Keki Ya Chokoleti Ilokoza Na Kahawa

Keki Ya Chokoleti Ilokoza Na  Kahawa  

    

Vipimo

Unga - 2 vikombe

Sukari - 2 vikombe

Mafuta  - ½ kikombe

Mayai - 2

Kaukau (cocoa) - ¾  kikombe

Kahawa ya unga - 2 vijiko vya supu

Baking powder - 1 kijiko cha chai

Baking soda - 2 vijiko vya chai

Maziwa - 1 ¾  kikombe

Chumvi - ½  kijiko cha chai 

Namna Kupika:

  1. Washa jiko la oveni moto wa 350° - 375° F 
  2. Paka mafuta treya ya kupikia keki ya saizi 9” x 13” ikiwa ni yenye shimo la wazi kama ilivyo katika picha. Ikiwa huna treya hiyo, tumia ya kawaida. 
  3. Katika bakuli, tia unga, sukari, kaukau, unga wa kahawa, baking powder, baking soda, chumvi. 
  4. Piga mayai katika kibakuli kidogo kisha changanya katika unga pamoja na mafuta  na maziwa.  
  5. Mimina katika treya ya kupikia keki, pika katika oveni kwa muda wa dakika 35 takriban. 
  6. Epua ipoe kisha ikate saizi ya vipande upendavyo.

  

 

Share