Wanaume Watatu Wanataka Kunioa, Nimchague Yupi?

SWALI

 

 

aslm alkm,natanguliza jina la ALLAH muumba mbingu na ardhi na vote viliomo.swali langu lahusu mi mwenyewe.Nimefikia umri wa kuolewa, na ALLAHAMDULILAH kumetokea wanaume watatu wote wataka nioa.famillia yangu imenipa uhuru wa kuchagua yule ntakae mpenda lakini sijui nchague yupi kwani wote wameshika dini na mienendo yao ni ya kiislam.JE KUNA DUA AMA SWALA NAWEZA SWALI ILI ALLAH ANIONYESHE YULE ALIE NA KHERI NAMI?shukran


 

JIBU

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 Inakupasa kwanza dada yetu umshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa Neema hiyo Aliyokujaalia ambayo wanawake wengi wanaitamani. Neema zaidi kwako kwamba si mtu mmoja anayetaka kukuoa bali watatu! Wenzako wanatamani hata mmoja tu atokee hawapati! Ni hii imekuwa ni fitna kubwa inayotukabili kuwa wanawake wengi wamo majumbani hawakuolewa. Bila shaka ni dalili za Qiyaamah zilizotajwa na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa utafika wakati wanawake watazidi kuliko wanaume.

 

Muumini anapofikwa na jambo na akawa hajui la kufanya, basi hukimbilia haraka kumtaka Ushauri Mola Mtukufu kwa  kuswali Swaaah ya Istikhaarah. Hii ni zawadi kubwa mno tuliyopewa sisi Waislamu na inapasa kwa tuitekeleza kwa kila jambo letu kubwa na dogo linalopasa kuhusiana na Swalaah hiyo.

 

Pia ukishaswali Swalaah hiyo, taka ushauri kwa jamaa zako wa karibu, jambo ambalo limeamrishwa kwetu kufanya hivyo na ni kwa ajili ya manufaa yetu wenyewe.

 

Bonyeza viungo vifautavyo upate maelezo zaidi ya Swalaah ya Istikhaara na kisha haraka ufanye maamuzi utakayoona sawa na Inshaa-Allaah itakuletea kheri nyingi.

 

 

Kwa Nini Tuswali Istikhaarah Na Iswaliwe Kwa Ajili Ya Nini?

 

Muda Wa Swalah ya Istikhaarah

 

 

Anataka Kuoa Lakini Hajui Taratibu Za Kutafuta Mchumba Kisheria?

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share