Sherehe Za Harusi Ya Kiislamu Yanayohusu Kuimba Na kupiga Dufu

 

SWALI

 

Ndugu zetu AL-HIDAAYA. Kwanza kabisa nakuombeeni kila la kheri katika kuiendeleza mtandao huu.

 

Swali 1

Dadayangu anasoma katika chuo cha ummusalam kilichokuwepo Tanga na chuo hicho ni cha kisunna. Sasa aliwahi kunieleza kwamba kupiga ngoma haikubaliwi kiislam ila kupiga madufu pekeyake inakubaliwa, na anyeruhusika kughanni kasida au nasheed ni mwanamke tu. je! hii ni kweli?

 

Swali 2

Jee! inajuzu sisi wasichana kuzichezea hizo kasida au nasheed?

 

Swali 3 

Katika harusi kitugani kitakachopendeza kuwekwa ili watu wafurahike badala ya maulidi au ngoma?

 

JAZAAKUMU LLAAH KHEIR

 


 

 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola  wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

  
Majibu ya maswali yako ni kama ifuatavyo:

 
Jibu la kwanza:

Ni kweli kuwa anayeruhusiwa kuimba Qaswiydah (Nashiyd) na kupiga dufu ni wanawake tu na si wanaume tutaona katika Ahaadiyth mbalimbali kuwa waliotajwa ni wanawake.

عن الرُّبيِّعُ بنتُ مُعّوِّذِ بن عفراء: جاء النبيُّ صلى الله عليه وسلم فدخُلُ حين بُنِيَ عليَّ فجلسَ على فِراشي كمجلِسكَ منّي، (الخطاب للراوي عنها ) فجعلتْ جُوَيْرِياتٌ لنا يَضربنَ بالدُفِّ ويَندُبنَ مَن قُتلَ من آبائي يومَ بدرٍ، إذ قالت إحداهنَّ: "وفينا نبيٌّ يَعلمُ ما في غَدِ"، فقال: ((دَعي هذِهِ وقولي بالذيِ كنتِ تقولين))

Imetoka kwa Ar-Rubayy'i bin Mu'awwidh (Radhiya Allaahu ‘anha) ambaye amesema: "Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia nyumbani kwangu baada ya usiku wa harusi na akakaa katika busati, akiwa karibu kama ulivyokuwa umekaa karibu na mimi (akiwa anamuelezea aliyeisimulia Hadiyth kutokwa kwake). Kisha vijakazi vyetu vya kike vikaanza kupiga duff na kuimba kwa kuwasifu waliouawa katika vita vya Badr". Kisha mmoja wao akasema: "Na miongoni mwetu yupo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye anajua yatakayotokea kesho. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema, ((Acheni haya na rudieni kuimba miliyokuwa mkisema kabla ya haya)).


Jibu la pili:

 
Wameruhusiwa kucheza katika michezo ambayo haina ubaya na si kukatika viuno wanaweza kuimba kupiga daff (dufu) na makofi hili kwa wanawake linafaa na nyimbo zinaweza kuimbwa kwa lugha yoyote almuhim nyimbo (Nashiyd) zisiwe za matusi au kuhamasisha mambo ya zinaa au maneno ambayo yataleta chuki na watu kugombana bali wanatakiwa waimbe kwa maneno ambayo ndani yake kutapatikana mashairi yenye mafunzo na faida ndani yake haya yote yanafaa katika dini yetu.

Hadiyth zifuatazo zimethibitisha yanayohusu Nashiyd na kupiga dufu katika sherehe kwa wanawake.

Ya Kwanza:

عن الرُّبيِّعُ بنتُ مُعّوِّذِ بن عفراء: جاء النبيُّ صلى الله عليه وسلم فدخُلُ حين بُنِيَ عليَّ فجلسَ على فِراشي كمجلِسكَ منّي، (الخطاب للراوي عنها ) فجعلتْ جُوَيْرِياتٌ لنا يَضربنَ بالدُفِّ ويَندُبنَ مَن قُتلَ من آبائي يومَ بدرٍ، إذ قالت إحداهنَّ: "وفينا نبيٌّ يَعلمُ ما في غَدِ"، فقال: ((دَعي هذِهِ وقولي بالذيِ كنتِ تقولين))

Imetoka kwa Ar-Rubayy'i bin Mu'awwidh (Radhiya Allaahu ‘anha) ambaye amesema: "Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia nyumbani kwangu baada ya usiku wa harusi na akakaa katika busati, akiwa karibu kama ulivyokuwa umekaa karibu na mimi (akiwa anamuelezea aliyeisimulia Hadiyth kutokwa kwake). Kisha vijakazi vyetu vya kike vikaanza kupiga duff na kuimba kwa kuwasifu waliouawa katika vita vya Badr". Kisha mmoja wao akasema: "Na miongoni mwetu yupo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye anajua yatakayotokea kesho. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema, ((Acheni haya na rudieni kuimba miliyokuwa mkisema kabla ya haya)). [Al-Bukhaariy]

 Ya pili:

عن عائشةَ أنها زَفَّتِ امرأةً إلى رجُلٍ منَ الأنصار، فقال نبيُّ الله صلى الله عليه وسلم: ((يَا عَائِشَةُ! أَمَا كَانَ مَعَكُمْ لَهْوٌ؟ فَإِنَّ الأَنْصَارَ يُعْجِبُهُمُ اللَّهْوُ))

وفي رواية بلفظ : فقال

((فَهَلْ بَعَثْتُمْ مَعَهَا جَارِيَةً تَضْرِبُ بالدُّفِّ وتُغَنِّي؟)) قالت: تقول ماذا؟ قال: ((تقُولُ:  ((أَتَيْنَاكُمْ أَتَيْنَاكُمْ   - فَحَيُّونَا نُحَيِّكُمْ - لَوْلاَ الذَّهَبُ أَلاحْمَـرُ - مَا حَلَّتْ بِوَادِيْكُمْ  - لَوْلا الحِنْطَةُ السَّمْرَاءُ  - مَا سَمِنَتْ عَذَارِيْكُمْ))

Imetoka kwa mama wa waumini ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) kwamba alimharakiza? Au Alimsindikiza mwanamke kwa mumewe, siku ya harusi ya mwanamke kwa mume wa ki-Answaar. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuambia, ((Ewe ‘Aaishah, hukuwa na nyimbo zozote (ulipokuwa unamsindikiza) kwani ma-Answaar wanapenda burudani au viburudisho?)) [al-Bukhaariy]

Na katika riwaaya nyingine ya Hadiyth hii, inasemekana kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema, ((Ulimpeleka kijakazi mwanamke pamoja naye kumpigia duff na kuimba?)) Nikamuuliza: Aseme nini (aimbe nini)? Akasema, ((Mwache aseme: Tumekujieni, Tumekujieni Kwa hiyo tuamkieni ili tukuamkieni Ingelikuwa sio dhahabu nyekundu, Asingelitwaa katika bonde lenu, Na isingelikuwa kwa mtama wa dhahabu, Wasingelinenepa Wanawari wenu)) [At-Twabaraaniy katika 'Al-Awsatw' Hasan]

Ya Tatu:

عن عائشةَ رضي الله عنها أَنَّ النبـيَّ سمع ناساً يُغَنُّونَ فـي عُرْسٍ وهم يقولونَ : وأَهْدَى لَهَا أَكْبُشا ً يُبَحْبِحْنَ فِـي الـمِرْبَدِ وحِبُّكِ فـي النَّادِي   ويَعْلَـمُ ما فِـي غَد

 وفي رواية:

  وزَوْجُكِ فـي النَّادِي ويَعْلَـمُ مَا فِـي غَدِ، قالتْ: فقالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : ((لا يَعْلَـمُ مَا فِـي غَدٍ إلاَّ الله سُبْحَانَهُ))  

Imetoka kwa mama wa waumini ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) ambaye amesema: "Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwasikia watu wakiimba katika sherehe ya harusi wakisema: "Na nitampa kondoo wake akichachawa (akirukaruka katika majani kwa furaha) katika karamu – Na mapenzi yako yapo katika klabu, na anajua kesho italeta nini.

Au katika maelezo mengine:


Na mumeo yuko katika klabu – Na anajua kesho italeta nini.  Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema, ((Hakuna anayejua kesho italeta nini (kutatokea nini) isipokuwa Allaah [Subhaanahu wa Ta’ala]))


Ya Nne:
 

عن عامرِ بنِ سعدٍ البَجَلِـيِّ قالَ: دَخَـلْتُ علـى قَرَظَةَ بنِ كعبٍ وأبـي مسعودٍ وذَكَرَ ثالثاً،   ذَهَبَ عَلَـيَّ، وَجَوَارِي يَضْرِبْنَ بالدُّفِّ يُغَنِّـينَ، فقلتُ: تُقِرُّونَ علـى هَذَا وأَنْتُـمْ أصحابُ مـحمدٍ قالُوا: إنَّهُ قَدْ رُخِّصَ لَنَا فـي العُرُسَاتِ والنـياحةِ عندَ الـمُصِيْبَة  .وفي رواية:   وَفِي الْبُكاءِ عَلى الْمَيِّت فِي غَيْرِ نِيَاحَة

Kutoka kwa 'Aamir ibn Sa'ad Al Bajaliy ambaye amesema: "Nilimtembelea Qaradhwah bint Ka'ab na Abu Mas'uud na (akamtaja mwingine ambaye kanitoka), na nikawaona wajakazi wakipiga dufu na kuimba. Nikasema:  Nyote nyinyi mmenyamaza na mnakubali mambo haya na hali nyinyi ni Maswahaba wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)? Wakasema: 'Kwa kweli, alitupa rukhsa ya kufanya haya katika sherehe za harusi na katika wakati wa maombolezo ya msiba".

Na katika riwaya nyingine (Wakati wa kilio kwa maiti bila kuwa na maombolezo (yenye kutaja kuhusu maiti na makelele) [Al-Haakim, Al-Bayhaaqiy, An-Nasaaiy na wengineo]


Ya Tano:

عن أبي بلج يحيى بن سليم قال: قلت لمحمد بن حاطب: تزوجت امرأتين ما كان في واحدة منهما صوت، يعني دفاً، فقال محمد رضي الله عنه: قال رسول الله: ((فَصْلٌ مَا بَيْنَ الحَلالِ والحَرَامِ الصَوْتُ بالدَّفِّ)).

Kutoka kwa Abu Balaj Yahya ibn Saliym ambaye amesema: "Nilimuambia Muhammad ibn Haatwib: Nimeoa wanawake wawili na hakukuwa na sauti (yaani dufu) katika harusi yoyote. Muhammad akasema: Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema, ((Yanayobainisha baina ya halaal (yaani ndoa za dhahiri) na yaliyoharamishwa (ndoa za siri) ni sauti za dufu))   [An-Nasaaiy, At-Tirmidhiy na wengineo: Hasan]  

Jibu la tatu:

 
Katika harusi haifai kupiga ngoma, muziki wala kusoma Maulidi bali ni kupiga dufu na kuimba Nashiyd kama tulivyopokea kutoka katika mafundisho tuliyoyasoma katika Ahaadiyth zilizotangulia.

Ama nini cha kuwekwa kama ulivyoouliza, hatuoni kama kuna haja ya kuwekwa chengine ilihali hayo tuliyoyaona yalifanywa wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ya wanawake kuimba na kupiga dufu na kufurahi yanatosha kabisa. Ama ikiwa hayo hayatoshi kwa wengine, basi kunapendekezwa zaidi kuwepo na mawaidha kuhusiana na mnasaba huo wa Ndoa na mwanamke mwenzao mwenye elimu awakumbushe wenzake umuhimu wa ndoa, taratibu na adabu zake, jinsi ya mke kuishi na mumewe, na maisha ya Ndoa kwa ujumla.

Tunatumai tumejibu pande zote za maswali yako na kama kuna kipengele unataka ufafanuzi zaidi kuhusiana na hayo, usisite kutuandikia. Pia unaweza kusoma zaidi mambo yote yanayohusiana na Ndoa na Harusi kwenye viungo vifuatavyo:

Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika (Aadabu Az-Zafaaf Fiy As-Sunnat Al-Mutwahharah)

Zawadi kwa Wanandoa


Kwa maelezo zaidi soma Maswali na Majibu katika viungo vifuatavyo:

Kusoma Maulidi Kwenye Harusi Badala Kupiga Ngoma Inafaa?

Nashiyd QaswiydaNa Hukmu Zake

Uzinduzi: Dufu linatakiwa lisiwe na mlio wowote mwengine zaidi ya ule wa dufu peke yake kwani tumezoea kuona dufu ikitiwa visoda pembeni kuongeza mlio mwingine; inatakiwa iwe dufu lisitiwe chochote cha ziada.

 

Na Allah Anajua zaidi

Share