Sherehe Za Kukaribisha Na Kuagana Wanafunzi Zinafaa?

 

Sherehe Za Kukaribisha Na Kuagana Wanafunzi Zinafaa?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Assalam Aleykum Warahmatullah Wabarakatu.

 

Naomba kupata ufafanuzi juu ya sherehe zinazo endeshwa na jumuiya za wanafunzi wa kiislamu je ni sahihi kwa mujibu wa mafundisho? Mfano sherehe za kuwaaga au kuwakaribisha wanafunzi kwa kuweka vyakula na vinywaji mbalimbali.

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Sherehe hizo hazina tatizo katika Dini ikiwa zitafanywa kwa misingi ya Dini. Kuwepo na kuamrishana mema na kukataza maovu, kuusiana katika mema na kusiwepo mambo yoyote yale ya haramu.

 

 

Ni lazima kuwe na udhibiti wa kisheria kama kutochanganyikana baina ya wavulana na wasichana. Hii ni fursa muhimu ambayo mwaweza kuitumia kuwapata wale wanafunzi wapya kwa kuwapatia muelekeo na kuwasaidia kidini. Usaidizi kwa wageni katika chuo ni mkubwa sana mwanzoni na kwa ajili hiyo huenda mkaweza kuwashika kuanzia mwanzo hadi kumaliza kwao kwa njia ambayo itawafaidisha kwa kiasi kikubwa. Na vile vile wakati wa kutoka na kuwapatia nasaha za kuaga waendelee kumcha Allaah katika sehemu zote watakazokuwepo baada ya masomo.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share