Keki Ya Tende -1

 Keki Ya Tende - 1

Vipimo

Unga -  3 kikombe

Baking powder  -  3 Vijiko vya chai

Sukari  -  ½ Kikombe

Tende iliyokatwa ndogo ndogo - 2 vikombe

Maji yamoto -  2 vikombe

Siagi - 4 Vijiko vya supu (au vikombe 2 vya kahawa)

Mayai - 2

Cream -  300 gm (au vikombe 2 Vya Kahawa)

Tangawizi ya powder -   2 Vijiko vya chai

Mdalasini - 1  kijiko cha chai

Hiliki -   ½  kijiko cha chai

Vanilla - 4  vijiko vya chai 

Vipimo Vya Karamel 

Sukari ya buni (brown sugar) -  5 Vijiko vya supu

Siagi -  6 Vijiko vya supu

Lozi zilizomenywa na kukatwa Nyembamba -   1 kikombe  

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Tia maji ya moto katika tende kuiroweka kidogo.
  2. Changanya unga na baking powder vizuri katika bakuli.
  3. Tia vitu vyote vingine na uchanganye vizuri.
  4. Mimina katika bati la duara la kupikia keki ulilolipaka siagi kidogo la kiasi ya 10 in dia x 2 in    
  5. Ipikie (bake) katika moto  wa 300° kwa muda wa kama ¾  saa au zaidi hadi iwive.
  6. Iweke katika sahani au bakuli la keki na mwagia karamel juu yake, kisha haraka upambie lozi.

Namna ya kutayarisha Karamel

Yayusha siagi katika sufuria ndogo au frying pan kisha tia sukari ya brown.

Inapoyayuka, mwagia katika keki.

 

Share