَلَىٰ وَجْهِهِ أَهْدَىٰ أَمَّن يَمْشِي سَوِيًّا عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٢٢﴾

Je, yule anayekwenda akiwa gubigubi juu ya uso wake ameongoka zaidi, au yule anayekwenda sawasawa kuelekea njia iliyonyooka?  [Al-Mulk: 22]

 

 

Muumini kwa ajili ya kufikia lengo ameona ni madogo mazito, amepata kila aina ya tabu, amejitolea kwa kila kitu, anaendelea hali yuko radhi na kuwa na bishara njema, mfano Khabiyb bin Zayd aliposulubiwa hali wamemzunguka wanaomuadhibu wakadhani atatetereka, bali aliwatizama akiwa na yakini na kusema mashairi:

 

“Wala sijali wakati nitakapouliwa Muislam

Kwa upande wowote marejeo yangu ni kwa Allaah

Na hilo ni kwa dhati ya Allaah,

na Akitaka Hubariki kwa kuunganisha vilivyotenganishwa.”

 

 

Swahaba mwengine yupo vitani anaingia na mauti yapo machoni naye anasema:

 

وَعَجِلْتُ إِلَيْكَ رَبِّ لِتَرْضَىٰ ﴿٨٤﴾

Na na nimeharakiza kukujia Rabb wangu ili Uridhike. [Twahaa: 84]

 

 

Mwengine mkuki umemchoma kifuani umejitokeza mgongoni haikuwa kwake ila kusema:

 

“Nimefaulu kwa Rabb wa Ka’abah.”

 

 

Katika vita vya Al-Ahzaab walipata mitihani Waumini walitetemeshwa pindi walipowaijia maadui juu yao na chini ardhi ikawa dhiki pamoja na upana wake.

 

 

Katika hali hii ya kutisha ulikuwa msimamo wao Waumini utulivu na matumaini kwa waliyoahidiwa.

 

 

وَلَمَّا رَأَى الْمُؤْمِنُونَ الْأَحْزَابَ قَالُوا هَـٰذَا مَا وَعَدَنَا اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَصَدَقَ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ ۚ وَمَا زَادَهُمْ إِلَّا إِيمَانًا وَتَسْلِيمًا ﴿٢٢﴾

Basi Waumini walipoona makundi, walisema: Haya ndio yale Aliyotuahidi Allaah na Rasuli Wake, na Amesema kweli Allaah na Rasuli Wake; na haikuwazidishia isipokuwa iymaan na kujisalimisha. [Al-Ahzaab: 22]

 

 

Nani aliwapa hawa wapiganaji utulivu na matumaini huku vita vikiendelea na mauti yapo machoni mwao. Ni imani peke yake. Anasema Allaah katika Qur-aan:

 

 

هُوَ الَّذِي أَنزَلَ السَّكِينَةَ فِي قُلُوبِ الْمُؤْمِنِينَ لِيَزْدَادُوا إِيمَانًا مَّعَ إِيمَانِهِمْ ۗ وَلِلَّـهِ جُنُودُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا﴿٤﴾

Yeye Ndiye Aliyeteremsha utulivu katika nyoyo za Waumini ili Awazidishie iymaan pamoja na iymaan zao. Na ni ya Allaah Pekee majeshi ya mbinguni na ardhini, na Allaah ni daima Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote. [Al-Fat-h:  4]

 

 

Ameelewa Muumin lengo na njia iliyonyooka ni njia aliyowaneemesha Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Manabii, AswSwidiyqiyn (wa kweli), Shuhdaa na Swaalihiyn. Ni njia iliyonyooka (Swiraatw al-Mustaqiym) ambayo anaongoza nayo Nabiy (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Anasema Allaah (‘Azza wa Jalla):

 

وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٥٢﴾ صِرَاطِ اللَّـهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ أَلَا إِلَى اللَّـهِ تَصِيرُ الْأُمُورُ﴿٥٣﴾

Na hakika wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) bila shaka unaongoza kuelekea njia iliyonyooka. Njia ya Allaah Ambaye ni Vyake Pekee vyote vilivyomo mbinguni na vyote vilivyomo ardhini. Tanabahi! Kwa Allaah Pekee yanaishia mambo yote.” [Ash-Shuuraa: 52-53]

 

Kutokana na njia hii iliyonyooka (Swiraatw al-Mustaqiym) alikuwa Muumin katika tabia na mwenendo wake mwenye matumaini bila ya kuwa na shaka, thabiti bila ya kukengeuka, muwazi bila ya kusitasita, mwenye msimamo bila ya kupinda, haimtii shaka mielekeo inayogongana, haimuadhibu migongano ya matakwa, haivunjiki shakhsiyah yake kwa migongano ya ndani ya nafsi, afanye (jambo) au aache? afanye hili au lile?

 

 

Muumin ana misingi iliyo  wazi.Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

 قَدْ جَاءَكُم مِّنَ اللَّـهِ نُورٌ وَكِتَابٌ مُّبِينٌ ﴿١٥﴾ يَهْدِي بِهِ اللَّـهُ مَنِ اتَّبَعَ رِضْوَانَهُ سُبُلَ السَّلَامِ وَيُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِهِ وَيَهْدِيهِمْ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿١٦﴾

Kwa yakini imekufikieni kutoka kwa Allaah Nuru na Kitabu kinachobainsiha. Allaah Anamwongoza kwa hicho (Kitabu) yeyote atayefuata radhi Zake katika njia za salama; na Anawatoa katika viza kuingia katika nuru kwa idhini Yake, na Anawaongoza kuelekea njia iliyonyooka.” [Al-Maaidah: 15-16]

 

 

Kisa cha Nabiy Ibraahiym aliporuzukiwa mtoto ukubwani akamlea kwa mapenzi makubwa kisha akatakiwa amchinje mwanae na hawakutetereka bali walijawa na utulivu na matumaini wakati wa shida. Hapa inatuonesha ujasiri na uthibiti wa baba kumtoa mhanga mwanae na subira ya mtoto mwema.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

فَبَشَّرْنَاهُ بِغُلَامٍ حَلِيمٍ ﴿١٠١﴾ فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ السَّعْيَ قَالَ يَا بُنَيَّ إِنِّي أَرَىٰ فِي الْمَنَامِ أَنِّي أَذْبَحُكَ فَانظُرْ مَاذَا تَرَىٰ ۚ قَالَ يَا أَبَتِ افْعَلْ مَا تُؤْمَرُ ۖ سَتَجِدُنِي إِن شَاءَ اللَّـهُ مِنَ الصَّابِرِينَ ﴿١٠٢﴾ فَلَمَّا أَسْلَمَا وَتَلَّهُ لِلْجَبِينِ ﴿١٠٣﴾ وَنَادَيْنَاهُ أَن يَا إِبْرَاهِيمُ ﴿١٠٤﴾ قَدْ صَدَّقْتَ الرُّؤْيَا ۚإِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ﴿١٠٥﴾ إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ الْبَلَاءُ الْمُبِينُ ﴿١٠٦﴾ وَفَدَيْنَاهُ بِذِبْحٍ عَظِيمٍ ﴿١٠٧﴾  وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِي الْآخِرِينَ ﴿١٠٨﴾ سَلَامٌ عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ ﴿١٠٩﴾ كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿١١٠﴾ إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ ﴿١١١﴾

“Basi Tukambashiria ghulamu mvumilivu. Alipofikia makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye; akasema: Ee mwanangu! Hakika mimi nimeona ndoto usingizini kwamba mimi nakunchinja, basi tazama unaonaje? (Ismaa’iyl) Akasema: Ee baba yangu! Fanya yale uliyoamrishwa, utanikuta In Shaa Allaah miongoni mwa wanaosubiri. Basi wote wawili walipojisalimisha, na akamlaza kifudifudi juu ya kipaji. Na tukamwita: Ee Ibraahiym. Kwa yakini umesadikisha ndoto. Hakika Sisi hivyo ndivyo Tunavyolipa wafanyao ihsaan. Hakika hili bila shaka ni jaribio bayana. Na Tukamtolea fidia kwa dhabihu adhimu. Na Tukamuachia (sifa nzuri) kwa karne za baadaye. Salaamun! Amani iwe juu ya Ibraahiym. Hakika hivyo ndivyo Tunavyolipa wafanyao ihsaan. Hakika yeye ni miongoni mwa waja Wetu Waumini.” [As-Swaaffaat: 101-111]

 

 

Anayeabudiwa ni Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Pekee, Anasema katika Qur-aan:

 

قُلْ إِنَّنِي هَدَانِي رَبِّي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ دِينًا قِيَمًا مِّلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۚ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ﴿١٦١﴾   قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦٢﴾ لَا شَرِيكَ لَهُ ۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ ﴿١٦٣﴾ قُلْ أَغَيْرَ اللَّـهِ أَبْغِي رَبًّا وَهُوَ رَبُّ كُلِّ شَيْءٍ ۚ وَلَا تَكْسِبُ كُلُّ نَفْسٍ إِلَّا عَلَيْهَا ۚ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُم مَّرْجِعُكُمْ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ ﴿١٦٤﴾

 

Sema (ee Muhammad  صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika mimi, Ameniongoza Rabb wangu kuelekea njia iliyonyooka, Dini iliyosimama thabiti, mila ya Ibraahiym aliyeelemea haki na hakuwa miongoni mwa washirikina. Sema: Hakika Swalaah yangu, na kuchinja kafaara na ‘ibaadah zangu na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah Pekee, Rabb wa walimwengu. Hana mshirika, na kwa hayo ndio nimeamrishwa, nami ni Muislamu wa kwanza.  Sema Je, nitake ghairi ya Allaah kuwa ni Rabb na hali Yeye ni Rabb wa kila kitu? Na wala nafsi yoyote haitochuma (khayr au shari) ila ni juu yake. Na wala habebi mbebaji, mzigo (wa dhambi) wa mwengine. Kisha kwa Rabb wenu ndio marejeo yenu, Atakujulisheni kwa yale mliyokuwa mkikhitilafiana nayo.” [Al-An’aam: 161-164]

 

 

Kheri ya dunia na Aakhirah inapatikana katika kumfuata na kumridhia Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa). Anasema Allaah (‘Azza wa Jalla):

 

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ 

Na haiwi kwa Muumini mwanamume na wala kwa Muumini mwanamke, Anapohukumu Allaah na Rasuli Wake jambo lolote, iwe wana hiari katika jambo lao[Al-Ahzaab: 36]

 

 

Na Anasema pia Allaah (‘Azza wa Jalla):

 

 

إِنَّمَا كَانَ قَوْلَ الْمُؤْمِنِينَ إِذَا دُعُوا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ أَن يَقُولُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٥١﴾

Hakika kauli ya Waumini wa kweli wanapoitwa kwa Allaah na Rasuli Wake ili Awahakumu baina yao; husema: Tumesikia na Tumetii. Na hao ndio wenye kufaulu[An-Nuwr:   51]

 

 

 

5. Kufarijika Muumin Kwa Vilivyomo Ulimwenguni

 

 

Muumin anaishi akiunganika na vilivyopo vyote na vinamliwaza Kwani huu ulimwengu si adui kwake wala kitu kigeni bali ni sehemu ya fikra zake na mazingatio katika kutazama kwake anazingatia madhw-har ya neema za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na athari ya Rehma Zake.

 

 

Huu ulimwengu mpana unanyenyekea kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kama anavyonyenyekea Muumin na unamtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kama Muumin anavyomtukuza.

 

 

Muumin anatazama dalili itakayompeleka kwa Rabb wake na rafiki atakayemliwaza katika matatizo na kwa hilo (mtizamo wa upendo unaokubali kuwepo kwake) kinapanuka kifua cha Muumin na maisha yake yanatanuka.

 

 

Hakuna kitu chenye dhiki kama moyo wa asiyemuamini Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) mwenye shaka na Aakhirah hakika maisha yake ni ya dhiki kuliko jela yupo mbali na chenye kuondoka (dunia) na kinachobaki (Aakhirah) hajui isipokuwa leo wala hajui katika siku hiyo ila matamanio ya kinyama na kuwepo kwake kimwili tu, huu ndio ukweli tangu aliposhuka Nabiy Aadam na mkewe katika ardhi.

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَىٰ ﴿١٢٣﴾ وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا ﴿١٢٤﴾

Kisha utakapokufikieni kutoka Kwangu Mwongozo, basi atakayefuata Mwongozo Wangu, hatopotea na wala hatopata mashaka. Na atakayejitenga na ukumbusho Wangu basi hakika atapata maisha ya dhiki. [Twahaa: 123 - 124]

 

 

6. Muumini Anaishi Katika Upamoja Na Allaah (Subhaanahu Wa Ta’aalaa)

 

 

Hakuna katika maisha haya kikubwa kama nafsi. Kibaya wanachofanyiwa wafungwa ni kuwekwa peke yao na kukosa hisia za kuchanganyika na wenzao, je, ni vipi anayejitia nafsi yake mwenyewe jela akaishi kwa hisia zake na muono wake pekee japo dunia imejaa binaadamu pembezoni mwake na haya ni maradhi (ya nafsi) mabaya kabisa anapuuzia vinavyomzunguka haoni ila anayotaka kila ageukapo haoni ila nafsi yake, jela aliyojitia haina milango wala madirisha kimbilio lake liko wapi?

 

 

Maradhi haya ya nafsi inadhihiri athari yake katika mwili kama inavyodhihiri katika harakati zake na ayatendayo inaweza kumpata kizunguzungu kutokwa na jasho moyo kwenda mbio kana kwamba anaogopa adui mwenye nguvu au anapelekwa sehemu nzito au kunyata kama anayetaka kutoroka.

 

Anasema Dr. Moses Gilbert mkuu wa idara ya afya ya wagonjwa wa akili iliyopo New York, “Hakika maradhi ya kuhisi mwanaadamu yupo peke yake ni sababu ya msingi ya kuchanganyikiwa kiakili.”

 

 

Madaktari na wajuzi wa nafsi wamefanya juhudi kubwa na majaribio katika kutafuta tiba hawakufanikiwa mpaka baadhi yao mwishoni wakaelekeza tiba kuelekea dini na kushikamana na imani na kufarijika mgonjwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).

 

 

Imani yenye nguvu ndio dawa ya maradhi haya ya hatari na ni kinga bora ya shari yake.

 

 

Dr. Frank Lupark mjuzi wa elimu ya nafsi wa Kijerumani anasema, “Vyovyote itakapofikia hisia yako ya upweke jua hupo peke yako kamwe ukiwa upande wa njia tembea hali ukiwa na yakini kwamba Mungu Yupo upande wa pili.”

 

 

Itikadi ya Muumin ni zaidi ya hivyo Kwani yeye anaamini yupo naye popote (kwa elimu Yake), popote atakapokuwa basi Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anamuona na siyo upande wa pili wa njia.

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) katika Hadiyth Al-Qudsiy:

 

“Mimi Nipo katika dhana ya mja Wangu, Niko naye anaponitaja.”

 

Anasema katika Qur-aan:

 

فَلَا تَهِنُوا وَتَدْعُوا إِلَى السَّلْمِ وَأَنتُمُ الْأَعْلَوْنَ وَاللَّـهُ مَعَكُمْ وَلَن يَتِرَكُمْ أَعْمَالَكُمْ﴿٣٥﴾

Basi msinyong’onyee, mkaomba usalama kwani nyinyi ndio mko juu na Allaah Yu pamoja nanyi na Hatapunguza (thawabu za) ‘amali zenu.  [Muhammad: 35]

 

 

Anasema mshairi wa Kimagharibi katika kuupokea mwaka, “Nilimwambia mtu aliyesimama mlango wa kuingilia nipe mwanga niangaze katika kiza cha njia, akasema weka mkono wako katika mkono wa Mwabudiwa atakuongoza katika njia.”

 

 

Hao sio waumini wa kweli ama Muumin wa kweli anaamini mkono wake upo na Mkono wa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na usaidizi Wake u pamoja Naye, na Macho Yake hayafumbi anaondokana na hisia ya upweke na ndoto mbaya.

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

وَلِلَّـهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ ۚ فَأَيْنَمَا تُوَلُّوا فَثَمَّ وَجْهُ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿١١٥﴾

Na Mashariki na Magharibi ni ya Allaah; basi popote mnapogeuka kuna Wajihi wa Allaah. Hakika Allaah ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote.  [Al-Baqarah: 115]

 

 

Na Anasema pia Allaah (‘Azza wa Jalla):

 

وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٤﴾

Naye Yu Pamoja nanyi popote mlipo. Na Allaah ni Mwenye kuona yote myatendayo.  [Al- Hadyd: 4]

 

 

Anapata hisia (shu’uwr) aliyopata Nabiy Muwsaa pindi alipowaambia Bani Israaiyl:

 

إِنَّ مَعِيَ رَبِّي سَيَهْدِينِ ﴿٦٢﴾

Hakika Rabb wangu Yu pamoja nami Ataniongoza[Ash-Shu’araa: 62]

 

 

Na hisia alizokuwa nazo Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pangoni pindi alipomwambia Swahibu wake (Abu Bakr):

 

 لَا تَحْزَنْ إِنَّ اللَّـهَ مَعَنَا ۖ  

Usihuzunike, hakika Allaah Yu Pamoja nasi[At-Tawbah: 40]

 

 

Hisia ya Muumin kuwa karibu na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) daima inamjaalia kuliwazika na neema ya kumkaribisha kwake anahisi daima nuru imeufunika moyo wake hata kama atakuwa katika giza la usiku anahisi utulivu umejaa katika maisha yake hata kama atakuwa katika ubaya wa anaoishi nao na kuchanganyika.

 

 

 

…/3

 

 

 

 

 

Share