Millefeuille: Tabaka Za Puff Pastry Kwa Mjazo Wa Cream Na Fruti.

 

 

Millefeuille: Tabaka Za Puff Pastry Kwa Mjazo Wa Cream Na Fruti.

 

Vipimo

Kutengeneza Idadi 4 Kila moja tabaka 3 

 

Puff pastry -  Paketi 1

Icing sugar ¼ kikombe

Viini vya Mayai – 4

Raspberries – mjazo wa mkono

Strawberries – mjazo wa mkono

Sukari – vijiko 4 vya chai

Unga – Kijiko 1 cha kulia

Vanilla – kijiko 1 cha chai

Maziwa – 300 ml

Icing sugar – 200 gm

Unga wa cocoa – 1 kijiko cha supu

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

 

 

Kupika Pastries:

 

 1. Washa oveni moto wa 200°C
 2. Sukuma unga wa puff pastry katika kibao ulichonyunyizia sukari kisha kata vipande 12 kiasi vya mraba (rectangle) kiasi ya saizi ya 10 cm kwa urefu na 5 cm kwa upana.
 3. Panga katika treya iliyowekewa karatasi ya kuchomea (baking paper) na nyunyizia icing sugar.
 4. Weka pastry katika katika friji kiaisi ya nusu saa kabla ya kuchoma katika oveni.
 5. Choma katika oveni kwa dakika 10 takriban mpaka zigeuke rangi ya hudhurungi (golden brown) kisha epua zipoe.

 

Namna Ya Kutengeneza Mjazo Wa Cream Na Kutia Katika Tabaka Za Pastries:

 

 1. Chemsha maziwa kiasi cha kushika moto na kukaribia kuchemka.
 2. Katika kibakuli, piga viini vya mayai, sukari, vanilla, unga.
 3. Mimina mchanganyiko wa mayai katika maziwa kisha rudisha katika moto uache huku unakoroga mpaka vifanye vipovu na kuwa nzito.
 4. Acha mchanganyiko ufanye vipovu kwa dakika moja takriban kisha ondosha.  Mimina juu ya chujio kisha funika kwa karatasi ya plastic (clingfilm) na iache ipoe.
 5. Piga icing sugar na cocoa na mnyunyizo wa maji kidogo mpaka iwe nzito na ya kugandaganda.
 6. Chovya baadhi ya puff pastry katika icing sugar au nyunyizia juu yake kwa kisu.
 7. Panga tabaka za pasty moja yenye icing na nyengine bila ya icing, kisha cream, na fruit, kisha kariri tena mpaka mwishowe umalizie kwa pastry uliochovya kwa chocolate.
 8.  

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

 

Share