Okra/Bamia Za Kukaanga

Okra/Bamia Za Kukaanga

  

Vipimo: 

Bamia  

Kitunguu - 1 

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 3 chembe 

Methi/Uwatu/fenugreek ilosagwa - ½ kijiko cha chai 

Pilipili manga -  ½  kijiko cha chai 

Pilipili mbichi -  1 

Chumvi -  kiasi 

Mafuta -  3 vijiko vya supu  

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Osha okra/bamia kata vikonyo, kisha zikate vipande kwa urefu. 
  2. Katakata kitunguu maji, kitunguu thomu, pilipili mbichi weka kando. 
  3. Weka mafuta katika karai kisha kaanga kitunguu hadi kianze kugeuka rangi kuwa hudhurungi (golden brown) kisha tia kitunguu thomu kaanga kidogo tu. 
  4. Tia bamia, pilipili mbichi, methi, pilipili mbichi, chumvi endelea kukaanga kwa moto mdogo mdogo hadi bamia ziwive na ziwe tayari.

 

 

.

 

Share