007 - Al-A'raaf

 

الأَعْرَاف

Al-A’raaf: 007

 

(Imeteremka Makkah)

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

المص ﴿١﴾

1. Alif Laam Miym Swaad.[1]

 

 

 

كِتَابٌ أُنزِلَ إِلَيْكَ فَلَا يَكُن فِي صَدْرِكَ حَرَجٌ مِّنْهُ لِتُنذِرَ بِهِ وَذِكْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ ﴿٢﴾

2. Kitabu (hiki) kimeteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) basi isiwe katika kifua chako dhiki kwa ajili yake, ili uwaonye kwacho na ni ukumbusho kwa Waumini.

 

 

 

اتَّبِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلَا تَتَّبِعُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ ۗ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ ﴿٣﴾

3. Fuateni yale mliyoteremshiwa kutoka kwa Rabb wenu na wala msifuate badala Yake marafiki walinzi. Ni machache mnayoyakumbuka.

 

 

 

وَكَم مِّن قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَاهَا فَجَاءَهَا بَأْسُنَا بَيَاتًا أَوْ هُمْ قَائِلُونَ ﴿٤﴾

4. Ni miji mingi sana Tumeiangamiza ikaifikia Adhabu Yetu usiku au walipokuwa katika usingizi wa mchana (qayluwlah).

 

 

 

فَمَا كَانَ دَعْوَاهُمْ إِذْ جَاءَهُم بَأْسُنَا إِلَّا أَن قَالُوا إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ ﴿٥﴾

5. Basi hakikuwa kilio chao ilipowajia Adhabu Yetu isipokuwa walisema: Hakika sisi tulikuwa madhalimu.

 

 

 

فَلَنَسْأَلَنَّ الَّذِينَ أُرْسِلَ إِلَيْهِمْ وَلَنَسْأَلَنَّ الْمُرْسَلِينَ ﴿٦﴾

6. Basi bila shaka Tutawauliza wale waliopelekewa Rusuli, na bila shaka Tutawauliza hao Rusuli.

 

 

 

فَلَنَقُصَّنَّ عَلَيْهِم بِعِلْمٍ ۖ وَمَا كُنَّا غَائِبِينَ ﴿٧﴾

7. Kisha Tutawasimulia kwa elimu (‘amali zao), na Hatukuwa Wenye Kukosekana.

 

 

 

وَالْوَزْنُ يَوْمَئِذٍ الْحَقُّ ۚ فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٨﴾

8. Upimaji wa haki utathibiti Siku hiyo. Basi ambao mizani zao zitakuwa nzito, hao ndio watakaofaulu.

 

 

 

وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُم بِمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَظْلِمُونَ ﴿٩﴾

9. Na ambao mizani zao zitakuwa khafifu, basi hao ni wale waliojikhasiri wenyewe kwa sababu ya kutozitendea haki Aayaat Zetu.

 

 

 

وَلَقَدْ مَكَّنَّاكُمْ فِي الْأَرْضِ وَجَعَلْنَا لَكُمْ فِيهَا مَعَايِشَ ۗ قَلِيلًا مَّا تَشْكُرُونَ ﴿١٠﴾

10. Kwa yakini Tumekumakinisheni katika ardhi na Tukawawekeeni humo mahitaji ya maisha. Kidogo sana kushukuru kwenu. 

 

 

 

وَلَقَدْ خَلَقْنَاكُمْ ثُمَّ صَوَّرْنَاكُمْ ثُمَّ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ لَمْ يَكُن مِّنَ السَّاجِدِينَ ﴿١١﴾

11. Na kwa yakini Tumekuumbeni kisha Tukakutieni sura, kisha Tukawaambia Malaika: Msujudieni Aadam. Wakasujudu isipokuwa Ibliys hakuwa miongoni mwa waliosujudu.

 

 

 

 

قَالَ مَا مَنَعَكَ أَلَّا تَسْجُدَ إِذْ أَمَرْتُكَ ۖ قَالَ أَنَا خَيْرٌ مِّنْهُ خَلَقْتَنِي مِن نَّارٍ وَخَلَقْتَهُ مِن طِينٍ ﴿١٢﴾

12. (Allaah) Akasema: Nini kilichokuzuia usisujudu Nilipokuamrisha? (Ibliys) Akasema: Mimi ni mbora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, na yeye Umemuumba kwa udongo.

 

 

 

قَالَ فَاهْبِطْ مِنْهَا فَمَا يَكُونُ لَكَ أَن تَتَكَبَّرَ فِيهَا فَاخْرُجْ إِنَّكَ مِنَ الصَّاغِرِينَ ﴿١٣﴾

13. (Allaah) Akasema: Basi shuka kutoka humo, kwani haikupasa kwako utakabari humo. Hivyo toka! Hakika wewe ni miongoni mwa walio duni na dhalili.

 

 

 

قَالَ أَنظِرْنِي إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ ﴿١٤﴾

14. (Ibliys) Akasema: Nipe muhula hadi Siku watakapofufuliwa

 

 

 

قَالَ إِنَّكَ مِنَ الْمُنظَرِينَ ﴿١٥﴾

15. (Allaah) Akasema: Hakika wewe ni miongoni mwa waliopewa muhula.

 

 

 

قَالَ فَبِمَا أَغْوَيْتَنِي لَأَقْعُدَنَّ لَهُمْ صِرَاطَكَ الْمُسْتَقِيمَ ﴿١٦﴾

16. (Ibliys) Akasema: Basi kwa kuwa Umenihukumia kupotoka, nitawakalia chonjo (Waja Wako) katika Njia Yako iliyonyooka.

 

 

 

ثُمَّ لَآتِيَنَّهُم مِّن بَيْنِ أَيْدِيهِمْ وَمِنْ خَلْفِهِمْ وَعَنْ أَيْمَانِهِمْ وَعَن شَمَائِلِهِمْ ۖ وَلَا تَجِدُ أَكْثَرَهُمْ شَاكِرِينَ ﴿١٧﴾

17. Kisha nitawaandama mbele yao na nyuma na kuliani kwao na kushotoni kwao, na wala Hutopata wengi wao wenye kushukuru.

 

 

 

قَالَ اخْرُجْ مِنْهَا مَذْءُومًا مَّدْحُورًا ۖ لَّمَن تَبِعَكَ مِنْهُمْ لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنكُمْ أَجْمَعِينَ ﴿١٨﴾

18. (Allaah) Akasema: Toka humo ukiwa umekosa heshima na umefukuzwa! Atakayekufuata miongoni mwao, bila shaka Nitaijaza Jahannam kwa nyinyi nyote.

 

 

 

وَيَا آدَمُ اسْكُنْ أَنتَ وَزَوْجُكَ الْجَنَّةَ فَكُلَا مِنْ حَيْثُ شِئْتُمَا وَلَا تَقْرَبَا هَـٰذِهِ الشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿١٩﴾

19. Na ee Aadam! Ishi wewe na mkeo Jannah na mle humo popote mpendapo, na wala msikaribie mti huu, msijekuwa miongoni mwa madhalimu.

 

 

 

فَوَسْوَسَ لَهُمَا الشَّيْطَانُ لِيُبْدِيَ لَهُمَا مَا وُورِيَ عَنْهُمَا مِن سَوْآتِهِمَا وَقَالَ مَا نَهَاكُمَا رَبُّكُمَا عَنْ هَـٰذِهِ الشَّجَرَةِ إِلَّا أَن تَكُونَا مَلَكَيْنِ أَوْ تَكُونَا مِنَ الْخَالِدِينَ ﴿٢٠﴾

20. Basi shaytwaan (naye ni Ibliys) akawatia wasiwasi ili awafichulie sehemu zao za siri zilizositiriwa. Na akasema: Rabb wenu Hakukukatazeni huu mti isipokuwa msijekuwa Malaika wawili au kuwa miongoni mwa wenye kudumu milele.

 

 

 

وَقَاسَمَهُمَا إِنِّي لَكُمَا لَمِنَ النَّاصِحِينَ ﴿٢١﴾

21. Naye akawaapia: Hakika mimi ni katika wenye kukunasihini kidhati.

 

 

 

 

فَدَلَّاهُمَا بِغُرُورٍ ۚ فَلَمَّا ذَاقَا الشَّجَرَةَ بَدَتْ لَهُمَا سَوْآتُهُمَا وَطَفِقَا يَخْصِفَانِ عَلَيْهِمَا مِن وَرَقِ الْجَنَّةِ ۖ وَنَادَاهُمَا رَبُّهُمَا أَلَمْ أَنْهَكُمَا عَن تِلْكُمَا الشَّجَرَةِ وَأَقُل لَّكُمَا إِنَّ الشَّيْطَانَ لَكُمَا عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿٢٢﴾

22. Basi akawachota (wote wawili) kwa kuwalaghai. Walipoonja mti ule tupu zao zilifichuka, hapo wakaanza kuzibandika majani ya Jannah. Na Rabb wao Akawaita: Je, kwani Mimi Sikukukatazeni mti huo na kukuambieni kwamba shaytwaan ni adui bayana kwenu?

 

 

 

 

قَالَا رَبَّنَا ظَلَمْنَا أَنفُسَنَا وَإِن لَّمْ تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٢٣﴾

23. Wakasema: Rabb wetu! Tumedhulumu nafsi zetu, na basi Usipotughufuria na Ukaturehemu, bila shaka tutakuwa miongoni mwa waliokhasirika.

 

 

 

 

قَالَ اهْبِطُوا بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ وَلَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُسْتَقَرٌّ وَمَتَاعٌ إِلَىٰ حِينٍ ﴿٢٤﴾

24. (Allaah) Akasema: Shukeni! Nyinyi kwa nyinyi ni maadui. Na ardhi itakuwa ndio mastakimu yenu na starehe kwenu mpaka muda mahsusi.

 

 

 

قَالَ فِيهَا تَحْيَوْنَ وَفِيهَا تَمُوتُونَ وَمِنْهَا تُخْرَجُونَ ﴿٢٥﴾

25. Akasema: Humo mtaishi, na humo mtakufa, na kutoka humo mtatolewa (kufufuliwa).

 

 

 

يَا بَنِي آدَمَ قَدْ أَنزَلْنَا عَلَيْكُمْ لِبَاسًا يُوَارِي سَوْآتِكُمْ وَرِيشًا ۖ وَلِبَاسُ التَّقْوَىٰ ذَٰلِكَ خَيْرٌ ۚ ذَٰلِكَ مِنْ آيَاتِ اللَّـهِ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ ﴿٢٦﴾

26. Enyi wana wa Aadam! Kwa yakini Tumekuteremshieni libasi (nguo) inayositiri tupu zenu na libasi ya mapambo. Na libasi ya taqwa ndiyo bora zaidi. Hizo ni katika Ishara za Allaah ili wapate kukumbuka.

 

 

 

يَا بَنِي آدَمَ لَا يَفْتِنَنَّكُمُ الشَّيْطَانُ كَمَا أَخْرَجَ أَبَوَيْكُم مِّنَ الْجَنَّةِ يَنزِعُ عَنْهُمَا لِبَاسَهُمَا لِيُرِيَهُمَا سَوْآتِهِمَا ۗ إِنَّهُ يَرَاكُمْ هُوَ وَقَبِيلُهُ مِنْ حَيْثُ لَا تَرَوْنَهُمْ ۗ إِنَّا جَعَلْنَا الشَّيَاطِينَ أَوْلِيَاءَ لِلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٢٧﴾

27. Enyi wana wa Aadam! Asikufitinisheni kabisa shaytwaan kama alivyowatoa wazazi wenu katika Jannah huku akiwavua nguo zao ili awaonyeshe sehemu zao za siri. Hakika yeye (Ibliys) na kabila yake (ya mashaytwaan) wanakuoneni, na nyinyi hamuwaoni. Hakika Sisi Tumewafanya mashaytwaan kuwa ni marafiki wandani kwa wale wasioamini.

 

 

 

وَإِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً قَالُوا وَجَدْنَا عَلَيْهَا آبَاءَنَا وَاللَّـهُ أَمَرَنَا بِهَا ۗ قُلْ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَأْمُرُ بِالْفَحْشَاءِ ۖ أَتَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٢٨﴾

28. Na wanapofanya jambo chafu husema: Tumewakuta katika hali hii baba zetu, na Allaah Ametuamrisha hayo. Sema: Hakika Allaah Haamrishi machafu. Je mnamzulia Allaah msiyoyajua?

 

 

 

قُلْ أَمَرَ رَبِّي بِالْقِسْطِ ۖ وَأَقِيمُوا وُجُوهَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَادْعُوهُ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ ۚ كَمَا بَدَأَكُمْ تَعُودُونَ ﴿٢٩﴾

29. Sema: Rabb wangu Ameniamrisha uadilifu. Na elekezeni nyuso zenu (Kwake Pekee Allaah) katika kila sehemu (au nyakati) mnaposujudu na mwombeni Yeye kwa kumtakasia Yeye Dini. Kama Alivyokuanzisheni mtarudi (tena Kwake).

 

 

 

فَرِيقًا هَدَىٰ وَفَرِيقًا حَقَّ عَلَيْهِمُ الضَّلَالَةُ ۗ إِنَّهُمُ اتَّخَذُوا الشَّيَاطِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ اللَّـهِ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُم مُّهْتَدُونَ ﴿٣٠﴾

30. Kundi Ameliongoa, na kundi (jingine) limethibitikiwa upotofu. Hakika wao wamewafanya mashaytwaan kuwa marafiki wandani badala ya Allaah na wanadhani kwamba wao wamehidika.

 

 

 

يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ ﴿٣١﴾

31. Enyi wana wa Aadam! Chukueni mapambo yenu (ya mavazi ya sitara na twahara) katika kila mahala pa ‘Ibaadah.[2] Na kuleni na kunyweni na wala msifanye israfu.[3] Hakika Yeye (Allaah) Hapendi wanaofanya israfu.

 

 

 

قُلْ مَنْ حَرَّمَ زِينَةَ اللَّـهِ الَّتِي أَخْرَجَ لِعِبَادِهِ وَالطَّيِّبَاتِ مِنَ الرِّزْقِ ۚ قُلْ هِيَ لِلَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا خَالِصَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٣٢﴾

32. Sema: Nani aliyeharamisha Mapambo ya Allaah ambayo Amewatolea Waja Wake na vilivyo vizuri katika riziki? Sema: Hivyo ni kwa ajili ya wale walioamini katika uhai wa dunia; makhsusi (kwa Waumini) Siku ya Qiyaamah. Hivyo ndivyo Tunavyofasili waziwazi Aayaat kwa watu wanaojua.

 

 

 

قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَالْإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَأَن تُشْرِكُوا بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٣٣﴾

33. Sema: Hakika Rabb wangu Ameharamisha machafu ya wazi na ya siri, na dhambi, na ukandamizaji bila ya haki, na kumshirikisha Allaah kwa ambayo Hakuyateremshia mamlaka, na kusema juu ya Allaah yale ambayo hamyajui.[4]

 

 

 

وَلِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌ ۖ فَإِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ لَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً ۖ وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ ﴿٣٤﴾

34. Na kila ummah una muda uliokadiriwa. Basi utakapofika muda wao huo, hawatataakhari wala hawatatangulia saa.

 

 

 

يَا بَنِي آدَمَ إِمَّا يَأْتِيَنَّكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ يَقُصُّونَ عَلَيْكُمْ آيَاتِي ۙ فَمَنِ اتَّقَىٰ وَأَصْلَحَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٣٥﴾

35. Enyi wana wa Aadam! Watakapokufikieni Rusuli miongoni mwenu wakakubainishieni Aayaat Zangu, basi atakayekuwa na taqwa na akajiweka sawa, haitokuwa khofu juu yao na hawatohuzunika.

 

 

 

وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَاسْتَكْبَرُوا عَنْهَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٣٦﴾

36. Na wale waliokadhibisha Aayaat Zetu na wakazifanyia kiburi, hao ni watu wa motoni, wao humo ni wenye kudumu.

 

 

 

فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ ۚ أُولَـٰئِكَ يَنَالُهُمْ نَصِيبُهُم مِّنَ الْكِتَابِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا جَاءَتْهُمْ رُسُلُنَا يَتَوَفَّوْنَهُمْ قَالُوا أَيْنَ مَا كُنتُمْ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ قَالُوا ضَلُّوا عَنَّا وَشَهِدُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ أَنَّهُمْ كَانُوا كَافِرِينَ ﴿٣٧﴾

37. Basi nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyemtungia Allaah uongo au aliyekadhibisha Aayaat Zake. Hao itawafikia sehemu yao waliyoandikiwa mpaka watakapowajia Wajumbe Wetu kuwafisha watawaambia: Wako wapi wale mliokuwa mkiwaomba pasi na Allaah? Watasema: Wametupotea. Na watajishuhudia nafsi zao wenyewe kwamba walikuwa makafiri.

 

 

 

قَالَ ادْخُلُوا فِي أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِكُم مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ فِي النَّارِ ۖ كُلَّمَا دَخَلَتْ أُمَّةٌ لَّعَنَتْ أُخْتَهَا ۖ حَتَّىٰ إِذَا ادَّارَكُوا فِيهَا جَمِيعًا قَالَتْ أُخْرَاهُمْ لِأُولَاهُمْ رَبَّنَا هَـٰؤُلَاءِ أَضَلُّونَا فَآتِهِمْ عَذَابًا ضِعْفًا مِّنَ النَّارِ ۖ قَالَ لِكُلٍّ ضِعْفٌ وَلَـٰكِن لَّا تَعْلَمُونَ ﴿٣٨﴾

38. (Allaah) Atasema: Ingieni motoni pamoja na ummah zilizokwishapita kabla yenu za majini na wana Aadam. Kila utakapoingia ummah utalaani nduguye. Mpaka watakapokusanyika mrundo humo wote pamoja, wa mwisho wao (waliofuata wakuu) watawasema wa mwanzo wao (wakuu wao): Rabb wetu! Hawa wametupoteza, basi Wape adhabu maradufu ya moto. (Allaah) Atasema: Kila mmoja atapata (adhabu ya) maradufu lakini hamjui.

 

 

 

وَقَالَتْ أُولَاهُمْ لِأُخْرَاهُمْ فَمَا كَانَ لَكُمْ عَلَيْنَا مِن فَضْلٍ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْسِبُونَ ﴿٣٩﴾

39. Na wa mwanzo wao watawaambia wa mwisho wao: Basi hamkuwa na ubora kuliko sisi.  Hivyo onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyachuma.

 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَاسْتَكْبَرُوا عَنْهَا لَا تُفَتَّحُ لَهُمْ أَبْوَابُ السَّمَاءِ وَلَا يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ حَتَّىٰ يَلِجَ الْجَمَلُ فِي سَمِّ الْخِيَاطِ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُجْرِمِينَ ﴿٤٠﴾

40. Hakika wale waliokadhibisha Aayaat Zetu na wakazifanyia kiburi, hawatofunguliwa kamwe milango ya mbingu na wala hawatoingia Jannah mpaka ngamia aingie katika tundu ya sindano. Na hivyo ndivyo Tunavyowalipa wakhalifu.[5]  

 

 

 

 

لَهُم مِّن جَهَنَّمَ مِهَادٌ وَمِن فَوْقِهِمْ غَوَاشٍ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الظَّالِمِينَ ﴿٤١﴾

41. Jahannam itakuwa ni kitanda chao na juu yao miguo ya kuwafunika, na hivyo ndivyo Tunavyowalipa madhalimu.

 

 

 

وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٤٢﴾

42. Na wale walioamini na wakatenda mema - Nasi Hatuikalifishi nafsi ila kadiri ya uwezo wake - hao ni watu wa Jannah, wao humo ni wenye kudumu.

 

 

 

وَنَزَعْنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنْ غِلٍّ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ ۖ وَقَالُوا الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي هَدَانَا لِهَـٰذَا وَمَا كُنَّا لِنَهْتَدِيَ لَوْلَا أَنْ هَدَانَا اللَّـهُ ۖ لَقَدْ جَاءَتْ رُسُلُ رَبِّنَا بِالْحَقِّ ۖ وَنُودُوا أَن تِلْكُمُ الْجَنَّةُ أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٤٣﴾

43. Na Tutaondosha mizizi ya mafundo ya kinyongo yaliyomo vifuani mwao,[6] itapita chini yao mito. Na watasema: AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah), Ambaye Ametuongoza kwa haya, na tusingelikuwa wenye kuhidika kama Allaah Asingetuongoza. Kwa yakini wamekuja Rusuli wa Rabb wetu na haki. Na wataitwa (kuambiwa): Hii ndiyo Jannah mliyorithishwa kwa sababu ya yale mliyokuwa mnayatenda.[7]

 

 

 

وَنَادَىٰ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ أَصْحَابَ النَّارِ أَن قَدْ وَجَدْنَا مَا وَعَدَنَا رَبُّنَا حَقًّا فَهَلْ وَجَدتُّم مَّا وَعَدَ رَبُّكُمْ حَقًّا ۖ قَالُوا نَعَمْ ۚ فَأَذَّنَ مُؤَذِّنٌ بَيْنَهُمْ أَن لَّعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الظَّالِمِينَ ﴿٤٤﴾

44. Na watu wa Jannah watawaita watu wa motoni kuwaambia: Kwa yakini tumekwishayapata Aliyotuahidi Rabb wetu kuwa ni kweli. Je, basi nyinyi mmekwishapata Aliyokuahidini Rabb wenu kuwa ni kweli? Watasema: Naam! Basi mtangazaji atatangaza baina yao kwamba: Laana ya Allaah iwe juu ya madhalimu! 

 

 

 

الَّذِينَ يَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجًا وَهُم بِالْآخِرَةِ كَافِرُونَ ﴿٤٥﴾

45. Ambao wanazuia Njia ya Allaah na wanaitafutia upogo, na wao wanaikanusha Aakhirah.

 

 

 

 

وَبَيْنَهُمَا حِجَابٌ ۚ وَعَلَى الْأَعْرَافِ رِجَالٌ يَعْرِفُونَ كُلًّا بِسِيمَاهُمْ ۚ وَنَادَوْا أَصْحَابَ الْجَنَّةِ أَن سَلَامٌ عَلَيْكُمْ ۚ لَمْ يَدْخُلُوهَا وَهُمْ يَطْمَعُونَ ﴿٤٦﴾

46. Na baina yao kitakuwepo kizuizi. Na juu ya Al-A’raaf (ukuta wa mwinuko) patakuweko watu watakaowatambua wote (wabaya na wema) kwa alama zao. Na watawaita watu wa Jannah: Salaamun ‘Alaykum!  Hawakuingia humo lakini bado wanatumaini.[8] 

 

 

 

وَإِذَا صُرِفَتْ أَبْصَارُهُمْ تِلْقَاءَ أَصْحَابِ النَّارِ قَالُوا رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٤٧﴾

47. Na yatakapogeuzwa macho yao kuelekea watu wa motoni watasema: Rabb wetu! Usitujaalie kuwa pamoja na watu madhalimu.

 

 

 

وَنَادَىٰ أَصْحَابُ الْأَعْرَافِ رِجَالًا يَعْرِفُونَهُم بِسِيمَاهُمْ قَالُوا مَا أَغْنَىٰ عَنكُمْ جَمْعُكُمْ وَمَا كُنتُمْ تَسْتَكْبِرُونَ ﴿٤٨﴾

48. Na watu wa Al-A’raaf watawaita watu (wa motoni) wanaowatambua kwa alama zao, watasema: Hakukufaeni kujumuika kwenu (duniani) na vile mlivyokuwa mkitakabari.

 

 

 

أَهَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ أَقْسَمْتُمْ لَا يَنَالُهُمُ اللَّـهُ بِرَحْمَةٍ ۚ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ لَا خَوْفٌ عَلَيْكُمْ وَلَا أَنتُمْ تَحْزَنُونَ ﴿٤٩﴾

49. Je, hawa si wale ambao mliapa kwamba Allaah Hatowapa Rahmah yoyote ile? (Leo wanaambiwa) Ingieni Jannah! Hakuna khofu juu yenu na wala nyinyi hamtohuzunika. 

 

 

 

وَنَادَىٰ أَصْحَابُ النَّارِ أَصْحَابَ الْجَنَّةِ أَنْ أَفِيضُوا عَلَيْنَا مِنَ الْمَاءِ أَوْ مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّـهُ ۚ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ حَرَّمَهُمَا عَلَى الْكَافِرِينَ ﴿٥٠﴾

50. Na watu wa motoni watawaita watu wa Jannah: Tumiminieni maji au katika ambavyo Amekuruzukuni Allaah. Watasema: Hakika Allaah Ameviharamisha kwa makafiri.

 

 

 

الَّذِينَ اتَّخَذُوا دِينَهُمْ لَهْوًا وَلَعِبًا وَغَرَّتْهُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا ۚ فَالْيَوْمَ نَنسَاهُمْ كَمَا نَسُوا لِقَاءَ يَوْمِهِمْ هَـٰذَا وَمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَجْحَدُونَ ﴿٥١﴾

51. Ambao wameifanya dini yao pumbao na mchezo, na ukawaghuri uhai wa dunia. Basi leo Tunawasahau kama walivyosahau kukutana na Siku yao hii, na kuwa kwao wakizikanusha kwa jeuri Aayaat Zetu.

 

 

 

وَلَقَدْ جِئْنَاهُم بِكِتَابٍ فَصَّلْنَاهُ عَلَىٰ عِلْمٍ هُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٥٢﴾

52. Kwa yakini Tumewaletea Kitabu Tulichokifasili waziwazi kwa ujuzi; ni Mwongozo na Rahmah kwa watu wanaoamini.

 

 

 

 

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا تَأْوِيلَهُ ۚ يَوْمَ يَأْتِي تَأْوِيلُهُ يَقُولُ الَّذِينَ نَسُوهُ مِن قَبْلُ قَدْ جَاءَتْ رُسُلُ رَبِّنَا بِالْحَقِّ فَهَل لَّنَا مِن شُفَعَاءَ فَيَشْفَعُوا لَنَا أَوْ نُرَدُّ فَنَعْمَلَ غَيْرَ الَّذِي كُنَّا نَعْمَلُ ۚ قَدْ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٥٣﴾

53. Je, wanangojea nini isipokuwa matokeo yake? Siku (ya Qiyaamah) yatakapofika matokeo yake watasema wale walioisahau kabla: Kwa yakini walikuja Rusuli wa Rabb wetu kwa haki. Je, tuna waombezi wowote watuombee, au turudishwe (duniani) ili tufanye ghairi ya yale tuliyokuwa tunafanya? Kwa yakini wamekhasiri nafsi zao na yamewapotea yale waliyokuwa wakiyatunga.

 

 

 

 

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ يَطْلُبُهُ حَثِيثًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ وَالنُّجُومَ مُسَخَّرَاتٍ بِأَمْرِهِ ۗ أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ ۗ تَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٥٤﴾

54. Hakika Rabb wenu ni Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha Akawa juu (Istawaa)[9] ya ‘Arsh, Anafunika usiku kwa mchana, unaufuatia upesi upesi, na (Ameumba) jua na mwezi na nyota, (vyote) vimetiishwa kwa Amri Yake. Tanabahi! Uumbaji ni Wake Pekee na kupitisha amri. Amebarikika Allaah Rabb wa walimwengu.[10]

 

 

 

ادْعُوا رَبَّكُمْ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿٥٥﴾

55. Muombeni Rabb wenu kwa unyenyekevu na kwa siri, hakika Yeye Hapendi wenye kupindukia mipaka.[11]

 

 

 

وَلَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَاحِهَا وَادْعُوهُ خَوْفًا وَطَمَعًا ۚ إِنَّ رَحْمَتَ اللَّـهِ قَرِيبٌ مِّنَ الْمُحْسِنِينَ ﴿٥٦﴾

56. Na wala msifanye ufisadi katika ardhi baada ya (Allaah) kuitengeneza sawa, na muombeni kwa khofu na matumaini. Hakika Rahmah ya Allaah iko karibu na wafanyao ihsaan.

 

 

 

وَهُوَ الَّذِي يُرْسِلُ الرِّيَاحَ بُشْرًا بَيْنَ يَدَيْ رَحْمَتِهِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا أَقَلَّتْ سَحَابًا ثِقَالًا سُقْنَاهُ لِبَلَدٍ مَّيِّتٍ فَأَنزَلْنَا بِهِ الْمَاءَ فَأَخْرَجْنَا بِهِ مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ ۚ كَذَٰلِكَ نُخْرِجُ الْمَوْتَىٰ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ ﴿٥٧﴾

57. Naye Ndiye Anayetuma upepo mzuri kuwa bishara kabla ya Rahmah Yake. Hadi unapobeba mawingu mazito Tunayasukuma kwenye nchi iliyokufa. Kisha Tunateremsha kwayo maji na kisha Tunatoa kwayo kila (aina ya) mazao. Hivyo ndivyo Tunavyotoa wafu, ili mpate kukumbuka (au kuwaidhika).

 

 

 

وَالْبَلَدُ الطَّيِّبُ يَخْرُجُ نَبَاتُهُ بِإِذْنِ رَبِّهِ ۖ وَالَّذِي خَبُثَ لَا يَخْرُجُ إِلَّا نَكِدًا ۚ كَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَشْكُرُونَ ﴿٥٨﴾

58. Na nchi nzuri mimea yake hutoka kwa idhini ya Rabb wake. Na ile ambayo ni mbaya haitoki ila kwa uadimu. Hivyo ndivyo Tunavyosarifu namna kwa namna ishara na dalili kwa watu wanaoshukuru.[12]

 

 

 

لَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ فَقَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿٥٩﴾

59. Kwa yakini Tulimpeleka Nuwh kwa kaumu yake akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Hakika mimi nakukhofieni adhabu ya Siku kubwa mno.

 

 

 

قَالَ الْمَلَأُ مِن قَوْمِهِ إِنَّا لَنَرَاكَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٦٠﴾

60. Wakasema wakuu katika kaumu yake: Hakika sisi tunakuona umo katika upotofu bayana.

 

 

 

قَالَ يَا قَوْمِ لَيْسَ بِي ضَلَالَةٌ وَلَـٰكِنِّي رَسُولٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٦١﴾

61. (Nuwh) Akasema: Enyi kaumu yangu! Mimi siko katika upotofu lakini mimi ni Rasuli kutoka kwa Rabb wa walimwengu.

 

 

 

أُبَلِّغُكُمْ رِسَالَاتِ رَبِّي وَأَنصَحُ لَكُمْ وَأَعْلَمُ مِنَ اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٦٢﴾

62. Nakubalighishieni Risala ya Rabb wangu na nakunasihini, na ninajua kutoka kwa Allaah msiyoyajua.

 

 

 

أَوَعَجِبْتُمْ أَن جَاءَكُمْ ذِكْرٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَلَىٰ رَجُلٍ مِّنكُمْ لِيُنذِرَكُمْ وَلِتَتَّقُوا وَلَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٦٣﴾

63. Je, mmestaajabu kwamba umekujieni ukumbusho kutoka kwa Rabb wenu kupitia kwa mtu miongoni mwenu ili akuonyeni na ili muwe na taqwa na mpate kurehemewa?

 

 

 

فَكَذَّبُوهُ فَأَنجَيْنَاهُ وَالَّذِينَ مَعَهُ فِي الْفُلْكِ وَأَغْرَقْنَا الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا عَمِينَ ﴿٦٤﴾

64. Basi walimkadhibisha na Tukamuokoa pamoja na wale waliokuwa naye katika jahazi, na Tukawagharikisha wale waliokadhibisha Aayaat (ishara, dalili) Zetu. Hakika wao walikuwa watu vipofu.

 

 

 

وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمْ هُودًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۚ أَفَلَا تَتَّقُونَ ﴿٦٥﴾

65. Na kwa ‘Aad (Tuliwapelekea) kaka yao Huwd.  Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Je, basi hamtokuwa na taqwa

 

 

 

قَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَوْمِهِ إِنَّا لَنَرَاكَ فِي سَفَاهَةٍ وَإِنَّا لَنَظُنُّكَ مِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿٦٦﴾

66. Wakasema wakuu waliokufuru katika kaumu yake: Hakika sisi tunakuona umo katika upumbavu, na sisi tuna yakini wewe ni miongoni mwa waongo.

 

 

 

قَالَ يَا قَوْمِ لَيْسَ بِي سَفَاهَةٌ وَلَـٰكِنِّي رَسُولٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٦٧﴾

67. (Huwd) Akasema: Enyi kaumu yangu! Mimi sina upumbavu lakini mimi ni Rasuli kutoka kwa Rabb wa walimwengu.

 

 

 

أُبَلِّغُكُمْ رِسَالَاتِ رَبِّي وَأَنَا لَكُمْ نَاصِحٌ أَمِينٌ ﴿٦٨﴾

68. Nakubalighishieni Risala ya Rabb wangu, nami kwenu ni mtoaji nasiha mwaminifu.

 

 

 

أَوَعَجِبْتُمْ أَن جَاءَكُمْ ذِكْرٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَلَىٰ رَجُلٍ مِّنكُمْ لِيُنذِرَكُمْ ۚ وَاذْكُرُوا إِذْ جَعَلَكُمْ خُلَفَاءَ مِن بَعْدِ قَوْمِ نُوحٍ وَزَادَكُمْ فِي الْخَلْقِ بَسْطَةً ۖ فَاذْكُرُوا آلَاءَ اللَّـهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٦٩﴾

69. Je, mmestaajabu kwamba umekujieni ukumbusho kutoka kwa Rabb wenu kupitia kwa mtu miongoni mwenu ili akuonyeni? Na kumbukeni Alipokufanyeni warithi baada ya kaumu ya Nuwh, na Akakuzidisheni kwa maumbo (ya mwili) na nguvu. Basi kumbukeni Neema Nyingi za Allaah mpate kufaulu.

 

 

 

قَالُوا أَجِئْتَنَا لِنَعْبُدَ اللَّـهَ وَحْدَهُ وَنَذَرَ مَا كَانَ يَعْبُدُ آبَاؤُنَا ۖ فَأْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٧٠﴾

70. Wakasema: Je, umetujia ili tumwabudu Allaah Pekee na tuache yale waliyokuwa wakiabudu baba zetu? Basi tuletee hayo unayotutishia ukiwa ni miongoni mwa wakweli.

 

 

 

قَالَ قَدْ وَقَعَ عَلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ رِجْسٌ وَغَضَبٌ ۖ أَتُجَادِلُونَنِي فِي أَسْمَاءٍ سَمَّيْتُمُوهَا أَنتُمْ وَآبَاؤُكُم مَّا نَزَّلَ اللَّـهُ بِهَا مِن سُلْطَانٍ ۚ فَانتَظِرُوا إِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُنتَظِرِينَ ﴿٧١﴾

71. (Huwd) Akasema: Kwa yakini imekwishakuangukieni adhabu na ghadhabu kutoka kwa Rabb wenu. Je, mnabishana nami kuhusu majina (ya masanamu) mliyoyaita nyinyi na baba zenu bila ya Allaah kuyateremshia kwayo mamlaka? Basi ngojeeni, hakika mimi niko pamoja nanyi katika wanaongojea.

 

 

 

فَأَنجَيْنَاهُ وَالَّذِينَ مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَقَطَعْنَا دَابِرَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۖ وَمَا كَانُوا مُؤْمِنِينَ ﴿٧٢﴾

72. Basi Tukamuokoa (Huwd) na wale waliokuwa pamoja naye kwa Rahmah kutoka Kwetu na Tukakata mizizi ya wale waliokadhibisha Aayaat (ishara, dalili) Zetu na hawakuwa wenye kuamini.

 

 

 

وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ قَدْ جَاءَتْكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ ۖ هَـٰذِهِ نَاقَةُ اللَّـهِ لَكُمْ آيَةً ۖ فَذَرُوهَا تَأْكُلْ فِي أَرْضِ اللَّـهِ ۖ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٣﴾

73. Na kwa Thamuwd (Tuliwapelekea) kaka yao Swaalih. Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Kwa yakini imekujieni hoja bayana kutoka kwa Rabb wenu. Huyu ngamia jike wa Allaah ni dalili kwenu. Basi muacheni ale katika Ardhi ya Allaah, na wala msimguse kwa uovu isije ikakuchukueni adhabu iumizayo.

 

 

 

وَاذْكُرُوا إِذْ جَعَلَكُمْ خُلَفَاءَ مِن بَعْدِ عَادٍ وَبَوَّأَكُمْ فِي الْأَرْضِ تَتَّخِذُونَ مِن سُهُولِهَا قُصُورًا وَتَنْحِتُونَ الْجِبَالَ بُيُوتًا ۖ فَاذْكُرُوا آلَاءَ اللَّـهِ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ ﴿٧٤﴾

74. Na kumbukeni Alipokufanyeni warithi baada ya ‘Aad, Akakufanyieni makazi katika ardhi mnajenga katika nyanda zake tambarare majumba ya fakhari na mnachonga majumba katika majabali. Basi kumbukeni Neema Nyingi za Allaah na wala msifanye vitendo vya hujuma katika ardhi mkifisidi.

 

 

 

قَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا مِن قَوْمِهِ لِلَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا لِمَنْ آمَنَ مِنْهُمْ أَتَعْلَمُونَ أَنَّ صَالِحًا مُّرْسَلٌ مِّن رَّبِّهِ ۚ قَالُوا إِنَّا بِمَا أُرْسِلَ بِهِ مُؤْمِنُونَ ﴿٧٥﴾

75. Wakasema wakuu waliotakabari katika kaumu yake kuwaambia wale waliokandamizwa ambao wameamini miongoni mwao: Kwa uhakika gani mnajua kwamba Swaalih ametumwa kutoka kwa Rabb wake?  Wakasema: Hakika sisi tunayaamini aliyotumwa nayo. 

 

 

 

قَالَ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا إِنَّا بِالَّذِي آمَنتُم بِهِ كَافِرُونَ ﴿٧٦﴾

76. Wakasema wale waliotakabari: Basi sisi tunayakanusha hayo mliyoyaamini.

 

 

 

فَعَقَرُوا النَّاقَةَ وَعَتَوْا عَنْ أَمْرِ رَبِّهِمْ وَقَالُوا يَا صَالِحُ ائْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِن كُنتَ مِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٧٧﴾

77. Wakamuua yule ngamia jike na wakaasi Amri ya Rabb wao, na wakasema: Ee Swaalih, tuletee hayo unayotutishia ukiwa ni miongoni mwa Rusuli.

 

 

 

فَأَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دَارِهِمْ جَاثِمِينَ ﴿٧٨﴾

78. Basi likawachukua tetemeko la ardhi wakawa majumbani mwao wameanguka kifudifudi (wamekufa).

 

 

 

فَتَوَلَّىٰ عَنْهُمْ وَقَالَ يَا قَوْمِ لَقَدْ أَبْلَغْتُكُمْ رِسَالَةَ رَبِّي وَنَصَحْتُ لَكُمْ وَلَـٰكِن لَّا تُحِبُّونَ النَّاصِحِينَ ﴿٧٩﴾

79. (Swaalih) akajitenga nao na akasema: Enyi kaumu yangu! Kwa yakini nilishakubalighishieni Risala ya Rabb wangu na nilikunasihini, lakini nyinyi hamuwapendi wenye kunasihi.

 

 

 

وَلُوطًا إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ أَتَأْتُونَ الْفَاحِشَةَ مَا سَبَقَكُم بِهَا مِنْ أَحَدٍ مِّنَ الْعَالَمِينَ ﴿٨٠﴾

80.  Na (Tulimtuma) Luutw, alipowaambia kaumu yake: Je, mnafanya uchafu (wa liwati) ambao hajakutangulieni nao yeyote katika walimwengu?

 

 

 

إِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ الرِّجَالَ شَهْوَةً مِّن دُونِ النِّسَاءِ ۚ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ مُّسْرِفُونَ ﴿٨١﴾

81. Hakika nyinyi mnawaingilia wanaume kwa matamanio badala ya wanawake? Bali nyinyi ni watu wapindukiaji mipaka.

 

 

 

وَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِ إِلَّا أَن قَالُوا أَخْرِجُوهُم مِّن قَرْيَتِكُمْ ۖ إِنَّهُمْ أُنَاسٌ يَتَطَهَّرُونَ ﴿٨٢﴾

82. Na halikuwa jibu la kaumu yake isipokuwa walisema: Wafukuzeni kutoka mji wenu, kwani wao eti ni watu wanaojitakasa.

 

 

 

فَأَنجَيْنَاهُ وَأَهْلَهُ إِلَّا امْرَأَتَهُ كَانَتْ مِنَ الْغَابِرِينَ ﴿٨٣﴾

83. Basi Tukamuokoa (Luutw) na ahli yake isipokuwa mkewe alikuwa miongoni mwa waliobaki nyuma.

 

 

 

وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِم مَّطَرًا ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُجْرِمِينَ ﴿٨٤﴾

84. Na Tukawanyeshea mvua, (ya mawe). Basi tazama vipi ilikuwa khatima ya wakhalifu.

 

 

 

وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ قَدْ جَاءَتْكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ ۖ فَأَوْفُوا الْكَيْلَ وَالْمِيزَانَ وَلَا تَبْخَسُوا النَّاسَ أَشْيَاءَهُمْ وَلَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَاحِهَا ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٨٥﴾

85. Na kwa (watu wa) Madyan (Tuliwapelekea) kaka yao Shu’ayb.  Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake.  Kwa yakini imekujieni hoja bayana kutoka kwa Rabb wenu. Basi timizeni kipimo na mizani wala msipunje watu vitu vyao wala msifanye ufisadi ardhini baada ya (Allaah) kuitengeneza vyema. Hivyo ni bora kwenu ikiwa mmeamini.

 

 

 

وَلَا تَقْعُدُوا بِكُلِّ صِرَاطٍ تُوعِدُونَ وَتَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ مَنْ آمَنَ بِهِ وَتَبْغُونَهَا عِوَجًا ۚ وَاذْكُرُوا إِذْ كُنتُمْ قَلِيلًا فَكَثَّرَكُمْ ۖ وَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُفْسِدِينَ ﴿٨٦﴾

86. Na wala msikae katika kila njia kutisha watu na kuwazuilia Njia ya Allaah wale wenye kumuamini, na huku mnaitafutia upogo. Na kumbukeni mlipokuwa wachache Akakukithirisheni. Na tazameni vipi ilikuwa khatima ya mafisadi.

 

 

 

وَإِن كَانَ طَائِفَةٌ مِّنكُمْ آمَنُوا بِالَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ وَطَائِفَةٌ لَّمْ يُؤْمِنُوا فَاصْبِرُوا حَتَّىٰ يَحْكُمَ اللَّـهُ بَيْنَنَا ۚ وَهُوَ خَيْرُ الْحَاكِمِينَ ﴿٨٧﴾

87. Na kama liko kundi miongoni mwenu limeamini yale niliyotumwa nayo na kundi halikuamini, basi subirini mpaka Allaah Ahukumu baina yetu. Naye Ndiye Mbora wa Kuhukumu kuliko wote.

 

 

 

 

قَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا مِن قَوْمِهِ لَنُخْرِجَنَّكَ يَا شُعَيْبُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَكَ مِن قَرْيَتِنَا أَوْ لَتَعُودُنَّ فِي مِلَّتِنَا ۚ قَالَ أَوَلَوْ كُنَّا كَارِهِينَ ﴿٨٨﴾

88. Wakasema wakuu waliotakabari katika kaumu yake: Lazima tutakutoa ewe Shua’yb na wale walioamini pamoja nawe kutoka mji wetu, au mrejee katika millah yetu. (Shu’ayb) Akasema: Hata kwa kulazimishwa bila kuiridhia?

 

 

 

 

قَدِ افْتَرَيْنَا عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا إِنْ عُدْنَا فِي مِلَّتِكُم بَعْدَ إِذْ نَجَّانَا اللَّـهُ مِنْهَا ۚ وَمَا يَكُونُ لَنَا أَن نَّعُودَ فِيهَا إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ رَبُّنَا ۚ وَسِعَ رَبُّنَا كُلَّ شَيْءٍ عِلْمًا ۚ عَلَى اللَّـهِ تَوَكَّلْنَا ۚ رَبَّنَا افْتَحْ بَيْنَنَا وَبَيْنَ قَوْمِنَا بِالْحَقِّ وَأَنتَ خَيْرُ الْفَاتِحِينَ ﴿٨٩﴾

89. Kwa yakini itakuwa tumemtungia Allaah uongo ikiwa tutarudi katika millah yenu baada ya Allaah kutuokoa nayo. Na haiwi kwetu kurejea humo isipokuwa Akitaka Allaah Rabb wetu. Rabb wetu Amekienea kila kitu kwa ujuzi. Kwa Allaah tunatawakali. Rabb wetu! Hukumu baina yetu na baina ya kaumu yetu kwa haki, Nawe Ndiye Mbora wa kuhukumu kuliko wote.

 

 

 

وَقَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَوْمِهِ لَئِنِ اتَّبَعْتُمْ شُعَيْبًا إِنَّكُمْ إِذًا لَّخَاسِرُونَ ﴿٩٠﴾

90. Na wakasema wakuu waliokufuru katika kaumu yake: Mkimfuata Shu’ayb hakika hapo mtakuwa bila shaka wenye kukhasirika.

 

 

 

فَأَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دَارِهِمْ جَاثِمِينَ ﴿٩١﴾

91. Basi likawachukua tetemeko la ardhi wakawa majumbani mwao wameanguka kifudifudi (wamekufa).

 

 

 

الَّذِينَ كَذَّبُوا شُعَيْبًا كَأَن لَّمْ يَغْنَوْا فِيهَا ۚ الَّذِينَ كَذَّبُوا شُعَيْبًا كَانُوا هُمُ الْخَاسِرِينَ ﴿٩٢﴾

92. Wale waliomkadhibisha Shu’ayb (wakawa) kama kwamba hawakuishi wakineemeka humo. Waliomkadhibisha Shu’ayb wakawa ndio wenye kukhasirika. 

 

 

 

فَتَوَلَّىٰ عَنْهُمْ وَقَالَ يَا قَوْمِ لَقَدْ أَبْلَغْتُكُمْ رِسَالَاتِ رَبِّي وَنَصَحْتُ لَكُمْ ۖ فَكَيْفَ آسَىٰ عَلَىٰ قَوْمٍ كَافِرِينَ ﴿٩٣﴾

93. Basi (Shu’ayb) akajitenga nao na akasema: Enyi kaumu yangu!  Kwa yakini nimekubalighishieni Risala ya Rabb wangu na nimekunasihini, basi vipi niwe na majonzi juu ya watu makafiri?

 

 

 

وَمَا أَرْسَلْنَا فِي قَرْيَةٍ مِّن نَّبِيٍّ إِلَّا أَخَذْنَا أَهْلَهَا بِالْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ لَعَلَّهُمْ يَضَّرَّعُونَ ﴿٩٤﴾

94. Na Hatukutuma katika mji Nabiy yeyote (akakanushwa) isipokuwa Tunawashika watu wake kwa dhiki za ufukara, na maafa ya magonjwa na njaa, huenda wapate kunyenyekea (kwa Allaah).

 

 

 

ثُمَّ بَدَّلْنَا مَكَانَ السَّيِّئَةِ الْحَسَنَةَ حَتَّىٰ عَفَوا وَّقَالُوا قَدْ مَسَّ آبَاءَنَا الضَّرَّاءُ وَالسَّرَّاءُ فَأَخَذْنَاهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٩٥﴾

95. Kisha Tukabadilisha mahali pa hali mbaya kwa hali nzuri hata wakaongezeka na kutengenekewa na maisha. Hapo wakasema: Hata baba zetu pia yaliwagusa madhara na raha. Basi Tukawachukuwa ghafla nao huku hawahisi. 

 

 

 

وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَىٰ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِم بَرَكَاتٍ مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ وَلَـٰكِن كَذَّبُوا فَأَخَذْنَاهُم بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿٩٦﴾

96. Na lau kama watu wa miji wangeliamimi na wakashikamana na taqwa, Tungeliwafungulia Baraka tele kutoka mbinguni na ardhini, lakini walikadhibisha, Nasi Tukawachukua kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma.

 

 

 

أَفَأَمِنَ أَهْلُ الْقُرَىٰ أَن يَأْتِيَهُم بَأْسُنَا بَيَاتًا وَهُمْ نَائِمُونَ ﴿٩٧﴾

97. Je, watu wa miji wameaminisha ya kuwa haitowafikia Adhabu Yetu wakati wa usiku hali wao wamelala?

 

 

 

أَوَأَمِنَ أَهْلُ الْقُرَىٰ أَن يَأْتِيَهُم بَأْسُنَا ضُحًى وَهُمْ يَلْعَبُونَ ﴿٩٨﴾

98. Au watu wa miji wameaminisha ya kuwa haitowafikia Adhabu Yetu wakati wa kabla ya mchana hali wao wanacheza?

 

 

 

أَفَأَمِنُوا مَكْرَ اللَّـهِ ۚ فَلَا يَأْمَنُ مَكْرَ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٩٩﴾

99. Je, wameaminisha Mipango ya (adhabu za) Allaah? Basi hawaaminishi Mipango ya Allaah isipokuwa watu wenye kukhasirika.

 

 

 

أَوَلَمْ يَهْدِ لِلَّذِينَ يَرِثُونَ الْأَرْضَ مِن بَعْدِ أَهْلِهَا أَن لَّوْ نَشَاءُ أَصَبْنَاهُم بِذُنُوبِهِمْ ۚ وَنَطْبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ ﴿١٠٠﴾

100. Je, haikuwabainikia wale wanaorithi ardhi baada ya watu wake (walioangamizwa) kwamba lau Tungelitaka Tungeliwasibu kwa dhambi zao! Na Tutapiga chapa juu ya nyoyo zao wasisikie tena?

 

 

 

تِلْكَ الْقُرَىٰ نَقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنبَائِهَا ۚ وَلَقَدْ جَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَمَا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا بِمَا كَذَّبُوا مِن قَبْلُ ۚ كَذَٰلِكَ يَطْبَعُ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِ الْكَافِرِينَ ﴿١٠١﴾

101. Hiyo ni miji Tunakusimulia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) baadhi ya khabari zake. Na kwa yakini waliwajia Rusuli wao kwa hoja bayana, lakini hawakuwa wenye kuamini yale waliyoyakadhibisha kabla. Hivyo ndivyo Allaah Anavyopiga chapa juu ya nyoyo za makafiri.

 

 

 

وَمَا وَجَدْنَا لِأَكْثَرِهِم مِّنْ عَهْدٍ ۖ وَإِن وَجَدْنَا أَكْثَرَهُمْ لَفَاسِقِينَ ﴿١٠٢﴾

102. Na Hatukuwakuta wengi wao kuwa ni wakweli wa ahadi. Bali kwa yakini Tumewakuta wengi wao ni mafasiki.

 

 

 

ثُمَّ بَعَثْنَا مِن بَعْدِهِم مُّوسَىٰ بِآيَاتِنَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَظَلَمُوا بِهَا ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُفْسِدِينَ ﴿١٠٣﴾

103. Kisha Tukamtuma baada yao Muwsaa na Miujiza Yetu kwa Fir’awn na wakuu wake nao wakaipinga na kukataa. Basi tazama vipi ilikuwa khatima ya mafisadi. 

 

 

 

وَقَالَ مُوسَىٰ يَا فِرْعَوْنُ إِنِّي رَسُولٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٠٤﴾

104. Na Muwsaa akasema: Ee Fir’awn! Hakika mimi ni Rasuli kutoka kwa Rabb wa walimwengu.

 

 

 

حَقِيقٌ عَلَىٰ أَن لَّا أَقُولَ عَلَى اللَّـهِ إِلَّا الْحَقَّ ۚ قَدْ جِئْتُكُم بِبَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ فَأَرْسِلْ مَعِيَ بَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿١٠٥﴾

105. Napaswa nisiseme juu ya Allaah isipokuwa ya haki. Kwa yakini nimekujieni kwa hoja bayana kutoka kwa Rabb wenu, basi waachie wana wa Israaiyl wawe pamoja nami. 

 

 

 

قَالَ إِن كُنتَ جِئْتَ بِآيَةٍ فَأْتِ بِهَا إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿١٠٦﴾

106. (Fir’awn) Akasema: Ikiwa umekuja na dalili yoyote basi ilete, ukiwa ni miongoni mwa wakweli.

 

 

 

فَأَلْقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعْبَانٌ مُّبِينٌ ﴿١٠٧﴾

107. Basi (Muwsaa) akaitupa fimbo yake, na mara tahamaki imegeuka joka la kweli.

 

 

 

وَنَزَعَ يَدَهُ فَإِذَا هِيَ بَيْضَاءُ لِلنَّاظِرِينَ ﴿١٠٨﴾

108. Na akatoa mkono wake, basi mara tahamaki umekuwa mweupe (unang’ara) kwa watazamao.

 

 

 

قَالَ الْمَلَأُ مِن قَوْمِ فِرْعَوْنَ إِنَّ هَـٰذَا لَسَاحِرٌ عَلِيمٌ ﴿١٠٩﴾

109. Wakasema wakuu katika kaumu ya Fir’awn: Bila shaka huyu ni mchawi mjuzi.

 

 

 

يُرِيدُ أَن يُخْرِجَكُم مِّنْ أَرْضِكُمْ ۖ فَمَاذَا تَأْمُرُونَ ﴿١١٠﴾

110. Anataka kukutoeni kutoka ardhini mwenu, basi mnaamrisha nini?

 

 

 

قَالُوا أَرْجِهْ وَأَخَاهُ وَأَرْسِلْ فِي الْمَدَائِنِ حَاشِرِينَ ﴿١١١﴾

111. Wakasema: Muahirishe kidogo na kaka yake na tuma katika miji wenye kukusanya.

 

 

 

يَأْتُوكَ بِكُلِّ سَاحِرٍ عَلِيمٍ ﴿١١٢﴾

112. Wakuletee kila mchawi mjuzi.

 

 

 

وَجَاءَ السَّحَرَةُ فِرْعَوْنَ قَالُوا إِنَّ لَنَا لَأَجْرًا إِن كُنَّا نَحْنُ الْغَالِبِينَ ﴿١١٣﴾

113. Wakaja wachawi kwa Fir’awn, wakasema: Je, tutapata ujira ikiwa sisi tutashinda?

 

 

 

قَالَ نَعَمْ وَإِنَّكُمْ لَمِنَ الْمُقَرَّبِينَ ﴿١١٤﴾

114. (Fir’awn) Akasema: Naam! Bila shaka nanyi mtakuwa miongoni mwa waliokurubishwa (kwangu).

 

 

 

قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِمَّا أَن تُلْقِيَ وَإِمَّا أَن نَّكُونَ نَحْنُ الْمُلْقِينَ ﴿١١٥﴾

115. (Wachawi) Wakasema: Ee Muwsaa, ima utupe wewe au tuanze sisi kutupa? 

 

 

 

قَالَ أَلْقُوا ۖ فَلَمَّا أَلْقَوْا سَحَرُوا أَعْيُنَ النَّاسِ وَاسْتَرْهَبُوهُمْ وَجَاءُوا بِسِحْرٍ عَظِيمٍ ﴿١١٦﴾

116. (Muwsaa) Akasema: Tupeni! Basi walipotupa, waliyasihiri macho ya watu na wakawatia woga, na wakaja na sihiri kuu.

 

 

 

وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنْ أَلْقِ عَصَاكَ ۖ فَإِذَا هِيَ تَلْقَفُ مَا يَأْفِكُونَ ﴿١١٧﴾

117. Na Tukamtia ilhamu Muwsaa ya kwamba: Tupa fimbo yako! Basi mara tahamaki ikameza vyote walivyovibuni.

 

 

 

فَوَقَعَ الْحَقُّ وَبَطَلَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١١٨﴾

118. Ukweli ukathibiti na yakabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda.

 

 

 

فَغُلِبُوا هُنَالِكَ وَانقَلَبُوا صَاغِرِينَ ﴿١١٩﴾

119. Wakashindwa hapo, na wakageuka kuwa wenye kudhalilika.

 

 

 

وَأُلْقِيَ السَّحَرَةُ سَاجِدِينَ ﴿١٢٠﴾

120.  Na wachawi wakajiangusha wakisujudu.

 

 

 

قَالُوا آمَنَّا بِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٢١﴾

121. Wakasema: Tumemwamini Rabb wa walimwengu.

 

 

 

رَبِّ مُوسَىٰ وَهَارُونَ ﴿١٢٢﴾

122. Rabb wa Muwsaa na Haaruwn.

 

 

 

قَالَ فِرْعَوْنُ آمَنتُم بِهِ قَبْلَ أَنْ آذَنَ لَكُمْ ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَمَكْرٌ مَّكَرْتُمُوهُ فِي الْمَدِينَةِ لِتُخْرِجُوا مِنْهَا أَهْلَهَا ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿١٢٣﴾

123. Fir’awn akasema: Je, mumemwamini kabla sijakupeni rukhsa? Hakika hii bila shaka ni makri mliyoipanga (na Muwsaa) katika mji ili muwatoe watu wake humo. Basi mtanitambua!

 

 

 

لَأُقَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُم مِّنْ خِلَافٍ ثُمَّ لَأُصَلِّبَنَّكُمْ أَجْمَعِينَ ﴿١٢٤﴾

124. Nitaikatakata mikono yenu na miguu yenu kwa kutofautisha kisha nitakusulubuni vibaya nyote.[13]

 

 

 

قَالُوا إِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ ﴿١٢٥﴾

125. (Wachawi) Wakasema: Hakika sisi kwa Rabb wetu tutarudi.

 

 

 

وَمَا تَنقِمُ مِنَّا إِلَّا أَنْ آمَنَّا بِآيَاتِ رَبِّنَا لَمَّا جَاءَتْنَا ۚ رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَتَوَفَّنَا مُسْلِمِينَ ﴿١٢٦﴾

126. Na huchukizwi nasi isipokuwa tu kwa kuwa tumeamini Ishara na Dalili za Rabb wetu zilipotujia. Ee Rabb wetu! Tumiminie subira na Tufishe tukiwa Waislamu.

 

 

 

وَقَالَ الْمَلَأُ مِن قَوْمِ فِرْعَوْنَ أَتَذَرُ مُوسَىٰ وَقَوْمَهُ لِيُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَيَذَرَكَ وَآلِهَتَكَ ۚ قَالَ سَنُقَتِّلُ أَبْنَاءَهُمْ وَنَسْتَحْيِي نِسَاءَهُمْ وَإِنَّا فَوْقَهُمْ قَاهِرُونَ ﴿١٢٧﴾

127. Na wakasema wakuu katika kaumu ya Fir’awn: Je, unamwacha Muwsaa na kaumu yake wafisidi katika ardhi, na akuache wewe na waabudiwa wako? (Fir’awn) Akasema: Tutawaua watoto wao wa kiume na tutaacha hai wanawake wao, na hakika sisi ni wenye kushinda nguvu juu yao.

 

 

 

قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ اسْتَعِينُوا بِاللَّـهِ وَاصْبِرُوا ۖ إِنَّ الْأَرْضَ لِلَّـهِ يُورِثُهَا مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۖ وَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ ﴿١٢٨﴾

128. Muwsaa akawaambia kaumu yake: Ombeni msaada kwa Allaah na subirini. Hakika ardhi ni ya Allaah, Humrithisha Amtakaye katika Waja Wake. Na mwisho (mzuri) ni kwa wenye taqwa.

 

 

 

قَالُوا أُوذِينَا مِن قَبْلِ أَن تَأْتِيَنَا وَمِن بَعْدِ مَا جِئْتَنَا ۚ قَالَ عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يُهْلِكَ عَدُوَّكُمْ وَيَسْتَخْلِفَكُمْ فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرَ كَيْفَ تَعْمَلُونَ ﴿١٢٩﴾

129. Wakasema: Tumeudhiwa kabla ya kutujia na baada ya kutujia. (Muwsaa) akasema: Asaa Rabb wenu Akamuangamiza adui yenu na Akufanyeni watawala katika nchi, Atazame mtakavyotenda. 

 

 

 

وَلَقَدْ أَخَذْنَا آلَ فِرْعَوْنَ بِالسِّنِينَ وَنَقْصٍ مِّنَ الثَّمَرَاتِ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ ﴿١٣٠﴾

130. Na kwa yakini Tuliwatia majaribuni watu wa Fir’awn kwa ukame na upungufu wa mazao ili wapate kukumbuka.

 

 

 

فَإِذَا جَاءَتْهُمُ الْحَسَنَةُ قَالُوا لَنَا هَـٰذِهِ ۖ وَإِن تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌ يَطَّيَّرُوا بِمُوسَىٰ وَمَن مَّعَهُ ۗ أَلَا إِنَّمَا طَائِرُهُمْ عِندَ اللَّـهِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٣١﴾

131. Na likiwajia zuri husema: Hili letu. Na likiwasibu ovu basi hunasibisha nuksi kwa Muwsaa na walio pamoja naye. Tanabahi!  Hakika nuksi yao iko kwa Allaah lakini wengi wao hawajui.

 

 

 

وَقَالُوا مَهْمَا تَأْتِنَا بِهِ مِنْ آيَةٍ لِّتَسْحَرَنَا بِهَا فَمَا نَحْنُ لَكَ بِمُؤْمِنِينَ ﴿١٣٢﴾

132. Na wakasema: Hata ukituletea ishara gani ili utusihiri nayo, basi sisi hatutokuamini.

 

 

 

فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمُ الطُّوفَانَ وَالْجَرَادَ وَالْقُمَّلَ وَالضَّفَادِعَ وَالدَّمَ آيَاتٍ مُّفَصَّلَاتٍ فَاسْتَكْبَرُوا وَكَانُوا قَوْمًا مُّجْرِمِينَ ﴿١٣٣﴾

133. Tukawapelekea tufani na nzige na chawa na vyura na damu kama ishara wazi bainishi, lakini walitakabari wakawa watu wakhalifu.

 

 

 

وَلَمَّا وَقَعَ عَلَيْهِمُ الرِّجْزُ قَالُوا يَا مُوسَى ادْعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِندَكَ ۖ لَئِن كَشَفْتَ عَنَّا الرِّجْزَ لَنُؤْمِنَنَّ لَكَ وَلَنُرْسِلَنَّ مَعَكَ بَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿١٣٤﴾

134. Na kila ilipowaangukia adhabu walisema: Ee Muwsaa! Tuombee kwa Rabb wako kwa yale Aliyokuahidi. Ukituondolea adhabu, bila shaka tutakuamini na bila shaka tutawaachia wana Israaiyl (waondoke) pamoja nawe.

 

 

 

فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُمُ الرِّجْزَ إِلَىٰ أَجَلٍ هُم بَالِغُوهُ إِذَا هُمْ يَنكُثُونَ ﴿١٣٥﴾

135.  Tulipowaondolea adhabu mpaka muda maalumu wao waufikie, tahamaki wao wanavunja ahadi.

 

 

 

فَانتَقَمْنَا مِنْهُمْ فَأَغْرَقْنَاهُمْ فِي الْيَمِّ بِأَنَّهُمْ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَكَانُوا عَنْهَا غَافِلِينَ ﴿١٣٦﴾

136. Basi Tukawalipiza, Tukawagharikisha baharini kwa kuwa wao walikadhibisha Ishara Zetu na walikuwa ni wenye kughafilika nazo.

 

 

 

 

وَأَوْرَثْنَا الْقَوْمَ الَّذِينَ كَانُوا يُسْتَضْعَفُونَ مَشَارِقَ الْأَرْضِ وَمَغَارِبَهَا الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا ۖ وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ الْحُسْنَىٰ عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ بِمَا صَبَرُوا ۖ وَدَمَّرْنَا مَا كَانَ يَصْنَعُ فِرْعَوْنُ وَقَوْمُهُ وَمَا كَانُوا يَعْرِشُونَ ﴿١٣٧﴾

137. Na Tukawarithisha watu waliokuwa wakikandamizwa Mashariki ya ardhi na Magharibi yake ambayo Tumeibariki. Na likatimia Neno Zuri la Rabb wako kwa wana wa Israaiyl kwa kule kusubiri kwao. Na Tukayadamirisha yale aliyokuwa Fir’awn na kaumu yake wakiyaamirisha na yale waliyokuwa wakiyajenga.

 

 

 

وَجَاوَزْنَا بِبَنِي إِسْرَائِيلَ الْبَحْرَ فَأَتَوْا عَلَىٰ قَوْمٍ يَعْكُفُونَ عَلَىٰ أَصْنَامٍ لَّهُمْ ۚ قَالُوا يَا مُوسَى اجْعَل لَّنَا إِلَـٰهًا كَمَا لَهُمْ آلِهَةٌ ۚ قَالَ إِنَّكُمْ قَوْمٌ تَجْهَلُونَ ﴿١٣٨﴾

138. Na Tukawavusha wana wa Israaiyl bahari. Wakawafikia watu waliokuwa wanasabilia kwa utiifu masanamu yao. Wakasema: Ee Muwsaa! Tufanyie nasi mwabudiwa kama walivyokuwa hao wana waabudiwa.  (Muwsaa) Akasema: Hakika nyinyi ni watu mfanyao ujinga.

 

 

 

إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ مُتَبَّرٌ مَّا هُمْ فِيهِ وَبَاطِلٌ مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٣٩﴾

139. Hakika hawa yatateketezwa waliyo nayo, na ni batili waliyokuwa wakiyatenda.

 

 

 

قَالَ أَغَيْرَ اللَّـهِ أَبْغِيكُمْ إِلَـٰهًا وَهُوَ فَضَّلَكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿١٤٠﴾

140. (Muwsaa) Akasema: Je, nikutafutieni mwabudiwa ghairi ya Allaah, na hali Yeye Amekufadhilisheni juu ya walimwengu?

 

 

 

وَإِذْ أَنجَيْنَاكُم مِّنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَسُومُونَكُمْ سُوءَ الْعَذَابِ ۖ يُقَتِّلُونَ أَبْنَاءَكُمْ وَيَسْتَحْيُونَ نِسَاءَكُمْ ۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَاءٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَظِيمٌ ﴿١٤١﴾

141. Na Tulipokuokoeni kutoka kwa watu wa Fir’awn walipokusibuni adhabu mbaya, wakiwaua watoto wenu wa kiume na wakiacha hai wanawake wenu, na katika hayo ulikuwa ni mtihani mkuu kutoka kwa Rabb wenu kwenu.

 

 

 

وَوَاعَدْنَا مُوسَىٰ ثَلَاثِينَ لَيْلَةً وَأَتْمَمْنَاهَا بِعَشْرٍ فَتَمَّ مِيقَاتُ رَبِّهِ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً ۚ وَقَالَ مُوسَىٰ لِأَخِيهِ هَارُونَ اخْلُفْنِي فِي قَوْمِي وَأَصْلِحْ وَلَا تَتَّبِعْ سَبِيلَ الْمُفْسِدِينَ ﴿١٤٢﴾

142. Na Tukamuahidi Muwsaa masiku thelathini na Tukayatimiza kwa kumi, na ukatimia muda wa miadi wa Rabb wake siku arubaini. Muwsaa akamwambia kaka yake Haaruwn: Kuwa kaimu wangu kwa watu wangu na tengeneza, na wala usifuate njia ya mafisadi.

 

 

 

وَلَمَّا جَاءَ مُوسَىٰ لِمِيقَاتِنَا وَكَلَّمَهُ رَبُّهُ قَالَ رَبِّ أَرِنِي أَنظُرْ إِلَيْكَ ۚ قَالَ لَن تَرَانِي وَلَـٰكِنِ انظُرْ إِلَى الْجَبَلِ فَإِنِ اسْتَقَرَّ مَكَانَهُ فَسَوْفَ تَرَانِي ۚ فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا وَخَرَّ مُوسَىٰ صَعِقًا ۚ فَلَمَّا أَفَاقَ قَالَ سُبْحَانَكَ تُبْتُ إِلَيْكَ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٤٣﴾

143. Na alipokuja Muwsaa katika muda na pahala pa Miadi Yetu, na Rabb wake Akamsemesha, akasema Rabb wangu! Nionyeshe ili nikutazame. (Allaah) Akasema: Hutoniona! Lakini tazama mlima. Ukitulia mahali pake, basi utaniona. Basi Rabb wake Alipojidhihirisha katika mlima, Aliufanya uvurugike kuwa vumbi, na Muwsaa akaanguka hali ya kuzimia. Alipozindukana akasema: Utakasifu ni Wako Nimetubu Kwako, nami ni wa kwanza wa wanaoamini.

 

 

 

قَالَ يَا مُوسَىٰ إِنِّي اصْطَفَيْتُكَ عَلَى النَّاسِ بِرِسَالَاتِي وَبِكَلَامِي فَخُذْ مَا آتَيْتُكَ وَكُن مِّنَ الشَّاكِرِينَ ﴿١٤٤﴾

144. (Allaah) Akasema: Ee Muwsaa hakika Mimi Nimekukhitari juu ya watu kwa Risala Yangu na Maneno Yangu. Basi pokea Niliyokupa na kuwa miongoni mwa wanaoshukuru.

 

 

 

وَكَتَبْنَا لَهُ فِي الْأَلْوَاحِ مِن كُلِّ شَيْءٍ مَّوْعِظَةً وَتَفْصِيلًا لِّكُلِّ شَيْءٍ فَخُذْهَا بِقُوَّةٍ وَأْمُرْ قَوْمَكَ يَأْخُذُوا بِأَحْسَنِهَا ۚ سَأُرِيكُمْ دَارَ الْفَاسِقِينَ ﴿١٤٥﴾

145. Na Tukamwandikia kwenye vibao kila kitu; mawaidha na tafsili ya waziwazi ya kila kitu. (Tukamwambia): Basi yashikilie kwa nguvu na uwaamrishe watu wako wayashike mazuri yake. Nitakuonyesheni miji ya mafasiki. 

 

 

 

سَأَصْرِفُ عَنْ آيَاتِيَ الَّذِينَ يَتَكَبَّرُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَإِن يَرَوْا كُلَّ آيَةٍ لَّا يُؤْمِنُوا بِهَا وَإِن يَرَوْا سَبِيلَ الرُّشْدِ لَا يَتَّخِذُوهُ سَبِيلًا وَإِن يَرَوْا سَبِيلَ الْغَيِّ يَتَّخِذُوهُ سَبِيلًا ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَكَانُوا عَنْهَا غَافِلِينَ ﴿١٤٦﴾

146. Nitawaepusha na Aayaat (ishara, dalili) Zangu wale waliotakabari katika ardhi bila ya haki. Na wanapoona kila Aayah hawaiamini. Na wanapoona njia ya uongofu hawaishiki kuwa ndio njia. Na wanapoona njia ya upotofu wanaishika kuwa ndio njia. Hivyo ni kwa kuwa wao walikadhibisha Aayaat Zetu na walikuwa wenye kughafilika nazo.

 

 

 

وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَلِقَاءِ الْآخِرَةِ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ ۚ هَلْ يُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٤٧﴾

147. Na wale waliokadhibisha Aayaat Zetu na makutano ya Aakhirah, zimeporomoka ‘amali zao. Je, kwani watalipwa isipokuwa yale waliyokuwa wakiyatenda?

 

 

 

وَاتَّخَذَ قَوْمُ مُوسَىٰ مِن بَعْدِهِ مِنْ حُلِيِّهِمْ عِجْلًا جَسَدًا لَّهُ خُوَارٌ ۚ أَلَمْ يَرَوْا أَنَّهُ لَا يُكَلِّمُهُمْ وَلَا يَهْدِيهِمْ سَبِيلًا ۘ اتَّخَذُوهُ وَكَانُوا ظَالِمِينَ ﴿١٤٨﴾

148. Na watu wa Muwsaa baada ya kuondoka kwake, walijifanyia ndama; kiwiliwili chenye sauti ya ng’ombe kwa kutumia mapambo yao. Je, hawakuona kwamba huyo (ndama) hawasemeshi wala hawaongozi njia? Walimfanya (mwabudiwa) na wakawa madhalimu.

 

 

 

وَلَمَّا سُقِطَ فِي أَيْدِيهِمْ وَرَأَوْا أَنَّهُمْ قَدْ ضَلُّوا قَالُوا لَئِن لَّمْ يَرْحَمْنَا رَبُّنَا وَيَغْفِرْ لَنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿١٤٩﴾

149. Na walipojuta na wakaona kwamba kwa yakini wamepotoka walisema: Asipoturehemu Rabb wetu na Akatughufuria, bila shaka tutakuwa miongoni mwa waliokhasirika.

 

 

 

وَلَمَّا رَجَعَ مُوسَىٰ إِلَىٰ قَوْمِهِ غَضْبَانَ أَسِفًا قَالَ بِئْسَمَا خَلَفْتُمُونِي مِن بَعْدِي ۖ أَعَجِلْتُمْ أَمْرَ رَبِّكُمْ ۖ وَأَلْقَى الْأَلْوَاحَ وَأَخَذَ بِرَأْسِ أَخِيهِ يَجُرُّهُ إِلَيْهِ ۚ قَالَ ابْنَ أُمَّ إِنَّ الْقَوْمَ اسْتَضْعَفُونِي وَكَادُوا يَقْتُلُونَنِي فَلَا تُشْمِتْ بِيَ الْأَعْدَاءَ وَلَا تَجْعَلْنِي مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿١٥٠﴾

150. Na Muwsaa aliporejea kwa kaumu yake hali ya kuwa ameghadhibika na kusikitika, alisema: Ubaya ulioje mmeniwakilisha baada yangu. Je, mmeharakiza Amri ya Rabb wenu? Akatupa vile vibao na akakamata kichwa cha kaka yake akimvuta kwake. (Haaruwn) Akasema: Ee mwana wa mama yangu! Hakika watu (hawa) walinizidi nguvu na walikaribia kuniua, basi usinifanye kifurahisho cha maadui, na wala usiniweke pamoja na watu madhalimu.

 

 

 

قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي وَلِأَخِي وَأَدْخِلْنَا فِي رَحْمَتِكَ ۖ وَأَنتَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ ﴿١٥١﴾

151. (Muwsaa) Akasema: Rabb wangu! Nighufurie mimi na kaka yangu, na Utuingize katika Rahmah Yako. Nawe Ndiye Mbora zaidi wa Kurehemu kuliko wengine wote wenye kurehemu.

 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ اتَّخَذُوا الْعِجْلَ سَيَنَالُهُمْ غَضَبٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَذِلَّةٌ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُفْتَرِينَ ﴿١٥٢﴾

152. Hakika wale waliomchukua ndama (kumwabudu) itawafika ghadhabu kutoka kwa Rabb wao na udhalilifu katika uhai wa dunia. Na hivyo ndivyo Tunavyowalipa wenye kuzusha (ubatilifu).

 

 

 

وَالَّذِينَ عَمِلُوا السَّيِّئَاتِ ثُمَّ تَابُوا مِن بَعْدِهَا وَآمَنُوا إِنَّ رَبَّكَ مِن بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٥٣﴾

153. Na wale waliotenda maovu kisha wakatubu baada yake na wakaamini, hakika Rabb wako baada ya hayo bila shaka Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

وَلَمَّا سَكَتَ عَن مُّوسَى الْغَضَبُ أَخَذَ الْأَلْوَاحَ ۖ وَفِي نُسْخَتِهَا هُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلَّذِينَ هُمْ لِرَبِّهِمْ يَرْهَبُونَ ﴿١٥٤﴾

154. Na ghadhabu zilipomtulia Muwsaa, alivichukua vile vibao. Na katika maandiko yake mna mwongozo na Rahmah kwa ambao wao wanamkhofu Rabb wao.

 

 

 

 

 

وَاكْتُبْ لَنَا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ إِنَّا هُدْنَا إِلَيْكَ ۚ قَالَ عَذَابِي أُصِيبُ بِهِ مَنْ أَشَاءُ ۖ وَرَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ ۚ فَسَأَكْتُبُهَا لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَالَّذِينَ هُم بِآيَاتِنَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٥٦﴾

156. Na Tuandikie katika dunia hii mazuri na katika Aakhirah. Hakika sisi tumerudi kutubu Kwako. (Allaah) Akasema: Adhabu Yangu Nitamsibu nayo Nimtakaye. Na Rahmah Yangu imeenea kila kitu. Basi Nitawaandikia wale wenye taqwa na wanaotoa Zakaah na ambao wao wanaziamini Aayaat (ishara, dalili) Zetu.[14]

 

 

 

الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الرَّسُولَ النَّبِيَّ الْأُمِّيَّ الَّذِي يَجِدُونَهُ مَكْتُوبًا عِندَهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ يَأْمُرُهُم بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَاهُمْ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ وَيَضَعُ عَنْهُمْ إِصْرَهُمْ وَالْأَغْلَالَ الَّتِي كَانَتْ عَلَيْهِمْ ۚ فَالَّذِينَ آمَنُوا بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ الَّذِي أُنزِلَ مَعَهُ ۙ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿١٥٧﴾

157. Wale wanaomfuata Rasuli; Nabiy asiyejua kusoma wala kuandika ambaye wanamkuta ameandikwa kwao katika Tawraat na Injiyl, anawaamrisha mema na anawakataza munkari, na anawahalalishia vilivyo vizuri na anawaharamishia vilivyo vibaya na anawaondoshea mizigo yao na minyororo iliyokuwa juu yao. Basi wale waliomwamini na wakamtukuza, na wakamnusuru na wakafuata Nuru (Qur-aan) ambayo imeteremshwa pamoja naye, hao ndio wenye kufaulu.

 

 

 

قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ النَّبِيِّ الْأُمِّيِّ الَّذِي يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَكَلِمَاتِهِ وَاتَّبِعُوهُ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ﴿١٥٨﴾

158. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika mimi ni Rasuli wa Allaah kwenu nyinyi nyote. (Allaah) Ambaye ni Wake ufalme wa mbingu na ardhi. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye. Anahuisha na Anafisha. Basi mwaminini Allaah na Rasuli Wake; Nabiy asiyejua kusoma wala kuandika ambaye anamwamini Allaah na Maneno Yake, na mfuateni ili mpate kuongoka.

 

 

 

وَمِن قَوْمِ مُوسَىٰ أُمَّةٌ يَهْدُونَ بِالْحَقِّ وَبِهِ يَعْدِلُونَ ﴿١٥٩﴾

159. Na katika kaumu ya Muwsaa (walikuweko) ummah wanaongoza kwa haki, na kwayo wanahukumu kiadilifu.

 

 

 

وَقَطَّعْنَاهُمُ اثْنَتَيْ عَشْرَةَ أَسْبَاطًا أُمَمًا ۚ وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ إِذِ اسْتَسْقَاهُ قَوْمُهُ أَنِ اضْرِب بِّعَصَاكَ الْحَجَرَ ۖ فَانبَجَسَتْ مِنْهُ اثْنَتَا عَشْرَةَ عَيْنًا ۖ قَدْ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٍ مَّشْرَبَهُمْ ۚ وَظَلَّلْنَا عَلَيْهِمُ الْغَمَامَ وَأَنزَلْنَا عَلَيْهِمُ الْمَنَّ وَالسَّلْوَىٰ ۖ كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ ۚ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿١٦٠﴾

160. Na Tukawagawanya makabila kumi na mbili yakiwa mataifa (ya Bani Israaiyl). Na Tukamfunulia Wahy Muwsaa walipomuomba maji kaumu yake, kwamba: Piga jiwe kwa fimbo yako. Zikachimbuka toka humo chemchemu kumi na mbili. Kila kabila likajua mahali pake pa kunywea maji. Na Tukawawekea kivuli kwa mawingu na Tukawateremshia manna na salwaa.[15] (Tukawaambia): Kuleni katika vizuri Tulivyokuruzukuni. Hawakutudhulumu Sisi lakini walikuwa wakizidhulumu nafsi zao.

 

 

 

وَإِذْ قِيلَ لَهُمُ اسْكُنُوا هَـٰذِهِ الْقَرْيَةَ وَكُلُوا مِنْهَا حَيْثُ شِئْتُمْ وَقُولُوا حِطَّةٌ وَادْخُلُوا الْبَابَ سُجَّدًا نَّغْفِرْ لَكُمْ خَطِيئَاتِكُمْ ۚ سَنَزِيدُ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٦١﴾

161. Na pale walipoambiwa: Kaeni katika mji huu (Quds), na kuleni humo popote mpendapo, na semeni: Hittwah[16] (Tuondolee uzito wa madhambi) na ingieni katika mlango wake huku mmeinama kwa unyenyekevu. Tutakughufurieni makosa yenu, Tutawazidishia (Neema na Thawabu) wafanyao ihsaan.  

 

 

 

فَبَدَّلَ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْهُمْ قَوْلًا غَيْرَ الَّذِي قِيلَ لَهُمْ فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِجْزًا مِّنَ السَّمَاءِ بِمَا كَانُوا يَظْلِمُونَ ﴿١٦٢﴾

162. Lakini waliodhulumu miongoni mwao walibadilisha kauli tofauti na ile waliyoambiwa, Tukawapelekea adhabu ya kufadhaika kutoka mbinguni kwa sababu ya wao kujidhulumu.

 

 

 

وَاسْأَلْهُمْ عَنِ الْقَرْيَةِ الَّتِي كَانَتْ حَاضِرَةَ الْبَحْرِ إِذْ يَعْدُونَ فِي السَّبْتِ إِذْ تَأْتِيهِمْ حِيتَانُهُمْ يَوْمَ سَبْتِهِمْ شُرَّعًا وَيَوْمَ لَا يَسْبِتُونَ ۙ لَا تَأْتِيهِمْ ۚ كَذَٰلِكَ نَبْلُوهُم بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴿١٦٣﴾

163. Na waulize kuhusu mji ambao ulikuwa kando ya bahari, waliporuka mipaka ya As-Sabt walipowajia samaki wao waziwazi siku yao ya As-Sabt lakini siku zisizokuwa za As-Sabt hawakuwajia. Hivyo ndivyo Tulivyowajaribu kutokana na kukhalifu kwao amri.[17]

 

 

 

وَإِذْ قَالَتْ أُمَّةٌ مِّنْهُمْ لِمَ تَعِظُونَ قَوْمًا ۙ اللَّـهُ مُهْلِكُهُمْ أَوْ مُعَذِّبُهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا ۖ قَالُوا مَعْذِرَةً إِلَىٰ رَبِّكُمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿١٦٤﴾

164. Na pale kundi miongoni mwao waliposema: Kwa nini mnawawaidhi watu ambao Allaah Atawahilikisha tu au Atawaadhibu adhabu kali? Wakasema: Tupate kuwa na udhuru mbele ya Rabb wenu na huenda wakawa watu wa taqwa.

 

 

 

فَلَمَّا نَسُوا مَا ذُكِّرُوا بِهِ أَنجَيْنَا الَّذِينَ يَنْهَوْنَ عَنِ السُّوءِ وَأَخَذْنَا الَّذِينَ ظَلَمُوا بِعَذَابٍ بَئِيسٍ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴿١٦٥﴾

165. Waliposahau yale waliyokumbushwa nayo, Tuliwaokoa wale wanaokataza uovu, na Tukawachukua wale waliodhulumu kwa adhabu mbaya kabisa kwa sababu ya kukhalifu kwao amri.

 

 

 

فَلَمَّا عَتَوْا عَن مَّا نُهُوا عَنْهُ قُلْنَا لَهُمْ كُونُوا قِرَدَةً خَاسِئِينَ ﴿١٦٦﴾

166. Basi walipozidi kuasi kwenye hilo walilokatazwa, Tulisema: Kuweni manyani waliotezwa.

 

 

 

وَإِذْ تَأَذَّنَ رَبُّكَ لَيَبْعَثَنَّ عَلَيْهِمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَن يَسُومُهُمْ سُوءَ الْعَذَابِ ۗ إِنَّ رَبَّكَ لَسَرِيعُ الْعِقَابِ ۖ وَإِنَّهُ لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٦٧﴾

167. Na pindi Alipotangaza Rabb wako kwamba bila shaka Atawatumia (Mayahudi) watu waliowazidi nguvu, ambao watawaonjesha adhabu mbaya mpaka Siku ya Qiyaamah. Hakika Rabb wako Ni Mwepesi wa Kuadhibu, na hakika Yeye bila shaka Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

وَقَطَّعْنَاهُمْ فِي الْأَرْضِ أُمَمًا ۖ مِّنْهُمُ الصَّالِحُونَ وَمِنْهُمْ دُونَ ذَٰلِكَ ۖ وَبَلَوْنَاهُم بِالْحَسَنَاتِ وَالسَّيِّئَاتِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿١٦٨﴾

168. Na Tuliwafarikisha katika ardhi mataifa mbalimbali. Miongoni mwao wako wema na miongoni mwao wako kinyume chake. Na Tukawajaribu kwa ya faraja na ya dhiki ili wapate kurejea (katika utiifu).  

 

 

 

فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ وَرِثُوا الْكِتَابَ يَأْخُذُونَ عَرَضَ هَـٰذَا الْأَدْنَىٰ وَيَقُولُونَ سَيُغْفَرُ لَنَا وَإِن يَأْتِهِمْ عَرَضٌ مِّثْلُهُ يَأْخُذُوهُ ۚ أَلَمْ يُؤْخَذْ عَلَيْهِم مِّيثَاقُ الْكِتَابِ أَن لَّا يَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ إِلَّا الْحَقَّ وَدَرَسُوا مَا فِيهِ ۗ وَالدَّارُ الْآخِرَةُ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿١٦٩﴾

169. Basi wakafuatia baada yao kizazi kiovu waliorithi Kitabu. Wanachukua manufaa duni ya hii dunia na wanasema: Tutaghufuriwa. Na yakiwajia tena manufaa kama hayo hayo wanayachukua. Je, halikuchukuliwa kwao fungamano la Kitabu kwamba wasiseme juu ya Allaah isipokuwa haki tu na hali wao wameshayadurusu yaliyomo humo? Na nyumba ya Aakhirah ni bora zaidi kwa wale wenye taqwa. Je, basi hamtii akilini?

 

 

 

وَالَّذِينَ يُمَسِّكُونَ بِالْكِتَابِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجْرَ الْمُصْلِحِينَ ﴿١٧٠﴾

170. Na wale wanaoshikilia imara Kitabu na wakasimamisha Swalaah, hakika Sisi Hatupotezi ujira wa watendao mema.

 

 

 

وَإِذْ نَتَقْنَا الْجَبَلَ فَوْقَهُمْ كَأَنَّهُ ظُلَّةٌ وَظَنُّوا أَنَّهُ وَاقِعٌ بِهِمْ خُذُوا مَا آتَيْنَاكُم بِقُوَّةٍ وَاذْكُرُوا مَا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٧١﴾

171. Na pindi Tulipong’oa na kuinua mlima juu yao kama kwamba ni kanopi na wakadhani kwamba utawaangukia. (Tukawaambia): Chukueni Tuliyokupeni kwa nguvu, na kumbukeni yale yaliyomo humo ili mpate kuwa na taqwa.

 

 

 

وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِن بَنِي آدَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَأَشْهَدَهُمْ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ ۖ قَالُوا بَلَىٰ ۛ شَهِدْنَا ۛ أَن تَقُولُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَـٰذَا غَافِلِينَ ﴿١٧٢﴾

172. Na pindi Rabb wako Alipowaleta wana wa Aadam kutoka migongoni mwao kizazi chao, Akawashuhudisha juu ya nafsi zao, Je, Mimi siye Rabb wenu? Wakasema: Ndio bila shaka, tumeshuhudia! (Allaah Akawaambia): Msije kusema Siku ya Qiyaamah: hakika sisi tulikuwa tumeghafilika nayo haya.[18]

 

 

 

أَوْ تَقُولُوا إِنَّمَا أَشْرَكَ آبَاؤُنَا مِن قَبْلُ وَكُنَّا ذُرِّيَّةً مِّن بَعْدِهِمْ ۖ أَفَتُهْلِكُنَا بِمَا فَعَلَ الْمُبْطِلُونَ ﴿١٧٣﴾

173. Au mkasema: Hakika baba zetu ndio walioshirikisha kabla, nasi tulikuwa kizazi baada yao. Basi Utatuangamiza kwa yale waliyoyafanya wabatilifu?

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ وَلَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿١٧٤﴾

174. Na hivyo ndivyo Tunavyofasili waziwazi Aayaat na ili wapate kurejea (katika utiifu).

 

 

 

وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ الَّذِي آتَيْنَاهُ آيَاتِنَا فَانسَلَخَ مِنْهَا فَأَتْبَعَهُ الشَّيْطَانُ فَكَانَ مِنَ الْغَاوِينَ ﴿١٧٥﴾

175. Na wasomee (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) khabari za yule Tuliyempa Aayaat (ishara, dalili) Zetu, akajivua nazo na shaytwaan akamfuata, na akawa miongoni mwa waliopotoka.

 

 

 

وَلَوْ شِئْنَا لَرَفَعْنَاهُ بِهَا وَلَـٰكِنَّهُ أَخْلَدَ إِلَى الْأَرْضِ وَاتَّبَعَ هَوَاهُ ۚ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ الْكَلْبِ إِن تَحْمِلْ عَلَيْهِ يَلْهَثْ أَوْ تَتْرُكْهُ يَلْهَث ۚ ذَّٰلِكَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۚ فَاقْصُصِ الْقَصَصَ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ ﴿١٧٦﴾

176. Na lau Tungelitaka Tungelimnyanyua kwazo (hizo Aayaat), lakini aligandamana na dunia na akafuata hawaa zake. Basi mfano wake ni kama mfano wa mbwa, ukimhujumu ananing’iniza ulimi nje na kuhema, na ukimwacha pia ananing’iniza ulimi nje na kuhema. Hivyo ndiyo mfano wa watu waliokadhibisha Aayaat Zetu. Basi simulia visa huenda wakatafakari.

 

 

 

سَاءَ مَثَلًا الْقَوْمُ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَأَنفُسَهُمْ كَانُوا يَظْلِمُونَ ﴿١٧٧﴾

177. Uovu ulioje mfano wa watu waliokadhibisha Aayaat Zetu na wakawa wanajidhulumu nafsi zao!   

 

 

 

مَن يَهْدِ اللَّـهُ فَهُوَ الْمُهْتَدِي ۖ وَمَن يُضْلِلْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿١٧٨﴾

178. Atakaowaongoza Allaah, basi ndio watakaohidika, na Atakaowaachia kupotoka, basi hao ndio wenye kukhasirika.

 

 

 

وَلَقَدْ ذَرَأْنَا لِجَهَنَّمَ كَثِيرًا مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ ۖ لَهُمْ قُلُوبٌ لَّا يَفْقَهُونَ بِهَا وَلَهُمْ أَعْيُنٌ لَّا يُبْصِرُونَ بِهَا وَلَهُمْ آذَانٌ لَّا يَسْمَعُونَ بِهَا ۚ أُولَـٰئِكَ كَالْأَنْعَامِ بَلْ هُمْ أَضَلُّ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْغَافِلُونَ ﴿١٧٩﴾

179. Kwa yakini Tumeumba Jahannam kwa ajili ya wengi katika majini na wana Aadam. Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo. Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama, bali wao ni wapotovu zaidi. Hao ndio walioghafilika.

 

 

 

وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٨٠﴾

180. Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanaopotoa na kuharibu Majina Yake, watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda.[19]

 

 

 

وَمِمَّنْ خَلَقْنَا أُمَّةٌ يَهْدُونَ بِالْحَقِّ وَبِهِ يَعْدِلُونَ ﴿١٨١﴾

181. Na katika Tuliowaumba, wako ummah wanaoongoza kwa haki na kwayo wanahukumu kiadilifu.[20]

 

 

وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا سَنَسْتَدْرِجُهُم مِّنْ حَيْثُ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٨٢﴾

182. Na wale waliokadhibisha Aayaat Zetu Tutawavuta polepole (kuwaadhibu) kwa namna wasiyoijua.

 

 

 

وَأُمْلِي لَهُمْ ۚ إِنَّ كَيْدِي مَتِينٌ ﴿١٨٣﴾

183. Nami Ninawapa muhula. Hakika Mpango Wangu (wa adhabu) ni wenye nguvu.

 

 

 

أَوَلَمْ يَتَفَكَّرُوا ۗ مَا بِصَاحِبِهِم مِّن جِنَّةٍ ۚ إِنْ هُوَ إِلَّا نَذِيرٌ مُّبِينٌ ﴿١٨٤﴾

184. Je, hawatafakari? Swahibu yao (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) hana wazimu! Hakuwa yeye ila ni mwonyaji bayana.

 

 

 

أَوَلَمْ يَنظُرُوا فِي مَلَكُوتِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا خَلَقَ اللَّـهُ مِن شَيْءٍ وَأَنْ عَسَىٰ أَن يَكُونَ قَدِ اقْتَرَبَ أَجَلُهُمْ ۖ فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَهُ يُؤْمِنُونَ ﴿١٨٥﴾

185. Je, hawatazami ufalme mkuu wa mbingu na ardhi na vitu Alivyoviumba Allaah, na asaa ukawa muda wao uliopangwa umeshakaribia? Basi ujumbe gani baada yake (hii Qur-aan) wataamini?

 

 

 

مَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَلَا هَادِيَ لَهُ ۚ وَيَذَرُهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ ﴿١٨٦﴾

186. Ambao Allaah Amewapotoa, basi hakuna wa kuwahidi. Na Atawaacha katika upindukaji mipaka ya kuasi kwao, wakitangatanga kwa upofu.

 

 

 

يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا ۖ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ رَبِّي ۖ لَا يُجَلِّيهَا لِوَقْتِهَا إِلَّا هُوَ ۚ ثَقُلَتْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ لَا تَأْتِيكُمْ إِلَّا بَغْتَةً ۗ يَسْأَلُونَكَ كَأَنَّكَ حَفِيٌّ عَنْهَا ۖ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ اللَّـهِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٨٧﴾

187. Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Saa (Qiyaamah), lini kutokea kwake? Sema: Hakika ujuzi wake uko kwa Rabb wangu. Hakuna wa kuidhihirisha wakati wake isipokuwa Yeye. Ni nzito katika mbingu na ardhi. Haitokufikieni isipokuwa kwa ghafla. Wanakuuliza kama kwamba wewe unaijua vyema. Sema: Hakika ujuzi wake uko kwa Allaah (Pekee), lakini watu wengi hawajui.[21]

 

 

 

قُل لَّا أَمْلِكُ لِنَفْسِي نَفْعًا وَلَا ضَرًّا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ ۚ وَلَوْ كُنتُ أَعْلَمُ الْغَيْبَ لَاسْتَكْثَرْتُ مِنَ الْخَيْرِ وَمَا مَسَّنِيَ السُّوءُ ۚ إِنْ أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿١٨٨﴾

188. Sema: Siimilikii nafsi yangu manufaa yoyote wala dhara yoyote isipokuwa Apendavyo Allaah. Na lau ningekuwa najua ya ghaibu, bila shaka ningelijikithirishia ya kheri, na wala lisingelinigusa ovu. Mimi si chochote isipokuwa ni mwonyaji na mbashiriaji kwa watu wanaoamini.

 

 

 

هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَجَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا لِيَسْكُنَ إِلَيْهَا ۖ فَلَمَّا تَغَشَّاهَا حَمَلَتْ حَمْلًا خَفِيفًا فَمَرَّتْ بِهِ ۖ فَلَمَّا أَثْقَلَت دَّعَوَا اللَّـهَ رَبَّهُمَا لَئِنْ آتَيْتَنَا صَالِحًا لَّنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ ﴿١٨٩﴾

189. Yeye (Allaah) Ndiye Aliyekuumbeni kutokana na nafsi moja na Akafanya kutokana nayo mke wake ili apate utulivu. Basi anapomuingilia hubeba mimba khafifu anayotembea nayo. Kisha inapokuwa nzito humwomba Allaah Rabb wao: Ukitupa (mwana) mwema asiyekuwa na kasoro, bila shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru.

 

 

 

فَلَمَّا آتَاهُمَا صَالِحًا جَعَلَا لَهُ شُرَكَاءَ فِيمَا آتَاهُمَا ۚ فَتَعَالَى اللَّـهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿١٩٠﴾

190. Basi Anapowapa (mwana) mwema asiyekuwa na kasoro, wanamfanyia (Allaah) washirika katika kile Alichowapa. Basi Ametukuka Allaah kwa Uluwa kutokana na yale yote wanayoshirikisha.

 

 

 

أَيُشْرِكُونَ مَا لَا يَخْلُقُ شَيْئًا وَهُمْ يُخْلَقُونَ ﴿١٩١﴾

191. Je, wanawashirikisha (na Allaah) wale ambao hawaumbi kitu na hali wao wameumbwa?

 

 

 

وَلَا يَسْتَطِيعُونَ لَهُمْ نَصْرًا وَلَا أَنفُسَهُمْ يَنصُرُونَ ﴿١٩٢﴾

192. Na wala hawawezi kuwanusuru na wala hawawezi kujinusuru nafsi zao.

 

 

 

وَإِن تَدْعُوهُمْ إِلَى الْهُدَىٰ لَا يَتَّبِعُوكُمْ ۚ سَوَاءٌ عَلَيْكُمْ أَدَعَوْتُمُوهُمْ أَمْ أَنتُمْ صَامِتُونَ ﴿١٩٣﴾

193. Na mkiwaita kwenye uongofu hawatokufuateni. Ni sawasawa kwenu, mkiwaita au mkiwanyamazia.

 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ عِبَادٌ أَمْثَالُكُمْ ۖ فَادْعُوهُمْ فَلْيَسْتَجِيبُوا لَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٩٤﴾

194. Hakika wale mnaowaomba badala ya Allaah ni waja kama nyinyi. Hebu waiteni wakuitikieni ikiwa nyinyi ni wakweli.

 

 

 

أَلَهُمْ أَرْجُلٌ يَمْشُونَ بِهَا ۖ أَمْ لَهُمْ أَيْدٍ يَبْطِشُونَ بِهَا ۖ أَمْ لَهُمْ أَعْيُنٌ يُبْصِرُونَ بِهَا ۖ أَمْ لَهُمْ آذَانٌ يَسْمَعُونَ بِهَا ۗ قُلِ ادْعُوا شُرَكَاءَكُمْ ثُمَّ كِيدُونِ فَلَا تُنظِرُونِ ﴿١٩٥﴾

195. Je, kwani wana miguu wanayotembelea nayo? Au wana mikono wanayokamatia kwayo? Au wana macho wanayoonea kwayo? Au wana masikio wanayosikilizia kwayo? Sema: Waiteni washirika wenu, kisha nifanyieni njama, wala msinipe muhula.

 

 

 

إِنَّ وَلِيِّيَ اللَّـهُ الَّذِي نَزَّلَ الْكِتَابَ ۖ وَهُوَ يَتَوَلَّى الصَّالِحِينَ ﴿١٩٦﴾

196. Hakika Mlinzi wangu Ni Allaah Ambaye Ameteremsha Kitabu, Naye Ndiye Anayewalinda na kuwasaidia Swalihina.[22]

 

 

 

وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَكُمْ وَلَا أَنفُسَهُمْ يَنصُرُونَ ﴿١٩٧﴾

197. Na wale mnaowaomba (na kuwaabudu) badala ya Allaah hawawezi kuwanusuru na wala hawawezi kujinusuru nafsi zao.

 

 

 

وَإِن تَدْعُوهُمْ إِلَى الْهُدَىٰ لَا يَسْمَعُوا ۖ وَتَرَاهُمْ يَنظُرُونَ إِلَيْكَ وَهُمْ لَا يُبْصِرُونَ ﴿١٩٨﴾

198. Na ukiwaita katika uongofu hawasikii, na utawaona wanakutazama na hali wao hawaoni.

 

 

 

خُذِ الْعَفْوَ وَأْمُرْ بِالْعُرْفِ وَأَعْرِضْ عَنِ الْجَاهِلِينَ ﴿١٩٩﴾

199.   Shikamana na usamehevu, na amrisha mema na jiepushe na majahili.

 

 

 

وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ ۚ إِنَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٠٠﴾

200. Na pindi utakapokuchochea uchochezi kutokana na shaytwaan, basi omba kinga kwa Allaah. Hakika Yeye Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ اتَّقَوْا إِذَا مَسَّهُمْ طَائِفٌ مِّنَ الشَّيْطَانِ تَذَكَّرُوا فَإِذَا هُم مُّبْصِرُونَ ﴿٢٠١﴾

201. Hakika wale wenye taqwa zinapowagusa pepesi za shaytwaan hukumbuka, basi mara wao huwa wenye kuona kwa utambuzi. 

 

 

 

وَإِخْوَانُهُمْ يَمُدُّونَهُمْ فِي الْغَيِّ ثُمَّ لَا يُقْصِرُونَ ﴿٢٠٢﴾

202. Na ndugu zao wanawavutia katika upotofu, kisha hawakasiri. 

 

 

 

وَإِذَا لَمْ تَأْتِهِم بِآيَةٍ قَالُوا لَوْلَا اجْتَبَيْتَهَا ۚ قُلْ إِنَّمَا أَتَّبِعُ مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ مِن رَّبِّي ۚ هَـٰذَا بَصَائِرُ مِن رَّبِّكُمْ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٢٠٣﴾

203. Na usipowaletea Aayah (muujiza, ishara) husema: Kwa nini hukuibuni? Sema: Hakika nafuata yale tu niliyofunuliwa Wahy kutoka kwa Rabb wangu. Hii (Qur-aan) ni hoja, ishara na dalili wazi kutoka kwa Rabb wenu, na ni Mwongozo na Rahmah kwa watu wanaoamini.

 

 

 

وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٢٠٤﴾

204. Na inaposomwa Qur-aan, basi isikilizeni kwa makini na bakieni kimya (mzingatie) ili mpate kurehemewa.

 

 

 

وَاذْكُر رَّبَّكَ فِي نَفْسِكَ تَضَرُّعًا وَخِيفَةً وَدُونَ الْجَهْرِ مِنَ الْقَوْلِ بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ وَلَا تَكُن مِّنَ الْغَافِلِينَ ﴿٢٠٥﴾

205. Na mdhukuru Rabb wako katika nafsi yako kwa unyenyekevu na kwa khofu   na kwa ulimi bila sauti kubwa asubuhi na jioni, na wala usiwe miongoni mwa walioghafilika.

 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ لَا يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِهِ وَيُسَبِّحُونَهُ وَلَهُ يَسْجُدُونَ ۩﴿٢٠٦﴾

206. Hakika wale (Malaika) walioko kwa Rabb wako hawatakabari wakaacha kumwabudu na wanamsabihi, na Yeye tu wanamsujudia.[23]

 

 

 

 

Share