Biskuti Ya Keki Kavu (Shortcake)
Biskuti Ya Keki Kavu (Shortcake)
    
Vipimo
Unga - 2 Magi (vikombe vya chai)
Sukari iliyosagwa - 2/3 Magi (kikombe cha chai)
Siagi - 220 g
Unga wa mchele - ½ Magi
Yai -1
Vanilla - 1 kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Changanya vitu vyote hivyo kwenye bakuli mpaka unga ushikamane.
 - Paka mafuta treya ya kuchomea kisha utandaze kwenye treya ya 20cm kwa 30 cm au (8 in kwa 12 in)
 - Choma kwenye moto 325˚C kwa muda wa saa nzima au mpaka ibadilike kuwa rangi ya dhahabu.
 - Epua acha ipoe kisha kata vipande kama mstatili, weak kwenye sahani tayari kunywewa na chai.
 
Kidokezo:
Kwa unga huo huo unaweza kutengeneza vibiskuti vya duara duara.
    
    