006 - Al-An'aam

 

 

 الأنْعَام

 

006-Al-An’aam

 

006-Al-An'aam: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَجَعَلَ الظُّلُمَاتِ وَالنُّورَ ۖ ثُمَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ يَعْدِلُونَ ﴿١

1. AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah), Ambaye Ameumba mbingu na ardhi na Akajaalia viza na nuru, kisha wale ambao wamekufuru wanawasawazisha wengine na Rabb wao.

 

 

 

هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن طِينٍ ثُمَّ قَضَىٰ أَجَلًا ۖ وَأَجَلٌ مُّسَمًّى عِندَهُ ۖ ثُمَّ أَنتُمْ تَمْتَرُونَ ﴿٢

2. Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni kutokana na udongo kisha Akahukumu muda maalumu, na uko Kwake muda maalumu uliokadariwa, kisha nyinyi mnatilia shaka!

 

 

 

وَهُوَ اللَّـهُ فِي السَّمَاوَاتِ وَفِي الْأَرْضِ ۖ يَعْلَمُ سِرَّكُمْ وَجَهْرَكُمْ وَيَعْلَمُ مَا تَكْسِبُونَ ﴿٣

3.  Na Yeye Ndiye Allaah mbinguni na ardhini, Anajua ya siri yenu na ya dhahiri yenu, na Anajua yale mnayoyachuma.[1]

 

وَمَا تَأْتِيهِم مِّنْ آيَةٍ مِّنْ آيَاتِ رَبِّهِمْ إِلَّا كَانُوا عَنْهَا مُعْرِضِينَ ﴿٤

4.  Na haiwafikii Aayah (Ishara, Muujiza, Hoja bayana) yoyote ile katika Aayaat (Ishara, Miujiza, Hoja bayana) za Rabb wao isipokuwa huwa ni wenye kuipuuza.

 

 

فَقَدْ كَذَّبُوا بِالْحَقِّ لَمَّا جَاءَهُمْ ۖ فَسَوْفَ يَأْتِيهِمْ أَنبَاءُ مَا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿٥

5. Kwa yakini wameikadhibisha haki ilipowajia, basi zitawafikia khabari muhimu za yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.

 

 

 

أَلَمْ يَرَوْا كَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَبْلِهِم مِّن قَرْنٍ مَّكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ مَا لَمْ نُمَكِّن لَّكُمْ وَأَرْسَلْنَا السَّمَاءَ عَلَيْهِم مِّدْرَارًا وَجَعَلْنَا الْأَنْهَارَ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمْ فَأَهْلَكْنَاهُم بِذُنُوبِهِمْ وَأَنشَأْنَا مِن بَعْدِهِمْ قَرْنًا آخَرِينَ ﴿٦

6. Je, hawaoni ni karne ngapi za vizazi Tumeziangamiza kabla yao? Tuliwamakinisha katika ardhi kwa namna ambayo Hatujapata kuwamakinisha nyinyi, na Tukawapelekea mvua tele iendeleayo, na Tukajaalia mito ipitayo chini yao. Hatimaye Tukawaangamiza kwa dhambi zao na Tukaanzisha baada yao karne nyingine ya vizazi.

 

 

 

وَلَوْ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ كِتَابًا فِي قِرْطَاسٍ فَلَمَسُوهُ بِأَيْدِيهِمْ لَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿٧

7. Na lau Tungelikuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) maneno yaliyoandikwa katika karatasi, kisha wakaigusa kwa mikono yao, bila shaka wale waliokufuru wangelisema: Hii si chochote isipokuwa ni sihiri (uchawi) bayana.

 

 

 

 

وَقَالُوا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ مَلَكٌ ۖ وَلَوْ أَنزَلْنَا مَلَكًا لَّقُضِيَ الْأَمْرُ ثُمَّ لَا يُنظَرُونَ ﴿٨

8. Na wakasema: Mbona hakuteremshiwa Malaika? Na lau Tungeliteremsha Malaika, basi amri ingepitishwa kisha wasingelipewa muhula.

 

 

 

 

وَلَوْ جَعَلْنَاهُ مَلَكًا لَّجَعَلْنَاهُ رَجُلًا وَلَلَبَسْنَا عَلَيْهِم مَّا يَلْبِسُونَ ﴿٩

9. Na lau Tungelimfanya Malaika, bila shaka Tungelimfanya binaadam mwanamume, na Tungeliwatatanishia yale wanayojitatanisha.

 

 

 

 

وَلَقَدِ اسْتُهْزِئَ بِرُسُلٍ مِّن قَبْلِكَ فَحَاقَ بِالَّذِينَ سَخِرُوا مِنْهُم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿١٠

10. Na kwa yakini walifanyiwa istihzai Rusuli kabla yako, lakini wale waliowafanyia dhihaka, yaliwazunguka yale yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.

 

 

 

قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ ثُمَّ انظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ ﴿١١

11. Sema: Nendeni katika ardhi, kisha mtazame vipi ilikuwa hatima ya wenye kukadhibisha.[2]

 

 

 

قُل لِّمَن مَّا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ قُل لِّلَّـهِ ۚ كَتَبَ عَلَىٰ نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ ۚ لَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۚ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٢

12.  Sema: Ni vya nani vilivyomo mbinguni na ardhini? Sema: Ni vya Allaah. Amejiwajibishia Nafsi Yake[3] Rahmah. Bila shaka Atakukusanyeni Siku ya Qiyaamah, hapana shaka yoyote ndani yake. Wale ambao wamekhasiri nafsi zao basi wao hawaamini.

 

 

 

وَلَهُ مَا سَكَنَ فِي اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١٣

13. Na ni Vyake vyote vinavyotulia katika usiku na mchana. Naye Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

 

قُلْ أَغَيْرَ اللَّـهِ أَتَّخِذُ وَلِيًّا فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَهُوَ يُطْعِمُ وَلَا يُطْعَمُ ۗ قُلْ إِنِّي أُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ أَوَّلَ مَنْ أَسْلَمَ ۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٤

14. Sema: Je, nimfanye rafiki mlinzi asiyekuwa Allaah Muanzilishi wa mbingu na ardhi, Naye Ndiye Anayelisha na wala Halishwi? Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza katika wenye kusilimu. Na wala usijekuwa kabisa miongoni mwa washirikina.

 

 

 

قُلْ إِنِّي أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّي عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿١٥

15. Sema: Hakika mimi nakhofu, ikiwa nitamuasi Rabb wangu, adhabu ya Siku iliyo kuu kabisa.

 

 

 

مَّن يُصْرَفْ عَنْهُ يَوْمَئِذٍ فَقَدْ رَحِمَهُ ۚ وَذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْمُبِينُ ﴿١٦

16. Atakayeepushwa nayo (adhabu) Siku hiyo, basi kwa yakini (Allaah) Amemrehemu. Na huko ndiko kufuzu kulio wazi.

 

 

 

 

وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّـهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِن يَمْسَسْكَ بِخَيْرٍ فَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٧

17. Na Allaah Akikugusisha kwa dhara, basi hakuna yeyote wa kuiondoa isipokuwa Yeye, na Akikugusisha kheri, basi Yeye juu ya kila kitu Ni Muweza.

 

 

 

 

وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ ﴿١٨

18. Naye Ndiye Aliyedhibiti vyote chini ya Mamlaka Yake Aliye juu ya Waja Wake. Naye Ndiye Mwenye Hikmah wa yote, Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.

 

 

 

قُلْ أَيُّ شَيْءٍ أَكْبَرُ شَهَادَةً ۖ قُلِ اللَّـهُ ۖ شَهِيدٌ بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ ۚ وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَـٰذَا الْقُرْآنُ لِأُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ ۚ أَئِنَّكُمْ لَتَشْهَدُونَ أَنَّ مَعَ اللَّـهِ آلِهَةً أُخْرَىٰ ۚ قُل لَّا أَشْهَدُ ۚ قُلْ إِنَّمَا هُوَ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ وَإِنَّنِي بَرِيءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ ﴿١٩

19. Sema: Kitu gani ushahidi wake ndio mkubwa zaidi? Sema: Allaah. Yeye Ni Shahidi baina yangu na baina yenu. Na nimefunuliwa Wahy hii Qur-aan ili nikuonyeni kwayo na kila itakayemfikia. Je, hivi kweli nyinyi mnashuhudia kwamba wako waabudiwa wengine pamoja na Allaah? Sema: Mimi sishuhudii (hayo). Sema: Hakika Yeye Ni Mwabudiwa wa haki Mmoja (Pekee), na hakika mimi sihusiki na mnavyomshirikisha navyo.

 

 

 

 

الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْرِفُونَهُ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَاءَهُمُ ۘ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٢٠

20. Wale Tuliowapa Kitabu wanamjua (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)  au wanaijua Tawhiyd) kama wanavyowajua watoto wao. Wale ambao wamekhasiri nafsi zao basi wao hawaamini.

 

 

 

 

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ ۗ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ ﴿٢١

21. Na nani mdhalimu zaidi kuliko yule anayemtungia Allaah uongo au anayekadhibisha Aayaat (na Ishara, Dalili bayana) Zake? Hakika madhalimu hawatofaulu.

 

 

 

 

وَيَوْمَ نَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشْرَكُوا أَيْنَ شُرَكَاؤُكُمُ الَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ﴿٢٢

22. Na Siku Tutakayowakusanya wote pamoja, kisha Tutawaambia wale walioshirikisha: Wako wapi washirika wenu ambao mlikuwa mnadai (kuwa waungu wawaombeeni)?

 

 

 

ثُمَّ لَمْ تَكُن فِتْنَتُهُمْ إِلَّا أَن قَالُوا وَاللَّـهِ رَبِّنَا مَا كُنَّا مُشْرِكِينَ ﴿٢٣

23. Kisha haitokuwa hoja yao ya kujitetea isipokuwa kusema: Wa-Allaahi Rabb wetu! Hatukuwa washirikina.

 

 

 

انظُرْ كَيْفَ كَذَبُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ ۚ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٢٤

24. Tazama vipi walivyojiongopea wenyewe na yamewapotea yale waliyokuwa wakiyatunga (ya uongo).

 

 

 

وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُ إِلَيْكَ ۖ وَجَعَلْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَن يَفْقَهُوهُ وَفِي آذَانِهِمْ وَقْرًا ۚ وَإِن يَرَوْا كُلَّ آيَةٍ لَّا يُؤْمِنُوا بِهَا ۚ حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوكَ يُجَادِلُونَكَ يَقُولُ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ ﴿٢٥﴾

25. Na wako miongoni mwao wanaotega sikio kukusikiliza. Nasi Tumeweka vifuniko kwenye nyoyo zao wasipate kuyafahamu na katika masikio yao uziwi.[4] Na wanapoona Aayah (Ishara, Ushahidi, Dalili) yoyote (ya kuthibitisha ukweli wako) hawaiamini. Hata wanapokujia kukubishia husema wale waliokufuru: Hizi si chochote ila ni hekaya za watu wa kale.

 

 

 

 

وَهُمْ يَنْهَوْنَ عَنْهُ وَيَنْأَوْنَ عَنْهُ ۖ وَإِن يُهْلِكُونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿٢٦

26. Wao wanazuia asifuatwe, na wenyewe wanajiweka mbali naye. Lakini hawaangamizi isipokuwa nafsi zao wala hawahisi. 

 

 

 

 

وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ وُقِفُوا عَلَى النَّارِ فَقَالُوا يَا لَيْتَنَا نُرَدُّ وَلَا نُكَذِّبَ بِآيَاتِ رَبِّنَا وَنَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢٧

27. Na lau ungeliona watakaposimamishwa kwenye moto kisha wakasema: Laiti tungelirudishwa (duniani) na wala hatutakadhibisha Aayaat (na Ishara) za Rabb wetu, na tutakuwa miongoni mwa waumini!

 

 

 

 

بَلْ بَدَا لَهُم مَّا كَانُوا يُخْفُونَ مِن قَبْلُ ۖ وَلَوْ رُدُّوا لَعَادُوا لِمَا نُهُوا عَنْهُ وَإِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ ﴿٢٨

28. Bali yamewadhihirikia yale waliyokuwa wakiyaficha kabla. Na lau wangelirudishwa, kwa yakini wangeyarudia yale waliyokatazwa, na hakika wao ni waongo!

 

 

 

وَقَالُوا إِنْ هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا وَمَا نَحْنُ بِمَبْعُوثِينَ ﴿٢٩

29. Na walisema: Haya si chochote isipokuwa ni uhai wetu wa dunia tu, na wala sisi hatutofufuliwa.[5]

 

 

 

وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ وُقِفُوا عَلَىٰ رَبِّهِمْ ۚ قَالَ أَلَيْسَ هَـٰذَا بِالْحَقِّ ۚ قَالُوا بَلَىٰ وَرَبِّنَا ۚ قَالَ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ ﴿٣٠

30. Na lau ungeliona watakaposimamishwa mbele ya Rabb wao. Atasema:  Je, haya si ya kweli? Watasema: Ndio (kweli kabisa), tunaapa kwa Rabb wetu! Atasema: Basi onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkikufuru.

 

 

 

 

قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِلِقَاءِ اللَّـهِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا جَاءَتْهُمُ السَّاعَةُ بَغْتَةً قَالُوا يَا حَسْرَتَنَا عَلَىٰ مَا فَرَّطْنَا فِيهَا وَهُمْ يَحْمِلُونَ أَوْزَارَهُمْ عَلَىٰ ظُهُورِهِمْ ۚ أَلَا سَاءَ مَا يَزِرُونَ ﴿٣١

31. Kwa yakini wamekhasirika wale waliokadhibisha kukutana na Allaah. Hata itakapowajia Saa (mauti) kwa ghafla watasema: Ee majuto yetu kwa yale tuliyokusuru humo! Na ilhali wao wanabeba mizigo yao (ya dhambi) migongoni mwao. Tanabahi!  Uovu ulioje wanayobeba!

 

 

 

 

وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا لَعِبٌ وَلَهْوٌ ۖ وَلَلدَّارُ الْآخِرَةُ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٣٢

32. Na uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni mchezo na pumbao. Na bila shaka nyumba ya Aakhirah ni bora zaidi kwa wenye taqwa. Je, basi hamtii akilini?

 

 

 

 

قَدْ نَعْلَمُ إِنَّهُ لَيَحْزُنُكَ الَّذِي يَقُولُونَ ۖ فَإِنَّهُمْ لَا يُكَذِّبُونَكَ وَلَـٰكِنَّ الظَّالِمِينَ بِآيَاتِ اللَّـهِ يَجْحَدُونَ ﴿٣٣

33. Kwa yakini Tunajua (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba yanakuhuzunisha yale wanayoyasema. Basi hakika wao hawakukadhibishi wewe (kwa vile wanakujua ni mkweli) lakini wanachokanusha madhalimu ni Aayaat (na Ishara) za Allaah.

 

 

 

 

وَلَقَدْ كُذِّبَتْ رُسُلٌ مِّن قَبْلِكَ فَصَبَرُوا عَلَىٰ مَا كُذِّبُوا وَأُوذُوا حَتَّىٰ أَتَاهُمْ نَصْرُنَا ۚ وَلَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِ اللَّـهِ ۚ وَلَقَدْ جَاءَكَ مِن نَّبَإِ الْمُرْسَلِينَ ﴿٣٤

34. Na kwa yakini walikadhibishwa Rusuli kabla yako, na wao walivuta subira kwa kukadhibishwa huko, na waliudhiwa na kusumbuliwa mpaka ilipowafikia Nusura Yetu. Na hakuna yeyote awezaye kubadilisha Maneno ya Allaah. Zimekwishakujia khabari za Rusuli (waliopita kukuliwaza).

 

 

 

 

وَإِن كَانَ كَبُرَ عَلَيْكَ إِعْرَاضُهُمْ فَإِنِ اسْتَطَعْتَ أَن تَبْتَغِيَ نَفَقًا فِي الْأَرْضِ أَوْ سُلَّمًا فِي السَّمَاءِ فَتَأْتِيَهُم بِآيَةٍ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَجَمَعَهُمْ عَلَى الْهُدَىٰ ۚ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْجَاهِلِينَ ﴿٣٥

35. Na kama kukengeuka kwao kumekuwa ni mashaka mno kwako, basi ukiweza kutafuta njia ya chini kwa chini katika ardhi au ngazi kwendea mbinguni ili uwaletee Aayah (Ishara, Dalili) yoyote (basi fanya). Na kama Allaah Angetaka Angeliwakusanya katika hidaaya. Basi chunga usiwe miongoni mwa majahili.

 

 

 

إِنَّمَا يَسْتَجِيبُ الَّذِينَ يَسْمَعُونَ ۘ وَالْمَوْتَىٰ يَبْعَثُهُمُ اللَّـهُ ثُمَّ إِلَيْهِ يُرْجَعُونَ ﴿٣٦

36. Hakika wanaitikia wale wanaosikia (kwa nyoyo za imaan). Ama wafu (wa nyoyo) Allaah Atawafufua, kisha Kwake watarejeshwa.

 

 

 

 

وَقَالُوا لَوْلَا نُزِّلَ عَلَيْهِ آيَةٌ مِّن رَّبِّهِ ۚ قُلْ إِنَّ اللَّـهَ قَادِرٌ عَلَىٰ أَن يُنَزِّلَ آيَةً وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٣٧

37.  Na walisema: Kwa nini hakuteremshiwa Aayah (Muujiza) kutoka kwa Rabb wake? Sema: Hakika Allaah Ni Muweza wa Kuteremsha Aayah (Muujiza) lakini wengi wao hawajui. 

 

 

 

 

وَمَا مِن دَابَّةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا طَائِرٍ يَطِيرُ بِجَنَاحَيْهِ إِلَّا أُمَمٌ أَمْثَالُكُم ۚ مَّا فَرَّطْنَا فِي الْكِتَابِ مِن شَيْءٍ ۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِمْ يُحْشَرُونَ ﴿٣٨

38. Na hakuna kiumbe chochote kinachotembea katika ardhi wala ndege anayeruka kwa mbawa zake mbili, isipokuwa ni nyumati mfano wenu. Hatujaacha wala kusahau chochote katika Kitabu[6]. Kisha watakusanywa kwa Rabb wao.

 

 

 

 

وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا صُمٌّ وَبُكْمٌ فِي الظُّلُمَاتِ ۗ مَن يَشَإِ اللَّـهُ يُضْلِلْـهُ وَمَن يَشَأْ يَجْعَلْهُ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٣٩

39. Na wale waliokadhibisha Aayaat (na Ishara, Dalili) Zetu ni viziwi na mabubu waliozama ndani ya viza. Allaah Humpotoa Amtakaye na Humweka Amtakaye juu ya njia iliyonyooka. 

 

 

 

 

قُلْ أَرَأَيْتَكُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُ اللَّـهِ أَوْ أَتَتْكُمُ السَّاعَةُ أَغَيْرَ اللَّـهِ تَدْعُونَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٤٠

40. Sema: Je, mnaonaje ikikufikieni adhabu ya Allaah au ikakufikieni Saa (Qiyaamah), je, mtamwomba ghairi ya Allaah? (Jibuni) mkiwa ni wakweli!

 

 

 

 

بَلْ إِيَّاهُ تَدْعُونَ فَيَكْشِفُ مَا تَدْعُونَ إِلَيْهِ إِن شَاءَ وَتَنسَوْنَ مَا تُشْرِكُونَ ﴿٤١

41. Bali Yeye Pekee Ndiye mtayemwomba, kisha Akitaka Ataondoa yale (ya dhiki) mliyomwomba na mtasahau mnayoyashirikisha (pamoja Naye).

 

 

 

 

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا إِلَىٰ أُمَمٍ مِّن قَبْلِكَ فَأَخَذْنَاهُم بِالْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ لَعَلَّهُمْ يَتَضَرَّعُونَ ﴿٤٢

42. Na kwa yakini Tulipeleka (Rusuli) kwa nyumati nyingi kabla yako, Tukawatia katika dhiki za ufukara na madhara ya magonjwa na misiba ili wapate kunyenyekea.

 

 

 

 فَلَوْلَا إِذْ جَاءَهُم بَأْسُنَا تَضَرَّعُوا وَلَـٰكِن قَسَتْ قُلُوبُهُمْ وَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٤٣

43. Basi kwa nini ilipowafikia adhabu Yetu wasinyenyekee? Lakini nyoyo zao zimekuwa ngumu na shaytwaan akawapambia yale waliyokuwa wakiyatenda.

 

 

 

فَلَمَّا نَسُوا مَا ذُكِّرُوا بِهِ فَتَحْنَا عَلَيْهِمْ أَبْوَابَ كُلِّ شَيْءٍ حَتَّىٰ إِذَا فَرِحُوا بِمَا أُوتُوا أَخَذْنَاهُم بَغْتَةً فَإِذَا هُم مُّبْلِسُونَ ﴿٤٤

44. Waliposahau yale waliyokumbushwa, Tuliwafungulia milango ya (neema za) kila kitu, mpaka walipofurahia kwa yale waliyopewa, Tukawachukua ghafla (kuwaadhibu), basi tahamaki wakawa wenye kukata tamaa.

 

 

 

 

فَقُطِعَ دَابِرُ الْقَوْمِ الَّذِينَ ظَلَمُوا ۚ وَالْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٤٥

45. Basi ikakatwa mizizi ya watu waliodhulumu, na AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah) Rabb wa walimwengu.

 

 

 

قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَخَذَ اللَّـهُ سَمْعَكُمْ وَأَبْصَارَكُمْ وَخَتَمَ عَلَىٰ قُلُوبِكُم مَّنْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ اللَّـهِ يَأْتِيكُم بِهِ ۗ انظُرْ كَيْفَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ ثُمَّ هُمْ يَصْدِفُونَ ﴿٤٦

46. Sema: Mnaonaje ikiwa Allaah Atakuondoleeni kusikia kwenu (mkawa viziwi) na kuona kwenu (mkawa vipofu) na Akapiga mhuri juu ya nyoyo zenu (mkawa hamufahamu), je, ni mwabudiwa wa haki yupi ghairi ya Allaah Atakuleteeni hayo? Tazama jinsi Tunavyosarifu Aayaat (Hoja, Dalili) namna kwa namna kisha wao wanakengeuka.

 

 

 

قُلْ أَرَأَيْتَكُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُ اللَّـهِ بَغْتَةً أَوْ جَهْرَةً هَلْ يُهْلَكُ إِلَّا الْقَوْمُ الظَّالِمُونَ ﴿٤٧

47. Sema: Mnaonaje ikikufikieni Adhabu ya Allaah ghafla au kwa kuiona inavyokujieni? Je, wataangamizwa isipokuwa watu madhalimu?  

 

 

 

 

وَمَا نُرْسِلُ الْمُرْسَلِينَ إِلَّا مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ ۖ فَمَنْ آمَنَ وَأَصْلَحَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٤٨

48. Na Hatupeleki Rusuli isipokuwa kuwa wabashiriaji na waonyaji tu. Na yeyote atakayeamini na akatengeneza (imaan yake na vitendo vyake), basi haitokuwa khofu juu yao na wala wao hawatohuzunika.

 

 

 

وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا يَمَسُّهُمُ الْعَذَابُ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴿٤٩

49. Na wale waliokadhibisha Aayaat (na Miujiza, Ishara) Zetu, itawagusa adhabu kwa sababu ya ufasiki waliokuwa wanaufanya.

 

 

 

قُل لَّا أَقُولُ لَكُمْ عِندِي خَزَائِنُ اللَّـهِ وَلَا أَعْلَمُ الْغَيْبَ وَلَا أَقُولُ لَكُمْ إِنِّي مَلَكٌ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ ۚ قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الْأَعْمَىٰ وَالْبَصِيرُ ۚ أَفَلَا تَتَفَكَّرُونَ ﴿٥٠

50. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Sikuambieni kuwa mimi nina hazina ya Allaah, na wala kwamba najua ya ghaibu, na wala sikuambieni kuwa mimi ni Malaika. Sifuati ila yale niliyofunuliwa Wahy. Sema: Je, analingana sawasawa kipofu na mwenye kuona?  Basi hamtafakari?

 

 

 

 

وَأَنذِرْ بِهِ الَّذِينَ يَخَافُونَ أَن يُحْشَرُوا إِلَىٰ رَبِّهِمْ ۙ لَيْسَ لَهُم مِّن دُونِهِ وَلِيٌّ وَلَا شَفِيعٌ لَّعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿٥١

51. Na waonye kwayo (Qur-aan) wale wanaokhofu ya kwamba watakusanywa kwa Rabb wao, na hali ya kuwa hawana rafiki mlinzi wala mwombezi isipokuwa Yeye ili wapate kumcha Allaah (zaidi).

 

 

 

وَلَا تَطْرُدِ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ مَا عَلَيْكَ مِنْ حِسَابِهِم مِّن شَيْءٍ وَمَا مِنْ حِسَابِكَ عَلَيْهِم مِّن شَيْءٍ فَتَطْرُدَهُمْ فَتَكُونَ مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٥٢

52. Na wala usiwafukuze wale wanaomwomba Rabb wao asubuhi na jioni wanataka Wajihi Wake. Si juu yako hisabu yao hata kidogo, na wala hisabu yako si juu yao hata kidogo, hata uwafukuze ukaja kuwa miongoni mwa madhalimu. 

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ فَتَنَّا بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لِّيَقُولُوا أَهَـٰؤُلَاءِ مَنَّ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّن بَيْنِنَا ۗ أَلَيْسَ اللَّـهُ بِأَعْلَمَ بِالشَّاكِرِينَ ﴿٥٣

53. Na hivyo ndivyo Tulivyowafanyia mtihani baadhi yao kwa baadhi ili waseme: Je, hawa ndio wale Aliowafadhilisha Allaah baina yetu? Je, kwani Allaah Hajui wanaoshukuru?

 

 

 

وَإِذَا جَاءَكَ الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِنَا فَقُلْ سَلَامٌ عَلَيْكُمْ ۖ كَتَبَ رَبُّكُمْ عَلَىٰ نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ ۖ أَنَّهُ مَنْ عَمِلَ مِنكُمْ سُوءًا بِجَهَالَةٍ ثُمَّ تَابَ مِن بَعْدِهِ وَأَصْلَحَ فَأَنَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٥٤

54. Na wanapokujia wale wanaoamini Aayaat (na Ishara) Zetu basi sema: Salaamun ‘alaykum! (Amani iwe juu yenu). Rabb wenu Amejiwajibishia Nafsi Yake[7] Rahmah; kwamba yeyote miongoni mwenu atakayetenda ovu kwa ujahili, kisha akatubia baada yake na akarekebisha (matendo yake), basi hakika Yeye Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ وَلِتَسْتَبِينَ سَبِيلُ الْمُجْرِمِينَ ﴿٥٥

55. Na hivyo ndivyo Tunavyofasili waziwazi Aayaat (na Ishara) na ili idhihirike njia ya wahalifu.

 

 

 

قُلْ إِنِّي نُهِيتُ أَنْ أَعْبُدَ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ ۚ قُل لَّا أَتَّبِعُ أَهْوَاءَكُمْ ۙ قَدْ ضَلَلْتُ إِذًا وَمَا أَنَا مِنَ الْمُهْتَدِينَ ﴿٥٦

56. Sema: Hakika mimi nimekatazwa kuabudu wale mnaowaomba badala ya Allaah. Sema: Sifuati hawaa zenu (kwani nikifuata,) kwa yakini nitakuwa nimepotoka, na hapo nami sitokuwa miongoni mwa waliohidika.

 

 

 

قُلْ إِنِّي عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَكَذَّبْتُم بِهِ ۚ مَا عِندِي مَا تَسْتَعْجِلُونَ بِهِ ۚ إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّـهِ ۖ يَقُصُّ الْحَقَّ ۖ وَهُوَ خَيْرُ الْفَاصِلِينَ ﴿٥٧

57. Sema: Hakika mimi niko juu ya hoja bayana kutoka kwa Rabb wangu nanyi mumeikadhibisha. Sina yale mnayoyahimiza. Hakuna hukumu isipokuwa ya Allaah Pekee. Anasimulia ya haki, Naye Ni Mbora wa Kuhukumu kuliko wote wenye kuhukumu.

 

 

 

قُل لَّوْ أَنَّ عِندِي مَا تَسْتَعْجِلُونَ بِهِ لَقُضِيَ الْأَمْرُ بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِالظَّالِمِينَ ﴿٥٨

58. Sema: Lau ningelikuwa ninayo yale mnayoyaharakiza, basi bila shaka lingehukumiwa jambo baina yangu na baina yenu. Na Allaah Anawajua zaidi madhalimu.

 

 

 

وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ ۚ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۚ وَمَا تَسْقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعْلَمُهَا وَلَا حَبَّةٍ فِي ظُلُمَاتِ الْأَرْضِ وَلَا رَطْبٍ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿٥٩

59. Na Kwake (Allaah) zipo funguo za ghaibu, hakuna azijuaye ila Yeye tu.[8] Na Anajua yale yote yaliyomo barani na baharini. Na halianguki jani lolote ila Hulijua, wala punje katika viza vya ardhi, wala kinyevu na kikavu isipokuwa kimo katika Kitabu kinachobainisha wazi.[9]

 

 

 

وَهُوَ الَّذِي يَتَوَفَّاكُم بِاللَّيْلِ وَيَعْلَمُ مَا جَرَحْتُم بِالنَّهَارِ ثُمَّ يَبْعَثُكُمْ فِيهِ لِيُقْضَىٰ أَجَلٌ مُّسَمًّى ۖ ثُمَّ إِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ ثُمَّ يُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٦٠

60. Naye Ndiye Anayekufisheni usiku (mnapolala)[10] na Anajua yale yote mnayoyafanya mchana, kisha Anakufufueni humo ili utimizwe muda maalumu uliokadariwa. Kisha Kwake Pekee ni marejeo yenu, kisha Atakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda.

 

 

 

وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ ۖ وَيُرْسِلُ عَلَيْكُمْ حَفَظَةً حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ تَوَفَّتْهُ رُسُلُنَا وَهُمْ لَا يُفَرِّطُونَ ﴿٦١

61. Naye Ndiye Aliyedhibiti vyote chini ya Mamlaka Yake, Aliye juu ya Waja Wake.  Na Anakutumieni Malaika wachungaji wadhibiti, hata yanapomfikia mmoja wenu mauti, Wajumbe Wetu humfisha, nao hawafanyi taksiri.

 

    

 

ثُمَّ رُدُّوا إِلَى اللَّـهِ مَوْلَاهُمُ الْحَقِّ ۚ أَلَا لَهُ الْحُكْمُ وَهُوَ أَسْرَعُ الْحَاسِبِينَ ﴿٦٢

62. Kisha watarudishwa (wote waliofishwa) kwa Allaah Rabb wao wa haki. Tanabahi! Hukumu ni Yake Pekee! Naye Ni Mwepesi zaidi wa Kuhisabu kuliko wote wanaohisabu.

 

 

 

قُلْ مَن يُنَجِّيكُم مِّن ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ تَدْعُونَهُ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً لَّئِنْ أَنجَانَا مِنْ هَـٰذِهِ لَنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ ﴿٦٣

63. Sema: Nani Anakuokoeni katika viza vya bara na bahari mnapomuomba kwa kunyenyekea na kwa siri (mkisema): Akituokoa kutokana na (janga) hili, bila shaka tutakuwa miongoni mwa wenye kushukuru.

 

 

 

قُلِ اللَّـهُ يُنَجِّيكُم مِّنْهَا وَمِن كُلِّ كَرْبٍ ثُمَّ أَنتُمْ تُشْرِكُونَ ﴿٦٤

64. Sema: Allaah Anakuokoeni kutokana na hayo na katika kila janga kisha nyinyi mnamshirikisha.

 

 

 

قُلْ هُوَ الْقَادِرُ عَلَىٰ أَن يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عَذَابًا مِّن فَوْقِكُمْ أَوْ مِن تَحْتِ أَرْجُلِكُمْ أَوْ يَلْبِسَكُمْ شِيَعًا وَيُذِيقَ بَعْضَكُم بَأْسَ بَعْضٍ ۗ انظُرْ كَيْفَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ لَعَلَّهُمْ يَفْقَهُونَ ﴿٦٥

65. Sema: Yeye ni Muweza wa kukuleteeni adhabu kutoka juu yenu, au kutoka chini ya miguu yenu, au Akutatanisheni mfarikiane kuwa makundi na Akuonjesheni baadhi yenu (vurugu la) nguvu za wengineo. Tazama jinsi Tunavyosarifu Aayaat (Ishara, Hoja, Dalili) namna kwa namna wapate kufahamu.

 

 

 

وَكَذَّبَ بِهِ قَوْمُكَ وَهُوَ الْحَقُّ ۚ قُل لَّسْتُ عَلَيْكُم بِوَكِيلٍ ﴿٦٦

66. Na watu wako wameikadhibisha (Qur-aan) nayo ni haki. Sema: Mimi si mdhamini wenu.

 

 

 

 

لِّكُلِّ نَبَإٍ مُّسْتَقَرٌّ ۚ وَسَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿٦٧

67. Kila khabari ina wakati maalumu, na mtakuja kujua.

 

 

 

 

وَإِذَا رَأَيْتَ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ الشَّيْطَانُ فَلَا تَقْعُدْ بَعْدَ الذِّكْرَىٰ مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٦٨

68. Na unapowaona wale wanaoshughulika kuzisakama Aayaat Zetu, jitenge nao mpaka watumbukie kwenye mazungumzo mengineyo. Na kama shaytwaan akikusahaulisha, basi baada ya kukumbuka, usikae pamoja na watu madhalimu.

 

 

 

وَمَا عَلَى الَّذِينَ يَتَّقُونَ مِنْ حِسَابِهِم مِّن شَيْءٍ وَلَـٰكِن ذِكْرَىٰ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿٦٩

69. Wenye taqwa, hawana jukumu la hisabu yao (kwa Allaah), lakini jukumu ni kuwakumbusha ili wapate kujirudi. 

 

 

 

 

وَذَرِ الَّذِينَ اتَّخَذُوا دِينَهُمْ لَعِبًا وَلَهْوًا وَغَرَّتْهُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا ۚ وَذَكِّرْ بِهِ أَن تُبْسَلَ نَفْسٌ بِمَا كَسَبَتْ لَيْسَ لَهَا مِن دُونِ اللَّـهِ وَلِيٌّ وَلَا شَفِيعٌ وَإِن تَعْدِلْ كُلَّ عَدْلٍ لَّا يُؤْخَذْ مِنْهَا ۗ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ أُبْسِلُوا بِمَا كَسَبُوا ۖ لَهُمْ شَرَابٌ مِّنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ ﴿٧٠

70. Na waachilie mbali wale walioifanya Dini yao mchezo na pumbao, na ukawaghuri uhai wa dunia. Basi wakumbushe kwayo (Qur-aan) isije kila nafsi ikaangamizwa kwa yale iliyoyachuma. Haina pasi na Allaah rafiki mlinzi wala mwombezi. Na hata ikitoa fidia ya kila aina haitopokelewa. Hao ndio wale walioangamizwa kwa sababu ya yale waliyoyachuma. Watapata kinywaji cha maji ya kutokota na adhabu iumizayo kwa sababu ya ukafiri wao.

 

 

 

قُلْ أَنَدْعُو مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُنَا وَلَا يَضُرُّنَا وَنُرَدُّ عَلَىٰ أَعْقَابِنَا بَعْدَ إِذْ هَدَانَا اللَّـهُ كَالَّذِي اسْتَهْوَتْهُ الشَّيَاطِينُ فِي الْأَرْضِ حَيْرَانَ لَهُ أَصْحَابٌ يَدْعُونَهُ إِلَى الْهُدَى ائْتِنَا ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّـهِ هُوَ الْهُدَىٰ ۖ وَأُمِرْنَا لِنُسْلِمَ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٧١

71. Sema: Je, badala ya Allaah tuviombe visivyoweza kutunufaisha wala kutudhuru tuje kurudishwa nyuma tulikotoka baada ya Allaah kutuhidi? Tuwe kama yule ambaye ameshawishiwa na mashaytwaan akikanganyika katika ardhi, anao marafiki wanamwita katika mwongozo:  Njoo kwetu!  Sema: Hakika Hidaya ya Allaah ndio Hidaya na tumeamrishwa tujisalimishe kwa Rabb wa walimwengu.

 

 

 

وَأَنْ أَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَاتَّقُوهُ ۚ وَهُوَ الَّذِي إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٧٢

72. Na kuwa simamisheni Swalaah na mcheni Yeye, Naye Ndiye Ambaye Kwake mtakusanywa.

 

 

 

وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۖ وَيَوْمَ يَقُولُ كُن فَيَكُونُ ۚ قَوْلُهُ الْحَقُّ ۚ وَلَهُ الْمُلْكُ يَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ ۚ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ ﴿٧٣

73. Naye Ndiye Ambaye Ameumba mbingu na ardhi kwa haki. Na Siku Atakaposema: Kun! Basi (jambo) huwa! Kauli Yake ni haki. Ni Wake Yeye tu ufalme Siku litakapopulizwa baragumu. Mjuzi wa ghaibu na dhahiri. Naye Ni Mwenye Hikmah wa yote, Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.

 

 

 

وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ آزَرَ أَتَتَّخِذُ أَصْنَامًا آلِهَةً ۖ إِنِّي أَرَاكَ وَقَوْمَكَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٧٤

74. Na pindi Ibraahiym alipomwambia baba yake Aazar: Je, unafanya masanamu kuwa ni waabudiwa? Hakika mimi nakuona wewe pamoja na watu wako katika upotofu bayana.

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ نُرِي إِبْرَاهِيمَ مَلَكُوتَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلِيَكُونَ مِنَ الْمُوقِنِينَ ﴿٧٥

75. Na hivyo ndivyo Tunavyomwonyesha Ibraahiym ufalme mkubwa wa mbingu na ardhi na ili awe miongoni mwa wenye yakini.

 

 

 

فَلَمَّا جَنَّ عَلَيْهِ اللَّيْلُ رَأَىٰ كَوْكَبًا ۖ قَالَ هَـٰذَا رَبِّي ۖ فَلَمَّا أَفَلَ قَالَ لَا أُحِبُّ الْآفِلِينَ ﴿٧٦

76. Na ulipomwingilia usiku akaona nyota. Akasema: Huyu ni Rabb wangu. Ilipotoweka akasema: Hakika mimi sipendi wanaotoweka. 

 

 

 

فَلَمَّا رَأَى الْقَمَرَ بَازِغًا قَالَ هَـٰذَا رَبِّي ۖ فَلَمَّا أَفَلَ قَالَ لَئِن لَّمْ يَهْدِنِي رَبِّي لَأَكُونَنَّ مِنَ الْقَوْمِ الضَّالِّينَ ﴿٧٧

77. Kisha alipoona mwezi umechomoza akasema: Huyu ni Rabb wangu. Ulipotoweka akasema: Asiponiongoza Rabb wangu bila shaka nitakuwa miongoni mwa watu waliopotea.

 

 

 

فَلَمَّا رَأَى الشَّمْسَ بَازِغَةً قَالَ هَـٰذَا رَبِّي هَـٰذَا أَكْبَرُ ۖ فَلَمَّا أَفَلَتْ قَالَ يَا قَوْمِ إِنِّي بَرِيءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ ﴿٧٨

78.  Kisha alipoliona jua limechomoza akasema: Huyu ni Rabb wangu, huyu ni mkubwa zaidi. Lilipotoweka akasema: Enyi watu wangu! Hakika mimi simo katika yale mnayoyashirikisha (na Allaah).

 

 

 

إِنِّي وَجَّهْتُ وَجْهِيَ لِلَّذِي فَطَرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ حَنِيفًا ۖ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٧٩

79. Hakika mimi nimeelekeza uso wangu kwa Ambaye Ameanzisha mbingu na ardhi, nikijitenga na itikadi potofu na kuelemea haki, nami si katika washirikina.

 

 

 

وَحَاجَّهُ قَوْمُهُ ۚ قَالَ أَتُحَاجُّونِّي فِي اللَّـهِ وَقَدْ هَدَانِ ۚ وَلَا أَخَافُ مَا تُشْرِكُونَ بِهِ إِلَّا أَن يَشَاءَ رَبِّي شَيْئًا ۗ وَسِعَ رَبِّي كُلَّ شَيْءٍ عِلْمًا ۗ أَفَلَا تَتَذَكَّرُونَ ﴿٨٠

80. Na watu wake wakamhoji. Akasema: Je, mnahojiana nami kuhusu Allaah na hali Amenihidi?  Na wala sikhofu hayo mnayomshirikisha Naye (kwani sitodhurika) isipokuwa Rabb wangu Akitaka jambo. Rabb wangu Amezunguka kila kitu (kwa Ujuzi).  Je, basi hamkumbuki?

 

 

 

وَكَيْفَ أَخَافُ مَا أَشْرَكْتُمْ وَلَا تَخَافُونَ أَنَّكُمْ أَشْرَكْتُم بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ عَلَيْكُمْ سُلْطَانًا ۚ فَأَيُّ الْفَرِيقَيْنِ أَحَقُّ بِالْأَمْنِ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٨١

81. Na vipi nikhofu yale mnayoyashirikisha, nanyi hamkhofu kwamba mnamshirikisha Allaah na ambayo Hakuyateremshia kwenu hoja. Je, basi kundi gani kati ya mawili linastahiki zaidi kuwa katika amani kama nyinyi mnajua?

 

 

 

الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ أُولَـٰئِكَ لَهُمُ الْأَمْنُ وَهُم مُّهْتَدُونَ ﴿٨٢

82. Wale walioamini na hawakuchanganya imaan zao na dhulma,[11] hao ndio watakaopata amani nao ndio waliohidika.

 

 

 

وَتِلْكَ حُجَّتُنَا آتَيْنَاهَا إِبْرَاهِيمَ عَلَىٰ قَوْمِهِ ۚ نَرْفَعُ دَرَجَاتٍ مَّن نَّشَاءُ ۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ ﴿٨٣

83. Na hiyo ndio hoja Yetu Tuliyompa Ibraahiym juu ya watu wake.  Tunampandisha cheo Tumtakaye. Hakika Rabb wako Ni Mwenye Hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.[12]

 

 

 

وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ ۚ كُلًّا هَدَيْنَا ۚ وَنُوحًا هَدَيْنَا مِن قَبْلُ ۖ وَمِن ذُرِّيَّتِهِ دَاوُودَ وَسُلَيْمَانَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ وَمُوسَىٰ وَهَارُونَ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿٨٤

84. Na Tukamtunukia Is-haaq na Ya’quwb. Wote Tukawahidi. Na Nuwh Tulimhidi kabla. Na katika dhuria wake (Tuliwahidi pia) Daawuwd, na Sulaymaan, na Ayyuwb, na Yuwsuf, na Muwsaa, na Haaruwn. Na hivyo ndivyo Tulipavyo wafanyao ihsaan.

 

 

 

وَزَكَرِيَّا وَيَحْيَىٰ وَعِيسَىٰ وَإِلْيَاسَ ۖ كُلٌّ مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿٨٥

85. Na Zakariyyaa, na Yahyaa, na ‘Iysaa, na Ilyaas. Wote ni miongoni mwa Swalihina.

 

 

 

وَإِسْمَاعِيلَ وَالْيَسَعَ وَيُونُسَ وَلُوطًا ۚ وَكُلًّا فَضَّلْنَا عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٨٦

86. Na Ismaa’iyl, na Al-Yasa’a na Yuwnus, na Luutw. Na wote Tuliwafadhilisha juu ya walimwengu.

 

 

 

 

وَمِنْ آبَائِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ وَإِخْوَانِهِمْ ۖ وَاجْتَبَيْنَاهُمْ وَهَدَيْنَاهُمْ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٨٧

87. Na katika baba zao, na dhuriya wao, na ndugu zao. Na Tukawateua na Tukawaongoza kuelekea njia iliyonyooka.

 

 

 

 

 

ذَٰلِكَ هُدَى اللَّـهِ يَهْدِي بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۚ وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٨٨

88. Hiyo ndiyo Hidaya ya Allaah, Humwongoza kwayo Amtakaye kati ya Waja Wake. Na kama wangemshirikisha basi yangeporomoka yale waliyokuwa wakiyatenda.[13]

 

 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ ۚ فَإِن يَكْفُرْ بِهَا هَـٰؤُلَاءِ فَقَدْ وَكَّلْنَا بِهَا قَوْمًا لَّيْسُوا بِهَا بِكَافِرِينَ ﴿٨٩

89. Hao ndio Tuliowapa Kitabu na Hikmah na Unabii. Wakiyakanusha hawa (makafiri), basi kwa yakini Tumekwishayawakilisha kwa watu wasioyakanusha.

 

 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ هَدَى اللَّـهُ ۖ فَبِهُدَاهُمُ اقْتَدِهْ ۗ قُل لَّا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا ۖ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْعَالَمِينَ ﴿٩٠

90. Hao ndio ambao Allaah Amewahidi. Basi fuata kama kigezo uongofu wao. Sema: Sikuombeni ujira kwa hayo. Hayakuwa haya ila ni ukumbusho kwa walimwengu.

 

 

 

وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ إِذْ قَالُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ عَلَىٰ بَشَرٍ مِّن شَيْءٍ ۗ قُلْ مَنْ أَنزَلَ الْكِتَابَ الَّذِي جَاءَ بِهِ مُوسَىٰ نُورًا وَهُدًى لِّلنَّاسِ ۖ تَجْعَلُونَهُ قَرَاطِيسَ تُبْدُونَهَا وَتُخْفُونَ كَثِيرًا ۖ وَعُلِّمْتُم مَّا لَمْ تَعْلَمُوا أَنتُمْ وَلَا آبَاؤُكُمْ ۖ قُلِ اللَّـهُ ۖ ثُمَّ ذَرْهُمْ فِي خَوْضِهِمْ يَلْعَبُونَ ﴿٩١

91. Na hawakumkadiria Allaah kama inavyostahiki kumkadiria, pale waliposema: Allaah Hakuteremsha chochote kwa mtu. Sema: Nani aliyeteremsha Kitabu ambacho amekuja nacho Muwsaa, (chenye) nuru na mwongozo kwa watu? Mnakifanya kurasa kurasa mkizifichua na mkificha mengi. Na mkafunzwa yale mliyokuwa hamuyajui nyinyi na baba zenu. Sema: Allaah (Ameiteremsha), kisha waachilie mbali katika shughuliko la porojo lao wakicheza.

 

 

 

وَهَـٰذَا كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ مُّصَدِّقُ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَلِتُنذِرَ أُمَّ الْقُرَىٰ وَمَنْ حَوْلَهَا ۚ وَالَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۖ وَهُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ ﴿٩٢

92. Na hiki ni Kitabu (Qur-aan) Tumekiteremsha chenye baraka kinachosadikisha yale yaliyokitangulia, na ili uonye (kwacho) Ummul-Quraa[14] (Mama wa miji [Makkah]), na wale ambao wameuzunguka. Na wale wanaoamini Aakhirah wanakiamini. Nao wanahifadhi Swalaah zao.

 

 

 

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ قَالَ أُوحِيَ إِلَيَّ وَلَمْ يُوحَ إِلَيْهِ شَيْءٌ وَمَن قَالَ سَأُنزِلُ مِثْلَ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ ۗ وَلَوْ تَرَىٰ إِذِ الظَّالِمُونَ فِي غَمَرَاتِ الْمَوْتِ وَالْمَلَائِكَةُ بَاسِطُو أَيْدِيهِمْ أَخْرِجُوا أَنفُسَكُمُ ۖ الْيَوْمَ تُجْزَوْنَ عَذَابَ الْهُونِ بِمَا كُنتُمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ غَيْرَ الْحَقِّ وَكُنتُمْ عَنْ آيَاتِهِ تَسْتَكْبِرُونَ ﴿٩٣

93. Na nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyemtungia uongo Allaah au akasema: Nimefunuliwa Wahy na hali hakufunuliwa Wahy wowote.   Na yule asemaye: Nitateremsha mfano wa yale Aliyoyateremsha Allaah.[15] Na lau ungeliona madhalimu pale wakiwa katika mateso makali ya mauti (ungeona jambo la kutisha mno), na Malaika wamenyosha mikono yao (wakiwaambia): Toeni nafsi zenu! Leo mnalipwa adhabu ya kudhalilisha kwa yale mliyokuwa mkiyasema juu ya Allaah pasi na haki, na mlikuwa mkitakabari msizifuate Aayaat Zake.

 

 

 

وَلَقَدْ جِئْتُمُونَا فُرَادَىٰ كَمَا خَلَقْنَاكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَتَرَكْتُم مَّا خَوَّلْنَاكُمْ وَرَاءَ ظُهُورِكُمْ ۖ وَمَا نَرَىٰ مَعَكُمْ شُفَعَاءَكُمُ الَّذِينَ زَعَمْتُمْ أَنَّهُمْ فِيكُمْ شُرَكَاءُ ۚ لَقَد تَّقَطَّعَ بَيْنَكُمْ وَضَلَّ عَنكُم مَّا كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ﴿٩٤

94. Na kwa yakini mmetujia mmoja mmoja kama Tulivyokuumbeni mara ya kwanza[16], na mmeyaacha nyuma yenu yote Tuliyokuruzukuni. Na Hatuwaoni pamoja nanyi waombezi wenu ambao mlidai kwamba wao ni washirika wenu. Kwa yakini yamekatika (mahusiano) baina yenu na yamekupoteeni mliyokuwa mkidai.

 

 

 

إِنَّ اللَّـهَ فَالِقُ الْحَبِّ وَالنَّوَىٰ ۖ يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَمُخْرِجُ الْمَيِّتِ مِنَ الْحَيِّ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ ﴿٩٥

95. Hakika Allaah Ni Mpasuaji wa mbegu na kokwa (zikawa miche). Anatoa kilicho hai kutokana na kilicho mfu, na Mtoaji wa kilicho mfu kutokana na kilicho hai.[17] Huyo Ndiye Allaah kwenu. Basi vipi mnaghilibiwa?

 

 

 

 

فَالِقُ الْإِصْبَاحِ وَجَعَلَ اللَّيْلَ سَكَنًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ حُسْبَانًا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ ﴿٩٦

96. Mpasuaji wa mapambazuko ya asubuhi, na Akajaalia usiku kuwa ni    mapumziko, na jua na mwezi kwenda kwa hisabu. Hiyo ndio Takdiri ya Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mjuzi wa yote.[18]

 

 

 

وَهُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ النُّجُومَ لِتَهْتَدُوا بِهَا فِي ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۗ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٩٧

97. Na Yeye Ndiye Aliyekufanyieni nyota ili zikusaidieni kujua mwendako katika viza vya bara na bahari.[19] Kwa yakini Tumezifasili waziwazi Aayaat (Ishara na vielelezo) kwa watu wanaojua.

 

 

 

وَهُوَ الَّذِي أَنشَأَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ فَمُسْتَقَرٌّ وَمُسْتَوْدَعٌ ۗ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَفْقَهُونَ ﴿٩٨

98. Na Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi moja, basi (pako) mahali pa kustakiri na pa kuhifadhiwa.[20] Kwa yakini Tumezifasili waziwazi Aayaat (Ishara, Hoja, Dalili) kwa watu wanaofahamu.

 

 

 

وَهُوَ الَّذِي أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجْنَا بِهِ نَبَاتَ كُلِّ شَيْءٍ فَأَخْرَجْنَا مِنْهُ خَضِرًا نُّخْرِجُ مِنْهُ حَبًّا مُّتَرَاكِبًا وَمِنَ النَّخْلِ مِن طَلْعِهَا قِنْوَانٌ دَانِيَةٌ وَجَنَّاتٍ مِّنْ أَعْنَابٍ وَالزَّيْتُونَ وَالرُّمَّانَ مُشْتَبِهًا وَغَيْرَ مُتَشَابِهٍ ۗ انظُرُوا إِلَىٰ ثَمَرِهِ إِذَا أَثْمَرَ وَيَنْعِهِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكُمْ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٩٩

99. Na Yeye Ndiye Ambaye Ameteremsha kutoka mbinguni maji, Tukatoa kwayo mimea ya kila kitu, na Tukatoa kutoka humo mimea ya kijani, Tunatoa kutoka humo punje zinazopandana. Na katika mitende, yanatoka katika makole yake mashada yenye kuning’inia chini kwa chini, na mabustani ya mizabibu na zaytuni, na makomamanga, yanayofanana na yasiyofanana. Tazameni matunda yake yanapozaa na kuiva kwake. Hakika katika hayo mna Aayaat (Ishara, Mazingatio) kwenu kwa watu wanaoamini.

 

 

 

وَجَعَلُوا لِلَّـهِ شُرَكَاءَ الْجِنَّ وَخَلَقَهُمْ ۖ وَخَرَقُوا لَهُ بَنِينَ وَبَنَاتٍ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿١٠٠

100. Na wakamfanyia Allaah majini kuwa ni washirika Wake ilhali Amewaumba. Na wakampachikia uongo bila ya ujuzi wowote kuwa Ana wana wa kiume na wa kike.[21] Utakasifu ni Wake na Ametukuka kwa ‘Uluwa kutokana na ambayo wanavumisha.

 

 

 

بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ وَلَدٌ وَلَمْ تَكُن لَّهُ صَاحِبَةٌ ۖ وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٠١

101. Mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Inamkinikaje kuwa Yeye Ana mwana ilhali Hana mke! Naye Ameumba kila kitu, Naye Ni Mjuzi wa kila kitu.

 

 

 

ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ فَاعْبُدُوهُ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ ﴿١٠٢

102. Huyo kwenu Ndiye Allaah, Rabb wenu. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye Muumbaji wa kila kitu, basi mwabuduni Yeye Pekee. Naye Ni Mtegemewa wa kila kitu.

 

 

 

 

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ ۖ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ ﴿١٠٣

103. Macho hayamzunguki bali Yeye Anayazunguka macho yote,[22] Naye Ni Mwenye Kudabiri mambo kwa Ulatifu, Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.

 

 

 

قَدْ جَاءَكُم بَصَائِرُ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَنْ أَبْصَرَ فَلِنَفْسِهِ ۖ وَمَنْ عَمِيَ فَعَلَيْهَا ۚ وَمَا أَنَا عَلَيْكُم بِحَفِيظٍ ﴿١٠٤

104. Kwa yakini zimekujieni hoja, ishara na dalili wazi kutoka kwa Rabb wenu. Atakayeona na kuzitambua, basi ni kwa faida yake mwenyewe, na atakayepofuka asizione basi hasara itamrudia mwenyewe, (sema) nami si msimamizi.

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ وَلِيَقُولُوا دَرَسْتَ وَلِنُبَيِّنَهُ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿١٠٥

105. Na hivyo ndivyo Tunavyosarifu namna kwa namna Aayaat ili (makafiri) waseme: Umedurusu (kutoka kwa Watu wa Kitabu), na ili pia Tuibainishe kwa watu wenye kujua.

 

 

 

اتَّبِعْ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٠٦

106. Fuata (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uliyofunuliwa Wahy toka kwa Rabb wako. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, na jitenge na washirikina.

 

 

 

وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا أَشْرَكُوا ۗ وَمَا جَعَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا ۖ وَمَا أَنتَ عَلَيْهِم بِوَكِيلٍ ﴿١٠٧

107. Na lau Allaah Angetaka wasingelifanya shirki. Na Hatukukufanya wewe msimamizi wa mambo yao na wala wewe si mdhamini wao.

 

 

 

وَلَا تَسُبُّوا الَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ فَيَسُبُّوا اللَّـهَ عَدْوًا بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ كَذَٰلِكَ زَيَّنَّا لِكُلِّ أُمَّةٍ عَمَلَهُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِم مَّرْجِعُهُمْ فَيُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٠٨

108. Na wala msiwatukane wale wanaowaomba asiyekuwa Allaah, wasije nao kumtukana Allaah kwa uadui bila ya ujuzi.[23] Hivyo ndivyo Tumewapambia kila ummah amali zao, kisha kwa Rabb wao Pekee yatakuwa marejeo yao, Atawajulisha yale waliyokuwa wakiyatenda.

 

 

 

 

وَأَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ لَئِن جَاءَتْهُمْ آيَةٌ لَّيُؤْمِنُنَّ بِهَا ۚ قُلْ إِنَّمَا الْآيَاتُ عِندَ اللَّـهِ ۖ وَمَا يُشْعِرُكُمْ أَنَّهَا إِذَا جَاءَتْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٠٩

109. Na wakaapa kwa Allaah, viapo vyao thabiti vya nguvu, kwamba ikiwafikia Aayah (Muujiza) bila shaka wataiamini. Sema: Hakika Aayaat (Miujiza, Ishara) ziko kwa Allaah. Na kitu gani kitakutambulisheni kwamba zitakapokuja hawatoamini?

 

 

 

وَنُقَلِّبُ أَفْئِدَتَهُمْ وَأَبْصَارَهُمْ كَمَا لَمْ يُؤْمِنُوا بِهِ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَنَذَرُهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ ﴿١١٠

110. Na Tunazigeuza nyoyo zao na macho yao kama wasivyoiamini mara ya kwanza. Na Tunawaacha katika upindukaji mipaka ya kuasi kwao, wanatangatanga kwa upofu.

 

 

 

وَلَوْ أَنَّنَا نَزَّلْنَا إِلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةَ وَكَلَّمَهُمُ الْمَوْتَىٰ وَحَشَرْنَا عَلَيْهِمْ كُلَّ شَيْءٍ قُبُلًا مَّا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ يَجْهَلُونَ ﴿١١١﴾

111. Na lau kama Sisi Tungeliwateremshia Malaika, na wao wakasemeshwa na wafu, na Tukawakusanyia kila kitu mbele yao, basi bado wasingeliamini ila Allaah Atake, lakini wengi wamo katika ujahili. 

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوًّا شَيَاطِينَ الْإِنسِ وَالْجِنِّ يُوحِي بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ زُخْرُفَ الْقَوْلِ غُرُورًا ۚ وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ مَا فَعَلُوهُ ۖ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ ﴿١١٢﴾

112. Na hivyo ndivyo Tulivyojaalia kwa kila Nabiy maadui mashaytwaan wa kibinaadam na kijini, wanadokezana wenyewe kwa wenyewe maneno ya kupambapamba na ya ghururi. Na lau Angetaka Rabb wako wasingeliyafanya hayo. Basi waachilie mbali na wanayoyatunga (ya uongo).

 

 

 

وَلِتَصْغَىٰ إِلَيْهِ أَفْئِدَةُ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ وَلِيَرْضَوْهُ وَلِيَقْتَرِفُوا مَا هُم مُّقْتَرِفُونَ ﴿١١٣﴾

113. Na ili zielemee katika (udanganyifu) nyoyo za wale wasioamini Aakhirah, na ili waridhike nayo, na ili wachume (madhambi) wanayoyachuma.

 

 

 

أَفَغَيْرَ اللَّـهِ أَبْتَغِي حَكَمًا وَهُوَ الَّذِي أَنزَلَ إِلَيْكُمُ الْكِتَابَ مُفَصَّلًا ۚ وَالَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْلَمُونَ أَنَّهُ مُنَزَّلٌ مِّن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ ۖ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ ﴿١١٤﴾

114. (Sema): Je, nitafute hakimu ghairi ya Allaah na hali Yeye Ndiye Aliyekuteremshieni Kitabu kilichofasiliwa waziwazi? Na wale Tuliowapa Kitabu (kabla) wanajua kwamba kimeteremshwa kutoka kwa Rabb wako kwa haki. Basi usijekuwa miongoni mwa wanaotia shaka. 

 

 

 

وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ صِدْقًا وَعَدْلًا ۚ لَّا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِهِ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١١٥﴾

115. Na limetimia Neno la Rabb wako kiukweli na kiadilifu. Hakuna awezaye kuyabadilisha Maneno Yake. Naye Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ ﴿١١٦﴾

116. Na kama ukiwatii wengi walioko ulimwenguni, watakupoteza Njia ya Allaah. Hawafuati isipokuwa dhana tu, na hawakuwa ila wenye kubuni uongo.

 

 

 

إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ مَن يَضِلُّ عَن سَبِيلِهِ ۖ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ ﴿١١٧﴾

117. Hakika Rabb wako Anajua zaidi mwenye kupotea Njia Yake. Naye Anajua zaidi wenye kuhidika.

 

 

 

فَكُلُوا مِمَّا ذُكِرَ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ إِن كُنتُم بِآيَاتِهِ مُؤْمِنِينَ ﴿١١٨﴾

118. Basi kuleni katika ambavyo limetajwa Jina la Allaah (wakati wa kuchinjwa) mkiwa nyinyi ni wenye kuziamini Aayaat (na Hukmu) Zake.

 

 

 

وَمَا لَكُمْ أَلَّا تَأْكُلُوا مِمَّا ذُكِرَ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا لَّيُضِلُّونَ بِأَهْوَائِهِم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِالْمُعْتَدِينَ ﴿١١٩﴾

119. Na mna nini hata msile katika ambavyo limetajwa Jina la Allaah na ilhali Ameshafasilisha waziwazi kwenu yale Aliyokuharamishieni isipokuwa vile mlivyofikwa na dharura navyo. Na hakika wengi wanapotoa (wengine) kwa hawaa zao bila ya ilimu. Hakika Rabb wako Yeye Anajua zaidi wenye kutaadi.

 

 

 

وَذَرُوا ظَاهِرَ الْإِثْمِ وَبَاطِنَهُ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَكْسِبُونَ الْإِثْمَ سَيُجْزَوْنَ بِمَا كَانُوا يَقْتَرِفُونَ ﴿١٢٠﴾

120. Na acheni dhambi za dhahiri na zilizofichika. Hakika wale wanaochuma dhambi watalipwa kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.

 

 

 

وَلَا تَأْكُلُوا مِمَّا لَمْ يُذْكَرِ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَإِنَّهُ لَفِسْقٌ ۗ وَإِنَّ الشَّيَاطِينَ لَيُوحُونَ إِلَىٰ أَوْلِيَائِهِمْ لِيُجَادِلُوكُمْ ۖ وَإِنْ أَطَعْتُمُوهُمْ إِنَّكُمْ لَمُشْرِكُونَ ﴿١٢١﴾

121. Na wala msile katika ambavyo halikutajwa Jina la Allaah (wakati wa kuchinjwa), kwani huo ni ukiukaji wa utiifu kwa Allaah. Na hakika mashaytwaan wanawashawishi marafiki wao wandani wabishane nanyi. Na kama mtawatii basi hakika mtakuwa washirikina.

 

 

 

أَوَمَن كَانَ مَيْتًا فَأَحْيَيْنَاهُ وَجَعَلْنَا لَهُ نُورًا يَمْشِي بِهِ فِي النَّاسِ كَمَن مَّثَلُهُ فِي الظُّلُمَاتِ لَيْسَ بِخَارِجٍ مِّنْهَا ۚ كَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلْكَافِرِينَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٢٢﴾

122. Je, aliyekuwa maiti kisha Tukamhuisha na Tukamjaalia nuru anatembea nayo kati ya watu, ni sawa na yule ambaye yumo katika viza hawezi kutoka humo?[24] Hivyo ndivyo walivyopambiwa makafiri yale waliyokuwa wakiyatenda.

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا فِي كُلِّ قَرْيَةٍ أَكَابِرَ مُجْرِمِيهَا لِيَمْكُرُوا فِيهَا ۖ وَمَا يَمْكُرُونَ إِلَّا بِأَنفُسِهِمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿١٢٣﴾

123. Na hivyo ndivyo Tulivyojaalia katika kila mji wahalifu wake wakuu ili wafanyie makri (njama) humo. Na hawafanyii makri ila nafsi zao, na wala hawahisi.

 

 

 

وَإِذَا جَاءَتْهُمْ آيَةٌ قَالُوا لَن نُّؤْمِنَ حَتَّىٰ نُؤْتَىٰ مِثْلَ مَا أُوتِيَ رُسُلُ اللَّـهِ ۘ اللَّـهُ أَعْلَمُ حَيْثُ يَجْعَلُ رِسَالَتَهُ ۗ سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِندَ اللَّـهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ ﴿١٢٤﴾

124. Na inapowajia Aayah (Muujiza, Ushahidi bayana) husema: Hatutoamini mpaka tupewe mfano wa yale waliopewa Rusuli wa Allaah.  Allaah Anajua zaidi wapi Aweke Ujumbe Wake. Utawasibu wale waliohalifu udhalilifu mbele ya Allaah na adhabu kali kwa sababu ya makri (njama) walizokuwa wakifanya.

 

 

 

فَمَن يُرِدِ اللَّـهُ أَن يَهْدِيَهُ يَشْرَحْ صَدْرَهُ لِلْإِسْلَامِ ۖ وَمَن يُرِدْ أَن يُضِلَّهُ يَجْعَلْ صَدْرَهُ ضَيِّقًا حَرَجًا كَأَنَّمَا يَصَّعَّدُ فِي السَّمَاءِ ۚ كَذَٰلِكَ يَجْعَلُ اللَّـهُ الرِّجْسَ عَلَى الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٢٥﴾

125. Basi yule ambaye Allaah Anataka kumhidi, Humfungulia kifua chake kwa Uislamu. Na yule ambaye Anataka kumpotoa, Hufanya kifua chake kiwe na dhiki chenye kubana kama kwamba anapanda kwa tabu mbinguni. Hivyo ndivyo Allaah Anavyojaalia adhabu (au Anavyowasalitishia shaytwaan) kwa wale wasioamini.  

 

 

 

وَهَـٰذَا صِرَاطُ رَبِّكَ مُسْتَقِيمًا ۗ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَذَّكَّرُونَ ﴿١٢٦﴾

126. Na hii ni Njia ya Rabb wako iliyonyooka. Kwa yakini Tumefasili waziwazi Aayaat kwa watu wanaokumbuka.

 

 

 

لَهُمْ دَارُ السَّلَامِ عِندَ رَبِّهِمْ ۖ وَهُوَ وَلِيُّهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٢٧﴾

127. Watapata Daarus-Salaam (nyumba ya amani Jannah) kwa Rabb wao.  Naye Ndiye Rafiki wao Mlinzi kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyatenda. 

 

 

 

وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ قَدِ اسْتَكْثَرْتُم مِّنَ الْإِنسِ ۖ وَقَالَ أَوْلِيَاؤُهُم مِّنَ الْإِنسِ رَبَّنَا اسْتَمْتَعَ بَعْضُنَا بِبَعْضٍ وَبَلَغْنَا أَجَلَنَا الَّذِي أَجَّلْتَ لَنَا ۚ قَالَ النَّارُ مَثْوَاكُمْ خَالِدِينَ فِيهَا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ ۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ ﴿١٢٨﴾

128. Na Siku Atakapowakusanya wote (Allaah Atasema):  Enyi hadhara ya majini! Kwa yakini mmewapoteza wanaadamu wengi sana. Na watasema marafiki wao wandani katika wanaadamu: Rabb wetu! Tulinufaishana sisi kwa sisi, na (leo) tumefikia muda wetu ambao Umetupangia. (Allaah) Atasema: Moto ndio makazi yenu, mtadumu humo, isipokuwa Atakavyo Allaah. Hakika Rabb wako Ni Mwenye Hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ نُوَلِّي بَعْضَ الظَّالِمِينَ بَعْضًا بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿١٢٩﴾

129. Na hivyo ndivyo Tunavyowafanya madhalimu kuwa marafiki wandani wao kwa wao kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma.

 

 

 

 

يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ أَلَمْ يَأْتِكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ يَقُصُّونَ عَلَيْكُمْ آيَاتِي وَيُنذِرُونَكُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا ۚ قَالُوا شَهِدْنَا عَلَىٰ أَنفُسِنَا ۖ وَغَرَّتْهُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَشَهِدُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ أَنَّهُمْ كَانُوا كَافِرِينَ ﴿١٣٠﴾

130. Enyi hadhara ya majini na wanaadamu! Je hawajakufikieni Rusuli miongoni mwenu wanakusimulieni Aayaat Zangu na wanakuonyeni kukutana na Siku yenu hii? Watasema: Tumeshuhudia dhidi ya nafsi zetu. Na uliwaghuri uhai wa dunia, na wameshuhudia dhidi ya nafsi zao kwamba hakika wao walikuwa ni makafiri.

 

 

 

ذَٰلِكَ أَن لَّمْ يَكُن رَّبُّكَ مُهْلِكَ الْقُرَىٰ بِظُلْمٍ وَأَهْلُهَا غَافِلُونَ ﴿١٣١﴾

131. Hivyo ni kwa kuwa Rabb wako Hakuwa Mwenye Kuangamiza mji kwa dhulma hali wenyewe hawajazindushwa.

 

 

 

وَلِكُلٍّ دَرَجَاتٌ مِّمَّا عَمِلُوا ۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَافِلٍ عَمَّا يَعْمَلُونَ ﴿١٣٢﴾

132. Na wote wana daraja mbalimbali kwa yale waliyoyatenda. Na Rabb wako Si Mwenye Kughafilika na yale wanayoyatenda.

 

 

 

وَرَبُّكَ الْغَنِيُّ ذُو الرَّحْمَةِ ۚ إِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ وَيَسْتَخْلِفْ مِن بَعْدِكُم مَّا يَشَاءُ كَمَا أَنشَأَكُم مِّن ذُرِّيَّةِ قَوْمٍ آخَرِينَ ﴿١٣٣﴾

133. Na Rabb wako Ni Mkwasi Mwenye Rahmah. Akitaka Atakuondosheni na Aweke wengine Awatakao badala yenu kama Alivyokuzalisheni nyinyi kutokana na vizazi vya watu wengine.

 

 

 

إِنَّ مَا تُوعَدُونَ لَآتٍ ۖ وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ ﴿١٣٤﴾

134. Hakika mnayoahidiwa bila shaka yatakuja tu! Nanyi si wenye kuweza kushinda (kukwepa adhabu).  

 

 

 

قُلْ يَا قَوْمِ اعْمَلُوا عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنِّي عَامِلٌ ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ مَن تَكُونُ لَهُ عَاقِبَةُ الدَّارِ ۗ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ ﴿١٣٥﴾

135. Sema: Enyi kaumu yangu! Tendeni kwa namna yenu, nami pia natenda yangu. Mtakuja kujua nani atakayekuwa na hatima njema ya makazi Aakhirah. Hakika madhalimu hawatofaulu.

 

 

 

وَجَعَلُوا لِلَّـهِ مِمَّا ذَرَأَ مِنَ الْحَرْثِ وَالْأَنْعَامِ نَصِيبًا فَقَالُوا هَـٰذَا لِلَّـهِ بِزَعْمِهِمْ وَهَـٰذَا لِشُرَكَائِنَا ۖ فَمَا كَانَ لِشُرَكَائِهِمْ فَلَا يَصِلُ إِلَى اللَّـهِ ۖ وَمَا كَانَ لِلَّـهِ فَهُوَ يَصِلُ إِلَىٰ شُرَكَائِهِمْ ۗ سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ ﴿١٣٦﴾

136. Na wamemfanyia Allaah fungu katika mimea na wanyama Aliyoumba. Wakasema: Hili ni la Allaah kwa madai yao, na hili ni kwa ajili ya washirika wetu. Basi yaliyokuwa kwa ajili ya washirika wao hayamfikii Allaah. Na yaliyokuwa kwa ajili ya Allaah hufika kwa washirika wao. Uovu ulioje wanayoyahukumu!  

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ زَيَّنَ لِكَثِيرٍ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ قَتْلَ أَوْلَادِهِمْ شُرَكَاؤُهُمْ لِيُرْدُوهُمْ وَلِيَلْبِسُوا عَلَيْهِمْ دِينَهُمْ ۖ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا فَعَلُوهُ ۖ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ ﴿١٣٧﴾

137. Na hivyo ndivyo washirika (mashaytwaan) wao walivyowapambia washirikina wengi kuua watoto wao ili wawateketeze na wawakorogee dini yao. Na lau Allaah Angetaka, wasingeliyafanya hayo. Basi waachilie mbali na wanayoyatunga (ya uongo).

 

 

 

وَقَالُوا هَـٰذِهِ أَنْعَامٌ وَحَرْثٌ حِجْرٌ لَّا يَطْعَمُهَا إِلَّا مَن نَّشَاءُ بِزَعْمِهِمْ وَأَنْعَامٌ حُرِّمَتْ ظُهُورُهَا وَأَنْعَامٌ لَّا يَذْكُرُونَ اسْمَ اللَّـهِ عَلَيْهَا افْتِرَاءً عَلَيْهِ ۚ سَيَجْزِيهِم بِمَا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿١٣٨﴾

138. Na wakasema kwa madai yao: Wanyama hawa (ngamia) na mazao ni marufuku, hawatowala ila wale tuwatakao, na wanyama (hawa) imeharamishwa migongo yao (kuwapanda).  Na wanyama (wengine) hawalitaji Jina la Allaah juu yao (wanapowachinja), wanamtungia uongo (Allaah). Atawalipa kwa yale waliyokuwa wakiyatunga.

 

 

 

وَقَالُوا مَا فِي بُطُونِ هَـٰذِهِ الْأَنْعَامِ خَالِصَةٌ لِّذُكُورِنَا وَمُحَرَّمٌ عَلَىٰ أَزْوَاجِنَا ۖ وَإِن يَكُن مَّيْتَةً فَهُمْ فِيهِ شُرَكَاءُ ۚ سَيَجْزِيهِمْ وَصْفَهُمْ ۚ إِنَّهُ حَكِيمٌ عَلِيمٌ ﴿١٣٩﴾

139. Na wakasema: Waliomo matumboni mwa wanyama hawa ni makhsusi kwa wanaume wetu na marufuku kwa wake zetu. Lakini wakiwa ni nyamafu (wanapozaliwa), basi wanashirikiana katika hao (na wanawake kula). Hakika Atawalipa uvumishi wao. Hakika Yeye Ni Mwenye Hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ قَتَلُوا أَوْلَادَهُمْ سَفَهًا بِغَيْرِ عِلْمٍ وَحَرَّمُوا مَا رَزَقَهُمُ اللَّـهُ افْتِرَاءً عَلَى اللَّـهِ ۚ قَدْ ضَلُّوا وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ ﴿١٤٠﴾

140. Kwa yakini wamekhasirika wale waliowaua watoto wao kwa upumbavu bila ya ujuzi na wakaharamisha vile Alivyowaruzuku Allaah kwa kumtungia uongo Allaah. Kwa yakini wamepotea na wala hawakuwa wenye kuhidika. 

 

 

 

 

وَهُوَ الَّذِي أَنشَأَ جَنَّاتٍ مَّعْرُوشَاتٍ وَغَيْرَ مَعْرُوشَاتٍ وَالنَّخْلَ وَالزَّرْعَ مُخْتَلِفًا أُكُلُهُ وَالزَّيْتُونَ وَالرُّمَّانَ مُتَشَابِهًا وَغَيْرَ مُتَشَابِهٍ ۚ كُلُوا مِن ثَمَرِهِ إِذَا أَثْمَرَ وَآتُوا حَقَّهُ يَوْمَ حَصَادِهِ ۖ وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ ﴿١٤١﴾

141. Naye (Allaah) Ndiye Aliyezalisha mabustani yanayotambaa na yasiyotambaa. Na mitende na mimea yenye kutofautiana ladha yake, na zaytuni na makomamanga yanayoshabihiana na yasiyoshabihiana. Kuleni katika matunda yake yanapotoa mazao na toeni haki yake (Zakaah) siku ya kuvunwa kwake na wala msifanye israfu. Hakika Yeye Hapendi wafanyao israfu.

 

 

 

وَمِنَ الْأَنْعَامِ حَمُولَةً وَفَرْشًا ۚ كُلُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّـهُ وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿١٤٢﴾

142. Na katika wanyama wa mifugo (Amekuumbieni) wabebao mzigo na wadogodogo. Kuleni katika Alivyokuruzukuni Allaah na wala msifuate hatua za shaytwaan, hakika yeye ni adui bayana kwenu.

 

 

 

ثَمَانِيَةَ أَزْوَاجٍ ۖ مِّنَ الضَّأْنِ اثْنَيْنِ وَمِنَ الْمَعْزِ اثْنَيْنِ ۗ قُلْ آلذَّكَرَيْنِ حَرَّمَ أَمِ الْأُنثَيَيْنِ أَمَّا اشْتَمَلَتْ عَلَيْهِ أَرْحَامُ الْأُنثَيَيْنِ ۖ نَبِّئُونِي بِعِلْمٍ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٤٣﴾

143. Jozi nane: (za dume na jike) katika kondoo wawili na katika mbuzi wawili. Sema: Je, Ameharamisha wote madume wawili au majike mawili, au waliomo ndani ya fuko la uzazi mwa majike yote mawili? Nijulisheni kwa ilimu ikiwa nyinyi mnasema kweli.

 

 

 

 

وَمِنَ الْإِبِلِ اثْنَيْنِ وَمِنَ الْبَقَرِ اثْنَيْنِ ۗ قُلْ آلذَّكَرَيْنِ حَرَّمَ أَمِ الْأُنثَيَيْنِ أَمَّا اشْتَمَلَتْ عَلَيْهِ أَرْحَامُ الْأُنثَيَيْنِ ۖ أَمْ كُنتُمْ شُهَدَاءَ إِذْ وَصَّاكُمُ اللَّـهُ بِهَـٰذَا ۚ فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا لِّيُضِلَّ النَّاسَ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿١٤٤﴾

144. Na katika ngamia wawili na katika ng’ombe wawili. Sema: Je, Ameharamisha madume wawili au majike mawili, au waliomo ndani ya fuko la uzazi mwa majike wawili? Au nyinyi mlishuhudia Allaah Alipokuusieni haya? Basi nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemtungia Allaah uongo ili apoteze watu bila ilimu. Hakika Allaah Hawaongozi watu madhalimu.

 

 

 

قُل لَّا أَجِدُ فِي مَا أُوحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَىٰ طَاعِمٍ يَطْعَمُهُ إِلَّا أَن يَكُونَ مَيْتَةً أَوْ دَمًا مَّسْفُوحًا أَوْ لَحْمَ خِنزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ أَوْ فِسْقًا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ ۚ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَإِنَّ رَبَّكَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٤٥﴾

145. Sema: Sipati katika yale niliyofunuliwa Wahyi kwangu kilichoharamishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu au damu inayomwagika au nyama ya nguruwe, kwani hivyo ni vichafu, au kilichochinjwa kinyume na utiifu kwa Allaah kwa kutajiwa asiyekuwa Allaah. Lakini atakayefikwa na dharura bila ya kutamani wala kuvuka mipaka, basi hakika Rabb wako Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

 

وَعَلَى الَّذِينَ هَادُوا حَرَّمْنَا كُلَّ ذِي ظُفُرٍ ۖ وَمِنَ الْبَقَرِ وَالْغَنَمِ حَرَّمْنَا عَلَيْهِمْ شُحُومَهُمَا إِلَّا مَا حَمَلَتْ ظُهُورُهُمَا أَوِ الْحَوَايَا أَوْ مَا اخْتَلَطَ بِعَظْمٍ ۚ ذَٰلِكَ جَزَيْنَاهُم بِبَغْيِهِمْ ۖ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ ﴿١٤٦﴾

146. Na kwa wale walio Mayahudi Tuliharamisha kila (mnyama) mwenye kucha. Na katika ng’ombe na mbuzi Tuliwaharamishia shahamu zao isipokuwa iliyobeba migongo yao au utumbo wao au iliyochanganyika na mifupa.  Hivyo ndivyo Tulivyowalipa kwa baghi[25] (dhulma) yao. Na bila shaka Sisi Ni Wakweli.

 

 

 

 

فَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل رَّبُّكُمْ ذُو رَحْمَةٍ وَاسِعَةٍ وَلَا يُرَدُّ بَأْسُهُ عَنِ الْقَوْمِ الْمُجْرِمِينَ ﴿١٤٧﴾

147. Wakikukadhibisha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) basi sema: Rabb wenu Ni Mwenye Rahmah iliyoenea. Na wala haizuiliwi Adhabu Yake kwa watu wahalifu.

 

 

 

 

سَيَقُولُ الَّذِينَ أَشْرَكُوا لَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا أَشْرَكْنَا وَلَا آبَاؤُنَا وَلَا حَرَّمْنَا مِن شَيْءٍ ۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ حَتَّىٰ ذَاقُوا بَأْسَنَا ۗ قُلْ هَلْ عِندَكُم مِّنْ عِلْمٍ فَتُخْرِجُوهُ لَنَا ۖ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ أَنتُمْ إِلَّا تَخْرُصُونَ ﴿١٤٨﴾

148. Watasema wale walioshirikisha: Lau Allaah Angetaka, tusingelifanya shirki, wala baba zetu pia na wala tusingeliharamisha chochote. Hivyo ndivyo walivyokadhibisha wale wa kabla yao mpaka walipoonja Adhabu Yetu.  Sema: Je, mna ilimu yoyote mtutolee? Hamfuati isipokuwa dhana tu, nanyi si lolote ila mnabuni uongo.

 

 

 

قُلْ فَلِلَّـهِ الْحُجَّةُ الْبَالِغَةُ ۖ فَلَوْ شَاءَ لَهَدَاكُمْ أَجْمَعِينَ ﴿١٤٩﴾

149. Sema: Basi Ni Allaah Pekee Mwenye hoja timilifu. Na Angelitaka Angelikuhidini nyote.

 

 

 

قُلْ هَلُمَّ شُهَدَاءَكُمُ الَّذِينَ يَشْهَدُونَ أَنَّ اللَّـهَ حَرَّمَ هَـٰذَا ۖ فَإِن شَهِدُوا فَلَا تَشْهَدْ مَعَهُمْ ۚ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَالَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ وَهُم بِرَبِّهِمْ يَعْدِلُونَ ﴿١٥٠﴾

150. Sema: Leteni mashahidi wenu wanaoshuhudia kwamba Allaah Ameharamisha (wanyama) hawa. Wakishuhudia, basi usishuhudie pamoja nao. Na wala usifuate hawaa za wale wanaokadhibisha Aayaat Zetu, na wale wasioamini Aakhirah, nao wanawasawazisha wengine na Rabb wao. 

 

 

 

 

قُلْ تَعَالَوْا أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ ۖ أَلَّا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۖ وَلَا تَقْتُلُوا أَوْلَادَكُم مِّنْ إِمْلَاقٍ ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُكُمْ وَإِيَّاهُمْ ۖ وَلَا تَقْرَبُوا الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ ۖ وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿١٥١﴾

151. Sema: Njooni nikusomeeni yale Aliyoyaharamisha Rabb wenu kwenu. Kwamba msimshirikishe na chochote, na muwafanyie ihsaan wazazi wawili, na wala msiwaue watoto wenu kutokana na umasikini. Sisi Tunakuruzukuni pamoja nao. Na wala msikaribie machafu yaliyo dhahiri na yaliyofichika. Na wala msiue nafsi ambayo Allaah Ameiharamisha (kuiua) isipokuwa kwa haki (ya sharia). Hivyo ndivyo Alivyokuusieni kwayo mpate kutia akilini.

 

 

 

 

وَلَا تَقْرَبُوا مَالَ الْيَتِيمِ إِلَّا بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ حَتَّىٰ يَبْلُغَ أَشُدَّهُ ۖ وَأَوْفُوا الْكَيْلَ وَالْمِيزَانَ بِالْقِسْطِ ۖ لَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۖ وَإِذَا قُلْتُمْ فَاعْدِلُوا وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۖ وَبِعَهْدِ اللَّـهِ أَوْفُوا ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ ﴿١٥٢﴾

152. Na wala msiikaribie mali ya yatima isipokuwa kwa njia njema ya manufaa mpaka afikie umri wa kupevuka. Na timizeni kipimo na mizani kwa uadilifu. Hatukalifishi nafsi isipokuwa kadiri ya uwezo wake. Na mnaposema basi fanyeni uadilifu japokuwa ni jamaa wa karibu. Na timizeni Ahadi ya Allaah. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni (Allaah) kwayo mpate kukumbuka.

 

 

 

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٥٣﴾

153. Na kwamba hii ndiyo njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Na wala msifuate njia nyinginezo zitakufarikisheni na Njia Yake.[26] Hivyo ndivyo Alivyokuusieni (Allaah) kwayo mpate kuwa na taqwa. 

 

 

 

ثُمَّ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ تَمَامًا عَلَى الَّذِي أَحْسَنَ وَتَفْصِيلًا لِّكُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً لَّعَلَّهُم بِلِقَاءِ رَبِّهِمْ يُؤْمِنُونَ ﴿١٥٤﴾

154. Tena Tulimpa Muwsaa Kitabu kutimiza (neema) juu ya yule aliyefanya vitendo vyema, na kiwe chenye kuchambua wazi kila kitu, na kiwe mwongozo na rahmah ili wapate kuamini kukutana na Rabb wao.

 

 

 

وَهَـٰذَا كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ فَاتَّبِعُوهُ وَاتَّقُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿١٥٥﴾

155. Na hiki ni Kitabu (Qur-aan) Tumekiteremsha kilichobarikiwa, basi kifuateni na muwe na taqwa mpate kurehemewa.

 

 

 

أَن تَقُولُوا إِنَّمَا أُنزِلَ الْكِتَابُ عَلَىٰ طَائِفَتَيْنِ مِن قَبْلِنَا وَإِن كُنَّا عَن دِرَاسَتِهِمْ لَغَافِلِينَ ﴿١٥٦﴾

156. Msije kusema: Hakika Kitabu kimeteremshwa juu ya makundi mawili kabla yetu, lakini tulikuwa hatuna habari yoyote kuhusu waliyokuwa wakiyasoma.

 

 

أَوْ تَقُولُوا لَوْ أَنَّا أُنزِلَ عَلَيْنَا الْكِتَابُ لَكُنَّا أَهْدَىٰ مِنْهُمْ ۚ فَقَدْ جَاءَكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ ۚ فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن كَذَّبَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَصَدَفَ عَنْهَا ۗ سَنَجْزِي الَّذِينَ يَصْدِفُونَ عَنْ آيَاتِنَا سُوءَ الْعَذَابِ بِمَا كَانُوا يَصْدِفُونَ ﴿١٥٧﴾

157. Au mkaseme: Lau tungeliteremshiwa Kitabu basi bila shaka tungelikuwa tumehidika zaidi kuliko wao. Kwa yakini imekwishakufikieni hoja bayana kutoka kwa Rabb wenu na mwongozo na rahmah. Hivyo basi nani ni dhalimu zaidi kuliko yule aliyekadhibisha Aayaat za Allaah na akajitenga nazo? Tutawalipa wale wanaojitenga na Aayaat Zetu adhabu ovu kwa sababu ya kujitenga kwao.

 

 

 

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن تَأْتِيَهُمُ الْمَلَائِكَةُ أَوْ يَأْتِيَ رَبُّكَ أَوْ يَأْتِيَ بَعْضُ آيَاتِ رَبِّكَ ۗ يَوْمَ يَأْتِي بَعْضُ آيَاتِ رَبِّكَ لَا يَنفَعُ نَفْسًا إِيمَانُهَا لَمْ تَكُنْ آمَنَتْ مِن قَبْلُ أَوْ كَسَبَتْ فِي إِيمَانِهَا خَيْرًا ۗ قُلِ انتَظِرُوا إِنَّا مُنتَظِرُونَ ﴿١٥٨﴾

158. Je, wanangojea nini isipokuwa Malaika wawafikie (kuwatoa roho), au Awafikie Rabb wako (kuwahukumu)[27], au ziwajie baadhi ya Aayaat (Ishara, Alama za Qiyaamah)[28] za Rabb wako? Siku zitakapokuja baadhi ya Aayaat za Rabb wako haitoifaa nafsi imaan yake, ikiwa haikuamini kabla au haikuchuma katika imaan yake kheri yoyote. Sema: Ngojeeni hakika nasi tunangojea.

 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا لَّسْتَ مِنْهُمْ فِي شَيْءٍ ۚ إِنَّمَا أَمْرُهُمْ إِلَى اللَّـهِ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُوا يَفْعَلُونَ ﴿١٥٩﴾

159. Hakika wale waliofarakisha dini yao na wakawa makundi makundi,[29] wewe huhusiki nao kwa lolote. Hakika kesi yao iko kwa Allaah, kisha Atawajulisha yale waliyokuwa wakiyatenda.

 

 

 

مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا ۖ وَمَن جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَلَا يُجْزَىٰ إِلَّا مِثْلَهَا وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿١٦٠﴾

160. Atakayekuja na amali njema basi atapata (thawabu) kumi mfano wake. Na Atakayekuja na ovu basi hatolipwa ila mfano wake,[30] nao hawatodhulumiwa.

 

 

 

قُلْ إِنَّنِي هَدَانِي رَبِّي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ دِينًا قِيَمًا مِّلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۚ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٦١﴾

161. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika mimi Ameniongoza Rabb wangu kuelekea njia iliyonyooka, Dini iliyosimama thabiti, mila ya Ibraahiym aliyejitenga na itikadi potofu na kuelemea haki na hakuwa miongoni mwa washirikina.

 

 

قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦٢﴾

162. Sema: Hakika Swalaah yangu, na ibaada yangu ya kuchinja, na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah Pekee Rabb wa walimwengu.[31]

 

 

لَا شَرِيكَ لَهُ ۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ ﴿١٦٣﴾

163. Hana mshirika, na kwa hayo ndio nimeamrishwa, nami ni Muislamu wa kwanza (katika ummah huu). 

 

 

 

قُلْ أَغَيْرَ اللَّـهِ أَبْغِي رَبًّا وَهُوَ رَبُّ كُلِّ شَيْءٍ ۚ وَلَا تَكْسِبُ كُلُّ نَفْسٍ إِلَّا عَلَيْهَا ۚ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُم مَّرْجِعُكُمْ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ ﴿١٦٤﴾

164. Sema Je, nitake ghairi ya Allaah kuwa ni Rabb ilhali Yeye Ndiye Rabb wa kila kitu? Na nafsi yoyote haichumi (kheri au shari) ila itabeba yenyewe. Na wala habebi mbebaji, mzigo (wa dhambi) wa mwengine. Kisha kwa Rabb wenu ndio marejeo yenu, Atakujulisheni yale mliyokuwa mkikhitilafiana.

 

 

 

 

وَهُوَ الَّذِي جَعَلَكُمْ خَلَائِفَ الْأَرْضِ وَرَفَعَ بَعْضَكُمْ فَوْقَ بَعْضٍ دَرَجَاتٍ لِّيَبْلُوَكُمْ فِي مَا آتَاكُمْ ۗ إِنَّ رَبَّكَ سَرِيعُ الْعِقَابِ وَإِنَّهُ لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٦٥﴾

165. Naye (Allaah) Ndiye Aliyekufanyeni warithi waandamizi wa duniani na Akanyanyua baadhi yenu juu ya wengine kwa daraja mbali mbali ili Akujaribuni katika yale Aliyokupeni. Hakika Rabb wako Ni Mwepesi wa Kuakibu, na hakika Yeye bila shaka Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

 

 

[1]  Yeye Ndiye Allaah Mwabudiwa Wa Mbinguni Na Ardhini:

 

Wafasiri wa Qur-aan wamekhitilafiana katika kauli nne kuhusu Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

وَهُوَ اللَّـهُ فِي السَّمَاوَاتِ وَفِي الْأَرْضِ ۖ يَعْلَمُ سِرَّكُمْ وَجَهْرَكُمْ وَيَعْلَمُ مَا تَكْسِبُونَ ﴿٣﴾

“Na Yeye Ndiye Allaah mbinguni na ardhini, Anajua ya siri yenu na ya dhahiri yenu, na Anajua yale mnayoyachuma.” [Al-An'aam (6:3)]

 

Kauli Ya Kwanza:

Maana yake ni: Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) ni Ilaah (Apasaye kuabudiwa kwa haki), Anayeabudiwa mbinguni na ardhini, kwa sababu Yeye Pekee Ndiye Mwabudiwa wa haki katika ardhi na mbingu, kwa ushahidi wa Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

وَهُوَ الَّذِي فِي السَّمَاءِ إِلَـٰهٌ وَفِي الْأَرْضِ إِلَـٰهٌ ۚ  

“Na Yeye Ndiye Mwabudiwa wa haki mbinguni na ardhini pia (Ndiye Huyo Huyo) Ilaah.” [Az-Zukhruf (43:84)]

 

[Al-Qurtwubiy, Ibn Kathiyr, Ash-Shanqiytwiy, Ibn Al-Anbaariy na wengineo. Rejea Al-Jaami’u li-Ahkaamil-Qur-aan (6/390), Tafsiyr Al-Qur-aan Al-‘Adhwiym (3/240) na Adhwaau Al-Bayaan (7/4)]  

 

Kauli Ya Pili: 

Maana yake ni: Yeye Allaah Anajua siri zenu mbinguni na ardhini, na ushahidi ni Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

قُلْ أَنزَلَهُ الَّذِي يَعْلَمُ السِّرَّ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ  

“Sema (ee Muhammad صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ): “Ameiteremsha Ambaye Anajua siri katika mbingu na ardhi.” [Al-Furqaan (25:6)]

 

Kwa kuzingatia kwamba Kauli Yake: 

 

mbinguni na ardhini [Al-An’aam (6:3)] inahusiana na: Anajua siri zenu.”

 

Imaam Ad-Daaniyy amesema: Na imesemwa kuwa maana yake ni: Yeye Ndiye Mwabudiwa mbinguni na ardhini. Na Al-Ashmuwniyy kaunga mkono ufafanuzi huo.

 

Na amesema An-Nahhaas kuwa kauli hiyo ni bora katika yaliyoelezwa juu ya Aayah hiyo.

 

[Al-Muktafaa Fiy Al-Waqf Wal-Ibtidaa Fiy KitaabiLLaah ‘Azza Wa Jalla (273), Manaaru Al-Hudaa Fiy Bayaan Al-Waqf Wal-Ibtidaa (265). Adhwaau Al-Bayaan Fiy Iydhwaah Al-Qur-aan bil-Qur-aan (4/7)]   

 

Kauli Ya Tatu:

Ni kwamba Yeye Allaah, Ambaye Yuko mbinguni na katika ardhi, Anajua siri zenu na ya dhahiri yenu katika ardhi.  Naye Yuko juu ya ‘Arsh Yake Akiwa juu ya Viumbe Vyake wote, Akiwa Anajua siri za watu wa ardhini na ya dhahiri yao, hakuna kinachofichika Kwake katika hayo. Na ushahidi ni Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ﴿١٦﴾

“Je, mnadhani mko katika amani na (Allaah) Aliyeko mbinguni kwamba Hatokudidimizeni ardhini, tahamaki hiyo inatikisika?”

 

أَمْ أَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ﴿١٧﴾

“Au mnadhani mko katika amani na (Allaah) Aliyeko mbinguni kwamba Hatokutumieni tufani ya mawe? Basi mtajua vipi Maonyo Yangu!” [Al-Mulk (67:16-17)]

 

Na Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ ﴿٥﴾

“Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah), Yuko juu (Istawaa) ya ‘Arsh.” [Twaahaa (20:5)]

 

Kauli Ya Nne: 

Ina maana kutangulizwa na kuakhirishwa, yaani: Yeye Allaah Anajua siri zenu na ya dhahiri yenu mbinguni na ardhini. Na hii ni kauli ya Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما).

 

Kauli iliyo na nguvu kabisa katika kauli hizo nne ni:

 

Kauli ya kwanza ambayo ni kauli ya wengi katika Wafasiri wa Qur-aan, pamoja na kwamba kuna uwezekano wa kauli nyingine katika hizo, kwa sababu kila kauli ina ushahidi wake katika Qur-aan.

 

Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (رحمه الله)     amesema: “Imaam wakubwa kama Imaam Ahmad na wengineo wameifasiri kwamba: “Kuwa Yeye Ni Mwabudiwa mbinguni na ardhini.” [Al-Furqaan Bayna Awliyaair-Rahmaan Wa-Awliyaa Ash-Shaytwaan (244)]

 

Ibn Kathiyr (رحمه الله)  amesema “Kauli iliyo sahihi kabisa ni kwamba: “Allaah Anaombwa mbinguni na ardhini, yaani Anaabudiwa, Anapwekeshwa, Anakiriwa kwa Uabudiwa na Anaitwa Allaah. Naye Anaombwa na wote kwa utashi na khofu isipokuwa wakanushaji katika majini na wanaadamu.”  [Tafsiyr Al-Qur-aan Al-‘Adhwiym, (3/240)]

 

[2] Makafiri Wanatakiwa Watembee Maeneo Mbalimbali Wakatambue Hatima Za Waliokanusha Kabla Yao:

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Anawatanabahisha makafiri, washirikina na wakanushaji wowote wale wa Tawhiyd Yake na Kuwakanusha Rusuli Wake kwa kuwataka waende nchi na maeneo mbalimbali ili wakajionee na watambue adhabu zilizowakumba wenzao wa kabla yao. Allaah (سبحانه وتعالى)  Anataja hivyo katika Suwrah na Aayah mbalimbali. Kati ya Suwrah hizo ni pamoja na Aal-‘Imraan (3:137), Faatwir (35:43-44), Yuwsuf (12:109), An-Naml (37:69), Al-‘Ankabuwt (29:20), Ar-Ruwm (30:9) (30:42), Al-Hajj (22:46), Ghaafir (40:82) na Muhammad (47:10).

 

[3] Kuthibitisha Sifa Za Allaah (سبحانه وتعالى): Rejea Al-Fat-h (48:10), Huwd (11:37).

 

[4] Nyoyo Za Makafiri Zimefunikwa Na Masikio Yao Yana Uziwi:

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Anafahamisha kuwa miongoni mwa washirikina ni wale wanaoisikiliza Qur-aan kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) lakini hawanufaiki na kusikiliza huku. Na kwa sababu hiyo, Allaah (سبحانه وتعالى) Anajaalia vifuniko juu ya nyoyo zao ili wasije wakaifahamu, na Anaweka uziwi masikioni mwao ili wasiisikie kwa sababu ya ukaidi wao na ukanushaji wao, na hata wangeona dalili gani na hoja zilizowazi vipi, wasingeliamini.

 

Na si kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Anawajaalia vifuniko nyoyoni mwao na uziwi masikioni bila ya sababu tu kama kwamba ni dhulma, Hasha! Allaah (سبحانه وتعالى)  Hadhulumu chembe ya uzito wa atomu! Bali Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Ujuzi Wake Ameshajua kuwa watu hawa kamwe hawataamini kama vile Alivyojua kuwa Abu Lahab ambaye ni ammi yake Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) hatoamini, Akateremsha Wahy wa Suwrat Al-Masad (111)  wakati Abu Lahab yungali hai, kwani Allaah (سبحانه وتعالى) Angelijua kuwa atakuja kuamini angali yuhai, basi Asingeteremsha Suwrah ya Qur-aan inayomtaja jina Lake, ukanushaji wake, ukafiri wake na adhabu yake. Na hivyo ndivyo hali ya washirikina na makafiri hawa, kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Ameshajua kuwa hawataamini kamwe ndipo Anapojaalia vifuniko nyoyoni mwao na uziwi masikioni mwao.

 

Na maneno haya Ayasemayo Allaah katika Aayah hii, yalisemwa na wenyewe makafiri na washirikina wa Makkah: 

 

وَقَالُوا قُلُوبُنَا فِي أَكِنَّةٍ مِّمَّا تَدْعُونَا إِلَيْهِ وَفِي آذَانِنَا وَقْرٌ وَمِن بَيْنِنَا وَبَيْنِكَ حِجَابٌ فَاعْمَلْ إِنَّنَا عَامِلُونَ﴿٥﴾

“Na wakasema: Nyoyo zetu zimo katika vifuniko kwa yale unayotuitia, na masikioni mwetu mna uziwi, na baina yetu na baina yako kuna kizuizi, basi tenda nasi tunatenda.” [Fusw-Swilat (41:5)]

 

Na Allaah (سبحانه وتعالى)  Anataja kuweka vifuniko nyoyoni ili zisifahamu kitu kama Anavyosema:

فَإِنَّهَا لَا تَعْمَى الْأَبْصَارُ وَلَـٰكِن تَعْمَى الْقُلُوبُ الَّتِي فِي الصُّدُورِ ﴿٤٦﴾

Kwani hakika hayapofuki macho, lakini zinazopofuka ni nyoyo zilizomo vifuani.” Rejea Al-Hajj (22:46) ambako kuna maelezo bayana kuhusu maana ya kupofuliwa nyoyo badala ya macho.

 

Kwa muktadha huu, mtu ambaye haamini Aakhirah, basi kamwe hatauona ujumbe wa Qur-aan kuwa una thamani kwake, wala hatokuwa na hisia ya imaan ya kuiamini Qur-aan, bali atahangaikia maisha na manufaa ya dunia na starehe za dunia anazoweza kuzihisi na kuzifurahikia.  Ama Qur-aan, hiyo haitamfikia moyoni mwake kamwe!

 

Na hii inarejelea Qadar ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwamba Anafanya hivyo kwa kuwa mtu ana uhuru wa kufuata njia mbili; ya hidaya na ya upotofu. Naye ni Mjuzi wa anayehidika na anayepotoka.  Kwa ajili hiyo, wale wanaomkanusha Yeye na Ujumbe Wake na wakamshirikisha, Anawaachia wafanye watakavyo bila ya kuwaadhibu, lakini huko Aakhirah watakapofika ndipo watakapojuta na wakatamani kurudi duniani waamini.

 

[5] Makafiri Hawakuamini Kwamba Watafufuliwa: Rejea Al-Israa (17:49).

 

[6] Kitabu: Lawh Al-Mahfuwdhw (Ubao Uliohifadhiwa) Au Qur-aan [Tafsiyr Imaam As-Sa’diy] Rejea Al-Buruwj (85:22).       

 

[7] Kuthibitisha Sifa Za Allaah (سبحانه وتعالى): Rejea Aayah (12) ya Suwrah hii.

 

[8] Maana Ya Ghaibu:  Rejea Al-Baqarah (2:3), Luqmaan (31:34) na An-Naml (27:65).

 

[9] Hakuna Kinachofichika Kwa Allaah (سبحانه وتعالى); Kiwe Cha Dhahiri Wala Cha Siri, Kikubwa Wala Kidogo Vipi:

 

Rejea Ghaafir (40:19) kwenye maelezo na rejea mbalimbali.

 

[10] Usingizi Ni Mauti Madogo. Rejea Az-Zumar (39:42).

 

[11] Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!: 

 

Rejea Luqmaan (31:13) kwenye maelezo bayana.

 

[12] Manabii Na Rusuli Kumi Na Nane Wametajwa Kuanzia Aayah Hii Na Zinazofuatia:

 

Kuanzia Aayah hii Al-An’aam (6:83) hadi (6:86) wametajwa Manabii kumi na nane, akijumuika na Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) ambaye ameelezewa katika Aayah zilizotangulia. Wengineo waliotajwa katika Suwrah nyenginezo ni: Aadam, Idriys, Huwd, Swaalih, Shu’ayb (عليهم السّلام) na Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم).

 

Suwrah nyenginezo zilotaja Manabii kwa wingi ni: Al-Anbiyaa (21), Maryam (19), Asw-Swaffaat (37), Swaad (38).

 

Rejea pia An-Nisaa (4:69) kupata maelezo kuhusu Manabii na tofauti ya Manabii na Rusuli.

 

Na Manabii na Rusuli, si wote waliosimuliwa katika Qur-aan kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Kauli Zake kwenye Suwrah An-Nisaa (4:164) na Ghaafir (40:78).

 

 

[13] Shirki Inabatilisha Amali: Rejea Az-Zumar (39:65) kwenye maelezo ya aina za shirki.

 

[14] Ummul-Quraa (Makkah): Sababu Za Kuitwa Ummul-Quraa (Mama Wa Miji), Umuhimu Na Fadhila Zake:

 

Mji wa Makkah unaitwa Ummul-Quraa (Mama wa miji) kwa sababu kadhaa. Miongoni mwazo ni:  

 

(i) Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):  

وَلِتُنذِرَ أُمَّ الْقُرَىٰ وَمَنْ حَوْلَهَا

“Na ili uonye (kwacho) Ummul-Quraa (Mama wa miji [Makkah]), na wale ambao wameuzunguka.”

 

Baadhi ya ‘Ulamaa wamesema: Mji wa Makkah umeitwa “Ummul Quraa” (Mama wa miji) kwa kuwa ndio asili ya miji yote ya ardhi, na kutokea hapo, ardhi ndipo ilipotandazwa. Na kwa sababu hiyo, mji wa Makkah uko katikati ya dunia.

 

Na ndio maana Makkah ukawa ni mji mkongwe kabisa uliojulikana kwa watu.

 

(ii) Mji wa Makkah una historia ya Nabiy Ismaa’iyl na baba yake Nabiy Ibraahiym (عليهما السلام). Pia Mama yake Nabiy Ismaa’iyl (Haajar) ambaye alisai baina ya Swafaa na Marwaa kusaka maji na kububujika kwa maji ya Zamzam. Pia Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام)  kujenga Al-Ka’bah, kisha akasimama kuomba duaa katika Maqaam Ibraahiym (Jiwe ambalo alisimama juu yake wakati wa ujenzi wa Al-Ka’bah) ambapo Waislamu wote wanaswali Rakaa mbili baada ya kutufu Al-Ka’bah. Rejea Al-Baqarah (2:125-129), Ibraahiym (14:35-42).

 

(iii) Nyumba ya kwanza ambayo imeasisiwa kwa ajili ya watu kufanya ibaada kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Suwrat Aal-‘Imraan (3:96).

 

(iv) Nabiy wa Mwisho kabisa Muhammad  (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye ametokana na kizazi cha Nabiy Ismaa’iyl (عليه السّلام), kuzaliwa humo na akaishi humo na ndipo alipoteremshiwa Wahy wa Qur-aan humo akaishi humo hadi kuhajiri Madiynah. 

 

(v) Masjid Al-Haraam iliyoko Makkah ni Msikiti wa kwanza kuanzishwa duniani kama ilivyothibiti katika Hadiyth: Abuu Dharr (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Masjid gani ilijengwa ardhini mwanzo?  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Masjid Al-Haraam (Makkah).” Nikasema: Kisha upi? Akasema: “Masjid Al-Aqswaa (Palestina).” Nikasema: Kuna muda gani baina ya kuwepo Masjid mbili hizo? Akasema: “Miaka arubaini na popote itakapokudiriki Swalaah basi swali hapo pia ardhi ni mahala pa kuswali.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

(vi) Ni kivutio na kipenzi cha Waumini wa ulimwengu wote kwa sababu, baada ya Nabiy Ibraahim (عليه السّلام) [na mwanawe Nabiy Ismaa’iyl  (عليه السّلام)] kujenga Al-Ka’bah, aliomba duaa kwamba nyoyo za watu zipendelee kuelekea huko. Rejea Ibraahiym (14:38).

 

(vii) Qibla cha Waislamu wote duniani kimo humo, kwa maana, Waislamu wote ulimwenguni wanaekelekea huko katika Swalaah zao, kitendo ambacho bila ya kuelekea Qiblah, Swalaah hitimii.

 

(viii) Swalaah inayoswaliwa humo ina thawabu maradufu: Amesimulia Jaabir (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)   amesema: “Swalaah katika Msikiti wangu ni bora kuliko Swalaah elfu kwengineko isipokuwa Al-Masjid Al-Haraam. Na Swalaah katika Al-Masjid Al-Haraam ni bora kuliko Swalaah elfu mia (laki moja) kwengineko.” [Ahmad, Ibn Maajah na imesahihishwa na Imaam Al-Albaaniy katika Swahiyh Ibn Maajah (1163), Swahiyh Al-Jaami’ (3838)]

 

(ix) Makkah ni mji Mtukufu kabisa na mambo kadhaa yameharamishwa ndani yake na ndio maana Makkah ikaitwa Haram Makkah. Hadiyth ifuatayo imetaja baadhi ya maharamisho: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah Ameuharamisha Mji huu Siku Allaah Alipoumba mbingu na ardhi. Basi Mji huu ni hifadhi isiyoguswa kwa Haramisho la Allaah hadi Siku ya Qiyaamah, na hakuruhusiwa yeyote kabla yangu kupigana ndani yake, na haikuruhusiwa kwangu isipokuwa saa moja ya mchana. Basi ni hifadhi isiyoguswa kwa Haramisho la Allaah mpaka Siku ya Qiyaamah. Mwiba wake haukatwi, wala wanyama wake wa kuwindwa hawatimuliwi, wala  haokoti chenye kupotezwa humo isipokuwa mwenye kukitangazia, na wala manyasi yake hayakatwi.” Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Isipokuwa “idh-khir” (aina ya mmea wenye harufu nzuri, [mchaichai]), kwani huo ni kwa mhunzi (kuwashia moto) na kwa (kuezekea paa za) nyumba zao. Akasema: “Isipokuwa idh-khir.” [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (1834) na Muslim (1353)]

 

(x) Umrah na Hajj inatekelezwa huko Makkah na Hajj ni nguzo mojawapo katika nguzo tano za Uislamu.

 

Na mengineyo yametajwa kuhusu utukufu wa Makkah na Allaah Mjuzi zaidi.

 

[15] Waongo Waliodai Unabii Baada Ya Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

Amesema ‘Ikrimah na Qataadah  (رضي الله عنهما): “Aayah hii imeteremshwa kumhusu Musaylamah Al-Kadh-dhaab Laana ya Allaah imfikie!” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

Na Imaam As-Sa’adiy (رحمه الله)   amesema: “Waliojumuishwa katika Aayah hii ni wale wote wanaodai Unabii kama Musaylamah Al-Kadh-dhaab, Al-Aswad Al-‘Ansiyy, Mukhtaar na wengineo.” [Tafsiyr As-Sa’diy]. Wametajwa wawili hao katika Hadiyth ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).  

 

Amesimulia Naafi’ Bin Jubayr (رضي الله عنه): Ibn ‘Abbaas  (رضي الله عنهما) amesema: Musaylamah Al-Kadh-dhaab (yaani mrongo), alikuja na watu wake wengi Madiynah) katika zama za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawa anasema: “Lau Muhammad atanifanya mimi kuwa mrithi baada yake, basi nitamfuata.” Na watu wengi katika kaumu yake wakamfuata. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)        alimwendea akiwa na Thaabit bin Qays bin Sham-maas, na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa ameshika mkononi mwake kitagaa cha mtende (kipande cha jani la mtende). Akasimama mbele ya Musaylamah na watu wake, akasema: “Lau utaniomba kipande hiki (kitagaa), sitokupatia. Na wala huwezi kuikwepa Amri ya Allaah Aliyokuhukumia. Na ukiukanusha Uislamu, basi Allaah Atakuangamiza. Na wewe kwa hakika nakuona ni mtu mwenye sifa zile zile nilizoonyeshwa kwenye njozi.”  Abu Hurayrah (رضي الله عنه) aliniambia kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)   amesema: “Nilipokuwa nimelala, niliona katika njozi vikuku viwili vya dhahabu mkononi mwangu, na hilo likanitia hamu mno. Kisha nikafunuliwa Wahy katika njozi hiyo nivipulize, nikavipuliza navyo vikaruka. Nikatafsiri njozi ya vikuku hivyo kuwa ni ishara ya waongo wawili watakaokuja baada yangu. Mmoja wao ni Al-‘Ansiyy, na mwengine ni Musaylamah Al-Kadh-dhaab kutoka Al-Yamaamah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

[16] Viumbe Watafufuliwa Wakiwa Kama Walivyozaliwa: Rejea Al-Kahf (18:48), Al-Anbiyaa (21:104).

 

[17] Allaah (سبحانه وتعالى)  Mpasuaji Mbegu Na Anatoa Kilicho Hai Kutokana Na Kilicho Mfu, Na Mtoaji Wa Kilicho Mfu Kutokana Na Kilicho Hai.

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Anaeleza kuwa Yeye huzifanya mbegu za nafaka na za matunda kupasuka na kuchipua ardhini, na kutoa aina mbalimbali ya nafaka, matunda, mboga na kadhaalika zikiwa katika rangi mbalimbali, umbo wa kila aina na ladha tofauti katika mazao hayo. Rejea Ar-Ra’d (13:3-4). Na kwamba Analeta mmea ulio hai kutoka mbegu ya nafaka na mbegu ya matunda, (mbegu) ambazo zisizokuwa  na uhai na hii ni ishara na dalili mojawapo ya kuwa Yeye Ni Muumbaji wa kila kitu [Az-Zumar (39:62)] Na kama Anavyosema:

 

وَآيَةٌ لَّهُمُ الْأَرْضُ الْمَيْتَةُ أَحْيَيْنَاهَا وَأَخْرَجْنَا مِنْهَا حَبًّا فَمِنْهُ يَأْكُلُونَ ﴿٣٣﴾

“Na Aayah (Ishara, Dalili) kwao ni ardhi iliyokufa, Tukaihuisha, na Tukatoa humo nafaka, wakapata kuzila.” [Yaasiyn (36:33)]

 

Hali kadhalika Kauli Yake hii Allaah (سبحانه وتعالى):

  

يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَمُخْرِجُ الْمَيِّتِ مِنَ الْحَيِّ

“Anatoa kilicho hai kutokana na kilicho mfu, na Mtoaji wa kilicho mfu kutokana na kilicho hai.” [Al-An’aam (6:95)]  

 

Ni mfano wa Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Kujaalia yai kutoka kwa kuku, kuzaliwa kuku kutokana na yai.  [Tafsiyr Ibn Kathiyr]  

 

Rejea Aal-‘Imraan (3:26-27), Yuwnus (10:31), Ar-Ruwm (30:19), (30:50),  na Yaasiyn (36:38) kwenye faida tele na maelezo bayana kuhusu Qudura, Takdiri ya Allaah (سبحانه وتعالى). 

 

[18] Takdiri (Qudura, Ukadariaji) Ya Allaah (سبحانه وتعالى): Rejea Aal-‘Imraan (3:190),  (3:26-27)  Yaasiyn (36:38), Al-Falaq (113:1).

 

[19] Nyota Zimeumbwa Kwa Ajili Ya Matatu:

 

Rejea pia An-Nahl (16:16).

 

Amesimulia Qataadah (رضي الله عنه) : “Allaah Ameumba hizi nyota kwa malengo matatu: (i) mapambo ya mbingu (ii) vimondo vya (kuwafukuza na kuwapiga) shaytwaan, (iii) alama za kuongoza njia (wasafiri wa majangwani na baharini). Basi atakayefasiri vingine amekosea na atakuta patupu Aakhirah (atakosa thawabu) kwani atakuwa amebeba asio na ilimu nayo kwa kuchupa mipaka ya ujuzi Wake.” [Al-Bukhaariy] 

 

Nyota zimeumbwa kwa ajili ya mambo matatu hayo tu! Basi Hadiyth hii inawakanusha wanajimu (watabiri wa nyota) jambo ambalo ni la kumshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى)  nayo ni shirki kubwa ambayo Allaah  (سبحانه وتعالى) Haisamehe.

 

[20] Mustaqarr (Mahali pa kustakiri) ni tumboni mwa mama au duniani. Mustawda’ (Mahali pa kuhifadhiwa) ima migongoni mwa baba au kaburini.

 

 

[21] Washirikina Wamempachikia Uongo Allaah Kuwa Ana Wana Wa Kike Na Wa Kiume: Rejea Asw-Swaffaat (37:149).

 

[22]  Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) Hakumuona Allaah (سبحانه وتعالى):

 

Masruwq (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Nilimwambia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Ee Mama! Je Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake? Akasema: Hayo uliyoyasema yamefanya nywele zangu zisimame kunisisimka mwili! Tambua kwamba mtu akikutajia mambo matatu yafuatayo basi yeye ni muongo! Atakayesema kwamba Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) amemuona Rabb wake, kisha akasoma:

 

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ ۖ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ ﴿١٠٣﴾

“Macho hayamzunguki bali Yeye Anayazunguka macho yote, Naye Ni Mwenye Kudabiri mambo kwa Ulatifu, Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.” [Al-An'aam (6:103)]

 

Na akasoma pia:

 

وَمَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُكَلِّمَهُ اللَّـهُ إِلَّا وَحْيًا أَوْ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ أَوْ يُرْسِلَ رَسُولًا فَيُوحِيَ بِإِذْنِهِ مَا يَشَاءُ ۚ إِنَّهُ عَلِيٌّ حَكِيمٌ﴿٥١﴾

“Na wala haikuwa kwa mtu yeyote kwamba Allaah Amsemeze isipokuwa kwa Wahy au kutoka nyuma ya kizuizi, au Hutuma Mjumbe, kisha Anamfunulia Wahy Ayatakayo kwa Idhini Yake. Hakika Yeye Ni Mwenye ‘Uluwa, Mwenye Hikmah wa yote.” [Ash-Shuwraa (42:51)]

 

Kisha akaendelea kusema: Na atakayesema kwamba Nabiy anajua yatakayotokea kesho basi ni muongo. Kisha Akasoma:

وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَّاذَا تَكْسِبُ غَدًا ۖ

“Na nafsi yoyote haijui nini itachuma kesho, na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani.” [Luqmaan (31:34)]

 

Kisha akasema: Na atakayesema kuwa Nabiy ameficha aliyofunuliwa Wahyi (na maamrisho) basi ni muongo! Kisha akasoma:

 

يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ ۚ  

“Ee Rasuli! Balighisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako. Na usipofanya, basi utakuwa hukubalighisha ujumbe Wake.” [Al-Maaidah (5:67)]

 

Kisha akasema: Lakini Nabiy alimuona Jibriyl katika umbile lake khalisi mara mbili. [Al-Bukhaariy]

 

Kwa upande mwengine Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Allaah, na akasema kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake mara mbili. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]  

 

Al-Haafidhw, Ibn Hajar amesema: “Maelezo ya Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) yamekuja katika hali ya kutodhibitiwa (hayaelezi kama Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake kwa macho yake au vipi) wakati kauli za Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) na wenziwe zimedhibitiwa kwa kusema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakumuona Allaah “Kwa macho yake.” Tunaweza kuunganisha kauli hizo mbili kwa kusema Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها)   alikataa muono “Kwa macho yake” na kauli ya Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  kuwa ni kamuona kiroho.” [Fat-hul-Baariy (8/608)]  

 

Na Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwa riwaaya nyingine alisema kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake wakati akiwa katika usingizi, na hii ni njozi ya kweli. Na kauli ya Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) inakataa, na kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakumuona Rabb wake wakati yeye akiwa macho, lakini kauli hiyo haikatazi kuwa  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake akiwa usingizini. Alichokana hapa ni kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakumuona Allaah kwa macho yake meupe, akiwa macho.  

 

Wale ambao wanao msimamo kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake kwa macho yake meupe wanaleta Hadiyth dhaifu. Hakuna Hadiyth Swahiyh ambayo inaeleza ya kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake kwa macho yake akiwa macho. Wenye msimamo huo wanaleta Hadiyth ya At-Tirmidhiy ambayo Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) anasema kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake. ‘Ikrimah alimuuliza: “Vipi Aayah ambayo inasema:

 

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ ۖ

“Macho hayamzunguki, bali Yeye Anayazunguka macho yote.” [Al-An’aam (6:103)]

 

Alijibu, kuwa ni wakati tu Allaah amezungukwa na Nuru, lakini Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake mara mbili. “Hadiyth hii ni dhaifu.”

 

Kwa hali hiyo, hakuna mgongano wa kauli, na Allaah Anajua zaidi [Sharh ya Uswuwl Al-I’itiqaad cha Al-Laalika’iy, (93/512), As-Sunnah (1/181) na Swifaat Al-Maqdisiy ukurasa (109-111]   

 

Hapa kunathibitishwa kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakumuona Rabb wake wakati alipopelekwa Al-Israa Wal Mi’raaj, na dalili nyengine ni Hadiyth ifuatayo:

 

Amesimulia Abu Dharr (رضي الله عنه): Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): Je ulimuona Rabb wako? Akasema: “(Yeye ni) Nuru; vipi niweze kumuona?” [Muslim]

 

Na hii ndio ‘Aqiydah ya Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah kuwa Allaah Haonekani duniani, kinyume na ‘Aqiydah ya Masufi wanaoamini kuwa Allaah Anaonekana duniani kwa kuegemeza tukio hilo la Al-Israa Wal Mi’raaj.

 

Kadhaalika, Aayah hiyo vilevile haikanushi kuonekana Allaah Qiyaamah, bali Qiyaamah Allaah Ataonekana katika kisimamo cha Qiyaamah katika Jannah (Peponi) kwa dalili nyingi kutoka katika Qur-aan na Sunnah, kinyume na ‘Aqiydah ya makundi potofu yanayoamini kuwa Allaah Hatoonekana Aakhirah.

 

[23] Haramisho La Kuwatukana Watu Ili Tusi Lisimrudie Asiyestahiki Kutukanwa:

 

Tahadharisho kama hili la kutokuwatukana waabudiwa wa washirikina ili tusi lisimrudie Allaah (سبحانه وتعالى), limeharamishwa pia vile mtu kumtukana mzazi wa mwenziwe, ili tusi lisimrudie mzazi wake:

 

 

عَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ ‏رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا‏ أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {مِنْ اَلْكَبَائِرِ شَتْمُ اَلرَّجُلِ وَالِدَيْهِ.‏ قِيلَ: وَهَلْ يَسُبُّ اَلرَّجُلُ وَالِدَيْهِ؟ قَالَ: نَعَمْ.‏ يَسُبُّ أَبَا اَلرَّجُلِ، فَيَسُبُّ أَبَاهُ، وَيَسُبُّ أُمَّهُ، فَيَسُبُّ أُمَّهُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Amesimulia ‘Abdullaah bin ‘Amr bin Al-‘Aasw (رضي الله عنهما):  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Miongoni mwa madhambi makubwa ni mtu kutukana wazazi wake.” Swahaba wakasema: Mtu anaweza kutukana wazazi wake? Akasema: “Ndiyo, atamtukana baba wa mtu naye anamtukana baba yake, na atamtukana mama wa mtu naye atamtukana mama yake.” [Bukhaariy, Muslim]

 

Imaam As-Sa’diy (رحمه الله) amesema: Allaah (سبحانه وتعالى) Anawakataza Waumini kufanya jambo ambalo mwanzo waliruhusiwa na hata kuamrishwa kulifanya; nalo ni kudharau na kutukana masanamu ya washirikina ambao wamewafanya ni waabudiwa wao badala ya Allaah. Kuruhusika kwake ilikuwa ni kwa sababu  kuwatukana waabudiwa wao ni kuwadhalilisha na  ilikuwa ni njia ya kujikurubisha kwa Allaah. Lakini kwa sababu kufanya hivyo kungeweza kupelekea washirikina kumtukana Rabb wa ulimwengu,  Ambaye Anatakasika na kila kosa na matukano au ovu lolote, Allaah Anakataza kuwatukana waabudiwa wa  washirikina, kwa sababu watahamasika kulinda dini yao na watataka kujikurubisha kwa waabudiwa wao. Hivyo ni kwa kuwa Allaah Amewapambia kila umma matendo yake,  wanafikiri kwamba njia zao ni nzuri, basi ikiwa Waislamu watatukana waabudiwa wao, wao washirikina watawalinda kwa njia zote, hata kama ni matusi kwa Allaah  Rabb wa walimwengu. 

 

Lakini watu wote watarejea kwa Allaah Siku ya Qiyaamah kisha watahudhurishwa wao na vitendo vyao mbele Yake, na Awajulishe yale waliyokuwa wakiyafanya, mema na mabaya.

 

Aayah hii ni dalili kwamba njia za kutumika kufikisha jambo,  zinapaswa kuzingatiwa kwa malengo, na kwamba njia ambazo zinaweza kusababisha kitu kuwa haramu- hata kama njia hizo zinaruhusiwa- basi zinapaswa kuzingatiwa kuwa ni haramu pia, ikiwa zitaongoza kwenye maovu. [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

[24] Mfano Wa Kafiri Aliyekuwa Maiti (Katika Viza) Na Muumini Aliyekuwa Hai (Katika Nuru):

 

Aliyekuwa maiti kabla ya hidaaya ya Allaah, yaani alikuwa mwanzo katika viza vya kufru, ujahili na uasi,  kisha Allaah Akamhuisha katika nuru ya imaan, ilimu na utiifu, akatembea na nuru kati ya watu, akawa ni mtu ambaye ana utambuzi wa mambo yake, akiiongoza njia yake na akajua lililo jema na akajitahidi kulitekeleza mwenyewe na pia akalitekeleza katika uhusiano wake na wengineo. Hali kadhalika akatambua uovu na akauchukia na akijitahidi kuuepuka mwenyewe na kuwaepushia wenziwe.  Je, huyu yuko sawa na aliye katika viza vya ujahili, upindukiaji mipaka, kufru na maasi, hawezi kutoka humo, kwa sababu amechanganyikiwa; hajui apitie njia gani, hivyo amefunikwa na wasiwasi, shaka, dhiki na huzuni.

 

Hapa Allaah Anabainisha watu wenye busara kwamba, wao tayari wanajua na kuelewa kwamba hawa wawili hawawezi kulingana  sawa, kama vile hauwezi usiku na mchana kuwa sawa au mwanga na giza au  walio hai na wafu... [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

Rejea pia Faatwir (35:19) kwenye maelezo na faida ziyada kuhusu mifano ya Allaah baina ya kafiri na Muumin.  Rejea pia Huwd (11:24).

 

[25] Maana Ya Baghi Katika Qur-aan:

 

Rejea Ash-Shuwraa (42:14) kupata maana zake mbalimbali.

 

[26] Maana Ya Kutokufarikiana:

 

Rejea Al-Faatihah (1:6), Aal-‘Imraan (3:103).

 

[27] Kuteremka Allaah Na Malaika Siku Ya Qiyaamah:

 

Rejea Al-Fuqaan (25:25), Al-Haaqah (69:13-18), Al-Baqarah (2:210).

 

[28] Alama Kubwa Za Qiyaamah: Makafiri Hawakuamini Kuwa Qiyaamah Kitatokea:

 

Washirikina wa Makkah walikuwa haweshi kuuliza lini Qiyaamah kitatokea.  Rejea Al-A’raaf (7:187), Al-Ahzaab (33:63), An-Naazi’aat (79:42). Al-Mulk (67:25), Ash-Shuwraa (42:18), Ghaafir (40:59).

 

Aayah hii tukufu imetaja kuwa kutatokea Alama kuu kabla ya kufika Qiyaamah ambazo wale wasioamini kabla ya kutokea alama hizo, watakapotaka kuamini, basi imaan zao hazitawafaa lolote kwa kuwa hawatakubaliwa kuamini kwao.

 

‘Ulamaa wametaja alama hizo kubwa ingawa wamekhitilafiana katika mpangilio wake na kuzitaja kwake nazo ni:

 

(i) Kuja kwa Mahdi: Mja kutoka katika ahli wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) (ii)  Kutokeza kwa Masiyh Ad-Dajjaal (iii) Kuteremka kwa Nabiy ‘Iysaa na (عليه السّلام)  na kumuua Masiyh Ad-Dajjaal na kuondosha misalaba, kuua nguruwe na kuondosha dini zote nyenginezo isipokuwa Uislamu (iv) Kuchomoza kwa Yaajuwj na Maajuwj (v) Kubomolewa Ka’bah na kutoka moshi (vi) Kuondoshwa Qur-aan nyoyoni mwa Waumini na Miswahafu (vii) Jua kuchomoza Magharibi (viii) Kutokeza mnyama mwitu mkubwa atakayewasemesha watu (ix) Mididimizo mitatu ya ardhi: Mdidimizo wa Mashariki, Magharibi na katika Jaziyrah ya Arabia (x) Moto utakaotoka kutoka Yemen utawapeleka watu kufika katika Ardhi ya Mkusanyiko.

 

Na Hadiyth ifuatayo imeorodhesha alama kumi: 

 

Amesimulia Hudhayfah Bin Asiyd (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa chumbani nasi tulikuwa chini yake, akachungulia na kutuuliza:   “Mnajadiliana nini?” Tukasema: (Tunajadili kuhusu) Saa (Qiyaamah). Hapo akasema: Saa (Qiyaamah) hakitatokea mpaka zionekane alama (au ishara) kumi: (i) Kudidimia kwa Mashariki (ii) Kudidimia kwa Magharibi. (iii) Kudidimia Bara la Arabu (iv) Moshi. (v) (Masiyh) Ad-Dajjaal. (vi) Mnyama mkubwa wa ardhi (atakayewasemesha watu) (vii) Ya-ajuwj na Ma-ajuwj (viii) Kuchomoza jua upande wa Magharibi (ix) Moto utakaotokea  upande wa chini ya ‘Aden utakaowasukuma watu (kufikia Ardhi ya Mkusanyiko).”  Shu'bah   amesema na amenihadithia   ‘Abdul-‘Aziyz bin Rufa’y kutoka kwa Abiy Atw-Twufayl kutoka kwa Abiy Sariyhah Hadiyth kama hiyo  ila Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuitaja (alama ya kumi) lakini alisema kuwa katika kumi, mojawapo ni kuteremka Nabiy ‘Iysaa  bin Maryam (عليه السّلام) na katika riwaaya nyengine ni: Upepo mkali utakaowaendesha watu na kutupwa   baharini. [Muslim]

 

Rejea Al-Kahf (18:94) kulikotajwa kuhusu Yaajuwj na Maajuwj.

 

[29] Kugawanyika Watu Makundi Makundi:

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Anawakemea wale wanaoigawa Dini yao, yaani, kuigawanya na kufarikiana ndani yake, na kila mmoja anajiwekea sehemu ya majina ambayo haimnufaishi mtu katika dini yake chochote, kama vile Uyahudi, Unaswara na Umajusi. Au (Majina hayo) hayamtimizii mtu imaan yake kwayo, kwa kuchukua kitu katika sharia na kukifanya kuwa ndio dini yake, na kuacha kitu mfano wake, au kinachostahiki zaidi yake. Hivyo ni kama ilivyo kwa watu wa makundi ya bid’ah na upotofu na wanao farakanisha ummah. Na Aayah tukufu ikaashiria kuwa Dini inaamrisha umoja na muungano, na inakataza mifarakano na khitilafu katika watu wa dini, na katika masuala yake yote ya msingi na matawi. Akamuamuru kuwatenga wale walioigawa dini yao.  [Imaam As-Sa’diy katika Tafisyr yake]

 

Rejea pia Aayah (153) Suwrah hii ya Al-An’aam. 

 

[30]  Rahmah Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Kwa Waumini Kuongezewa Thawabu Mara Kumi Kwa Amali Njema Moja Na Kuandikiwa Dhambi Moja Tu Kwa Tendo Ovu:

 

Ukitia niya kutenda amali moja lakini ukawa hukujaaliwa kuitenda utaandikiwa moja. Utakapoweza kuitenda utalipwa mara kumi yake.

Ukitia niya kutenda uovu haitoandikwa kwanza kwa kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Anampa mja muhula ajirudi ili asitende uovu au dhambi. Na atakapotenda basi ataandikiwa dhambi moja.

Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:Allaah Ameandika mema na mabaya, kisha Akayabainisha, basi atakayetia niya kutenda jema kisha asilifanye, ataandikiwa jema moja kamili. Atakapofanya hima na akalitenda, ataandikiwa mema kumi hadi kuzidi mia saba na ziada nyingi. Na atakayetia niya kufanya kitendo kibaya kisha asikifanye, ataandikiwa jema moja kamili. Atakapokifanya, ataandikiwa dhambi moja.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

[31] Dua Mojawapo Ya Kufungulia Swalaah:

 

Aayah (6:162-163) ni mojawapo ya Dua ya kufungulia Swalaah kama ilivyothibiti katika Sunnah kusema:

 

وَجَّهـتُ وَجْهِـيَ لِلَّذي فَطَرَ السَّمـواتِ وَالأَرْضَ حَنـيفَاً وَمـا أَنا مِنَ المشْرِكين، إِنَّ صَلاتـي، وَنُسُكي، وَمَحْـيايَ، وَمَماتـي للهِ رَبِّ العالَمين، لا شَريـكَ لَهُ وَبِذلكَ أُمِرْتُ وَأَنا مِنَ المسْلِـمين.

Nimeuelekeza uso wangu kwa yule Ambaye Ameanzisha mbingu na ardhi hali ya kuelemea katika haki, na sikuwa mimi ni katika washirikina, hakika Swalaah yangu na kuchinja kwangu na uhai wangu, na kufa kwangu ni kwa Allaah Rabb walimwengu, Hana mshirika, na kwa hilo nimeamrishwa nami ni katika Waislamu. 

 

Na katika riwaaya nyenginezo inaishia kwa:

وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ

nami ni Muislamu wa kwanza.

(Kisha dua inaendelea)

 

Pia Aayah hii ni dalili mojawapo ya haramisho la kuchinja kwa kukusudia asiyekuwa Allaah.

 

 

Share