Upweke Wa Kukosa Watoto Asome Du’aa Gani?

 

SWALI:

 

Asalamu alaikum ngugu na jamaa zangu waisilamu nawashukuru sana kwa msaada wenu mlionisaidia kwenye mambo ya mapishi sasa nimukuwa mtaaalamu sana .nawaomba pia nina tatizo jengine mkipata mda munitilie duwa kwani nina tatizo sijawahi kupata mtoto ni miaka mingi tangu niolewe na ninapolala usiku huwa natishika sana kwenye usingizi hivyo naomba munipe duwa nimuombe m/mungu anisaidie nina imana kuwa atanipokeya maombi yangu kwani mimi nina upweke sina mtoto na silali usiku naomba muniambie ni duwa mtoto nisome natumai siku yoyote mkipata mda mtanisaidia

 


 

 JIBU: 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Kwanza tunakukumbusha kwamba unapotuma Swali au kuwasiliana nasisi kwa lolote, tafadhali andika  maudhui iliyowazi hapo juua katika SUBJECT ili iwe wepesi kufuatilia ombi lako. Mfano kama tulivyoweka sisi Upweke wa Kukosa Watoto.

 

 

Tumefurahi kujua kwamba umefaidika na mapishi yetu ambayo bila ya shaka yatakuwa yamekupa faida kubwa ya kuimarisha ndoa yako kwa kupata ridhaa ya mume wako kwayo.  

 

Tunasikitika kwa kukosa kupata watoto lakini ndugu yetu tunakuomba ufahamu kuwa kila jambo la kheri au la shari basi ni kheri kwako. Haya ni mafunzo ambayo pia tumepata kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa alihi wa sallam]

 

((عجباً لأمر المؤمن إن أمره كله له خير إن أصابته سراء شكر فكان خيراً له وإن أصابته ضراء صبر فكان خيراً له وليس ذلك إلا للمؤمن )) مسلم

((Ajabu ya hali ya Muumini kuwa mambo yake yote ni kheri; anapofikwa na furaha hushukuru na huwa kheri kwake, na anapofika na matatizo husubiri na huwa ni kheri kwake, na haiwi hivyo (sifa hiyo) ila kwa Muumini)) [Muslim]

 

Kwa hiyo inakupasa uamini Qadhwaa na Qadar (Yaliyohukumiwa na Yaliyokadiriwa) na Mola wako, na uvutie subra na huku unaomba Allaah Akujaalie mtoto wa kheri na wewe. Na ikiwa uko uwezekano wa kulea yatima basi hiyo ni kheri kubwa kwenu kwani fadhila zake ni kubwa mno na tukufu. Ingia katika kiungo kifuatacho usome fadhila hizo: 

 

Jukumu La Kulea Yatima

 

 

Kwa maelezo zaidi soma tafadhali viungo vifuatavyo ambavyo vina mas-ala kama yako: 

 

Du’aa Gani Asome Mkewe Apate Kizazi? Je, Kusoma Majina Allaah Mara Kadhaa na kupuliza Katika Maji Inafaa? 

 

Ama kuhusu kushtuka usiku basi ni muhimu sana uwe unasoma nyiradi katika viungo viifuatavyo na uwe unazidumisha kila siku. Hii mbali na kuwa usome Qur-aan wa wingi sana kila siku.  

 

 

 

Na Allaah Anajua Zaidi

 

 

 

Share