Pudini Ya Karameli Ya Kutengeneza Mwenyewe (Home Made) Katika Vibakuli

Pudini Ya Karameli Ya Kutengeneza Mwenyewe (Home Made) Katika Vibakuli 

  

Vipimo Vya Karameli                                                                   

Sukari - 1 ½ kikombe   

Maji - ¾  kikombe                                                               

Namna Ya Kuatayarisha Na Kupika Karameli  

 1. Washa oveni moto wa 150° (350°F).
 2. Tia sukari na maji katika kisufuria, weka katika moto mdogo mdogo, koroga hadi sukari iyayuke.
 3. Rashia (brush) pembezoni mwa sufuria kuondosha chembechembe za sukari.
 4. Ongeza moto na acha ichemke kwa dakika 8-10 au hadi shira igeuke rangi ya ya hudhurungi iliyokoza.
 5. Mimina kwa kugawa katika vibakuli 8 vya oveni (oven proof)  vya saizi ya ¾ (6 oz).
 6. Weka kando dakika 5 iache karameli ipoe na itulie.

Vipimo Vya Kastadi: 

Maziwa - 1 1/3  kikombe (10 fl oz) 

Malai (Cream) - 1 ½    kikombe  (6fl oz) 

Mayai -  4 

Kiiniyai (egg yolks) - 8 mayai 

Sukari -  ¾  kikombe  

Vanilla - 3 vijiko vya chai   

Namna Ya Kutayarisha Kastadi  

 1. Tia maziwa na malai katika sufuria, weka katika moto mdogo mdogo hadi iwe dafudafu (warm).
 2. Tia mayai, na viini vya mayai, sukari na vanilla katika bakuli jengine na upigie kwa mchapo wa mayai (egg whipp) hadi vichanganyike.
 3. Mimina polepole katika mchanganyiko wa maziwa huku unakoroga ili iendelee kuchanganyika.
 4. Mimina kwa kugawa katika vibakuli 8 vilivyokuwa na karameli.
 5. Vipange vibakuli katika treya, kisha tia maji kiasi kufikia ¾ ya usawa wa vibakuli.
 6. Pika (Bake) katika oveni kwa muda wa dakila 35 - 40 hadi kastadi itulie na iwive.
 7. Epua katika treya weka nje kwa muda kisha viweke katika friji zishike baridi.

   

8.  Pindua katika sahani ikiwa tayari.

Kidokezo: 

Unaweza kutia flavour nyingine badala ya vanilla kama ya chungwa, au kahawa n.k.

Share