Kufanyiwa Dawa Kwa Ajili Ya Kuvutia Wateja Kwenye Biashara

SWALI:

Assalaam Alaykum,

M/Mungu awajalie kila lilo jema kwa kazi hii ya kuelimisha jamii (Elimu) Na pia ninashukuru kwa majibu ya maswali yenu ambayo yanazidi kunielimisha na kutoa utata ambao nilikuwa nao.

SWALI: Mimi nilifanya biashara ya duka, lakini ikawa pesa nikiza zinapotea katika mazingira ya utata na baadaye nikaona mtaji unakatika nikaacha kabisa.

Niliulizia nikaambiwa hiyo ni chuma ulete inatakiwa ufanyiwe dawa, ya kwanza ni yakuweka katika sehemu ya biasha naa ya pili ni ya kupakaa pamoja na mafuta ile kuvutia wateja na kuzuia chuma ulete.

Je, ni halali kutumia dawa hizi ilikuzuiya chuma ulete? Au itakuwa ni shirki?

Ni ndugu yenu katika Uislamu 

 

 

 


 

JIBU:

AlhamduliLlaah - Himdi Na Sifa Zote Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Kwanza tunapenda na sisi kutoa shukurani kwa du'aa zenu nzuri mnazotuombea nyote mnaotuma maswali yenu pamoja na wengineo wanaoingia ALHIDAAYA kutafuta faida mbali mbali. Tunamuomba Allaah (Subhaana wa Ta'aala)   Atutakabalie hizo du'aa na Atuzidishie uwezo wa kuelimishana kwa kadiri Anavyotujaalia. Aamiyn

Shukrani zetu za dhati kwa waulizaji maswali katika ukumbi wetu huu. Na tunawaombea Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) Awabariki pamoja na kuwaondolea matatizo tofauti ya kila aina.

Pia tunapenda  kutoa nasiha ya kwamba tunapoandika Jina la Allaah tusiwe ni wenye kuandika kwa mkato kama M/M au M/ Mungu kwani huku kutakuwa ni utovu wa adabu na heshima Kwake na ni bora zaidi kuandika Jina Lake la asili 'Allaah'.

Swali halikueleweka sawasawa japokuwa inaonekana kuwa ni mas-ala ya sihri na majini. Inaonyesha kichwa cha habari na swali lenyewe yanapishana. Na ibara ambayo haikueleweka ni “Chuma ulete”. Jambo muhimu kwa kila Muislamu ni kujikinga na mambo ya sihri na mashetani kwa kusoma badhi ya aya na Surah za Qur’ani na Adhkaar alizozifundisha Mtume Muhammad (Swalla Llaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Miongoni mwazo ni Suratul Faatihah, aya kumi za Suratil Baqarah (aya 1 – 5, 255 – 257 na 284 – 286), Suratul Kaafiruun, Suratul Ikhlaasw (mara 3), Suratul Falaq na Suratun Naas (mara tatu tatu) na Adhkaar ambazo kila mmoja anaweza kuzipata katika kitabu kidogo kinachoitwa Hisn al-Muslim ambacho kinapatika katika kiungo kifutacho:

Hiswnul-Muslim - Du'aa Na Adhkaar Katika Sunnah

 Na Allaah Anajua zaidi

 

Share