Mume Hatazami Nyumba Ipasavyo


SWALI:

A alykum mimi niko ..... naishi na mume wangu na watoto wangu mume wangu anafanya kazi ya kusafirisha magari kupeleka, wateja madukani kununua magari sasa inafika siku nyengine anakua kazini mpaka sasa saba usiku hajarud nyumbani na niko peke yangu na kazi za nyumba na watoto na nina watoto sita huyo wa kwanza anamiaka tisa sasa hivi tuseme bado nimdogo sasa kila kitu cha nyumbani nishuhulikie mimi na unajua tena kazi za nyumba hata nikilala nakua taabaani saana na mume wangu akirud kazini siku nyengine hata kama karudi mapema hanisaidii ktu chochote ukimwambia anakua mkali sasa vipi huyu mume wangu hapati dhambi nakuna mahitaji ya ndani anatakiwa atekeleze yeye kama kutengeneza nyumba kilichoharibika ukimueleza basi anakwambia achana nacho.

 


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allah Aliyetukuka Mola  wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), ahli zake, Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka siku ya Mwisho.

Hili kama tunavyosema mara nyingi limekuwa tatizo sugu katika jamii yetu. Kwa kawaida tatizo hili linaletwa na malezi ambayo hayajafuata mfumo wa Kiislamu. Hili linakuwa tatizo kubwa zaidi wakati mtu ameoa au ameolewa.

Mume na mke kawaida wanakuwa ni wenye kusaidiana hasa kukiwa na shughuli nyingi kama unavyosema lakini mara nyingi wanaume hawawasaidii wake zao katika hilo kuona kuwa kufanya hivyo ni kujiteremsha hadhi yao. Tukiangalia tunamuona Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa Sallam) akisaidia katika kazi za nyumba na pia Maswahaba walifuata mwendo huo.

Nasaha ambayo tunaweza kumpatia dada yetu ni:

  1. Kukaa chini wewe na mume wako na kuzungumza kinaganaga kuhusu  maisha yenu na kusaidiana. 

  2. Ikiwa haikufaulu, basi watumie marafiki zake ambao wameshikamana na  Dini kuweza kumnasihi.

  3. Tafuta Masheikh waje kumpatia ushauri na nasaha katika mas-ala ya unyumba.

  4. Ikiwa wazazi wapo karibu nanyi, jaribu kuwakutanisha wazazi wa familia zenu wayajadili matatizo hayo na kuyatafutia ufumbuzi.

 

Na Allah Anajua zaidi.

 

Share