Hariys- Bokoboko La Nyama Ya Ng’ombe

Hariys- Bokoboko La Nyama Ya Ng’ombe

 

Vipimo

Ngano nzima (shayiri) - 1 kilo

Nyama ng’ombe mchanga ya mifupa - 2 kilo

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai

Chumvi - kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Roweka ngano  kiasi masaa manne

Osha nyama, changanya na ngano, tia chumvi, pilipili manga, tia maji kiasi, funika uchemshe ipikikie moto wa kiasi kwanza.

Baada ya saa takriban, koroga, ongeza maji ikibidi, punguza moto uendelee kuiweka motoni ichemke na kuiva pole pole kabisa. 

Inapoanza nyama na ngano kuiva pamoja, koroga huku unaisonga, na huku mifupa ya nyama itenganike na nyama humo humo katika sufuria.

Unazidi kuendelea kusonga mpaka inajichanganya vizuri. Inakuwa tayari kuliwa

 

Kidokezo:

Ikiwa aina ya nyama ni ngumu, unaweza kuchemsha kwanza katika pressure  cooker pamoja na ngano. Kisha uimimine katika sufuria na kuendelea kuipika na kuisonga hadi ichanganyike iwe laini.

 

 

Share