Amepatwa Na Mashaytwaan – Asomewe Du’aa Gani Atibike?

SWALI:

 

Assalamu aleyikum warahimatu llahi wabarakatu ndugu zetu wa alhidaya,

 

Swali langu nataka kujua ni dua gani asomewe mtu anayekuwa na mashetani?

 

Kuna dada yetu mmoja kafiwa hivi karibuni na dada yake, toka kafariki dadaye yeye inamujia kama kupiga kelele na lazima wawepo watu watatu au wanne kumshikilia na hiyo inaweza kumjia kwa siku hata mara 4 au 5 kwa siku. Je vipi ndugu zetu kuna dua gani tunaweza kumsomea huyu dada?


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kisomo kwa dada aliyeonekana kuwa kakumbwa na Shaytwaan.

 

Kitu cha kwanza ambacho mnafaa kufanya ni kuhakikisha kama kweli dada huyo kakumbwa na Shaytwaan. Na kujua kama kweli kakumbwa na Shaytwaan ni kumsomea kisomo cha Ruqyah ya kisheria. Kwa kusoma kisomo hicho ambacho kinajumlisha kusoma Surah na Aayah za Qur-aan Tukufu zitatoka ishara ambazo zitakujulisha kuwa kweli dada huyo kakumbwa.

 

 

Visomo hivyo vyote utapata katika maelezo yaliyomo katika viungo vifuatavyo:

 

 

 Kuhusu Mashaytwaan Na Vipi Kujikinga Nao

 

Naingiliwa Na Majini

 

Mke Wangu Amevaliwa Na Majini Wa Mahaba? Hapendi Kutenda Kitendo Cha Ndoa Na Mimi

 

Mke Analalamika Mume Ana Mashetani Yanamfanya Asiweze Kukamilisha Tendo La Ndoa

 

 

 
 

 Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Amuafu na Ampe shifaa ya haraka.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share