Kujifunga Mwili Ili Kujikinga

 

Kujifunga Mwili Ili Kujikinga

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Assalam alaijkum, Ramadhan Kareem.

Ndugu wana alhidaaya, malipo mema akuandalieni Mola wetu mlezi kwa jitihada mnayoifanya katika kuuelimisha Umma wa Kiislam. Katika jamii zetu tunasikia baadhi ya watu kua kuna kinga (kufunga mwili) ambayo ukiifanya unaepukana na majaribu yao. Swali langu. Je kwa muislam ni vyema kujifunga mwili, kwa kuhofia matendo ya kimazingara yanayofanywa na baadhi ya jamii zetu yasikupate, au kuna kinga yoyote isio kua hii?

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Tufahamu kuwa hatuwezi kuepukana na majaribio na mitihani ya Allaah Aliyetukuka kwa njia moja au nyingine. Mitihani ni lazima katika maisha ya huu ulimwengu kwa kuwa ndivyo tulivyoumbwa na ndivyo tutakavyohukumiwa kulingana na kufeli au kufaulu mtihani huo. Hakuna awezae kufunga mwili ili asipatikane na majaribio; hayo ni mambo ya uongo. Na yeyote mwenye kufanya hivyo basi amemshirikisha Allaah Aliyetukuka. Na mwenye kumshirikisha Allaah Aliyetukuka basi makazi yake ni Motoni. Allaah Aliyetukuka Atuepushe na mtihani huu mkubwa wa kumshirikisha Yeye. 

 

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametupatia kinga nyingi kwa sisi kuweza kujikinga, hivyo tutumie njia hizo na tuache nyingine zozote zile. Bonyeza pia kupata maelezo zaidi:

 

Tiba Gani Zimo Katika Qur-aan?

 

Waweza kununua kijitabu kidogo kinachoitwa Hiswn al-Muslim (Kinga ya Muislamu), nacho kitakupatia yote hayo. Kinapatikana vilevile  hapa katika Alhidaaya:

 

Hiswnul Muslim

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

Share