Kaimati Za Shira Ya Karameli

Kaimati Za Shira Ya Karameli

 

 

Vipimo   

 

Unga vikombe 2

Maji kikombe ½

Hamira 1 kijiko cha chai

Mafuta ya kukaangia.

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Tia vitu vyote katika bakuli uchanganye vizuri unga. Acha uumuke
  2. Weka mafuta katika karai yashike moto vizuri kisha teka mteko mdogo mdogo ukaange vikaimati.
  3. Epua vichuje mafuta.
  4. Panga katika sahani kisha nyunyizia karamel kisha ukipenda nyunyizia kidogo kastadi (custard)

 

Upishi wa karamel unapatikana hapa:

Utengenezaji Wa Caramel Ya Sukari Na Maziwa ya Malai Whipping Cream

Utengenezaji Wa Caramel Au Tofi Kwa Maziwa Mazito

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

 

 

Share