Shurba Ya Nyama Mbuzi - 2

Shurba Ya Nyama Mbuzi - 2

Vipimo

Nyamna Ya mbuzi ya mifupa - 1 Kilo

*Ngano nzima - ¼ kikombe

Shayiri zilizopaazwa  (quacker oats) za tayari - ¼ kikombe

Kitunguu saumua(thomu/galic) na tangawizi - 2 vijiko vya supu

Kitunguu - 1

Mdalasini vijiti - 2

Bizari ya jiyra (cumin powder/bizair ya pilau) - 1 kijiko cha chai

Bizari ya majano (haldi/kurkum/tumeric powder) - 1 kijiko cha chai

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai

Kidonge cha supu - 1

Chumvi - kiasi

Siki au ndimu - 2 vijiko vya supu

Mafuta - ¼ kikombe

Maji - kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Chemsha nyama kwa maji kiasi mengi, tia  chumvi, mdalasini, thomu-tangawizi na pilipili manga. Funika nyama ichemke hadi iwive nyama.
  2. Toa nyama nusu kutoka katika supu au yote ukipenda, kisha itoe mafupa yake na utie nyama katika mashine ya kupaaza (chopper). Isage kidogo kiasi cha kuvurugika isisagike sana. Weka kando.
  3. Tia shayiri  katika supu iache iwivie kidogo pamoja na supu baada ya kutoa nyama.Katika kisufuria kidogo, tia mafuta katakata kitunguu ukaange hadi kianze kugeka rangi, tia bizari ya haldi na jiyra na endelea kukaanga kidogo.
  4. Irudishe nyama katika supu, kisha tia kitunguu ulichokaanga, tia kidonge cha supu, tia siki au ndimu iache kidogo tu ichemke ikiwa tayari.

 * Shayiri ikiwa ni nzima itabidi uroweke kisha uchemshe. Au unaweza kutumia zilizopaazwa za tayari ambazo huhitaji kuroweka.

 

 

 

 

 

 

 

Share