Tumo Masomoni Ni Bora Kuzuia Uzazi Au Kufanya Zinaa?

 

SWALI:

Bismillahi Rahmani Rahim namshukuru mola aliyenipa nguvu ya kuandika, Alhamdulilah. swala  lango ni hivi ifautavyo: 

kwa mfano mimi nipo ulayani marekani na ninataka kuoa dadangu muislamu anayesoma nami na shule kikuu.nina 2yrs  left four my major na sitaki kufanya zina so ningepende kumoa yule dada na hatumie medications ambaye itamzuulia kuzaa for the time namaliza shul yangu na Allah anajua kila chochote ipo duniani na therefore, nyinyi ndio wasome kuliko sisi so you can hepp four this question.  

Wasalamu Alleykum Warahmatullahi 



JIBU:  

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukurani kwa swali lako hilo muhimu kuhusu mas-ala ya zinaa. Na kutokana na umuhimu wake tumeona tukujibu haraka kabla ya maswali mengine yaliyoingia kabla yako ili tuweze kwa idhni ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kukuepusha na maasi makubwa ya zinaa.

Zinaa ni dhambi kubwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ametukataza japo kuyakaribia:

  ((وَلاَ تَقْرَبُواْ الزِّنَى إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاء سَبِيلاً))

((Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya)) [Al-Israa: 32]

Kuna makaripio mengi ambayo tumeonywa nayo kutoka katika Qur-aan na Sunnah, kwa hiyo ni bora kabisa kwenu kuoana haraka iwezekanavyo kabla ya kuingia katika maasi hayo. Kufanya hivyo, itakuwa ni kheri na mtajaaliwa Baraka na Tawfiyq ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) katika masomo yenu Insha-Allaah.

Ama kuhusu kuzuia kuzaa, ni jambo lilioko baina ya kukubaliwa na kukatazwa. Lakini makatazo yake ukilinganisha na kuingia katika zinaa basi utaona kwamba maasi ya zinaa ndiyo yanayopaswa kujiepusha nayo kwanza. Soma maelezo yake katika kiungo tunachokuwekea chini.

 

Lakini inapasa kutumia njia za kuzuia zinazokubalika katika sheria na sio nyinginezo kama inavyoelezwa katika dalili ifuatayo:

 عن جابر رضي الله عنه قال:  كنّا نَعزلُ والقرآنُ يَنزِل.  وفي رواية:  كُنَّا نَعْزِلُ عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم  :فَبَلَغَ ذلِكَ نَبِيَّ اللهِ صلى الله عليه وسلم فَلَمْ يَنْهَنَا عَنْهُ

Imetoka kwa Jaabir رضي الله عنه amesema: "Tulikuwa tunafanya 'azl wakati tunawaingilia wake zetu (hatumwagi ndani; tunachomoa utupu na kumwaga nje) na Qur-aan ilikuwa ikiteremshwa)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 
Na katika riwaaya nyingine amesema:
"Tulikuwa tukifanya tendo la 'azl wakati wa maisha ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم na hakutukataza kufanya hivyo: [Muslim, An-Nasaaiy na At-Tirmidhiy]

Ingia katika viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi kuhusu kukubalika kwake na kukatazwa kwake:

20 Kuhalalishwa 'Azl (Kuchopoa Kabla Ya Kushusha)

21 Kutofanya 'Azl Ni Bora Zaidi

Tunatumai kwamba utapokea nasaha hizi na haraka iwezekanavyo utafunga ndoa na dada huyo Muislamu.

Na Allaah Anajua zaidi

Share