Benki Inatoa Zawadi Kutokana Na Kiwango Cha Pesa Uloweka Badala Ya Fedha, Je, Ni Ribaa Pia?

SWALI:

 

Asalaam alaykum

Shukrani kwa makala zenu nzuri ambazo zinatupatia faida na elimu tukufu. Mola akulipeni ujira mwema nasi atupe elimu yenye manufaa pamoja nanyi Amin.

 

Kuna benki huku Afrika Mashariki imeanzisha kuweka akiba kwa muda maalum na badala ya kupewa riba unapewa zawadi kama Tv au gari inategemea kiwango cha fedha uliyoweka. Kuna viwango maalum ambavyo unahitajika uweke na kwa muda wa miaka maalum (miaka minne). Hizi zawadi utapewa lakini hutopewa ziada yoyote ya fedha (riba). Jee, hii zawadi inakubalika kupokea kwa mujibu wa sheria na haitohesabika kama riba.

 

 


 

 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu benki inayotoa zawadi kutokana na kiwango cha akiba yako badala ya pesa.

Hakika ni kuwa benki nyingi ni za Kiyahudi ambao kwa sasa wameunda njama ya kuwalisha Waislamu ribaa kwa njia tofauti.

 

Msingi wa benki takriban zote ni wa kukopesha kwa ribaa na kutoa ribaa baada ya kila mwaka au muda maalumu waliouweka. Hii ni njia ya kuwavutia watu na hasa Waislamu kujiunga na benki hizo kwa kuwashawishi. Kwa kuwa msingi wake (benki) ni ribaa, zawadi zinazo tolewa ni aina ya ribaa.

 

Kwa hiyo, Muislamu hafai kuchukua zawadi hiyo.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share