Maana Ya Majina Luqmaan, Lutwfiyyah, Rawhiyyah

 

SWALI:

ASALAAM ALAYKUM WARAHMATULLAHI WABARAKATU. NILIKUWA NNAOMBA KUFAHAMISHWA MAANA YA MAJINA YAFUATAYO LUQMAN, RUTFIA, RAUHIYA. Wahadha salaam alakum.   

 


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu maana ya baadhi ya majina.

Ama jina Luqmaan ni jina la mwanamme nalo limetajawa katika Qur-aan Surah ya 31 ambayo imechukua jina la mja mwema huyo aliyekuwa na busara. Maana yake ni njia iliyo dhahiri au kukinaisha.

Kuhusu jina Rutfia tunadhani muulizaji alikuwa anamaanisha Lutwfiyyah ambayo ina maana ya upole, raufu, latifu, asiye mkali. Jina Latwiyfah pia lina maana hiyo hiyo. Hili ni jina la kike.

Ama jina la mwisho lililoandikwa kama Rauhiya ambalo linaweza kuwa ni Ruuhiyyah ambalo lina maana ya kiroho au roho.

Tunatumai kuwa majibu hayo yatakuwa yamefuma.

Na Allaah Anajua zaidi

Share