Utukufu Wa Siku Ya Ijumaa

 

Utukufu Wa Siku ya Ijumaa

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

 

ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ حُرُمَاتِ اللَّـهِ فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ عِندَ رَبِّهِ ۗ  

Ndio hivyo iwe na yeyote anayeadhimisha vitukufu vya Allaah basi hivyo ni kheri kwake mbele ya Rabb wake.  [Al-Hajj: 30]

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّـهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى الْقُلُوبِ ﴿٣٢﴾

Ndivyo hivyo, na yeyote anayeadhimisha Ishara za Allaah, basi hayo ni katika taqwa ya nyoyo.  [Al-Hajj: 32]

 

 

Siku ya Ijumaa ni siku tukufu ya Waislamu kwa dalili mbali mbali, miongoni mwazo ni kuwa ni siku   aliyoumbwa Nabiy Aadam  (‘Alayhis-salaam) na ni siku ambayo aliingia Jannah (Peponi) na kutolewa, na pia ni Siku  ambayo Qiyaamah  kitasimama:

 

 

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: (( خَيْرُ يَوْمٍ طَلَعَتْ عَلَيْهِ الشَّمْسُ يَوْمُ الْجُمُعَةِ فِيهِ خُلِقَ آدَمُ وَفِيهِ أُدْخِلَ الْجَنَّةَ وَفِيهِ أُخْرِجَ مِنْهَا وَلاَ تَقُومُ السَّاعَةُ إِلاَّ فِي يَوْمِ الْجُمُعَةِ))

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Siku bora kabisa iliyochomoza jua ni siku ya Ijumaa, na hiyo ndio ameumbwa Aadam na hiyo ndio aliingizwa Jannah (Peponi) na akatolewa humo. Na Qiyaamah hakitosimamia siku yoyote isipokuwa siku ya Ijumaa.” [Muslim]

 

 

Share