Sifa za Mke Bora (Kielelezo)

SWALI:

 

Asalam alaikum warahmatul Allah wabarakat.

Mimi ni kijana wa kiislam ninaishi Zanzibar. Sina suala ila nimefikia umri wa kutaka kuowa hivyo naomba munitumie sifa sahihi na vigezo vya mke bora katika uislam. Najua mtume katuamrisha kuwa tuangalie vitu vinne, kama mali, uzuri, ukoo au familia pamoja na dini. Ila naomba munielimishe sifa nyengine muhim za kuangalia kwan unapochagua mchumba unatakiwa kuwa makini kwan mke ndie anaetangeneza familia na anae harib familia. Pia wake zetu ni mtihan kwetu hivyo ili kuweza kujikinga na mtihan huu ningepend munipatie siza hizo.

 

Ahsanten, Nakutakieni kazi njema na inshhaallah awalipe ujira ulio mwema kwa jihan yenu. 

Assallam alaikum warrahmatullahi wabarakat


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu sifa zinazohitajika katika kuchagua mke. Uislamu ikiwa ndiyo Dini ya kimaumbile imetupatia muongozo katika kila nyanja ya maisha pamoja na kuchagua mke, ambaye ni mshirika wa mwanaume wa maisha. Miongoni mwa sifa zinazohitajika katika kuchagua mke ni:

 

  1. Mwanamke kuwa na Dini, tabia na maadili mema. Ama mas-ala ya Dini ni ile Hadiyth ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) aliyosema: Chagua mwenye Dini usije ukapata hasara (al-Bukhaariy na Muslim). Dini si ya kinadharia bali imfanye abadilike katika mambo yake yote kama kuwa na tabia njema na maadili mema.

 

  1. Kumpendeza mume anapomuangalia. Kupendeza na uzuri ni vitu ambavyo kila mwanamme ana kile anachokiona kuwa ni kizuri. Ndiyo nasaha aliyotoa Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) kwa Mughiyrah bin Shu‘bah (Radhiya Allaahu ‘anhu): Kamwangalie kwali kufanya hivyo kutaleta mapenzi baina yenu (an-Nasaa’iy).

 

  1. Kuwa ni mwenye kuingiliana na watu na mwenye moyo wa bashasha kabisa. Mafungano ni baina ya familia mbili, yako na yake. Kwa ajili hiyo anatakiwa awe ni mwanamke mwenye kufanya mahusiano na watu wako wa karibu ili kuwe na maendeleo na uhusiano mwema.

 

  1. Mwenye kuzaa, na hili kama wanavyuoni walivyosema ni kuangalia kizazi cha madada zake na jamaa zake wa karibu

 

Hata hivyo, muhimu zaidi ni Dini na ikiwa ana sifa nyingine ziwe ni baada ya hiyo sifa ya kwanza.

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

 

Sifa Gani Za Kutafuta Mke?

 

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

 

Share