Gulab Jamun (Pakistani)

Gulab Jamun (Pakistani)

Vipimo

Maziwa ya unga - 1 Magi

Samli - 2 Vijiko vya chai

Yai - 1

Unga wa semolina - 3 Vijiko vya chai

Baking powder - 1 Kijiko cha chai

Mafuta ya kukaangia - Kiasi

Shira

Sukari - 1 Magi

Maji - 1 Magi

Illiki - Kiasi

Zaafarani - Kidogo

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Tayarisha shira kwa kuchanganya vipimo vyote na iache motoni ichemke hadi iwe nzito kiasi.
  2. Katika bakuli changanya vizuri vipimo vyote isipokuwa mafuta ya kukaangia.
  3. Kisha fanya viduara vidogo vidogo na weka kando.
  4. Katika karai weka mafuta kwenye moto na ukaange viduara vya gulab jamun hadi zibadilike rangi ya hudhurungi kama ilivyo katika picha.
  5. Kisha mimina vile viduara vya gulab jamun kwenye shira na iachie  dakika chache na itakuwa tayari kwa kuliwa.
Share