Wanja Unafaa Kupakwa Kwa Wanawake?

 

Wanja Unafaa Kupakwa Kwa Wanawake?

 

Alhidaaya.com

 

SWALI:

 

A. Aleykum

 

Nilikuwa nauliza mwanamke kupaka wanja ni haramu? Watu wengine wanasema Sunna. Sasa sielewi ni ruksa ama si ruksa.

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Kupaka wanja inafaa na ni Sunnah lakini mpakie mumeo ukiwa nyumbani kwako kwani wanja ni urembo na mapambo na hayo anayefaa kuyaona ni mumeo na si watu wengine huko nje. Hivyo, haifai kupaka wanja ukitoka nje kwani hayo ni mapambo na hayafai kuonwa na wasio Mahram zako.

 

 

Wanja pia ni dawa kwa magonjwa ya macho, hivyo kukiwa na dharura ya mwanamke au mwanamme kupaka kwa ajili ya kuondoa ugonjwa kutakuwa hakuna tatizo.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share