Karameli Ya Fagi

VIPIMO
Mtindi (Yoghurt) 8 vikombe vya kahawa
Maziwa ya Unga 8 " "
Sukari 4 " "
Chenga za Biskuti za Marie 5 mugs
Siagi (Butter) 10 Vijiko vya supu
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1) Saga katika mashine (Blender) Mtindi (Yoghurt) pamoja na Maziwa ya Unga Sukari, na siagi mpaka iwe laini (creamy)
2) Changanya Chenga za Biskuti (crumbs)
3) Tandaza katika trea uliopaka siagi
4) Pika (bake) katika moto wa 300 Deg kwa muda wa takriban dakika 45 huku unahakikisha kama imewiva kwa kuichoma na kijiti.
TOPPING (Ya kutandaza juu yake)
Caramel 1 Packet
Nescaffe au cocoa kiasi
Lozi (Almonds) zilizomenywa (sliced) kiasi
· Changanya Unga wa Caramel na cocoa na tandaza juu ya Biskuti ya Fagi wakati bado imoto kisha mwagia lozi juu yake.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


