Skip navigation.
Home kabah

Je, Inapasa Kufanya Ghuslu Baada Ya Kutokwa Na Manii Bila Ya Kujimai?

SWALI:

 

Asalam alaykum

Naomba kuuliza ikiwa mtu na mkewe wanaongea kwa njia ya simu na katika maongezi yao yakaja maongezi ya kutamanishana yaani maongezi ya kimapenzi... ambayo maongezi hayo yakasisimua hisia hadi yakamfanya yule mwanamme kutokwa na maji ya uzazi na mwanammke hali kadhalika, suala langu linakuja hivi kwanza yanakubalika maongezi hayo pili kama itawakuta hali hio ya kutokwa

maji wanatakiwa wakoge janaba au wakoge kikawaida tu?

Ahsante

 



JIBU:

BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu wa Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa  aalihi wa Aswhaabihil Kiraam, wa ba’ad:  

Hakuna vibaya mtu kuongea na mke wake katika simu na kuzungumza maongezi ya mapenzi kwani huyo ni halali yako, kwa hiyo hakuna tofauti ya kuongea naye kwa simu au unapokuwa naye.

Inapofika hali hiyo uliyoitaja ya baada ya mazungumzo na kutokwa na manii japo kuwa hukujimai naye mke wako, inakubidi ufanye Ghuslu na hii ni kutokana na dalili ya Hadiyth ifuatayo, kwamba Ummu Sulaym رضي الله عنها alimuendea Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akamuambia:

  "إن الله لا يستحي من الحق فهل على المرأة من غسل إذا هي احتلمت"   فقال صلى الله عليه وسلم : " نعم إذا هي رأت الماء"

 “Ewe Mtume wa Allah! Allah Haoni haya juu ya ukweli. Je, mwanamke inampasa afanye Ghuslu pindi akiota?" (Akiota ndoto ya kujimai)  Akasema: “Ndio, anapoona maji” (Al-Bukhaariy na Muslim).

Kwa kupata maelezo zaidi kuhusu mas-ala haya tafadhali soma jibu la swali katika kiungo kifuatacho kwenye ALHIDAAYA:

Ikiwa Mtachezeana Tu Na Kutokwa Manii Inapasa Kukoga Josho?

Na Allaah Anajua zaidi.