Supu Ya Mahindi, Karoti Na Viazi

VIPIMO
Karoti (katakata ndogo ndogo) 3
Viazi (katakata vidogo vidogo – cubes) 3
Mahindi (chembe) 2 vikombe
Supu ya vidonge (stock – Maggi cubes) 1 kidonge
Pilipili manga 1 kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Ndimu 1 kijiko cha chai
Siagi au mafuta 2 vijiko vya supu
NAMNA YA KUTAYARISHA
1. Tia siagi au mafuta katika sufuria, kaanga viazi, vikiwa karibu na kuwiva tia karoti, endelea kukaanga
2. Tia mahindi changanya vizuri katika moto mdogo.
3. Tia maji kiasi, tia kidonge cha supu (Stock), tia pilipili manga, chumvi na ndimu
4. Acha ichemke hadi viazi na karoti ziwive vizuri.
5. Saga nusu yake katika mashine ya kusagia (blender) urudishe ndani ya sufuria. Changanya pamoja.
6. Mimina katika bakuli ikiwa tayari.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


