Baadhi Ya Amali Na Mambo Yanayosababisha Kupata Mapenzi Ya Allaah (سبحانه وتعالى)

 

Baadhi Ya Amali Na Mambo Yanayosababisha Kupata Mapenzi Ya Allaah (سبحانه وتعالى)

 

Alhidaaya.com

 

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atakapompenda mja Wake, basi hakika itatangazwa mbinguni na ardhini na hapo kila kiumbe mwema atakupenda na kila jambo lako litakuwa lenye mafanikio, na pindi Akikuchukia basi kila kiumbe mwema atakuchukia.  Hadiyth zifuatazo zimethibitisha:

 

عن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( إِذَا أَحَبَّ اللهُ تَعَالَى العَبْدَ ، نَادَى جِبْريلَ : إنَّ الله تَعَالَى يُحِبُّ فُلاناً ، فَأَحْبِبْهُ ، فَيُحِبُّهُ جِبريلُ ، فَيُنَادِي في أَهْلِ السَّمَاءِ : إنَّ اللهَ يُحِبُّ فُلاناً ، فَأحِبُّوهُ ، فَيُحِبُّهُ أهْلُ السَّمَاءِ ، ثُمَّ يُوضَعُ لَهُ القَبُولُ في الأرْضِ )) متفق عليه .

وفي رواية لمسلم : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( إنَّ الله تعالى إذا أحب عبداً دعا جبريلَ ، فقال : إنّي أُحِبُّ فلاناً فأحببهُ ، فيحبُّهُ جبريلُ ، ثمَّ ينادي في السماءِ ، فيقول : إنَّ اللهَ يحبُّ فلاناً فأحبوهُ ، فيحبُّهُ أهلُ السماءِ ، ثمَّ يوضعُ لهُ القبولُ في الأرضِ ، وَإِذَا أبْغَضَ عَبْداً دَعَا جِبْريلَ ، فَيَقُولُ : إنّي أُبْغِضُ فُلاناً فَأبْغِضْهُ . فَيُبغِضُهُ جِبريلُ ثُمَّ يُنَادِي في أَهْلِ السَّماءِ : إنَّ الله يُبْغِضُ فُلاناً فَأبْغِضُوهُ ، ثُمَّ تُوضَعُ لَهُ البَغْضَاءُ في الأَرْضِ )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anapompenda mja anamuita Jibriyl na kumwambia: “Hakika Mimi nampenda fulani, hivyo nawe mpende.” Hivyo Jibriyl anampenda mtu huyo na baada ya hapo anatangaza kwa watu wa mbinguni kwamba: ‘Hakika Allaah anampenda fulani, kwa hivyo nanyi nyote mpendeni.’ Hapo watu wa mbinguni wanampenda mtu huyo. Kisha anawekewa kabuli (kukubaliwa) na watu wa ardhini. [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

Na katika riwaayah ya Muslim: Amesema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)   Anapompenda mja, anamuita Jibriyl, na kumwambia: “Hakika Mimi nampenda fulani, nawe mpende.” Hivyo Jibriyl anampenda mtu huyo na baada ya hapo anatangaza mbinguni kwa kusema: ‘Hakika Allaah Anampenda fulani, kwa hivyo nanyi nyote mpendeni.’ Hapo watu wa mbinguni nao pia wanampenda mtu huyo. Kisha anawekewa kabuli (kukubaliwa) na watu wa ardhini. Na Allaah Anapomchukia mtu yeyote anamuita Jibriyl na kumwambia: “Hakika Mimi namchukia fulani, nawe mchukie.” Hivyo Jibriyl (‘Alayhis-salaam) anamchukia mtu huyo na baada ya hapo anatangaza kwa watu wa mbinguni kwamba: “Hakika Allaah Anamchukia fulani, kwa hivyo nanyi nyote mchukieni.” Hapo watu wa mbinguni nao pia wanamchukia mtu huyo. Kisha anawekewa chuki na watu wa ardhini.” 

 

Na pindi Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akikupenda, basi utakuwa katika ulinzi Wake na kila adui yako atakuwa ni adui wa Allaah ('Azza wa Jalla) na Atakutaqabalia haja zako:

 

 

عن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( إنَّ الله تَعَالَى قَالَ : مَنْ عَادَى ليَ وَلِيّاً ، فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالحَرْبِ ، وَمَا تَقَرَّبَ إِلَيَّ عَبْدِي بِشَيءٍ أَحَبَّ إِلَيَّ مِمَّا افْتَرَضْتُ عَلَيهِ ، وَمَا يَزالُ عَبْدِي يَتَقَرَّبُ إِلَيَّ بِالنَّوَافِلِ حَتَّى أُحِبَّهُ ، فَإِذَا أحْبَبْتُهُ ، كُنْتُ سَمْعَهُ الَّذِي يَسْمَعُ بِهِ ، وَبَصَرَهُ الَّذِي يُبْصِرُ بِهِ ، ويَدَهُ الَّتي يَبْطِشُ بِهَا ، وَرجْلَهُ الَّتِي يَمْشِي بِهَا وَإنْ سَألَنِي أعْطَيْتُهُ ، وَلَئِن اسْتَعَاذَنِي لأعِيذَنَّهُ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah Ta'aalaa Amesema: "Mwenye kumfanyia uadui rafiki yangu basi Nimemtangazia vita. Hajikurubishi Kwangu mja Wangu kwa kitu ninachokipenda zaidi kuliko nilichomfaradhishia, Na mja haachi kujikurubishi kwangu kwa Sunnah mpaka Nimpende. Ninapompenda, Ninakuwa sikio lake analosikilizia, na jicho lake analoonea, na mkono wake anaoshikia, na mguu wake anayotembelea, Akiniomba Nitampa, na akijilinda kwangu Nitamlinda." [Al-Bukhaariy]

 

 

Basi jitahidi upate mapenzi ya Allaah ('Azza wa Jalla) kwa kutekeleza yafuatayo:

 

 

 

Kuwa na iymaan

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):   

 

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ ۗ  

Na miongoni mwa watu wako wenye kuchukua asiyekuwa Allaah na kuwafanya kuwa ni wanaolingana (na Allaah) wanawapenda kama kumpenda Allaah. Na wale walioamini wana mapenzi zaidi kwa Allaah. [Al-Baqarah 2: 165].

 

 

Kumfuata Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

  

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣١﴾

 

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu”. [Aal-‘Imraan: 31]

 

 

Kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kumdhukuru mno na pia kurejea Kwake kwa kila jambo:

 

Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):  

 

 

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ (( يَقُولُ اللَّهُ تَعَالَى: أَنَا عِنْدَ ظَنِّ عَبْدِي بِي وَأَنَا مَعَهُ إِذَا ذَكَرَنِي، فَإِنْ ذَكَرَنِي فِي نَفْسِهِ ذَكَرْتُهُ فِي نَفْسِي، وَإِنْ ذَكَرَنِي فِي مَلَإٍ ذَكَرْتُهُ فِي مَلَإٍ خَيْرٍ مِنْهُمْ، وَإِنْ تَقَرَّبَ إِلَيَّ بِشِبْرٍ تَقَرَّبْتُ إِلَيْهِ ذِرَاعًا، وَإِنْ تَقَرَّبَ إِلَيَّ ذِرَاعًا تَقَرَّبْتُ إِلَيْهِ بَاعًا، وَإِنْ أَتَانِي يَمْشِي أَتَيْتُهُ هَرْوَلَةً)) البخاري، مسلم، الترمذي و ابن ماجه

 

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema, ((Allaah Ta’aalaa, Anasema: Mimi ni vile mja Wangu anavyonidhania. Niko pamoja naye Anaponikumbuka katika nafsi yake, Ninamkumbuka  katika nafsi Yangu, anaponikumbuka katika hadhara, Ninamkumbuka katika hadhara bora zaidi. Na anaponikaribia shibiri Ninamkaribia dhiraa; anaponikaribia dhiraa, Ninamkaribia pima, anaponijia kwa mwendo (wa kawaida) ninamwendea mbio)) [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na Ibn Maajah]

 

 

Kutimiza fardhi kwanza kisha kuzidisha ‘amali za Sunnah:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ اللَّهَ قَال:َ مَنْ عَادَى لِي وَلِيًّا فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالْحَرْبِ، وَمَا تَقَرَّبَ إِلَيَّ عَبْدِي بِشَيْءٍ أَحَبَّ إِلَيَّ مِمَّا افْتَرَضْتُ عَلَيْهِ،  وَمَا يَزَالُ عَبْدِي يَتَقَرَّبُ إِلَيَّ بِالنَّوَافِلِ حَتَّى أُحِبَّهُ، فَإِذَا أَحْبَبْتُهُ كُنْتُ سَمْعَهُ الَّذِي يَسْمَعُ بِهِ، وَبَصَرَهُ الَّذِي يُبْصِرُ بِهِ، وَيَدَهُ الَّتِي يَبْطِشُ بِهَا، وَرِجْلَهُ الَّتِي يَمْشِي بِهَا، وَإِنْ سَأَلَنِي لَأُعْطِيَنَّهُ، وَلَئِنْ اسْتَعَاذَنِي لَأُعِيذَنَّهُ)) البخاري

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema: “Atakayemfanyia uadui kipenzi changu Ninatangaza vita dhidi yake. Mja Wangu hanikaribii na kitu chochote Ninachokipenda kama ‘amali nilizomfaridhishia. Na mja Wangu huzidi kunikaribia kwa ‘amali za Sunnah ili nimpende. Ninapompenda, huwa masikio yake yanayosikilizia, macho yake anayoonea, mikono yake anayonyoshea, miguu yake anayotembelea nayo, lau angeniomba kitu bila shaka ningempa, lau angeniomba himaya bila shaka ningelimkinga.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Kupenda kuisoma Suwrah Al-Ikhlaasw:

 

عَنْ عَائِشَةَ أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم بَعَثَ رَجُلاً عَلَى سَرِيَّةٍ، وَكَانَ يَقْرَأُ لأَصْحَابِهِ فِي صَلاَتِهِ فَيَخْتِمُ بِ ـ {‏قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ‏}‏ فَلَمَّا رَجَعُوا ذَكَرُوا ذَلِكَ لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ ‏"‏ سَلُوهُ لأَىِّ شَىْءٍ يَصْنَعُ ذَلِكَ ‏"‏‏.‏ فَسَأَلُوهُ فَقَالَ لأَنَّهَا صِفَةُ الرَّحْمَنِ، وَأَنَا أُحِبُّ أَنْ أَقْرَأَ بِهَا‏.‏ فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ أَخْبِرُوهُ أَنَّ اللَّهَ يُحِبُّهُ ‏"‏‏

Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alituma kikosi cha jeshi chini ya uongozi wa mtu aliyekuwa akiwaongoza Swahaba zake katika Swalaah. Akawa katika Swalaah zake zote alizokuwa akiswalisha wenzake, akimalizia kwa:

قُل هُوَ الله أَحَدٌ

Waliporudi (Madiynah), Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitajiwa hilo, naye akawaambia: "Muulizeni ni kwa sababu gani anafanya hivyo?" Wakamuuliza, naye akasema: Kwa sababu humo ndani zipo Sifa za Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma), nami napenda kuzisoma. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akasema: "Mpeni khabari kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Anampenda." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Na Ibn Qayyim Al-Jawziyy (Rahimahu Allaah) ametaja katika kitabu chake: Madaarij As-Saalikiyn alama kumi zifuatazo zinazosababisha mapenzi ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):   

 

1. Kusoma Qur-aan kwa kuzingatia na kufahamu maana yake.

 

 

2. Kujikurubisha kwa Allaah ('Azza wa Jalla)  kwa ‘amali za Nawaafil (Sunnah) baada ya yaliyofaridishwa kwani yanamfikisha mtu daraja kubuwa kabisa ya mapenzi. (Kama ilivyotajwa katika Hadiyth ya Qudsiyy hapo juu).

 

 

3. Kumdhukuru Allaah katika kila hali; kwa ulimi, moyo, vitendo. Daraja ya mapenzi hulingana na kadiri ya ‘amali za mja. 

 

 

4. Kukhiari Anayoyapenda Allaah ('Azza wa Jalla)  kuliko unayoyapenda pale unapoghilibiwa na matamanio yako.

 

 

5. Kuufanya moyo wako uzingatie Majina na Sifa Zake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na kuzishuhudia, kuzitambua, na kuzifanyia kazi mafunzo yake.

 

 

6. Kukumbuka fadhila na neema Zake nyingi, zinazodhihirika na zilofichika, kwani zinapeleka kwenye mapenzi Yake.

 

 

7. (Na ajabu zaidi ni) Kuulainisha moyo wako kwa kila hali, kuwa na unyenyekevu, kujidhalilisha unapomwabudu Allaah ('Azza wa Jalla).

 

 

8.  Kujipwekeksha Kwake Anapoteremka thuluthi ya mwisho ya usiku kwa kuomba kuokoka, kusoma maneno Yake (Qur-aan), kusimama (katika Qiyaamul-Layl) kwa unyenyekevu na kwa adabu nzuri kisha umalizie kwa kuomba maghfirah na tawbah.

 

 

9.  Kushikamana na wenye mapenzi ya kweli katika vikao vyao unufaike na kauli (na mafunzo) yao.

 

 

10.  Kujiweka mbali na kila kinachosababisha moyo kuwa mbali na Allaah (‘Azza wa Jalla), na kuu zaidi ni kujiepusha na matamanio yanayopeleka kwenye shirki hasa katika kutafuta mapenzi ya Allaah ('Azza wa Jalla).

 

 

Share