005 - Al-Maaidah

 

 

 الْمَائِدَة

 

005-Al-Maaidah

 

 

005-Al-Maaidah: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَوْفُوا بِالْعُقُودِ ۚ أُحِلَّتْ لَكُم بَهِيمَةُ الْأَنْعَامِ إِلَّا مَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ غَيْرَ مُحِلِّي الصَّيْدِ وَأَنتُمْ حُرُمٌ ۗ إِنَّ اللَّـهَ يَحْكُمُ مَا يُرِيدُ ﴿١﴾

1. Enyi walioamini! Timizeni mikataba. Mmehalalishiwa wanyama wa mifugo wanaopelekwa malishoni, isipokuwa mnaosomewa (humu kuwa si halali). Ila tu msijiruhusu mkawinda mkiwa katika ihraam,[1] ni marufuku. Hakika Allaah Anahukumu Atakayo.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُحِلُّوا شَعَائِرَ اللَّـهِ وَلَا الشَّهْرَ الْحَرَامَ وَلَا الْهَدْيَ وَلَا الْقَلَائِدَ وَلَا آمِّينَ الْبَيْتَ الْحَرَامَ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّن رَّبِّهِمْ وَرِضْوَانًا ۚ وَإِذَا حَلَلْتُمْ فَاصْطَادُوا ۚ وَلَا يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ أَن صَدُّوكُمْ عَنِ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ أَن تَعْتَدُوا ۘ وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿٢﴾

2. Enyi walioamini! Msikhalifu utukufu wa Ishara za Allaah, wala Miezi Mitukufu wala wanyama wanaopelekwa Haram kuchinjwa, wala vigwe (vyao), wala (kukhalifu) amani kwa) wanaoiendea Nyumba Tukufu (Makkah) wanatafuta Fadhila kutoka kwa Rabb wao na Radhi. Na mkishatoka kwenye ihraam basi windeni (mkitaka). Na wala isikuchocheeni chuki mliyonayo kwa watu kwa vile walikuzuieni na Al-Masjid-Al-Haraam ikakupelekeni kufanya uonevu. Na shirikianeni katika wema na taqwa, na wala msishirikiane katika dhambi na uadui. Na Mcheni Allaah, hakika Allaah Ni Mkali wa Kuakibu.[2]

 

 

 

حُرِّمَتْ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ وَالْمُنْخَنِقَةُ وَالْمَوْقُوذَةُ وَالْمُتَرَدِّيَةُ وَالنَّطِيحَةُ وَمَا أَكَلَ السَّبُعُ إِلَّا مَا ذَكَّيْتُمْ وَمَا ذُبِحَ عَلَى النُّصُبِ وَأَن تَسْتَقْسِمُوا بِالْأَزْلَامِ ۚ ذَٰلِكُمْ فِسْقٌ ۗ الْيَوْمَ يَئِسَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن دِينِكُمْ فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِ ۚ الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ فَمَنِ اضْطُرَّ فِي مَخْمَصَةٍ غَيْرَ مُتَجَانِفٍ لِّإِثْمٍ ۙ فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣﴾

3. Mmeharamishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na kilichotajiwa asiyekuwa Allaah katika kuchinjwa kwake, na (pia) mnyama aliyekufa kwa kukosa hewa au aliyepigwa akafa, au aliyeporomoka toka juu, au aliyepigwa pembe, na aliyeliwa na mnyama mwitu, isipokuwa mliyewahi kumchinja kihalali (kabla ya kufa), na waliochinjwa kwa ajili ya ibaada ya waabudiwa, na kupiga ramli kwa mishale. Hayo kwenu ni ufasiki. Leo wamekata tamaa wale waliokufuru na Dini yenu, basi msiwaogope, bali Niogopeni Mimi. Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na Nimekutimizieni Neema Yangu, na Nimekuridhieni Uislamu uwe Dini yenu. Basi atakayelazimika katika njaa kali bila kulalia kwenye dhambi (akala vilivyoharamishwa), basi hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.[3]

 

 

يَسْأَلُونَكَ مَاذَا أُحِلَّ لَهُمْ ۖ قُلْ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۙ وَمَا عَلَّمْتُم مِّنَ الْجَوَارِحِ مُكَلِّبِينَ تُعَلِّمُونَهُنَّ مِمَّا عَلَّمَكُمُ اللَّـهُ ۖ فَكُلُوا مِمَّا أَمْسَكْنَ عَلَيْكُمْ وَاذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ عَلَيْهِ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿٤﴾

4. Wanakuuliza wamehalalishiwa nini? Sema: Mmehalalishiwa vilivyo vizuri na mlivyowindiwa na wanyama na ndege wakali mliowafundisha kiweledi, na mnawafunza katika ambayo Allaah Amekufunzeni. Basi kuleni walichokukamatieni, na mkitajie Jina la Allaah. Na mcheni Allaah, hakika Allaah Ni Mwepesi wa Kuhesabu.

 

 

الْيَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۖ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَّكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَّهُمْ ۖ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ مُحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ وَلَا مُتَّخِذِي أَخْدَانٍ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِالْإِيمَانِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٥﴾

5. Leo mmehalalishiwa vilivyo vizuri. Na nyama iliyochinjwa na waliopewa Kitabu ni halali kwenu, na nyama mliyochinja nyinyi ni halali kwao. Na (mmehalalishiwa pia) wanawake waungwana wema katika Waumini na wanawake waungwana wema katika wale waliopewa Kitabu kabla yenu, mtakapowapa mahari yao bila kuwa maasherati wala kuchukua hawara. Na yeyote atakayekanusha imani basi kwa yakini imeporomoka amali yake naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ ۚ وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ ۚ مَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيَجْعَلَ عَلَيْكُم مِّنْ حَرَجٍ وَلَـٰكِن يُرِيدُ لِيُطَهِّرَكُمْ وَلِيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٦﴾

6. Enyi walioamini!  Mnaposimama kwa ajili ya Swalaah, osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye visugudi, na panguseni (kwa kupaka maji) vichwa vyenu na (osheni) miguu yenu hadi vifundoni. Na mkiwa na janaba basi jitwaharisheni. Na mkiwa wagonjwa au mko safarini au mmoja wenu ametoka msalani, au mmewagusa wanawake, kisha hamkupata maji, basi ikusudieni ardhi safi ya mchanga (mtayammam), panguseni kwayo nyuso zenu na mikono yenu. Allaah Hataki kukufanyieni magumu, lakini Anataka kukutwaharisheni na Akutimizieni Neema Yake juu yenu ili mpate kushukuru.[4]

 

 

وَاذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَمِيثَاقَهُ الَّذِي وَاثَقَكُم بِهِ إِذْ قُلْتُمْ سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ﴿٧﴾

7. Na kumbukeni Neema ya Allaah juu yenu na fungamano Lake ambalo Amekufungamanisheni nalo mliposema: Tumesikia na Tumetii. Na mcheni Allaah, hakika Allaah Ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا قَوَّامِينَ لِلَّـهِ شُهَدَاءَ بِالْقِسْطِ ۖ وَلَا يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ عَلَىٰ أَلَّا تَعْدِلُوا ۚ اعْدِلُوا هُوَ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿٨﴾

8. Enyi walioamini!  Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Allaah na wenye kutoa ushahidi kwa uadilifu. Na wala chuki mliyonayo kwa watu isikuchocheeni ikakupelekeeni kutokufanya uadilifu. Fanyeni uadilifu, huko ndiko kuliko karibu zaidi na taqwa. Na mcheni Allaah, hakika Allaah Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri kwa yale myatendayo. 

 

 

وَعَدَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ ۙ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ عَظِيمٌ ﴿٩﴾

9. Allaah Amewaahidi wale walioamini na wakatenda mema kwamba watapata maghfirah na ujira mkubwa mno.

 

 

وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ ﴿١٠﴾

10. Na waliokufuru na wakakadhibisha Aayaat (na Ishara, Dalili, Hoja) Zetu, hao ni watu wa moto uwakao vikali mno.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ هَمَّ قَوْمٌ أَن يَبْسُطُوا إِلَيْكُمْ أَيْدِيَهُمْ فَكَفَّ أَيْدِيَهُمْ عَنكُمْ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١١﴾

11. Enyi walioamini! Kumbukeni Neema ya Allaah juu yenu, pale walipopania watu kukunyosheeni mikono yao (kukushambulieni), kisha Allaah Akazuia mikono yao isikufikieni. Na mcheni Allaah, na kwa Allaah Pekee watawakali Waumini.

 

 

وَلَقَدْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَبَعَثْنَا مِنْهُمُ اثْنَيْ عَشَرَ نَقِيبًا ۖ وَقَالَ اللَّـهُ إِنِّي مَعَكُمْ ۖ لَئِنْ أَقَمْتُمُ الصَّلَاةَ وَآتَيْتُمُ الزَّكَاةَ وَآمَنتُم بِرُسُلِي وَعَزَّرْتُمُوهُمْ وَأَقْرَضْتُمُ اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا لَّأُكَفِّرَنَّ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَلَأُدْخِلَنَّكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۚ فَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ مِنكُمْ فَقَدْ ضَلَّ سَوَاءَ السَّبِيلِ﴿١٢﴾

12. Na kwa yakini Allaah Alichukua fungamano la nguvu la wana wa Israaiyl, na Tukawapelekea miongoni mwao wakuu kumi na mbili. Na Allaah Akasema: Hakika Mimi Niko pamoja nanyi. Mkisimamisha Swalaah, na mkatoa Zakaah, na mkawaamini Rusuli Wangu, na mkawaunga mkono na kuwasaidia, na mkamkopesha Allaah karadha mzuri, bila shaka Nitakufutieni maovu yenu, na Nitakuingizeni Jannaat zipitazo chini yake mito. Na yeyote atakayekufuru baada ya hapo miongoni mwenu, basi kwa yakini amepotea njia iliyo sawa.

 

 

فَبِمَا نَقْضِهِم مِّيثَاقَهُمْ لَعَنَّاهُمْ وَجَعَلْنَا قُلُوبَهُمْ قَاسِيَةً ۖ يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِ ۙ وَنَسُوا حَظًّا مِّمَّا ذُكِّرُوا بِهِ ۚ وَلَا تَزَالُ تَطَّلِعُ عَلَىٰ خَائِنَةٍ مِّنْهُمْ إِلَّا قَلِيلًا مِّنْهُمْ ۖ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاصْفَحْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٣﴾

13. Kwa sababu ya kuvunja kwao fungamano lao, Tuliwalaani na Tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu. Wanageuza maneno (ya Allaah) kutoka mahali pake, na wakasahau sehemu ya yale waliyokumbushwa. Na utaendelea kujionea khiyana kutoka kwao isipokuwa wachache tu miongoni mwao. Basi wasamehe na achilia mbali. Hakika Allaah Anapenda wafanyao ihsaan.

 

 

 

وَمِنَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّا نَصَارَىٰ أَخَذْنَا مِيثَاقَهُمْ فَنَسُوا حَظًّا مِّمَّا ذُكِّرُوا بِهِ فَأَغْرَيْنَا بَيْنَهُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ ۚ وَسَوْفَ يُنَبِّئُهُمُ اللَّـهُ بِمَا كَانُوا يَصْنَعُونَ ﴿١٤﴾

14. Na kwa wale waliosema: Hakika sisi ni Naswara, Tulichukua fungamano lao, nao wakasahau sehemu ya yale waliyokumbushwa. Basi Tukapandikiza baina yao uadui na bughudha mpaka Siku ya Qiyaamah. Na Allaah Atawajulisha waliyokuwa wakiyatenda.

 

 

يَا أَهْلَ الْكِتَابِ قَدْ جَاءَكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ كَثِيرًا مِّمَّا كُنتُمْ تُخْفُونَ مِنَ الْكِتَابِ وَيَعْفُو عَن كَثِيرٍ ۚ قَدْ جَاءَكُم مِّنَ اللَّـهِ نُورٌ وَكِتَابٌ مُّبِينٌ ﴿١٥﴾

15. Enyi Watu wa Kitabu! Hakika amekwishakujieni Rasuli Wetu anayekubainishieni mengi katika yale mliyokuwa mkiyaficha katika Kitabu, na ananyamazia mengi (yasiyo na lazima kuyafichua). Kwa yakini imekufikieni kutoka kwa Allaah Nuru na Kitabu kinachobainisha.

 

 

 

يَهْدِي بِهِ اللَّـهُ مَنِ اتَّبَعَ رِضْوَانَهُ سُبُلَ السَّلَامِ وَيُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِهِ وَيَهْدِيهِمْ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿١٦﴾

16. Allaah Anamwongoza kwacho yeyote atakayefuata Radhi Zake kumfikisha njia za salama, na Anawatoa (walio mfano wa huyo) katika viza kuingia katika nuru kwa Tawfiyq Yake, na Anawaongoza kuelekea njia iliyonyooka.

 

 

لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ ۚ قُلْ فَمَن يَمْلِكُ مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا إِنْ أَرَادَ أَن يُهْلِكَ الْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَأُمَّهُ وَمَن فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ۗ وَلِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۚ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٧﴾

17. Kwa yakini, wamekufuru wale waliosema: Allaah Ndiye Al-Masiyh mwana wa Maryam. Sema: Nani awezaye kuzuia lolote litokalo kwa Allaah Akitaka kumwangamiza Al-Masiyh mwana wa Maryam na mama yake na walioko ardhini wote? Na ufalme ni wa Allaah wa mbingu na ardhi na vyote vilivyo baina yake, Anaumba Atakacho. Na Allaah juu ya kila kitu Ni Muweza.[5]

 

 

وَقَالَتِ الْيَهُودُ وَالنَّصَارَىٰ نَحْنُ أَبْنَاءُ اللَّـهِ وَأَحِبَّاؤُهُ ۚ قُلْ فَلِمَ يُعَذِّبُكُم بِذُنُوبِكُم ۖ بَلْ أَنتُم بَشَرٌ مِّمَّنْ خَلَقَ ۚ يَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ ۚ وَلِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ وَإِلَيْهِ الْمَصِيرُ ﴿١٨﴾

18. Na Mayahudi na Manaswara wamesema: Sisi ni wana wa Allaah na vipenzi Vyake. Sema: Kwa nini basi Anakuadhibuni kwa dhambi zenu? Bali nyinyi ni watu kama wengine Aliowaumba. Anamghufuria Amtakaye na Anamuadhibu Amtakaye. Na ufalme ni wa Allaah wa mbingu na ardhi na vyote vilivyo baina yake, na Kwake Pekee ndio mahali pa kuishia. 

 

 

يَا أَهْلَ الْكِتَابِ قَدْ جَاءَكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ عَلَىٰ فَتْرَةٍ مِّنَ الرُّسُلِ أَن تَقُولُوا مَا جَاءَنَا مِن بَشِيرٍ وَلَا نَذِيرٍ ۖ فَقَدْ جَاءَكُم بَشِيرٌ وَنَذِيرٌ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٩﴾

19. Enyi Watu wa Kitabu! Kwa yakini amekwishakujieni Rasuli Wetu anayekubainishieni (mambo) katika wakati wa kusita ujio wa Rusuli wa kulingania. Msije kusema: Hakutujia mbashiriaji yeyote wala mwonyaji. Kwa yakini amekujieni mbashiriaji na mwonyaji. Na Allaah juu ya kila kitu Ni Muweza. 

 

 

وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ اذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ جَعَلَ فِيكُمْ أَنبِيَاءَ وَجَعَلَكُم مُّلُوكًا وَآتَاكُم مَّا لَمْ يُؤْتِ أَحَدًا مِّنَ الْعَالَمِينَ ﴿٢٠﴾

20. Na pindi Muwsaa alipowaambia kaumu yake:  Enyi kaumu yangu!  Kumbukeni Neema ya Allaah juu yenu Alipojaalia miongoni mwenu Manabii, na Akakufanyeni wenye kujitawala wenyewe (baada ya kumgharikisha Firawni) na Akakupeni yale Asiyowahi kumpa yeyote miongoni mwa walimwengu. 

 

 

 

يَا قَوْمِ ادْخُلُوا الْأَرْضَ الْمُقَدَّسَةَ الَّتِي كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ وَلَا تَرْتَدُّوا عَلَىٰ أَدْبَارِكُمْ فَتَنقَلِبُوا خَاسِرِينَ ﴿٢١﴾

21. Enyi kaumu yangu! Ingieni ardhi iliyotakaswa ambayo Amekuandikieni Allaah, na wala msirudi kugeuka nyuma mkakimbia (kupigana), hapo mtageuka kuwa wenye kukhasirika. 

 

 

قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِنَّ فِيهَا قَوْمًا جَبَّارِينَ وَإِنَّا لَن نَّدْخُلَهَا حَتَّىٰ يَخْرُجُوا مِنْهَا فَإِن يَخْرُجُوا مِنْهَا فَإِنَّا دَاخِلُونَ ﴿٢٢﴾

22. Wakasema: Ee Muwsaa! Hakika humo kuna watu majabari, nasi hatutoingia humo mpaka watoke humo. Watakapotoka humo, basi hakika sisi tutaingia.

 

 

قَالَ رَجُلَانِ مِنَ الَّذِينَ يَخَافُونَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِمَا ادْخُلُوا عَلَيْهِمُ الْبَابَ فَإِذَا دَخَلْتُمُوهُ فَإِنَّكُمْ غَالِبُونَ ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَتَوَكَّلُوا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٢٣﴾

23. Watu wawili[6] katika wenye kumcha Allaah ambao Allaah Amewaneemesha wakasema: Waingilieni katika mlango. Mkiwaingilia, basi hakika nyinyi mtashinda. Na kwa Allaah tawakalini ikiwa nyinyi ni Waumini.

 

 

قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِنَّا لَن نَّدْخُلَهَا أَبَدًا مَّا دَامُوا فِيهَا ۖ فَاذْهَبْ أَنتَ وَرَبُّكَ فَقَاتِلَا إِنَّا هَاهُنَا قَاعِدُونَ ﴿٢٤﴾

24. Wakasema: Ee Muwsaa!  Hakika sisi hatutoingia humo abadani madamu watabakia humo. Basi nenda wewe na Rabb wako mkapigane, hakika sisi tunakaa hapa hapa.

 

 

قَالَ رَبِّ إِنِّي لَا أَمْلِكُ إِلَّا نَفْسِي وَأَخِي ۖ فَافْرُقْ بَيْنَنَا وَبَيْنَ الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ ﴿٢٥﴾

25. (Muwsaa) akasema: Rabb wangu! Hakika mimi similiki ila nafsi yangu na ndugu yangu. Basi Tutenganishe sisi na watu mafasiki (kwa Hukmu Yako).  

 

 

قَالَ فَإِنَّهَا مُحَرَّمَةٌ عَلَيْهِمْ ۛ أَرْبَعِينَ سَنَةً ۛ يَتِيهُونَ فِي الْأَرْضِ ۚ فَلَا تَأْسَ عَلَى الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ ﴿٢٦﴾

26. (Allaah) Akasema: Kwa hiyo basi (ardhi tukufu) hiyo imeharamishwa kwao miaka arubaini. Watatangatanga ardhini. Basi usisikitike juu ya watu mafasiki.

 

 

وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ ابْنَيْ آدَمَ بِالْحَقِّ إِذْ قَرَّبَا قُرْبَانًا فَتُقُبِّلَ مِنْ أَحَدِهِمَا وَلَمْ يُتَقَبَّلْ مِنَ الْآخَرِ قَالَ لَأَقْتُلَنَّكَ ۖ قَالَ إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ اللَّـهُ مِنَ الْمُتَّقِينَ ﴿٢٧﴾

27. Na wasomee khabari ya wana wawili wa Aadam kwa haki walipotoa dhabihu ya kafara, ikakubaliwa ya mmoja wao lakini ya mwengine haikukubaliwa. (Asiyekubaliwa) akasema: Nitakuua tu!  (Aliyekubaliwa) akasema: Hakika Allaah Anatakabalia wenye taqwa.

 

 

لَئِن بَسَطتَ إِلَيَّ يَدَكَ لِتَقْتُلَنِي مَا أَنَا بِبَاسِطٍ يَدِيَ إِلَيْكَ لِأَقْتُلَكَ ۖ إِنِّي أَخَافُ اللَّـهَ رَبَّ الْعَالَمِينَ ﴿٢٨﴾

28. Ukininyoshea mkono wako ili uniue, mimi sitokunyoshea mkono wangu kukuua. Hakika mimi namkhofu Allaah Rabb wa walimwengu.

 

 

إِنِّي أُرِيدُ أَن تَبُوءَ بِإِثْمِي وَإِثْمِكَ فَتَكُونَ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ ۚ وَذَٰلِكَ جَزَاءُ الظَّالِمِينَ ﴿٢٩﴾

29. Hakika mimi nataka urudi na ubebe dhambi zangu na dhambi zako, hapo utakuwa miongoni mwa watu wa motoni. Na hiyo ndiyo jazaa ya madhalimu.

 

 

فَطَوَّعَتْ لَهُ نَفْسُهُ قَتْلَ أَخِيهِ فَقَتَلَهُ فَأَصْبَحَ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٣٠﴾

 30. Basi nafsi yake ikamwezesha kwa wepesi kumuua ndugu yake, akamuua na akawa miongoni mwa waliokhasirika.

 

 

فَبَعَثَ اللَّـهُ غُرَابًا يَبْحَثُ فِي الْأَرْضِ لِيُرِيَهُ كَيْفَ يُوَارِي سَوْءَةَ أَخِيهِ ۚ قَالَ يَا وَيْلَتَىٰ أَعَجَزْتُ أَنْ أَكُونَ مِثْلَ هَـٰذَا الْغُرَابِ فَأُوَارِيَ سَوْءَةَ أَخِي ۖ فَأَصْبَحَ مِنَ النَّادِمِينَ ﴿٣١﴾

31. Kisha Allaah Akamleta kunguru akifukua katika ardhi ili amwonyeshe vipi asitiri maiti ya ndugu yake. (Muuaji) akasema: Ole wangu! Hivi nimeshindwa kuwa mimi kama huyu kunguru nikamsitiri ndugu yangu? Akawa miongoni mwa wajutao.

 

 

مِنْ أَجْلِ ذَٰلِكَ كَتَبْنَا عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنَّهُ مَن قَتَلَ نَفْسًا بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الْأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ النَّاسَ جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ جَمِيعًا ۚ وَلَقَدْ جَاءَتْهُمْ رُسُلُنَا بِالْبَيِّنَاتِ ثُمَّ إِنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم بَعْدَ ذَٰلِكَ فِي الْأَرْضِ لَمُسْرِفُونَ ﴿٣٢﴾

32. Kwa ajili ya hilo, Tukawaandikia sharia wana wa Israaiyl kwamba: Atakayeiua nafsi bila ya nafsi (kuua), au kufanya ufisadi katika ardhi, basi ni kama ameua watu wote. Na atakayeiokoa na mauti, basi ni kama amewaokoa watu wote. Na bila shaka walifikiwa na Rusuli Wetu kwa hoja bayana, kisha wengi miongoni mwao baada ya hayo wamekuwa wapindukao mipaka ya kuasi.

 

 

إِنَّمَا جَزَاءُ الَّذِينَ يُحَارِبُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَيَسْعَوْنَ فِي الْأَرْضِ فَسَادًا أَن يُقَتَّلُوا أَوْ يُصَلَّبُوا أَوْ تُقَطَّعَ أَيْدِيهِمْ وَأَرْجُلُهُم مِّنْ خِلَافٍ أَوْ يُنفَوْا مِنَ الْأَرْضِ ۚ ذَٰلِكَ لَهُمْ خِزْيٌ فِي الدُّنْيَا ۖ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿٣٣﴾

33. Hakika jazaa ya wale wanaompiga vita Allaah na Rasuli Wake na wakapania kufanya ufisadi katika ardhi, wauawe au wasulubiwe au ikatwe mikono yao na miguu yao kwa kutofautisha[7] au watolewe katika nchi. Hiyo ndiyo hizaya yao duniani. Na Aakhirah watapata adhabu kubwa mno.

 

 

إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا مِن قَبْلِ أَن تَقْدِرُوا عَلَيْهِمْ ۖ فَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣٤﴾

34. Isipokuwa wale waliotubia kabla ya kuwashinda nguvu. Basi jueni kwamba hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ وَجَاهِدُوا فِي سَبِيلِهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٣٥﴾

35. Enyi walioamini! Mcheni Allaah na tafuteni njia ya kumkurubia, na fanyeni Jihaad katika Njia Yake ili mpate kufaulu.

 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْ أَنَّ لَهُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا وَمِثْلَهُ مَعَهُ لِيَفْتَدُوا بِهِ مِنْ عَذَابِ يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَا تُقُبِّلَ مِنْهُمْ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٣٦﴾

36. Hakika wale waliokufuru, kama watakuwa na yale yote yaliyomo ardhini na mengineyo mfano kama hayo, ili watoe fidia kwayo kuepukana na adhabu ya Siku ya Qiyaamah, hayatokubaliwa kutoka kwao, na watapata adhabu iumizayo.

 

 

يُرِيدُونَ أَن يَخْرُجُوا مِنَ النَّارِ وَمَا هُم بِخَارِجِينَ مِنْهَا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ مُّقِيمٌ ﴿٣٧﴾

37. Watataka kutoka katika moto, lakini wao hawatatoka kamwe humo, na watapata adhabu ya kudumu.

 

 

وَالسَّارِقُ وَالسَّارِقَةُ فَاقْطَعُوا أَيْدِيَهُمَا جَزَاءً بِمَا كَسَبَا نَكَالًا مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٣٨﴾

38. Mwizi mwanamume na mwizi mwanamke ikateni (kitanga cha) mikono yao, ni malipo kwa yale waliyoyachuma, na adhabu ya tahadharisho na fundisho kwa watu kutoka kwa Allaah. Na Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.[8]

 

 

فَمَن تَابَ مِن بَعْدِ ظُلْمِهِ وَأَصْلَحَ فَإِنَّ اللَّـهَ يَتُوبُ عَلَيْهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣٩﴾

 39. Lakini atakayetubia baada ya dhulma yake na akarekebisha matendo yake na kuwa mwema, basi hakika Allaah Atapokea tawbah yake. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ يُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ وَيَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٤٠﴾

40. Je, hujui ya kwamba Allaah Anao ufalme wa mbingu na ardhi? Humwadhibu Amtakae na Humghufiria Amtakae. Na Allaah juu ya kila kitu Ni Muweza.

 

 

 

يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ لَا يَحْزُنكَ الَّذِينَ يُسَارِعُونَ فِي الْكُفْرِ مِنَ الَّذِينَ قَالُوا آمَنَّا بِأَفْوَاهِهِمْ وَلَمْ تُؤْمِن قُلُوبُهُمْ ۛ وَمِنَ الَّذِينَ هَادُوا ۛ سَمَّاعُونَ لِلْكَذِبِ سَمَّاعُونَ لِقَوْمٍ آخَرِينَ لَمْ يَأْتُوكَ ۖ يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ مِن بَعْدِ مَوَاضِعِهِ ۖ يَقُولُونَ إِنْ أُوتِيتُمْ هَـٰذَا فَخُذُوهُ وَإِن لَّمْ تُؤْتَوْهُ فَاحْذَرُوا ۚ وَمَن يُرِدِ اللَّـهُ فِتْنَتَهُ فَلَن تَمْلِكَ لَهُ مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۚ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَمْ يُرِدِ اللَّـهُ أَن يُطَهِّرَ قُلُوبَهُمْ ۚ لَهُمْ فِي الدُّنْيَا خِزْيٌ ۖ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿٤١﴾

41. Ee Rasuli! Wasikuhuzunishe wale wanaokimbilia kukufuru, miongoni mwa wasemao kwa midomo yao: Tumeamini na hali nyoyo zao hazikuamini. Na miongoni mwa Mayahudi wako wanaosikiliza kwa makini kwa ajili ya uongo, wanaosikiliza kwa makini kwa ajili ya watu wengine wasiokufikia. Wanageuza maneno kutoka mahali pake wanasema: Mkipewa haya yachukueni, na msipopewa hayo basi jihadharini! Na yule ambaye Allaah Anataka kumtia mtihanini, hutokuwa na uwezo wowote (kusaidia) kwa ajili yake mbele ya Allaah. Hao ndio ambao Allaah Hakutaka kuzitakasa nyoyo zao. Watapata hizaya duniani na Aakhirah watapata adhabu kubwa mno.

 

 

 

سَمَّاعُونَ لِلْكَذِبِ أَكَّالُونَ لِلسُّحْتِ ۚ فَإِن جَاءُوكَ فَاحْكُم بَيْنَهُمْ أَوْ أَعْرِضْ عَنْهُمْ ۖ وَإِن تُعْرِضْ عَنْهُمْ فَلَن يَضُرُّوكَ شَيْئًا ۖ وَإِنْ حَكَمْتَ فَاحْكُم بَيْنَهُم بِالْقِسْطِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ﴿٤٢﴾

42. (Hao ni) wenye kusikiliza kwa makini uongo, walaji haramu kwa pupa. Basi wakikujia wahukumu baina yao au wapuuze. Na ukiwapuuza, hawatoweza kukudhuru chochote. Na kama ukihukumu, basi hukumu baina yao kwa uadilifu. Hakika Allaah Anapenda waadilifu.

 

 

وَكَيْفَ يُحَكِّمُونَكَ وَعِندَهُمُ التَّوْرَاةُ فِيهَا حُكْمُ اللَّـهِ ثُمَّ يَتَوَلَّوْنَ مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ ۚ وَمَا أُولَـٰئِكَ بِالْمُؤْمِنِينَ ﴿٤٣﴾

43. Na vipi watakufanya wewe kuwa hakimu wao na hali wana Tawraat yenye Hukumu ya Allaah ndani yake, kisha baada ya hayo wanakengeuka? Na hao si wenye kuamini.

 

 

إِنَّا أَنزَلْنَا التَّوْرَاةَ فِيهَا هُدًى وَنُورٌ ۚ يَحْكُمُ بِهَا النَّبِيُّونَ الَّذِينَ أَسْلَمُوا لِلَّذِينَ هَادُوا وَالرَّبَّانِيُّونَ وَالْأَحْبَارُ بِمَا اسْتُحْفِظُوا مِن كِتَابِ اللَّـهِ وَكَانُوا عَلَيْهِ شُهَدَاءَ ۚ فَلَا تَخْشَوُا النَّاسَ وَاخْشَوْنِ وَلَا تَشْتَرُوا بِآيَاتِي ثَمَنًا قَلِيلًا ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ ﴿٤٤﴾

44. Hakika Sisi Tumeteremsha Tawraat yenye mwongozo na nuru ambayo Manabii waliojisalimisha kikamilifu (kwa Allaah), pamoja na Ar-Rabbaaniyyuwn[9] (Marabi) na Al-Ahbaar[10] (Mafuqahaa weledi) wanawahukumia kwayo Mayahudi. Kwa sababu wao wamebebeshwa jukumu la kutakwa kukilinda na kukihifadhi Kitabu cha Allaah, na wakawa mashahidi juu yake. Basi msiwaogope watu, bali Niogopeni Mimi, na wala msibadilishe Aayaat (Hukmu, Sharia) Zangu kwa thamani ndogo. Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri.

 

 

وَكَتَبْنَا عَلَيْهِمْ فِيهَا أَنَّ النَّفْسَ بِالنَّفْسِ وَالْعَيْنَ بِالْعَيْنِ وَالْأَنفَ بِالْأَنفِ وَالْأُذُنَ بِالْأُذُنِ وَالسِّنَّ بِالسِّنِّ وَالْجُرُوحَ قِصَاصٌ ۚ فَمَن تَصَدَّقَ بِهِ فَهُوَ كَفَّارَةٌ لَّهُ ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٤٥﴾

45. Na Tumewaandikia sharia humo kwamba nafsi kwa nafsi, na jicho kwa jicho, na pua kwa pua, na sikio kwa sikio, jino kwa jino, na majaraha ni kisasi. Lakini atakayesamehe kwa kutolea sadaka, basi itakuwa ni kafara kwake. Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio madhalimu.

 

 

وَقَفَّيْنَا عَلَىٰ آثَارِهِم بِعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ التَّوْرَاةِ ۖ وَآتَيْنَاهُ الْإِنجِيلَ فِيهِ هُدًى وَنُورٌ وَمُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ التَّوْرَاةِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٤٦﴾

46. Na Tukamfuatishia katika njia yao (Manabii hao), ‘Iysaa mwana wa Maryam akisadikisha yale yaliyoko kabla yake katika Tawraat. Na Tukampa Injiyl yenye mwongozo na nuru ndani yake, inasadikisha yale yaliyokuwa kabla yake katika Tawraat, na Tumeifanya mwongozo na mawaidha kwa wenye taqwa.

 

 

وَلْيَحْكُمْ أَهْلُ الْإِنجِيلِ بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فِيهِ ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿٤٧﴾

47. Na watu wa Injiyl wahukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah ndani yake. Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio mafasiki.

 

 

وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ الْكِتَابِ وَمُهَيْمِنًا عَلَيْهِ ۖ فَاحْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ عَمَّا جَاءَكَ مِنَ الْحَقِّ ۚ لِكُلٍّ جَعَلْنَا مِنكُمْ شِرْعَةً وَمِنْهَاجًا ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَجَعَلَكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَلَـٰكِن لِّيَبْلُوَكُمْ فِي مَا آتَاكُمْ ۖ فَاسْتَبِقُوا الْخَيْرَاتِ ۚ إِلَى اللَّـهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ ﴿٤٨﴾

48. Na Tumekuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Kitabu kwa haki kinachosadikisha Vitabu vilivyokuwa kabla yake. Kinayadhibiti, kinayalinda na kuyashuhudia yaliyomo humo.[11] Basi hukumu baina yao kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, na wala usifuate hawaa zao ukaacha haki iliyokujia. Kila ummah katika nyinyi Tumeupangia sharia na manhaj. Na kama Allaah Angetaka, basi Angelikufanyeni ummah mmoja, lakini (Hakufanya) ili Akujaribuni katika yale Aliyokupeni. Basi shindaneni mambo ya kheri. Kwa Allaah Pekee ndio marejeo yenu nyote, kisha Atakujulisheni yale mliyokuwa mkikhitilafiana.

 

 

 

وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَن بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ إِلَيْكَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا فَاعْلَمْ أَنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُصِيبَهُم بِبَعْضِ ذُنُوبِهِمْ ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ لَفَاسِقُونَ ﴿٤٩﴾

49. Na wahukumu baina yao kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, na wala usifuate hawaa zao, na tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya yale Aliyokuteremshia Allaah. Na wakikengeuka, basi jua kuwa hakika Allaah Anataka kuwaadhibu kwa baadhi ya madhambi yao. Na hakika wengi katika watu ni mafasiki.

 

 

أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ ۚ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ ﴿٥٠﴾

50. Je, wanataka hukumu za kijahiliya? Na nani mbora zaidi kuliko Allaah katika kuhukumu kwa watu wenye yakini?

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٥١﴾

51. Enyi walioamini! Msifanye Mayahudi na Manaswara marafiki wandani na walinzi. Wao kwa wao ni marafiki wandani. Na yeyote atakayewafanya marafiki wao wandani, basi hakika yeye ni miongoni mwao. Hakika Allaah Haongoi watu madhalimu.

 

 

فَتَرَى الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ يُسَارِعُونَ فِيهِمْ يَقُولُونَ نَخْشَىٰ أَن تُصِيبَنَا دَائِرَةٌ ۚ فَعَسَى اللَّـهُ أَن يَأْتِيَ بِالْفَتْحِ أَوْ أَمْرٍ مِّنْ عِندِهِ فَيُصْبِحُوا عَلَىٰ مَا أَسَرُّوا فِي أَنفُسِهِمْ نَادِمِينَ ﴿٥٢﴾

52. Utawaona wale ambao katika nyoyo zao mna maradhi[12] (ya unafiki) wanakimbilia kwao wakisema: Tunakhofu usitusibu mgeuko. Basi asaa Allaah Akaleta ushindi au jambo (jengine) litokalo Kwake, wakawa wenye kujuta kwa waliyoyaficha katika nafsi zao.

 

 

وَيَقُولُ الَّذِينَ آمَنُوا أَهَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ أَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ ۙ إِنَّهُمْ لَمَعَكُمْ ۚ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فَأَصْبَحُوا خَاسِرِينَ ﴿٥٣﴾

 53. Na hapo walioamini watasema (wanafiki wakifichuka): Je, hawa ndio wale ambao waliapa kwa Allaah kwa viapo vyao thabiti vya nguvu, kwamba wao wapo pamoja nanyi? Zimeporomoka amali zao, na wamekuwa wenye kukhasirika.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَن يَرْتَدَّ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ يُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لَائِمٍ ۚ ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٥٤﴾

54. Enyi walioamini! Yeyote atakayeritadi miongoni mwenu akaacha Dini yake, basi Allaah Ataleta watu (badala yao) Atakaowapenda nao watampenda, wanyenyekevu kwa Waumini, washupavu juu ya makafiri, wanafanya Jihaad katika Njia ya Allaah na wala hawakhofu lawama za mwenye kulaumu. Hiyo ni Fadhila ya Allaah, Humpa Amtakaye. Na Allaah Ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote.

 

 

إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ رَاكِعُونَ ﴿٥٥﴾

55. Hakika Rafiki wenu Mlinzi ni Allaah na Rasuli Wake na wale walioamini, ambao wanasimamisha Swalaah na wanatoa Zakaah hali ya kuwa wananyenyekea.

 

 

وَمَن يَتَوَلَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا فَإِنَّ حِزْبَ اللَّـهِ هُمُ الْغَالِبُونَ ﴿٥٦﴾

56. Na atakayemfanya Allaah kuwa ni Rafiki Mlinzi na Rasuli Wake na wale walioamini, basi hakika kundi la Allaah ndio washindi.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الَّذِينَ اتَّخَذُوا دِينَكُمْ هُزُوًا وَلَعِبًا مِّنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَالْكُفَّارَ أَوْلِيَاءَ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٥٧﴾

57. Enyi walioamini!  Msiwafanye wale walioifanyia Dini yenu mzaha na mchezo miongoni mwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu na makafiri kuwa marafiki wandani na walinzi. Na mcheni Allaah, kama nyinyi ni Waumini kweli.

 

 

وَإِذَا نَادَيْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ اتَّخَذُوهَا هُزُوًا وَلَعِبًا ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْقِلُونَ ﴿٥٨﴾

58. Na mnapoinadia Swalaah, wao huifanyia mzaha na mchezo. Hivyo ni kwa kuwa wao ni watu hawana akili.

 

 

 

قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ هَلْ تَنقِمُونَ مِنَّا إِلَّا أَنْ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلُ وَأَنَّ أَكْثَرَكُمْ فَاسِقُونَ ﴿٥٩﴾

59. Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Je, mnatuchukia tu kwa vile tumemwamini Allaah na yale yaliyoteremshwa kwetu na yale yaliyoteremshwa kabla, na kwamba wengi wenu ni mafasiki?

 

 

قُلْ هَلْ أُنَبِّئُكُم بِشَرٍّ مِّن ذَٰلِكَ مَثُوبَةً عِندَ اللَّـهِ ۚ مَن لَّعَنَهُ اللَّـهُ وَغَضِبَ عَلَيْهِ وَجَعَلَ مِنْهُمُ الْقِرَدَةَ وَالْخَنَازِيرَ وَعَبَدَ الطَّاغُوتَ ۚ أُولَـٰئِكَ شَرٌّ مَّكَانًا وَأَضَلُّ عَن سَوَاءِ السَّبِيلِ ﴿٦٠﴾

60. Sema: Je, nikujulisheni la shari zaidi kuliko hayo kwa malipo (mabaya) mbele ya Allaah? Yule ambaye Allaah Amemlaani na Akamghadhibikia na Akawafanya miongoni mwao manyani na nguruwe na wakaabudu twaghuti, hao wana mahali pabaya mno (Aakhirah) na wapotofu zaidi na njia iliyo sawa (duniani).

 

 

وَإِذَا جَاءُوكُمْ قَالُوا آمَنَّا وَقَد دَّخَلُوا بِالْكُفْرِ وَهُمْ قَدْ خَرَجُوا بِهِ ۚ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا كَانُوا يَكْتُمُونَ ﴿٦١﴾

61. Na wanapokujieni husema: Tumeamini. Na hali wameingia na ukafiri wao na wakatoka nao. Na Allaah Anajua zaidi yale waliyokuwa wakiyaficha.

 

 

وَتَرَىٰ كَثِيرًا مِّنْهُمْ يُسَارِعُونَ فِي الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَأَكْلِهِمُ السُّحْتَ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٦٢﴾

62. Na utawaona wengi miongoni mwao wanakimbilia katika dhambi na uadui na kula kwao haramu. Bila shaka ni mabaya mno waliyokuwa wanatenda.

 

 

لَوْلَا يَنْهَاهُمُ الرَّبَّانِيُّونَ وَالْأَحْبَارُ عَن قَوْلِهِمُ الْإِثْمَ وَأَكْلِهِمُ السُّحْتَ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَصْنَعُونَ ﴿٦٣﴾

63. Basi mbona Ar-Rabbaaniyyuwn (Marabi) na Al-Ahbaar[13] hawawakatazi maneno yao ya dhambi na ulaji wao wa haramu?          Bila shaka ni mabaya mno waliyokuwa wanayafanya.

 

 

وَقَالَتِ الْيَهُودُ يَدُ اللَّـهِ مَغْلُولَةٌ ۚ غُلَّتْ أَيْدِيهِمْ وَلُعِنُوا بِمَا قَالُوا ۘ بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ ۚ وَلَيَزِيدَنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم مَّا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ طُغْيَانًا وَكُفْرًا ۚ وَأَلْقَيْنَا بَيْنَهُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ ۚ كُلَّمَا أَوْقَدُوا نَارًا لِّلْحَرْبِ أَطْفَأَهَا اللَّـهُ ۚ وَيَسْعَوْنَ فِي الْأَرْضِ فَسَادًا ۚ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ ﴿٦٤﴾

64. Na Mayahudi wakasema: Mkono wa Allaah umefumbwa. Mikono yao ndio iliyofumbwa na wamelaaniwa kwa yale waliyoyasema! Bali Mikono Yake (Allaah)[14] imefumbuliwa Hutoa Atakavyo. Kwa yakini yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako, yatawazidisha wengi miongoni mwao upindukaji mipaka ya kuasi na kufuru. Na Tumewatilia baina yao uadui na bughudha mpaka Siku ya Qiyaamah. Kila wanapouwasha moto wa vita (dhidi yako), Allaah Huuzima. Na wanapania kwa bidii kufanya ufisadi katika ardhi. Na Allaah Hapendi mafisadi.

 

 

وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْكِتَابِ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَكَفَّرْنَا عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَلَأَدْخَلْنَاهُمْ جَنَّاتِ النَّعِيمِ ﴿٦٥﴾

65. Na lau kama Watu wa Kitabu wangeamini na wakawa na taqwa, bila shaka Tungeliwafutia maovu yao, na bila shaka Tungeliwaingiza katika Jannaat (Pepo) za neema.

 

 

وَلَوْ أَنَّهُمْ أَقَامُوا التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِم مِّن رَّبِّهِمْ لَأَكَلُوا مِن فَوْقِهِمْ وَمِن تَحْتِ أَرْجُلِهِم ۚ مِّنْهُمْ أُمَّةٌ مُّقْتَصِدَةٌ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ سَاءَ مَا يَعْمَلُونَ ﴿٦٦﴾

66. Na lau kama wangeliishika vyema Tawraat na Injiyl na yale yaliyoteremshwa kwao kutoka kwa Rabb wao, bila shaka wangelikula (rizki) kutoka juu yao na kutoka chini ya miguu yao. Miongoni mwao liko kundi la watu walioko katika njia ya sawa na wengi wao wanayoyafanya ni mabaya mno.

 

 

 

يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ ۚ وَاللَّـهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ﴿٦٧﴾

67. Ee Rasuli! Balighisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako. Na usipofanya, basi utakuwa hukubalighisha Risala Yake. Na Allaah Atakuhifadhi na watu. Hakika Allaah Haongoi watu makafiri.[15]

 

 

قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَسْتُمْ عَلَىٰ شَيْءٍ حَتَّىٰ تُقِيمُوا التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ ۗ وَلَيَزِيدَنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم مَّا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ طُغْيَانًا وَكُفْرًا ۖ فَلَا تَأْسَ عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿٦٨﴾

68. Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Hamtaambulia chochote mpaka muishike ipasavyo Tawraat na Injiyl na yale yaliyoteremshwa kwenu kutoka kwa Rabb wenu. Kwa yakini yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako, yatawazidisha wengi miongoni mwao upindukaji mipaka ya kuasi na kufuru. Basi usisikitike juu ya watu makafiri.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَادُوا وَالصَّابِئُونَ وَالنَّصَارَىٰ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَعَمِلَ صَالِحًا فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٦٩﴾

69. Hakika wale walioamini na Mayahudi na Wasabai[16] na Manaswara; atakayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho na akatenda mema, basi hawatokuwa na khofu na wala hawatohuzunika.

 

   

 

لَقَدْ أَخَذْنَا مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَأَرْسَلْنَا إِلَيْهِمْ رُسُلًا ۖ كُلَّمَا جَاءَهُمْ رَسُولٌ بِمَا لَا تَهْوَىٰ أَنفُسُهُمْ فَرِيقًا كَذَّبُوا وَفَرِيقًا يَقْتُلُونَ ﴿٧٠﴾

70. Kwa yakini Tulichukua agano la wana wa Israaiyl na Tukawapelekea Rusuli. Basi kila alipowajia Rasuli kwa yale yasiyopenda nafsi zao, kundi waliwakadhibisha na kundi wakawaua.

 

 

 

وَحَسِبُوا أَلَّا تَكُونَ فِتْنَةٌ فَعَمُوا وَصَمُّوا ثُمَّ تَابَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ ثُمَّ عَمُوا وَصَمُّوا كَثِيرٌ مِّنْهُمْ ۚ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ ﴿٧١﴾

71. Na walidhani kwamba yatapita hayo bila adhabu, basi wakawa vipofu na wakawa viziwi, kisha Allaah Akapokea tawbah yao. Tena wengi wao wakawa vipofu na wakawa viziwi. Na Allaah Ni Mwenye Kuona yale wayatendayo.

 

 

لَقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ ۖ وَقَالَ الْمَسِيحُ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۖ إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ﴿٧٢﴾

72. Kwa yakini wamekufuru wale waliosema: Allaah ni Al-Masiyh mwana wa Maryam. Na ilhali Al-Masiyh alisema (kukadhibisha madai yao): Enyi wana wa Israaiyl! Mwabuduni Allaah, Rabb wangu na Rabb wenu. Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni motoni.[17] Na madhalimu hawatopata yeyote mwenye kunusuru.

 

 

لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ ۘ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۚ وَإِن لَّمْ يَنتَهُوا عَمَّا يَقُولُونَ لَيَمَسَّنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٣﴾

73. Kwa yakini wamekufuru wale waliosema Allaah ni wa tatu wa watatu. Ilhali hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Ilaah Mmoja Pekee. Na wasipoacha yale wanayoyasema, bila ya shaka itawagusa adhabu iumizayo wale waliokufuru miongoni mwao.

 

 

أَفَلَا يَتُوبُونَ إِلَى اللَّـهِ وَيَسْتَغْفِرُونَهُ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٧٤﴾

74. Je, hawatubii kwa Allaah na wakamwomba maghfirah? Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

مَّا الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ وَأُمُّهُ صِدِّيقَةٌ ۖ كَانَا يَأْكُلَانِ الطَّعَامَ ۗ انظُرْ كَيْفَ نُبَيِّنُ لَهُمُ الْآيَاتِ ثُمَّ انظُرْ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ ﴿٧٥﴾

75. Al-Masiyh mwana wa Maryam si chochote ila ni Rasuli tu, wamekwishapita kabla yake Rusuli (wengine). Na mama yake ni Muumini mkweli wa dhati. Wote wawili walikuwa wanakula chakula. Tazama jinsi Tunavyowabainishia Aayaat (Ishara, Hoja, Dalili) kisha tazama vipi wanavyoghilibiwa.

 

 

قُلْ أَتَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا نَفْعًا ۚ وَاللَّـهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٧٦﴾

76. Sema: Vipi mnaabudu visivyokuwa na uwezo wa kukudhuruni wala kukunufaisheni badala ya Allaah! Na Allaah Ndiye Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَا تَغْلُوا فِي دِينِكُمْ غَيْرَ الْحَقِّ وَلَا تَتَّبِعُوا أَهْوَاءَ قَوْمٍ قَدْ ضَلُّوا مِن قَبْلُ وَأَضَلُّوا كَثِيرًا وَضَلُّوا عَن سَوَاءِ السَّبِيلِ ﴿٧٧﴾

77. Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Msipindukie mipaka katika dini yenu bila ya haki, na wala msifuate hawaa za watu waliokwishapotea kabla na wakapotosha wengi na wakapotea njia iliyo sawa.

 

 

لُعِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَىٰ لِسَانِ دَاوُودَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴿٧٨﴾

78. Wamelaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa wana wa Israaiyl kwa lisani ya Daawuwd na ‘Iysaa mwana wa Maryam. Hivyo ni kwa sababu ya kuasi kwao na walikuwa wakitaadi.

 

 

كَانُوا لَا يَتَنَاهَوْنَ عَن مُّنكَرٍ فَعَلُوهُ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ ﴿٧٩﴾

79. Walikuwa hawakatazani munkari yoyote waliyofanya. Uovu ulioje waliyokuwa wakiyafanya!  

 

 

تَرَىٰ كَثِيرًا مِّنْهُمْ يَتَوَلَّوْنَ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ لَبِئْسَ مَا قَدَّمَتْ لَهُمْ أَنفُسُهُمْ أَن سَخِطَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ وَفِي الْعَذَابِ هُمْ خَالِدُونَ ﴿٨٠﴾

80. Utawaona wengi miongoni mwao wanawafanya marafiki wandani na walinzi wale waliokufuru. Ubaya ulioje yale yaliyowatangulizia nafsi zao, hata Allaah Amewaghadhibikia na katika adhabu wao watadumu.

 

 

وَلَوْ كَانُوا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالنَّبِيِّ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مَا اتَّخَذُوهُمْ أَوْلِيَاءَ وَلَـٰكِنَّ كَثِيرًا مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ ﴿٨١﴾

81. Na lau wangelikuwa wanamwamini Allaah na Nabiy (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kwake, wasingeliwafanya hao marafiki wandani na walinzi, lakini wengi miongoni mwao ni mafasiki.

 

 

لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَدَاوَةً لِّلَّذِينَ آمَنُوا الْيَهُودَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُوا ۖ وَلَتَجِدَنَّ أَقْرَبَهُم مَّوَدَّةً لِّلَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ قَالُوا إِنَّا نَصَارَىٰ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّ مِنْهُمْ قِسِّيسِينَ وَرُهْبَانًا وَأَنَّهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ ﴿٨٢﴾

82. Bila shaka utawakuta walio na uadui mkali zaidi kuliko watu wote, kwa walioamini, ni Mayahudi na wale walioshirikisha. Na bila shaka utawakuta walio karibu zaidi kimapenzi kwa Waumini ni wale wanaosema: Sisi ni Manaswara. Hivyo ni kwa kuwa miongoni mwao kuna Qissiysiyna[18] (Makasisi) na Ruhbaan[19] (Wamonaki) na kwamba wao hawatakabari.

 

 

 

 

وَإِذَا سَمِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَى الرَّسُولِ تَرَىٰ أَعْيُنَهُمْ تَفِيضُ مِنَ الدَّمْعِ مِمَّا عَرَفُوا مِنَ الْحَقِّ ۖ يَقُولُونَ رَبَّنَا آمَنَّا فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ ﴿٨٣﴾

83. Na wanaposikia yale yaliyoteremshwa kwa Rasuli utaona macho yao yanachuruzika machozi kutokana na yale waliyoyatambua ya haki. Wanasema: Rabb wetu tumeamini, basi Tuandike pamoja na wenye kushuhudia.

 

 

 

 

وَمَا لَنَا لَا نُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَمَا جَاءَنَا مِنَ الْحَقِّ وَنَطْمَعُ أَن يُدْخِلَنَا رَبُّنَا مَعَ الْقَوْمِ الصَّالِحِينَ ﴿٨٤﴾

84. Na kwa nini Tusimwamini Allaah na haki iliyotufikia na hali tunatumai Rabb wetu Atuingize (Jannah) pamoja na watu Swalihina?

 

 

 

 

فَأَثَابَهُمُ اللَّـهُ بِمَا قَالُوا جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ جَزَاءُ الْمُحْسِنِينَ ﴿٨٥﴾

85. Basi Allaah Akawalipa tuzo ya Jannaat zipitazo chini yake mito kwa yale waliyoyasema, wadumu humo. Na hiyo ndio jazaa ya wafanyao ihsaan.

 

 

 

 

وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ ﴿٨٦﴾

86. Na wale waliokufuru na wakazikadhibisha Aayaat (na Ishara, Dalili, Hoja) Zetu hao ni watu wa moto uwakao vikali mno. 

 

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُحَرِّمُوا طَيِّبَاتِ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿٨٧﴾

87. Enyi walioamini! Msiharamishe vilivyo vizuri Alivyokuhalalishieni Allaah, na wala msipindukie mipaka. Hakika Allaah Hapendi wapindukao mipaka. 

 

 

 

وَكُلُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّـهُ حَلَالًا طَيِّبًا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي أَنتُم بِهِ مُؤْمِنُونَ ﴿٨٨﴾

88. Na kuleni katika vile Alivyowaruzukuni Allaah vya halali na vizuri. Na mcheni Allaah Ambaye nyinyi mnamwamini. 

 

 

 

لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا عَقَّدتُّمُ الْأَيْمَانَ ۖ فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِ مَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّارَةُ أَيْمَانِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ ۚ وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٨٩﴾

89. Allaah Hatokuchukulieni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini Atakuchukulieni kwa (kuvunja) viapo mlivyoapa kwa niya mlioifunga thabiti. Basi kafara yake ni kulisha maskini kumi chakula cha wastani mnachowalisha ahli zenu, au kuwavisha nguo, au kuacha huru mtumwa. Lakini asiyeweza kupata (katika hayo), basi (afunge) Swiyaam siku tatu. Hiyo ndio kafara ya viapo vyenu mnapoapa. Na hifadhini yamini zenu.[20] Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat (na Hukmu, Sharia) Zake ili mpate kushukuru.

 

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٩٠﴾

90. Enyi walioamini! Hakika pombe na kamari na masanamu na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli, ni najisi na chukizo kutokana na kazi ya shaytwaan. Basi jiepusheni navyo mpate kufaulu.[21]

 

 

إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُوقِعَ بَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ وَعَنِ الصَّلَاةِ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّنتَهُونَ ﴿٩١﴾

91. Hakika shaytwaan anataka kukutilieni baina yenu uadui na bughudha, katika pombe na kamari na akuzuieni kumdhukuru Allaah na Swalaah, basi je mtakoma?

 

 

 

وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَاحْذَرُوا ۚ فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ ﴿٩٢﴾

92. Na mtiini Allaah na mtiini Rasuli na tahadharini! Mkikengeuka, basi jueni kwamba juu ya Rasuli Wetu ni kubalighisha ujumbe tu ulio bayana.

 

 

 

 

 

لَيْسَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جُنَاحٌ فِيمَا طَعِمُوا إِذَا مَا اتَّقَوا وَّآمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ ثُمَّ اتَّقَوا وَّآمَنُوا ثُمَّ اتَّقَوا وَّأَحْسَنُوا ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿٩٣﴾

93. Hakuna lawama juu ya wale walioamini na wakatenda mema katika vile walivyokula (kabla ya kuharimishwa) ikiwa watakuwa na taqwa na wakaamini na wakatenda mema, kisha wakawa na taqwa na wakaamini, kisha wakawa na taqwa na wakafanya ihsaan. Na Allaah Anapenda wafanyao ihsaan.

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَيَبْلُوَنَّكُمُ اللَّـهُ بِشَيْءٍ مِّنَ الصَّيْدِ تَنَالُهُ أَيْدِيكُمْ وَرِمَاحُكُمْ لِيَعْلَمَ اللَّـهُ مَن يَخَافُهُ بِالْغَيْبِ ۚ فَمَنِ اعْتَدَىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَلَهُ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٩٤﴾

94. Enyi walioamini! Bila shaka Allaah Atakujaribuni mtihani mdogo kwa baadhi ya wanyama wa kuwinda inayowafikia mikono yenu na mikuki yenu, ili Allaah Ampambanue mwenye kumkhofu bila kumwona. Na atakayetaadi baada ya hayo, basi atapata adhabu iumizayo. 

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْتُلُوا الصَّيْدَ وَأَنتُمْ حُرُمٌ ۚ وَمَن قَتَلَهُ مِنكُم مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاءٌ مِّثْلُ مَا قَتَلَ مِنَ النَّعَمِ يَحْكُمُ بِهِ ذَوَا عَدْلٍ مِّنكُمْ هَدْيًا بَالِغَ الْكَعْبَةِ أَوْ كَفَّارَةٌ طَعَامُ مَسَاكِينَ أَوْ عَدْلُ ذَٰلِكَ صِيَامًا لِّيَذُوقَ وَبَالَ أَمْرِهِ ۗ عَفَا اللَّـهُ عَمَّا سَلَفَ ۚ وَمَنْ عَادَ فَيَنتَقِمُ اللَّـهُ مِنْهُ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ ذُو انتِقَامٍ ﴿٩٥﴾

95. Enyi walioamini! Msiue mawindo na hali mko katika ihraam.[22] Na atakayemuua (mnyama) miongoni mwenu kwa kusudi, basi malipo yake itakuwa ni kilicho sawa na alichokiua katika wanyama wa mifugo. Watamkadiria anayelingana naye wajuzi wawili waadilifu miongoni mwenu. Mnyama huyo afikishwe Ka’bah, au atoe kafara ya kulisha maskini, au badala ya hayo, (afunge) Swiyaam ili aonje matokeo maovu ya jambo lake. Allaah Ameshasamehe yaliyopita, na yeyote atakayerudia tena, basi Allaah Atamlipiza (kumuadhibu). Na Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kulipiza.

 

 

 

أُحِلَّ لَكُمْ صَيْدُ الْبَحْرِ وَطَعَامُهُ مَتَاعًا لَّكُمْ وَلِلسَّيَّارَةِ ۖ وَحُرِّمَ عَلَيْكُمْ صَيْدُ الْبَرِّ مَا دُمْتُمْ حُرُمًا ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٩٦﴾

96. Mmehalalishiwa mawindo ya bahari, na chakula chake ni manufaa kwenu na kwa wasafiri. Na mmeharamishiwa mawindo ya nchi kavu madamu mtakuwa katika ihraam. Na mcheni Allaah Ambaye Kwake mtakusanywa.

 

 

 

 

جَعَلَ اللَّـهُ الْكَعْبَةَ الْبَيْتَ الْحَرَامَ قِيَامًا لِّلنَّاسِ وَالشَّهْرَ الْحَرَامَ وَالْهَدْيَ وَالْقَلَائِدَ ۚ ذَٰلِكَ لِتَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَأَنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٩٧﴾

97. Allaah Amejaalia Ka’bah ambayo ni Nyumba Tukufu kuwa kiini cha manufaa na matengeneo kwa watu, na pia Miezi Mitukufu na wanyama wa kafara na vigwe. Hivyo ili mpate kujua kuwa Allaah Anajua yale yaliyomo mbinguni na ardhini na kwamba Allaah Ni Mjuzi kwa kila kitu.

 

 

 

 

اعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ وَأَنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٩٨﴾

98. Jueni kuwa Allaah Ni Mkali wa Kuakibu[23] na kwamba Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

مَّا عَلَى الرَّسُولِ إِلَّا الْبَلَاغُ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا تُبْدُونَ وَمَا تَكْتُمُونَ ﴿٩٩﴾

99. Rasuli hana jingine zaidi ila kubalighisha tu. Na Allaah Anayajua yale mnayoyadhihirisha na yale mnayoyaficha.

 

 

 

 

قُل لَّا يَسْتَوِي الْخَبِيثُ وَالطَّيِّبُ وَلَوْ أَعْجَبَكَ كَثْرَةُ الْخَبِيثِ ۚ فَاتَّقُوا اللَّـهَ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿١٠٠﴾

100. Sema: Haviwi sawasawa viovu na vizuri japokuwa utakupendezea wingi wa viovu. Basi mcheni Allaah, enyi wenye akili ili mpate kufaulu.

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَسْأَلُوا عَنْ أَشْيَاءَ إِن تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ وَإِن تَسْأَلُوا عَنْهَا حِينَ يُنَزَّلُ الْقُرْآنُ تُبْدَ لَكُمْ عَفَا اللَّـهُ عَنْهَا ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿١٠١﴾

101. Enyi walioamini! Msiulizie mambo ambayo mkifichuliwa yatakuchukizeni. Na mkiyaulizia pale inapoteremshwa Qur-aan mtafichuliwa. Allaah Ameyasamehe hayo. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mvumilivu.

 

 

 

 

قَدْ سَأَلَهَا قَوْمٌ مِّن قَبْلِكُمْ ثُمَّ أَصْبَحُوا بِهَا كَافِرِينَ ﴿١٠٢﴾

102. Walikwishayauliza hayo watu wa kabla yenu, kisha kutokana nayo, wakawa makafiri.

 

 

 

مَا جَعَلَ اللَّـهُ مِن بَحِيرَةٍ وَلَا سَائِبَةٍ وَلَا وَصِيلَةٍ وَلَا حَامٍ ۙ وَلَـٰكِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ ۖ وَأَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ﴿١٠٣﴾

103. Allaah Hakuweka sharia yoyote ya kuharamisha bahiyrah[24], wala saaibah[25] wala waswiylah[26] wala haam[27] lakini wale waliokufuru wanamtungia Allaah uongo, na wengi wao hawatumii akili.

 

 

 

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا إِلَىٰ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَإِلَى الرَّسُولِ قَالُوا حَسْبُنَا مَا وَجَدْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا ۚ أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ شَيْئًا وَلَا يَهْتَدُونَ ﴿١٠٤﴾

104. Na wanapoambiwa: Njooni katika yale Aliyoyateremsha Allaah na kwa Rasuli Husema: Yanatutosheleza yale tuliyowakuta nayo baba zetu. Je, japokuwa walikuwa baba zao hawajui chochote na wala hawakuhidika?

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَيْكُمْ أَنفُسَكُمْ ۖ لَا يَضُرُّكُم مَّن ضَلَّ إِذَا اهْتَدَيْتُمْ ۚ إِلَى اللَّـهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٠٥﴾

105. Enyi walioamini! Jiangalieni nafsi zenu. Hawakudhuruni waliopotoka ikiwa mmehidika. Kwa Allaah Pekee ndio marejeo yenu nyote, kisha Atakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda.[28]

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا شَهَادَةُ بَيْنِكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ حِينَ الْوَصِيَّةِ اثْنَانِ ذَوَا عَدْلٍ مِّنكُمْ أَوْ آخَرَانِ مِنْ غَيْرِكُمْ إِنْ أَنتُمْ ضَرَبْتُمْ فِي الْأَرْضِ فَأَصَابَتْكُم مُّصِيبَةُ الْمَوْتِ ۚ تَحْبِسُونَهُمَا مِن بَعْدِ الصَّلَاةِ فَيُقْسِمَانِ بِاللَّـهِ إِنِ ارْتَبْتُمْ لَا نَشْتَرِي بِهِ ثَمَنًا وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۙ وَلَا نَكْتُمُ شَهَادَةَ اللَّـهِ إِنَّا إِذًا لَّمِنَ الْآثِمِينَ ﴿١٠٦﴾

106. Enyi walioamini! Ushahidi uliofaradhishwa kati yenu ni wa watu wawili waadilifu wakati wa kuandika (au kutamka) usia, anapohisi mmoja wenu dalili za kukurubia kufa, au wawili wengineo wasiokuwa nyinyi pale mnapokuwa safarini ukakufikeni msiba wa mauti. Muwazuie baada ya Swalaah, na waape kwa Allaah mkitilia shaka, (waseme): Hatutovibadilisha (viapo vyetu) kwa thamani yoyote ile japo akiwa ni jamaa yetu wa karibu. Na wala hatutoficha ushuhuda wa Allaah, kwani hakika hapo tutakuwa miongoni mwa wenye kutenda dhambi.  

 

 

 

فَإِنْ عُثِرَ عَلَىٰ أَنَّهُمَا اسْتَحَقَّا إِثْمًا فَآخَرَانِ يَقُومَانِ مَقَامَهُمَا مِنَ الَّذِينَ اسْتَحَقَّ عَلَيْهِمُ الْأَوْلَيَانِ فَيُقْسِمَانِ بِاللَّـهِ لَشَهَادَتُنَا أَحَقُّ مِن شَهَادَتِهِمَا وَمَا اعْتَدَيْنَا إِنَّا إِذًا لَّمِنَ الظَّالِمِينَ ﴿١٠٧﴾

107. Ikigundulikana kwamba hao wawili wana hatia ya kukhini, basi wawili wengine wanaostahiki kudai haki kisharia, na walio karibu zaidi (na mrithiwa) wasimame mahala pao, kisha waape kwa Allaah: Bila shaka ushahidi wetu ni wa kweli zaidi kuliko ushahidi wa wawili wao, nasi hatukufanya taksiri, kwani bila shaka hapo sisi tutakuwa miongoni mwa madhalimu.

 

 

 

 

ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يَأْتُوا بِالشَّهَادَةِ عَلَىٰ وَجْهِهَا أَوْ يَخَافُوا أَن تُرَدَّ أَيْمَانٌ بَعْدَ أَيْمَانِهِمْ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاسْمَعُوا ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ ﴿١٠٨﴾

108. Hivyo inaelekea zaidi ya kwamba watatoa ushahidi kama ipasavyo au watakhofu visije vikaletwa viapo (vingine) baada ya viapo vyao. Na mcheni Allaah na sikizeni!  Na Allaah Haongoi watu mafasiki.

 

 

 

 

يَوْمَ يَجْمَعُ اللَّـهُ الرُّسُلَ فَيَقُولُ مَاذَا أُجِبْتُمْ ۖ قَالُوا لَا عِلْمَ لَنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ ﴿١٠٩﴾

109. Siku Allaah Atakayowakusanya Rusuli na Kuwaambia: Mlijibiwa nini? Watasema: Hatujui lolote, hakika Wewe Ndiye Mjuzi wa Ghaibu.

 

 

 

 

إِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ اذْكُرْ نِعْمَتِي عَلَيْكَ وَعَلَىٰ وَالِدَتِكَ إِذْ أَيَّدتُّكَ بِرُوحِ الْقُدُسِ تُكَلِّمُ النَّاسَ فِي الْمَهْدِ وَكَهْلًا ۖ وَإِذْ عَلَّمْتُكَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَالتَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ ۖ وَإِذْ تَخْلُقُ مِنَ الطِّينِ كَهَيْئَةِ الطَّيْرِ بِإِذْنِي فَتَنفُخُ فِيهَا فَتَكُونُ طَيْرًا بِإِذْنِي ۖ وَتُبْرِئُ الْأَكْمَهَ وَالْأَبْرَصَ بِإِذْنِي ۖ وَإِذْ تُخْرِجُ الْمَوْتَىٰ بِإِذْنِي ۖ وَإِذْ كَفَفْتُ بَنِي إِسْرَائِيلَ عَنكَ إِذْ جِئْتَهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿١١٠﴾

110. (Siku) Allaah Ataposema: Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam! Kumbuka Neema Yangu juu yako na juu ya mama yako, pale Nilipokutia nguvu kupitia kwa Ruwhil-Qudus (Jibriyl (عليه السلام, unasemesha watu katika utoto na utu uzimani, na Nilipokufunza kuandika na hikmah (ilimu na ufahamu wa kina), na Tawraat na Injiyl, na ulipounda kutokana na udongo kama umbo la ndege kwa Idhini Yangu, ukapulizia likawa ndege kwa Idhini Yangu,   na ulipomponyesha aliyezaliwa na upofu na mwenye barasi kwa Idhini Yangu, na ulipowafufua wafu kwa Idhini Yangu, na Nilipowazuia wana wa Israaiyl dhidi yako ulipowajia kwa hoja bayana, wakasema wale waliokufuru miongoni mwao: Haya si chochote ila ni sihiri bayana.

 

 

 

 

وَإِذْ أَوْحَيْتُ إِلَى الْحَوَارِيِّينَ أَنْ آمِنُوا بِي وَبِرَسُولِي قَالُوا آمَنَّا وَاشْهَدْ بِأَنَّنَا مُسْلِمُونَ ﴿١١١﴾

111. Na Nilipowatia ilhamu wafuasi watiifu kwamba: Niaminini Mimi na Rasuli Wangu. Wakasema: Tumeamini na shuhudia kwamba sisi ni Waislamu.

 

 

 

 

إِذْ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ هَلْ يَسْتَطِيعُ رَبُّكَ أَن يُنَزِّلَ عَلَيْنَا مَائِدَةً مِّنَ السَّمَاءِ ۖ قَالَ اتَّقُوا اللَّـهَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١١٢﴾

112. Pindi waliposema wafuasi watiifu: Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam! Je, Anaweza Rabb wako Kututeremshia meza ya chakula kutoka mbinguni? Akasema: Mcheni Allaah, kama nyinyi ni Waumini.

 

 

 

 

قَالُوا نُرِيدُ أَن نَّأْكُلَ مِنْهَا وَتَطْمَئِنَّ قُلُوبُنَا وَنَعْلَمَ أَن قَدْ صَدَقْتَنَا وَنَكُونَ عَلَيْهَا مِنَ الشَّاهِدِينَ ﴿١١٣﴾

113. Wakasema: Tunataka kula kwenye meza hiyo ili nyoyo zetu zitulie, na tujue kwamba umetuambia kweli, na tuwe katika wenye kulishuhudia hilo.

 

 

 

 

قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ اللَّـهُمَّ رَبَّنَا أَنزِلْ عَلَيْنَا مَائِدَةً مِّنَ السَّمَاءِ تَكُونُ لَنَا عِيدًا لِّأَوَّلِنَا وَآخِرِنَا وَآيَةً مِّنكَ ۖ وَارْزُقْنَا وَأَنتَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ ﴿١١٤﴾

114. Akasema ‘Iysaa mwana wa Maryam: Ee Allaah, Rabb wetu!   Tuteremshie meza ya chakula kutoka mbinguni ili iwe kwetu ni sikukuu kwa wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu, na iwe Aayah (Ishara, Hoja, Dalili) itokayo Kwako, basi Turuzuku, kwani Wewe Ni Mbora wa wenye kuruzuku.

 

 

 

قَالَ اللَّـهُ إِنِّي مُنَزِّلُهَا عَلَيْكُمْ ۖ فَمَن يَكْفُرْ بَعْدُ مِنكُمْ فَإِنِّي أُعَذِّبُهُ عَذَابًا لَّا أُعَذِّبُهُ أَحَدًا مِّنَ الْعَالَمِينَ ﴿١١٥﴾

115. Akasema Allaah: Hakika Mimi Nitaiteremsha kwenu. Lakini atakayekufuru miongoni mwenu baada ya hapo, basi hakika Nitamuadhibu adhabu ambayo Sitomuadhibu mmoja yeyote katika walimwengu.

 

 

 

 

وَإِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ أَأَنتَ قُلْتَ لِلنَّاسِ اتَّخِذُونِي وَأُمِّيَ إِلَـٰهَيْنِ مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ قَالَ سُبْحَانَكَ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أَقُولَ مَا لَيْسَ لِي بِحَقٍّ ۚ إِن كُنتُ قُلْتُهُ فَقَدْ عَلِمْتَهُ ۚ تَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِي وَلَا أَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِكَ ۚ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ ﴿١١٦﴾

116. Na pindi Allaah Atakaposema: Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam!  Je, wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni waabudiwa wawili badala ya Allaah? (‘Iysaa) atasema: Subhaanak! (Utakasifu ni Wako). Hainipasi mimi kusema yasiyo kuwa haki kwangu. Ikiwa nimesema hayo basi kwa yakini Ungeliyajua. (Kwani) Unayajua yale yote yaliyomo katika nafsi yangu, na wala mimi sijui yale yaliyomo katika Nafsi Yako, hakika Wewe Ni Mjuzi wa Ghaibu.

 

 

 

 

مَا قُلْتُ لَهُمْ إِلَّا مَا أَمَرْتَنِي بِهِ أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۚ وَكُنتُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا مَّا دُمْتُ فِيهِمْ ۖ فَلَمَّا تَوَفَّيْتَنِي كُنتَ أَنتَ الرَّقِيبَ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنتَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿١١٧﴾

117. Sijawaambia (lolote) ila yale tu Uliyoniamrisha kwamba: Mwabuduni Allaah Rabb wangu na Rabb wenu. Na nilikuwa juu yao shahidi wakati nilipokuwa nao. Uliponikamilishia muda Ukanichukua juu, Ulikuwa Wewe Ndiye Mwangalizi juu yao. Na Wewe Ni Mwenye Kushuhudia kila kitu.

 

 

 

 

إِن تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ ۖ وَإِن تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١١٨﴾

118. Ukiwaadhibu, basi bila shaka hao ni Waja Wako, na Ukiwaghufuria basi hakika Wewe Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.[29]

 

 

 

 

قَالَ اللَّـهُ هَـٰذَا يَوْمُ يَنفَعُ الصَّادِقِينَ صِدْقُهُمْ ۚ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١١٩﴾

119. Allaah Atasema: Hii ndiyo Siku ambayo Asw-Swaadiqiyna utawafaa ukweli wao, watapata Jannaat zipitazo chini yake mito wadumu humo milele.  Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Huko ni kufuzu kukubwa mno.

 

 

 

لِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا فِيهِنَّ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٢٠﴾

120. Ni wa Allaah ufalme wa mbingu na ardhi na yote yaliyomo humo.  Naye juu ya kila kitu Ni Muweza.

 

 

 

 

 

[1] Ihraam: Rejea Aayah namba (95) Suwrah hii.

 

[2] Tofauti Ya Ikabu Na Adhabu: Rejea Al-Hashr (59:4).

 

[3] Aayah Ambayo Ingeliteremshwa Kwa Mayahudi, Wangelisherehekea Siku Iliyoteremshwa:

 

‘Umar bin Al-Khattwaab (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Myahudi mmoja alimwambia: Ee Amiri wa Waumini, lau ingeliteremka kwetu sisi Aayah hii:

 

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ

“Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na Nimekutimizieni Neema Yangu, na Nimekuridhieni Uislamu uwe Dini yenu.”  [Al-Maaidah (5:3)] Basi tungeliifanya kuwa ni siku ya kusherehekea. ‘Umar akasema: Wa-Allaahi, naijua siku gani imeteremka Aayah hii. Imeteremka Siku ya ‘Arafah, siku ya Ijumaa. [Al-Bukhaariy]

 

[4] Sababu Ya Kuteremshwa Hukmu Ya Tayammum (Kuikusudia Ardhi Safi Ya Mchanga Kwa Ajili Ya Wudhuu):

 

Mama wa ‘Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) amehadithia: “Tulikwenda katika moja ya safari tukafika Al-Baydaa au Dhaatul-Jaysh ambako kidani changu kilivunjika (na kikapotea). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawa anakitafuta, kisha pia watu wengineo wakainuka kukitafuta. Hapakuweko na maji sehemu hiyo, basi watu wakamwendea Abuu Bakr Asw-Swiddiyq na kusema: Huoni alivyofanya ‘Aaishah? Kamfanya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) pamoja na watu wakae sehemu ambayo hakuna maji! Abuu Bakr akaja wakati Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa amelala akiwa amelaza kichwa chake mapajani mwangu. Akaniambia: Umemzuia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na watu sehemu ambako hakuna maji na wala hawana (akiba ya) maji. Basi akanigombesha na akasema Aliyomjaalia (Allaah) kusema kuhusu mimi, na akanipiga ubavuni kwa mkono wake. Hakuna kilichonizuia kusogea (kutokana na maumivu) isipokuwa kwa vile Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa amelala mapajani mwangu. Hapo Allaah Akateremsha Aayah ya tayammum (kutia Wudhuu kwa mchanga), basi wakatayammam. ‘Usayd bin Al-Hudhwayr akasema: Ee ahli wa Abuu Bakr! Hii si baraka ya kwanza kwenu. Kisha akaendeshwa ngamia ambaye nilikuwa nimempanda na tukakipata kidani kilichokuwa (kimejificha) chini yake.” [Al-Bukhaariy]

 

Rejea pia An-Nisaa Aayah (4:43) ambayo pia ni sababu ya kuteremshwa hukmu ya Tayammum.

 

[5]  Al-Masiyh (Nabiy ‘Iysaa) Sio Allaah Bali Ni Mwana Wa Maryam Na Ni Rasuli Wa Allaah:

 

Rejeja An-Nisaa (4:171) na Rejea Suwrat Maryam (19:16-36) ambako kumetajwa kisa cha Maryam; Mama wa Nabiy ‘Iysaa, na yeye mwenyewe Nabiy ‘Iysaa amekanusha alipokuwa angali mtoto mchanga baada ya kuzaliwa tu kuwa yeye siye anayepaswa kuabudiwa, na kwamba yeye ni mja na Rasuli wa Allaah, na kwamba anayepaswa kuabudiwa ni Allaah. Hali kadhaalika Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام)    amekanusha hayo katika Suwrah hii (5:116-118). Amekanusha pia katika Suwrat Az-Zukhruf (43:64). Rejea pia Aal-‘Imraan (3:51).

 

[6] Watu Wawili Waliomcha Allaah:

 

Watu wawili hao waliomcha Allaah ni Yuwsha’ Bin Nuwn Na Kaalib Bin Yuwfaan [Tafsiyr Ibn Kathiyr] Rejea Al-Kahf (18:60)

 

[7]  Vipi Kukatwa Mikono Na Miguu Kwa Kutofautisha:

Kuhusu Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

أَوْ تُقَطَّعَ أَيْدِيهِمْ وَأَرْجُلُهُم مِّنْ خِلَافٍ

“Au ikatwe mikono yao na miguu yao kwa kutofautisha.”

 

Ni kukatwa mikono ya kulia kwa miguu ya kushoto au miguu ya kushoto kwa mikono ya kulia.

 

[8] Radd Kwa Kundi La Qur-aaniyyuwn Wanaoamini Qur-aan Pekee Na Kupinga Sunnah:

 

Aayah hii tukufu ambayo imetaja hukmu ya mwizi kukatwa mkono, ni Aayah mojawapo ambayo haiwezi kufahamika na wala kupata hukmu yake kamili ya suala la mwizi kukatwa mkono. Ni lazima mtu arudie katika Sunnah kupata ufafanuzi wa suala zima la hukmu hii kama vile kiwango gani cha chini alichoiba hata astahiki kukatwa mkono. Na je mkono gani, na kuanzia wapi? Na ‘Aliy (رضي الله عنه) alikuwa akikata mkono kuanzia kifundoni. Na Qataadah amesema kuhusiana na mwanamke aliyeiba naye akakatwa mkono wake wa kushoto: “Usiwe ni mwenye kukata chochote chengine.” [Imaam Al-Bukhaariy katika Kitaab cha Huduwd (Mipaka)]   

 

Hadiyth kadhaa zimethibiti kutoa hukmu ya suala hili. Ni kama hii ifuatayo inayotaja kiwango cha alichoiba mwizi:

Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Unakatwa mkono wa mwizi aliyeiba robo dinaar ya dhahabu.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth hii ni hoja bayana kwa kundi la Qur-aaniyuwn wanaoikubali Qur-aan pekee na kukanusha Hadiyth za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba hawawezi kuifahamu Qur-aan kwa waziwazi na kupata hukmu za baadhi ya mas-ala ila kupitia Hadiyth. Na ajabu mno kwa kundi hilo kukanusha Hadiyth za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ilhali Qur-aan haikufafanua mas-ala mengi ya ibaada za Muislamu ambazo bila ya Hadiyth za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) haiwezekani kufahamu jinsi ya kuzitekeleza. Na katika ibaada hizo ni nguzo za Kiislamu kama Swalaah kuanzia Twahara yake, idadi ya Rakaa zake kwa nyakati zote tano; Alfajiri, Adhuhuri, Alasiri, Magharibi na ‘Ishaa ambazo hazikutajwa katika Qur-aan, na utekelezaji mzima wa Swalaah ambayo ina nguzo zake, yanayowajibika, yaliyo Sunnah na kadhaalika. Hali kadhaalika Manaasik (taratibu) za Hajj; hukmu zake na utekelezaji wake hayakufafanuliwa katika Qur-aan.  Pia hukmu za Swawm ya Mwezi wa Ramadhwaan na wakati wa kuanzia kufunga hadi kufuturu. Kiwango cha utoaji wa Zakaah nacho hakikutajwa katika Qur-aan. Na mengi mengineyo ambayo yote hayakufafanuliwa katika Qur-aan bali Sunnah ndio imekuja kufafanua. Basi vipi waamini Qur-aan na wasifuate Anayoamrisha Allaah (سبحانه وتعالى) kumtii na kumfuata Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ilhali Anaamrisha hilo?! Na pia Allaah (سبحانه وتعالى) Mwenyewe Amemtaka Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) afafanue na awafahamishe Waumini yaliyomo ndani ya Qur-aan. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ﴿٤٤﴾

“Na Tumekuteremshia Ukumbusho (Qur-aan) ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao huenda wakapata kutafakari.” [An-Nahl (16:44)]

 

Na pia Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):  

وَمَا أَنزَلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ إِلَّا لِتُبَيِّنَ لَهُمُ الَّذِي اخْتَلَفُوا فِيهِ ۙ وَهُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ﴿٦٤﴾

“Na Hatukukuteremshia Kitabu (Qur-aan) isipokuwa uwabainishie yale waliyokhitilafiana, na pia ni mwongozo na rahmah kwa watu wanaoamini.” [An-Nahl (16:64)]

 

Na Aayah hii pia ni zingatio kwa makafiri wanaoitafutia upogo Qur-aan kuwa inatoa hukmu kali kama hii ya wizi na nyenginezo kama adhabu ya zinaa, bila ya kufahamu kwa kina hukmu zake ambazo ufafanuzi wake unapatikana katika Sunnah (Hadiyth) ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).

 

[9] Ar-Rabbaaniyyuwn (Marabi): Ni Wanavyuoni Waswalihina wa Kiyahudi wenye kufanya ibaada mno na kuitumia ilimu yao.  Rejea Aal-‘Imraan (3:79) kupata maelezo ziyada kuhusu maana hii na sifa zake.

 

[10] Al-Ahbaar: Mafuqahaa wa dini ya Kiyahudi ambao ni weledi mno.

 

[11]  Qur-aan Inashuhudia Na Inadhibiti Vitabu Vilivyotangulia.

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja katika Aayah kadhaa kwamba Vitabu Vyake vya nyuma Alivyoviteremsha toka mbinguni kwa Mayahudi na Manaswara vimebadilishwa maneno yake kwa sababu ya kuficha haki au kufuata manufaa ya kidunia. Akateremsha Qur-aan kuwa ni Kitabu cha mwisho kwa Rasuli wa mwisho kabisa Nabiy  Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) , na kwamba Qur-aan hii haina shaka kabisa, na wala hakuna awezaye kuibadilisha au kuleta mfano wake. Rejea Al-Baqarah (2:79) (2:174), Aal-‘Imraan (3:78), (3:187).

 

[12] Nyoyo Zenye Maradhi:

 

Rejea Suwrah Muhammad (47:20) kwenye maelezo na rejea mbalimbali kuhusu nyoyo zenye maradhi.

 

Rejea pia Al-Hajj (22:46) kwenye maelezo kuhusu maana ya moyo uliopofuka.

Rejea pia Ash-Shu’araa (26:88-89) kwenye ufafanuzi na maelezo kuhusu moyo uliosalimika.

 

[13]   Ar-Rabbaaniyyuwn (Marabi), Al-Ahbaar: Rejea Suwrah hii Al-Maaidah (5:44).

 

[14] Aqiydah Sahihi Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Ni Kuthibisha Sifa Za Allaah Kama Mikono Yake:

 

Rejea Al-Fat-h (48:10).

[15]  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)   Ametimiza Risala (Ujumbe) Ipasavyo:

 

Hakika Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  aliifikisha na kuitangaza Dini ya Allaah (سبحانه وتعالى)  na akaieneza daawah yake mpaka ikawafikia majini na watu.  Na akawafundisha yote Aliyoyaweka Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa ni sharia. Akausimamia uwajibu huu kwa nguvu zote, na Allaah (سبحانه وتعالى) Hakumfisha mpaka Alipoinyoosha kupitia yeye dini iliyopindishwa na Akayafungua kupitia yeye macho yenye upofu, na kuzifungua nyoyo zilizokuwa zimefunikwa na ujinga

 

[16]  Wasabai: Ni Akina Nani? Nini Imani Na ‘Aqiydah Zao? Rejea Al-Hajj (22:17).

 

 

[17] Kumshirikisha Allaah Ni Dhambi Pekee Asiyoighufuria Allaah (سبحانه وتعالى) Isipokuwa Mtu Atubie Kabla Ya Kufariki Kwake:

 

Rejea An-Nisaa (4:48), (4:116).

 

Na ‘Iysaa Hapasi Kuabudiwa Kwani Yeye Ni Mja Wa Allaah Na Rasuli Wake:

 

Rejea (4:171), At-Tawbah (9:30). Na pia Aayah (5:17) ya Suwrah hii Al-Maaidah.

 

[18]  Qissiysiyna: (Makasisi) Wanavyuoni Wakuu wa Kinaswara wenye kufanya ibaada mno.

 

[19] Ruhbaan:  Monaki wa Kinaswara wenye taqwa na wanaomkhofu mno Allaah (سبحانه وتعالى).

[20] Kafara Ya Kuapa Ifuatwe Kwa Mpangilio Wa Aayah Na Haifai Kuapa Ovyo Ovyo:

 

Aayah hii Tukufu imebainisha kwamba kafara ya yamini iliyofungika ni waajib kwa kuchaguzwa mhusika kwa mujibu wa utaratibu ufuatao: 

1-Kulisha.

2-Kuvisha nguo.         

 3-Kuacha huru mtumwa.

4-Swiyaam (kufunga) siku tatu pindi mtu akishindwa hayo matatu ya kwanza. Na haijuzu kufanya kafara hii ya Swawm ila baada ya kushindwa kuyafanya mambo matatu hayo ya kwanza.  Hili ndilo lililokubaliwa kwa ‘Ijmaa ya ‘Ulamaa wote. [Swahiyh Fiqh As-Sunnah Mlango Wa Viapo Na Nadhiri]

 

Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Anaamrisha kuhifadhi viapo Anaposema:

وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ

“Na hifadhini yamini zenu.”

 

Kwa maana haifai mtu kuapa ovyo ovyo. Na hikma ya watu kuamuriwa kuapa kwa ufinyu iwezekanavyo, ni kuwa mtu anayeapa kwa Allaah kwa kila kichache na kingi, basi ulimi wake utakuja kuzoea hilo, na kiapo hakitakuwa na uzito wala thamani kwenye moyo wake, na hatokuwa na muamana wa kuthubutu kuapa kiapo cha uongo.  Na hapo lengo asili la kiapo litapoteza mwelekeo. [Swahiyh Fiqh As-Sunnah Mlango Wa Viapo Na Nadhiri]

 

Rejea Al-Baqarah (2:225), Al-Qalam (68:10).

 

[21] Hatua Za Uharamisho Wa Pombe Na Kikomo Chake:

 

Rejea Al-Baqarah (2:219), An-Nisaa (4:43).

 

Hatua ya kwanza. Ni swali alilouliza Swahaba, na jibu lake lipo katika Suwratul-Baqarah (2:219):

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِن نَّفْعِهِمَا ۗ

Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema: Katika viwili hivyo mna dhambi kubwa na (baadhi ya) manufaa kwa watu. Na dhambi yake viwili hivyo ni kubwa kuliko manufaa yake.” [Al-Baqarah (2:219)]

 

Hatua ya pili. Ilikuwa ni kukatazwa pombe katika nyakati za Swalaah kwa sababu Swahaba walikosea kusoma Qur-aan katika Swalaah kutokana na kulewa. Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha Aayah katika Suwrat An-Nisaa (4:43):  

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنتُمْ سُكَارَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ  

“Enyi walioamini! Msikaribie Swalaah na hali mmelewa mpaka mjue mnayoyasema.” [An-Nisaa (4:43)]

 

Hatua ya tatu. Ni pale zilipofutwa hukmu hizo na ikabakia pombe kuwa ni haramu nyakati zote kwa Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٩٠﴾

“Enyi walioamini! Hakika pombe na kamari na masanamu na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli, ni najisi na chukizo kutokana na kazi ya shaytwaan. Basi jiepusheni navyo mpate kufaulu.”

 

إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُوقِعَ بَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ وَعَنِ الصَّلَاةِ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّنتَهُونَ ﴿٩١﴾

“Hakika shaytwaan anataka kukutilieni baina yenu uadui na bughudha katika pombe na kamari na akuzuieni kumdhukuru Allaah na Swalaah, basi je mtakoma?” [Al-Maaidah (5:90-91)]

 

Baada ya kuteremshwa Aayah hizo za Suwrat Al-Maaidah (5:90-91), hapo hapo Swahaba wakaacha moja kwa moja kulewa, na ikawa ndio kikomo cha kunywa pombe.

 

[22] Ihraam:

 

Ni mambo ambayo Allaah Amemkataza aliyehirimia kuyafanya, na Akamharamishia madhali yuko kwenye ihraam. Na ihraam (kuhirimia) ni kutia niya ya Hajj au ‘Umrah toka kwenye Miyqaat inayotambulika kisharia. Ni nguzo kati ya nguzo za Hajj na ‘Umrah kwa mujibu wa Jumhuri ya ‘Ulamaa, na ni sharti ya kuswihi Hajj au ‘Umrah. [Swahiyh Fiqh As-Sunnah]

 

[23] Tofauti Ya Ikabu Na Adhabu: Rejea Al-Hashr (59:4).

 

[24] Bahira: Ngamia aliyezaa matumbo matano.

 

[25] Saaibah: Ngamia aliyeachiliwa kwa nadhiri.

 

[26] Waswiylah: Kondoo aliyezaa matumbo saba.

 

[27] Haam: Fahali lililozalisha matumbo kumi.

 

[28] Kuzuia Dhulma Ili Kuepukana Na Adhabu Za Allaah (سبحانه وتعالى):

Abuu Bakr Asw-Swiddiyq (رضي الله عنه) amesema: Enyi watu! Hakika nyinyi mnaisoma Aayah hii:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَيْكُمْ أَنفُسَكُمْ ۖ لَا يَضُرُّكُم مَّن ضَلَّ إِذَا اهْتَدَيْتُمْ ۚ إِلَى اللَّـهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٠٥﴾

Enyi walioamini! Jiangalieni nafsi zenu. Hawakudhuruni waliopotoka ikiwa mmehidika. Kwa Allaah Pekee ndio marejeo yenu nyote, kisha Atakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda. [Al-Maaidah (5 :105)]

 

Hakika mimi nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Watu pindi watakapomuona mfanya dhulma na wakawa hawakumzuwia na hiyo dhulma, basi wafahamu kuwa  Allaah Hukaribia kuwaadhibu wote kwa adhabu itokayo Kwake.”  [At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Hadiyth Swahiyh]

 

[29] Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Akijali Mno Ummah Wake Na Akiwakhofia Adhabu:

 

Amesimulia ‘Abdullaah bin ‘Amru bin Al-‘Aasw (رضي الله عنه) : Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisoma Kauli ya Allaah (عزّ وجلّ) kuhusu Nabiy Ibraahiym:

رَبِّ إِنَّهُنَّ أَضْلَلْنَ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ ۖ فَمَن تَبِعَنِي فَإِنَّهُ مِنِّي ۖ  

“Rabb wangu! Hakika hao (masanamu) wamepoteza watu wengi.  Basi atakayenifuata, huyo yuko nami.” [Ibraahiym: 36]

Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasoma alivyosema ‘Iysaa (عليه السّلام) :

 

إِن تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ ۖ وَإِن تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١١٨﴾

“Ukiwaadhibu, basi bila shaka hao ni Waja Wako, na Ukiwaghufuria basi hakika Wewe Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.” [Al-Maaidah: 118]

 

Akanyanyua mikono yake akisema: “Ee Allaah! Ummah wangu! Ummah Wangu!  Akalia, kisha Allaah (عزّ وجلّ) Akasema: “Ee Jibriyl! Nenda kwa Muhammad, na Rabb wako Anajua zaidi, kisha muulize kitu kigani kinachomliza? Basi Jibriyl akamwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamuuliza (sababu ya kulia kwake), na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamjulisha, na Allaah Anajua zaidi, Hapo Allaah Akasema: “Ee Jibriyl! Nenda kwa Muhammad na mwambie: Hakika Sisi Tutauridhia ummah wako wala Hatutaudhika nawe.” [Muslim]

 

Imaam An-Nawawiy (رحمه الله) amesema katika Sharh Muslim: “Hadiyth hii imejumuisha aina za faida zikiwemo: Bainisho kamilifu la huruma zake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa ummah wake, kujali kwake kutunza maslahi yao, na kutilia hima mambo yao. Na hii ni bishara adhimu kwa ummah huu kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Ameuzidishia (ummah) sharaf (taadhima) kutokana na yale ambayo Allaah (سبحانه وتعالى)  Amemuahidi Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Kauli Yake: “Tutauridhia ummah wako wala Hatutaudhika nawe.”  Na hii ni Hadiyth itoayo matarajio makubwa kabisa kwa ummah huu.

 

Inaruhusika Kuirudia Aayah Moja Katika Swalaah Ya Sunnah:

 

Amesimulia Abuu Dharri (رضي الله عنه):  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliisoma Aayah hii akairudia rudia mpaka asubuhi. [Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (1010), Ahmad (20831) na Al-Haakim. Katika Sanad yake kuna ulaini]

 

 

 

 

Share