Hamuamini Mkewe Kwa Sababu Hakumkuta Bikira

 

SWALI:

 

Assalam alaikum.mimi ni kijana na nina mke na watoto.lakini tangu siku ya harusi yangu nimekuwa sina uaminifu kwa mke wangu. kwa sababu siku ya kwanza ya harusi yetu wakati tunafanya tendo la ndoa nimehisi kama mke wangu hayuko bikra. na nimejaribu kumuuliza nani alombikiri kaniapia kama hajawahi kufanya tendo la ndoa kabla ya mimi, na ananihakikishia kama hajawahi kabisa kuwa na mwanamme hasa. na anasema itakuwa mimi ndo niliyemuharibu bikra yake kwa sababu nilipimuingilia siku ya kwanza nilitumia vidole badala ya uume wangu. sasa nataka kujua kweli inawezekana bikira ikaondoka kwa kutia vidole au kwa njia yoyote isiyokuwa ya kufanya tendo la ndoa. naomba jibu kwani nipo mashakani mimi na mke wangu pia.

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu kutomuamini mkeo.

Kwanza tunataka kukunasihi sana kuwa uwe na Imani na mkeo na ufanye juhudi ya kuwa mbali na Shaytwaan. Inavyoonyesha katika swali lako ni kuwa unatiwa wasiwasi na Shaytwaan pasi na wewe kujua hilo.

 

Pili tufahamu kuwa kizinda cha mwanamke kinachomfanya yeye kubaki katika ubikira ni chororo sana. Kizinda hicho huenda kikakatika kwa hata kwa msichana kuruka ruka au michezo ambayo inamfanya yeye awe ni mwenye kupanua miguu yake, kupanda baiskeli, mnyama au wakati mwengine wapo wasichana ambao hawana kabisa. Na tufahamu kuwa kumuingizia msichana kidole au vidole inaondosha kabisa ubikira huo pasi na wasiwasi wa aina yoyote.

 

Hivyo, siku ya kwanza ulifanya makosa kumuingizia vidole na hivyo kuondosha ubikira wa mkeo. Kinachotakiwa ni wewe kumuamini mkeo kwa analosema kwani kutofanya hivyo kutaleta kukosekana uaminifu na kupotea mapenzi katika maisha yenu na hatimaye kuyaparaganya.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share