Mtu Kuswali Na Kaweka Nywele Za Bandia Nini Hukmu Yake?

 

Hukmu Ya Mtu Kuswali Na Kaweka Nywele Za Bandia

 

Alhidaaya.com 

 

 

SWALI:

 

Salaam alaikum,

Wanawake tuna mambo mengi sana,Leo Hii Utapata Msichana Wa Kislamu, Amesonga nyele na katika zile nyele zake amebandika nyele zengine ambazo sio zake,lakini ma shallah swala haimpiti na maashallah akikuona wafanya jambo ambalo sio sawa na dini yuwakukanya na kuweka mahali sawa ,sasa suali langu ni hii swala yake ama ikiwa ana saumu amefunga hii saumu yake au swala yake anayo swali mara 5 kwa siku yafaa ama haifai?

Hili ndio suali ambalo inshallah namaumaini kuwa nitapata jibu lake kutoka ndugu zangu wa alhidaaya.com

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Kubandika nywele za bandia ni katika maovu aliyotuhadharisha   Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Humlaani mwanamke anayefanya hivyo kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:

 

Mwanamke wa Ki-Answaariy aliyemuozesha binti yake ambaye nywele zake zilianza kung'ooka.  Mwanamke huyo wa Ki-Answaariy alikuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumtajia kwamba "Mumewe (mume wa mwanangu) ameona kwamba nimwachie avae nywele za bandia." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Usifanye hivyo kwani Allaah Ta’aalaa  Huteremsha laana Yake kwa  wanawake kama hao wanaoongeza nywele za bandia))   [Al-Bukhariy 7:133  kutoka kwa Mama wa Waumini 'Aaishah Radhwiya Allaahu 'anhaa]

 

 

Bila ya shaka hakuna atakaye kupata laana ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)   kwa hiyo dada zetu wajaribu kujiepusha na maovu kama haya na wajaribu kupeana nasiha na kukumbushana hatari kama hizi ili kuwaokoa wenzao kutoka hatari kama hii.

 

 

Kuhusu Swaalah na Swawm yake vitendo vyote hivyo vina hukmu zake tofauti kwa hiyo haimaanishi kwamba Swaalah na Swawm zake hazitokubaliwa, bali zitakubaliwa ikiwa amezitimiza ipasavyo na upande mwengine atapata malipo kwa kosa la kubandika nywele za bandia kama ilivyo katika Hadiyth hiyo.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share