Makhalifa 12 Waliotajwa Kuwa Watakuja Ni Hao Maimaam 12 Wa Kishia Kama Wanavyodai Wao?

SWALI:

 

Asalam aleykum...Ningependa msaada wenu kuna rafiki yangu mshia alinipa kitabu kilichosema kwamba "kutakuwa na makhalifa kumi na mbili kutoka kwa Makuraysh/ Bani Hashim baada ya Mtume (swala llahu aleyhi wasalam)" pia hii hadith inapatikana katika kitabu cha hadith cha muslim..Sasa ao makhalifa ni wapi?? Na vipi kumuelewesha kwamba ao makhalifa kumi na mbili sio wao akina shia ithna ashariya...jazakallah.


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu Makhalifa kumi na mbili.

Hakika masimulizi hayo ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yako si katika Muslim tu, bali pia katika Swahiyh al-Bukhaariy na Sunan ya Abu Daawuud. Hata hivyo, katika Hadiyth zote hizo wametajwa Makhalifa wenyewe watatoka katika kabla la Quraysh na wala si ukoo wa Banu Haashim. Kumaanisha kuwa wanaweza kutoka katika ukoo wa Banu Haashim, Banu Makhzuum, Banu Mutwtwalib, Banu ‘Abd ad-Daar, Banu Umayyah, Banu ‘Adiy, Banu Taym, na kadhalika. Tufahamu kuwa koo za Quraysh zimegawanyika kuwa kumi na mbili.

 

Katika Hadiyth ya Muslim inasema:

Dini ya Kiislamu itaendelea mpaka Saa (Qiyaamah) isimame au mmetawaliwa na Makhalifa kumi na mbili”.

 

Ama Mashia, wao hawawaiti viongozi wao kwa jina la Khaliyfah bali Imaam ambao sifa zao ni za kiungu si za kibinaadamu. Kisha wao, hao Maimamu wa kishia hawakuwahi kutawala na wala hawakufika 12 kama wanavyodai. Ila tu labda huyo wa 12 awe atazaliwa baadaye. Kwa nini tunasema hawakufika 12, ni kuwa Imaam wao wa 11, Hasan al-Askari hakuzaa kabisa. Kwa hiyo ni udanganyifu wao kusema kuwa Imaam wao wa 12 alizaliwa na yuko katika pango mpaka atakaporudi tena kueneza uadilifu kati ya wanaadamu duniani.

 Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo na manufaa zaidi:

 

Maimamu Wako Wangapi? Je Kuna Tofauti Baina Yao?

 

Qur-aan Na Uimamu Wa Mashia

 

Anataka Dalili Ya Kuwa Maimamu Wa Kishia Wanajipangia Wenyewe Kufa

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share