Mwanamme Kufanya DNA Test Ili Kuhakikisha Kuwa Mtoto Ni Wake Inajuzu?

 

Mwanamme Kufanya DNA Test Ili Kuhakikisha Kuwa Mtoto Ni Wake Inajuzu?

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

 

Je ni halali kwa mwanamme kufanya DNA test ili kutaka kujua kwamba mtoto kweli ni halali yako labda kwa kutaka kuondoa shaka?

 

 

JIBU:

 

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Ni ajabu kwa mwanamme kuanza kumshuku mkewe kuwa anatembea nje kwani kufanya hivyo kunavunja kabisa uhusiano wa kindoa na kukosa utulivu kwa kiroho na kimoyo. Mwanamme au mwanamke akianza tu kumshuku wapili wake katika ndoa ndio kuivunja ndoa yenyewe.

 

 

Ndoa ni mapenzi na kuhurumiana baina ya wanandoa. Na kupata natija hiyo ni lazima wanandoa wawe ni wenye kuaminiana kwa kiasi kikubwa kwani kutoaminiana ni wasiwasi unaoingiszwa na shaytwaan, na shaytwaan ni adui mkubwa sana mwa mwana-Aadam.

 

 

Kwa hiyo, ondoa shaka wala usiende kufanya DNA test kwa hali yoyote ile. Kuwa na Iymaan na mkeo kuwa ni mwaminifu na In Sha Allaah Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  Atakuondoshea wasiwasi huo usio mzuri.

 

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo na manufaa zaidi:

 

Nini Hukmu Ya DNA Katika Uislaam

 

Kuwatambulisha Watoto Bila DNA

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share