Crapes Za Stroberi Na Chokoleti

Crapes Za Stroberi Na Chokoleti

Vipimo

Unga - 2 vikombe

Baking Powder - 2 vijiko vya chai

Sukari - ½ kikombe

Yai - 1

Maziwa - 1 ¼ kikombe

Maziwa ya mvuke (evaporated milk) - ¾ kikombe

Siagi - 1 Kijiko cha supu

 

Mjazo

Jamu ya Stroberi - 1 kijiko cha chai

*Chokoleti - kiasi

Sukari ya unga - 1 kijiko cha chai

Yayusha baadhi ya chokoleti na kipande kimoja acha kando

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Tia unga, baking powder na sukari katika bakuli.
  2. Weka yai, maziwa yote na siagi katika bakuli jengine na upige kwa   wiski  (whisk – mwiko wa kupigia mayai) hadi ichanganyike, kisha changanya katika unga na endelea kupiga kwa wiski hadi uchanganyike vizuri na uwe nyororo.
  3. Weka motoni kikaango kisichoganda (non-stick frying pan), moto baina ya mdogo na wastani.
  4. Chota kwa mwiko kiasi nusu 1/3 kikombe (au takriban ½ kikombe) mimina katika kikaango.
  5. Subiri itoe viputo (bubbles) kisha geuza upike upande wa pili. Pande zote ziive kugeuka rangi ya dhahabu.
  6. Epua weka kando huku ukimaliza kupika mikate mingine.
  7. Panga katika sahani na fanya sandwich kwa kutia jamu ya stroberi.
  8. Nyunyizia chokoleti juu yake na weka kipande kimoja cha  chokoleti juu yake.
  9. Nyunyizia sukari ya unga ikiwa tayari

 

Kidokezo:

Kipimo Cha kiasi crapes 15

 

 

Share