Imefika Mchana Akaamua Kufunga Sunnah Bila Kuweka Niyyah Kabla, Inasihi?

 

Imefika Mchana Akaamua Kufunga Sunnah Bila Kuweka Niyyah Kabla, Inasihi?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

assalam alaykum warahmatullah nina swali moja ambalo nimejaribu kusoma kwenye maswali ambayo yameshaulizwa  naona hakuna linalo husiana "jee kama hujala kitu kuanzia asubuhi hadi jioni na baada ya kufika mchana ukasema kama mie nimefunga na nafikiri kuna hadithi ambayo imefanana na maneno yangu ambayo mtume (swala allahu alayhi wasallam) aliingia kwa bibi aisha na akauliza kuna chochote cha kula? Bibi Aisha (radhiya llahu anhaa) akasema hakuna na mtume akasema basi "nimefunga" wengine wanasema kama lazima unuwiye kabla ya kufunga na hiyo funga haikubaliwi.

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Hakika ni kuwa swali kama hilo lako tayari tumelijibu lakini hakuna shida wala tatizo kulijibu mara nyingine kwa faida ya kila mmoja wetu.

 

Ni hakika isiyopingika kuwa nia ni lazima ‘Ibaadah yoyote ile na funga si tofauti na hizo. Na huku kulala na niyah ni lazima kwa Swawm ya faradhi. Na kwa ajili hiyo amesema Nabiy  (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):  “Yeyote asiyejumlisha Swawm yake kabla ya Alfajiri hana Swawm” (Abu Daawuud).

 

Na pia,

 

Yeyote asiyelala na niyyah usiku basi hana Swawm” (an-Nasaa’iy).

 

Ama Swawm ya Sunnah mbali na kuwa ni ‘Ibaadah kama ‘Ibaadah nyingine lakini Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameitofautisha na Swawm za faradhi. Na hivyo imepatika wakati amezunguka katika nyumba za wakeze wote lakini kukawa hakuna chakula hivyo akasema mimi nafunga leo.

 

Kwa hiyo, katika Swawm ya Sunnah unaweza kuweka niyyah ya kufunga kabla ya mchana na Swawm yako itakuwa sahihi kabisa.

 

Bonyeza viungo vifuatavyo kwa faida zaidi:

 

 

Vipi Kutia Niyyah Ya 'Ibaadah Kama Swawm?

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Kutamka Niyyah Katika ‘Ibaadah Ni Bid’ah Bali Mahali Pake Ni Moyoni

 

Imaam Ibn Taymiyyah: Kutamka Niyyah Katika ‘Ibaadah Ni Upungufuu Katika Akili Na Dini

17-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Je, Inafaaa Swiyaam Za Sunnah Bila Ya Kutanguliza Niyyah?

Vipi Kutia Niyyah Swalaah Za Qiyaamul-Layl?

 Vipi kutia Niyyah Swalaah za Sunnah?

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

 

 

Share