Crapes Za Blue Berries na Asali

Crapes  Za Blue Berries na Asali 

 

Vipimo

Unga - 2 vikombe

Baking Powder - 2 vijiko vya chai

Sukari - ½ kikombe

Yai - 1

Maziwa - 1 ¼ kikombe

Maziwa ya mvuke (evaporated milk) - ¾ kikombe

Siagi - 1 Kijiko cha supu

Mjazo

Blue berries

Asali

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Tia unga, baking powder na sukari katika bakuli.
  2. Weka yai, maziwa yote na siagi katika bakuli jengine na upige kwa   wiski  (whisk – mwiko wa kupigia mayai) hadi ichanganyike, kisha changanya katika unga na endelea kupiga kwa wiski hadi uchanganyike vizuri na uwe nyororo.
  3. Weka motoni kikaango kisichoganda (non-stick frying pan), moto baina ya mdogo na wastani.
  4. Chota kwa mwiko kiasi nusu 1/3 kikombe (au takriban ½ kikombe) mimina katika kikaango.
  5. Subiri itoe viputo (bubbles) kisha geuza upike upande wa pili. Pande zote ziive kugeuka rangi ya dhahabu.
  6. Epua weka kando huku ukimaliza kupika mikate mingine.
  7. Panga katika sahani na kila juu ya mkate tia blue berries na asali, panga nyigninezo juu yake hivyo hivyo kiasi utakavyotaka kuhudumia.

Kidokezo:

  1. Unaweza kutumia matunda mengine.
  2. Kipimo Cha kiasi crapes  15

 

 

Share