Mtindi Wa Nafaka, Rasiberi, Chokoleti Na Malai

Mtindi Wa Nafaka, Rasiberi, Chokoleti Na  Malai

  

Vipimo  

Mtindi (yoghurt) -  3 Vijiko vya supu katika kila gilasi

*Sosi ya  rasiberi - 2 vijiko vya supu

Nafaka (Cereal) - 2 vijiko vya supu

Malai  (Ice-cream) - 2 mchoto (scoops)

Chokoleti iliyovurugwa - kiasi upendavyo   

Namna Ya Kutayarisha  

  1. Tia kwanza mtindi (yoghurt) katika gilasi. 
  2. Tia chokoleti iliyovurugwa (crushed)     
  3. Tia sosi ya Rasiberi  (Raspberry) 
  4. Tia michoto wa malai (ice-cream)  uipendayo     
  5. Mwagia juu  nafaka (cereal)  za mchanganyiko wa njugu na fruti kavu. 
  6. Pambia kwa kipande cha chokoleti – iko tayari kuliwa.             

Kidokezo:  * Ukikosa sosi ya tayari ya rasiberi unaweza kutumia jam yake.

 

 

 

 

Share