Supu Ya Nyama Ya Mbuzi, Adesi Na Mchicha
Vipimo
Nyama ya mbuzi 1 kilo
Kitunguu kikubwa 1
Thomu na tangawizi iliyosagwa 1 Kijiko cha supu
Pilipili manga 1 Kijiko cha chai
Mchicha 2 magi
Chumvi Kiasi
Viazi 2
Kidonge cha supu 1
Adesi (ukipenda) 1 Kikombe cha chai
Nyanya 1
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Osha adesi na chemsha hadi ziive
- Katakata kitunguu na nyanya.
- Katika sufuria tia nyama na viungo vyote isipikuwa mchicha, adesi na viazi, kisha iache motoni ichemke hadi nyama iive.
- Halafu katakata viazi na uvitia katika supu na ziache zichemke hadi ziive.
- Kisha mimina adesi na mwishoe mchicha na iache katika moto kwa muda mfupi tu.
- Mimina katika bakuli na supu tayari kuliwa.
- Login or register to post comments
- Chapisha
- Kutuma Kwa Email
