Vipi Aweze Kupunguza Unene?

 

Vipi Aweze Kupunguza Unene?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Napenda kuuliza swali langu kama ifuatavyo: Napenda kufahamishwa kuwa nifanye nini ili nipunguwe unene.

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Hakika hili ni suala la daktari kwani yapo mambo mengi ambayo yanaleta unene kama huo ambao hauna maana yoyote kwa mwanadamu. Unene unajaza mafuta mwilini hivyo kumfanya mtu asiwe na afya na maradhi kama ya moyo kumwangusha mara moja na kumuua.

 

Unene mara nyingi unaletwa kwa kula sana, kila wakati na pia kutumia mafuta mengi katika chakula. Hivyo kuweza kupunguza unene na kukata mafuta mtu anahitajika kufanya yafuatayo:

 

  1. Kutokula kupindukia (kula kiasi), nayo ni kufuata nasaha ya Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kuligawa tumbo: thuluthi ya chakula, thuluthi ya maji na thuluthi ya hewa.
  2. Kutokula ila unaposikia njaa, usiwe unatia kila kitu unachopata. Kula kila wakati japokuwa kidogo kidogo inaleta tatizo hilo.
  3. Kutotia mafuta mengi katika chakula na ikwia utaweza kula vyakula vya kuchemsha au kutia mafuta kidogo itakuwa kheri zaidi. Na pia kutotumia sukari nyingi.
  4. Kufanya mazoezi kama kukimbia, kutembea au kuogelea. Mazoezi haya na aina nyingine yanakata mafuta na unene.
  5.  Kupunguza au kuacha kutumia vyakula vya mikebe pamoja na vinywaji vya gesi kama pepsi, coca na nyinginezo.
  6. Muone daktari wako kwa maelezo zaidi.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

 

Share