Mwanamke Asiyempambia Mumewe Bali Anajipamba Akienda Harusini
SW
Je nawaulizaje kwani ikiwa mtu anaolewa na pia hampambi mumee, akijipamba huwa yuwenda harusini, hata kujifukiza hafanyi angoja mpaka harusi je huyo mtu ana makosa? Ama dhambi?
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kupambiana baina ya wanandoa. Hili ni suala muhimu la kijamii ambalo lau halitatekelezwa na wanandoa huwa linasababisha maafa na hata wanandoa hao kuachana.
Hapana budi si kwa mke pekee bali mume pia kujipamba. Wanandoa daima wanafaa wawe
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Nimependeshewa katika dunia yenu wanawake na vitu vizuri vilivyosalimika na uchafu (manukato)” (an-Nasaa’iy).
Kujipamba kunarithisha mapenzi na hujenga na kukuza sababu zote zinazopelekea katika kuzoeana. Kisha kumbuka, “Allaah Hupenda yaliyo mazuri” (Muslim na at-Tirmidhiy).
Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) amesema:
“Mimi napenda kujipamba kwa ajili ya mke wangu
Kujipamba ni haki ya wanandoa wote wawili – mwanamme na mwanamke. Ni vizuri
Kwa muhtasari, ikiwa mke hajipambi ila anapokwenda harusini atakuwa anapata dhambi mbele ya Allaah Aliyetukuka
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


