048 - Al-Fat-h

 

 

 

  الْفَتْح

Al-Fat-h: 048

 

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُّبِينًا﴿١﴾

1. Hakika Tumekupa ushindi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), ushindi bayana.

 

 

لِّيَغْفِرَ لَكَ اللَّـهُ مَا تَقَدَّمَ مِن ذَنبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ وَيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكَ وَيَهْدِيَكَ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا﴿٢﴾

2. Ili Allaah Akughufurie yale yaliyotangulia katika madhambi yako na yale yanayofuatia, na Akutimizie Neema Yake juu yako, na Akuongoze njia iliyonyooka.

 

 

وَيَنصُرَكَ اللَّـهُ نَصْرًا عَزِيزًا﴿٣﴾

3. Na Akunusuru Allaah nusura yenye nguvu kabisa.

 

 

هُوَ الَّذِي أَنزَلَ السَّكِينَةَ فِي قُلُوبِ الْمُؤْمِنِينَ لِيَزْدَادُوا إِيمَانًا مَّعَ إِيمَانِهِمْ ۗ وَلِلَّـهِ جُنُودُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا﴿٤﴾

4. Yeye Ndiye Aliyeteremsha utulivu katika nyoyo za Waumini ili wazidi Iymaan pamoja na iymaan zao. Na ni ya Allaah Pekee majeshi ya mbinguni na ardhini. Na Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

لِّيُدْخِلَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَيُكَفِّرَ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عِندَ اللَّـهِ فَوْزًا عَظِيمًا﴿٥﴾

5. Ili Awaingize Waumini wa kiume na Waumini wa kike Jannaat zipitazo chini yake mito, wadumu humo, na Awafutie maovu yao. Na hayo ndiyo mafanikio makubwa zaidi mbele ya Allaah.

 

 

وَيُعَذِّبَ الْمُنَافِقِينَ وَالْمُنَافِقَاتِ وَالْمُشْرِكِينَ وَالْمُشْرِكَاتِ الظَّانِّينَ بِاللَّـهِ ظَنَّ السَّوْءِ ۚ عَلَيْهِمْ دَائِرَةُ السَّوْءِ ۖ وَغَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ وَلَعَنَهُمْ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَهَنَّمَ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا﴿٦﴾

6. Na Awaadhibu wanafiki wa kiume na wanafiki wa kike na washirikina wa kiume na washirikina wa kike, wanaomdhania Allaah dhana ovu.  Utawafikia hao mgeuko mbaya. Na Allaah (pamoja na hayo) Amewaghadhibikia, Amewalaani, na Amewaandalia Jahannam. Na paovu palioje mahali pa kuishia!

 

 

 

وَلِلَّـهِ جُنُودُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا﴿٧﴾

7. Na ni ya Allaah Pekee majeshi ya mbinguni na ardhini. Na Allaah daima Ni Mwenye Enzi na Nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.

 

 

إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ شَاهِدًا وَمُبَشِّرًا وَنَذِيرًا﴿٨﴾

8.  Hakika Sisi Tumekutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ukiwa ni shahidi, mwenye kubashiri na mwonyaji.

 

 

لِّتُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَتُعَزِّرُوهُ وَتُوَقِّرُوهُ وَتُسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا﴿٩﴾

9. Ili mumwamini Allaah na Rasuli Wake, na mumsaidie kwa taadhima, na mumheshimu kwa utukuzo (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), na mumsabbih (Allaah سبحانه وتعالى) asubuhi na jioni.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ يُبَايِعُونَكَ إِنَّمَا يُبَايِعُونَ اللَّـهَ يَدُ اللَّـهِ فَوْقَ أَيْدِيهِمْ ۚ فَمَن نَّكَثَ فَإِنَّمَا يَنكُثُ عَلَىٰ نَفْسِهِ ۖ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِمَا عَاهَدَ عَلَيْهُ اللَّـهَ فَسَيُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا﴿١٠﴾

10. Hakika wale waliofungamana ahadi ya utiifu nawe, hakika hapana ila wanafungamana ahadi ya utiifu na Allaah, Mkono wa Allaah Uko juu ya mikono yao. Basi atakayevunja ahadi, hakika hapana ila anavunja dhidi ya nafsi yake. Na yeyote atimizaye yale aliyomuahidi Allaah, basi Atampa ujira adhimu.

 

 

سَيَقُولُ لَكَ الْمُخَلَّفُونَ مِنَ الْأَعْرَابِ شَغَلَتْنَا أَمْوَالُنَا وَأَهْلُونَا فَاسْتَغْفِرْ لَنَا ۚ يَقُولُونَ بِأَلْسِنَتِهِم مَّا لَيْسَ فِي قُلُوبِهِمْ ۚ قُلْ فَمَن يَمْلِكُ لَكُم مِّنَ اللَّـهِ شَيْئًا إِنْ أَرَادَ بِكُمْ ضَرًّا أَوْ أَرَادَ بِكُمْ نَفْعًا ۚ بَلْ كَانَ اللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا﴿١١﴾

11. Watakuambia mabedui waliobaki nyuma: Zimetushughulisha mali zetu na ahli zetu, basi tuombee Maghfirah. Wanasema kwa ndimi zao yasiyokuwemo nyoyoni mwao. Sema: Nani basi atayekuwa na uwezo kuzuia chochote toka kwa Allaah Akikusudia kukudhuruni au Akikusudia kukunufaisheni? Bali Allaah daima kwa yale myatendayo, Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.

 

 

بَلْ ظَنَنتُمْ أَن لَّن يَنقَلِبَ الرَّسُولُ وَالْمُؤْمِنُونَ إِلَىٰ أَهْلِيهِمْ أَبَدًا وَزُيِّنَ ذَٰلِكَ فِي قُلُوبِكُمْ وَظَنَنتُمْ ظَنَّ السَّوْءِ وَكُنتُمْ قَوْمًا بُورًا﴿١٢﴾

12. Bali mlidhania kwamba Rasuli na Waumini hawatorudi kwa ahli zao abadani, na likapambwa hilo katika nyoyo zenu, na mkadhania dhana ovu, na mkawa watu wa kuangamia.

 

 

وَمَن لَّمْ يُؤْمِن بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ فَإِنَّا أَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ سَعِيرًا﴿١٣﴾

13. Na asiyemuamini Allaah na Rasuli Wake, basi hakika Sisi Tumewaandalia makafiri moto uliowashwa vikali mno. 

 

 

وَلِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ يَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا﴿١٤﴾

14. Na ni wa Allaah Pekee ufalme wa mbingu na ardhi. Anamghufuria Amtakaye, na Anamuadhibu Amtakaye. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

سَيَقُولُ الْمُخَلَّفُونَ إِذَا انطَلَقْتُمْ إِلَىٰ مَغَانِمَ لِتَأْخُذُوهَا ذَرُونَا نَتَّبِعْكُمْ ۖ يُرِيدُونَ أَن يُبَدِّلُوا كَلَامَ اللَّـهِ ۚ قُل لَّن تَتَّبِعُونَا كَذَٰلِكُمْ قَالَ اللَّـهُ مِن قَبْلُ ۖ فَسَيَقُولُونَ بَلْ تَحْسُدُونَنَا ۚ بَلْ كَانُوا لَا يَفْقَهُونَ إِلَّا قَلِيلًا﴿١٥﴾

15. Waliobakia nyuma pale mtakapotoka kuelekea kwenye ghanima ili mzichukue watasema: Tuacheni tukufuateni! Wanataka kubadilisha Maneno ya Allaah. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hamtotufuata! Hivyo ndivyo Alivyosema Allaah kabla. Basi watasema: Hapana, bali mnatuhusudu! Hapana! Bali walikuwa hawafahamu isipokuwa kidogo.

 

 

قُل لِّلْمُخَلَّفِينَ مِنَ الْأَعْرَابِ سَتُدْعَوْنَ إِلَىٰ قَوْمٍ أُولِي بَأْسٍ شَدِيدٍ تُقَاتِلُونَهُمْ أَوْ يُسْلِمُونَ ۖ فَإِن تُطِيعُوا يُؤْتِكُمُ اللَّـهُ أَجْرًا حَسَنًا ۖ وَإِن تَتَوَلَّوْا كَمَا تَوَلَّيْتُم مِّن قَبْلُ يُعَذِّبْكُمْ عَذَابًا أَلِيمًا﴿١٦﴾

16. Waambie (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) waliobakia nyuma miongoni mwa mabedui: Mtaitwa kuwakabili watu wenye nguvu kali zaidi mpigane nao, au wasalimu amri. Lakini mkitii, Allaah Atakupeni ujira mzuri, na mkikengeuka kama mlivyokengeuka kabla Atakuadhibuni adhabu iumizayo.

 

 

لَّيْسَ عَلَى الْأَعْمَىٰ حَرَجٌ وَلَا عَلَى الْأَعْرَجِ حَرَجٌ وَلَا عَلَى الْمَرِيضِ حَرَجٌ ۗ وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ يُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ وَمَن يَتَوَلَّ يُعَذِّبْهُ عَذَابًا أَلِيمًا﴿١٧﴾

17. Hakuna dhambi juu ya kipofu, wala hakuna dhambi juu ya kilema, na wala hakuna dhambi juu ya mgonjwa (wasipokwenda vitani). Na yeyote atakayemtii Allaah na Rasuli Wake, (Allaah) Atamuingiza Jannaat zipitazo chini yake mito. Na atakayekengeuka, Atamuadhibu adhabu iumizayo.

 

 

لَّقَدْ رَضِيَ اللَّـهُ عَنِ الْمُؤْمِنِينَ إِذْ يُبَايِعُونَكَ تَحْتَ الشَّجَرَةِ فَعَلِمَ مَا فِي قُلُوبِهِمْ فَأَنزَلَ السَّكِينَةَ عَلَيْهِمْ وَأَثَابَهُمْ فَتْحًا قَرِيبًا﴿١٨﴾

18. Kwa yakini Allaah Amewawia radhi Waumini walipofungamana nawe ahadi ya utiifu (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) chini ya mti, (Allaah) Alijua yale yaliyomo nyoyoni mwao, basi Akawateremshia utulivu, na Akawalipa ushindi wa karibu.

 

 

وَمَغَانِمَ كَثِيرَةً يَأْخُذُونَهَا ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا﴿١٩﴾

19. Na ghanima nyingi watakazozichukua. Na Allaah daima Ni Mwenye Enzi na Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

وَعَدَكُمُ اللَّـهُ مَغَانِمَ كَثِيرَةً تَأْخُذُونَهَا فَعَجَّلَ لَكُمْ هَـٰذِهِ وَكَفَّ أَيْدِيَ النَّاسِ عَنكُمْ وَلِتَكُونَ آيَةً لِّلْمُؤْمِنِينَ وَيَهْدِيَكُمْ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا﴿٢٠﴾

20. Allaah Amekuahidini ghanima nyingi mtazichukua, Akakuharakizieni hizi, na Akazuia mikono ya watu dhidi yenu, na ili iwe ishara kwa Waumini, na Akuongozeni njia iliyonyooka.

 

 

وَأُخْرَىٰ لَمْ تَقْدِرُوا عَلَيْهَا قَدْ أَحَاطَ اللَّـهُ بِهَا ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرًا﴿٢١﴾

21. Na nyenginezo hamkuwa na uwezo nazo, Allaah Amekwishazizingia. Na Allaah daima juu ya kila kitu Ni Muweza.

 

 

وَلَوْ قَاتَلَكُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوَلَّوُا الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يَجِدُونَ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا﴿٢٢﴾

22. Na kama wangelipigana nanyi wale waliokufuru, basi wangeligeuza migongo yao, kisha wasipate mlinzi yoyote wala mwenye kunusuru.

 

 

سُنَّةَ اللَّـهِ الَّتِي قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلُ ۖ وَلَن تَجِدَ لِسُنَّةِ اللَّـهِ تَبْدِيلًا﴿٢٣﴾

23. Desturi ya Allaah ambayo imekwishapita kabla, na wala hutapata mabadiliko katika Desturi ya Allaah.

 

 

وَهُوَ الَّذِي كَفَّ أَيْدِيَهُمْ عَنكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ عَنْهُم بِبَطْنِ مَكَّةَ مِن بَعْدِ أَنْ أَظْفَرَكُمْ عَلَيْهِمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرًا﴿٢٤﴾

24. Naye Ndiye Aliyeizuia mikono yao dhidi yenu na mikono yenu dhidi yao katikati ya Makkah baada ya kukupeni ushindi juu yao. Na Allaah daima Ni Mwenye Kuona yale myatendayo.

 

 

هُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوكُمْ عَنِ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَالْهَدْيَ مَعْكُوفًا أَن يَبْلُغَ مَحِلَّهُ ۚ وَلَوْلَا رِجَالٌ مُّؤْمِنُونَ وَنِسَاءٌ مُّؤْمِنَاتٌ لَّمْ تَعْلَمُوهُمْ أَن تَطَئُوهُمْ فَتُصِيبَكُم مِّنْهُم مَّعَرَّةٌ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۖ لِّيُدْخِلَ اللَّـهُ فِي رَحْمَتِهِ مَن يَشَاءُ ۚ لَوْ تَزَيَّلُوا لَعَذَّبْنَا الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا﴿٢٥﴾

25. Wao ndio wale waliokufuru na wakakuzuieni na Al-Masjidil-Haraam, na wanyama wa kuchinjwa wakazuiliwa kufika mahali pa kuchinjwa. Na ingekuwa si wanaume Waumini na wanawake Waumini msiowajua nyinyi, mkawasaga kuwaua, na kwa sababu yao yakakusibuni madhambi (na fedheha) bila ya kujua (basi Angeliwaacheni muwamalize), ili Allaah Amuingize katika Rahmah Yake Amtakaye. Na lau kama (Waumini na makafiri) wangelitengana, basi Tungeliwaadhibu wale waliokufuru miongoni mwao adhabu iumizayo.

 

 

إِذْ جَعَلَ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي قُلُوبِهِمُ الْحَمِيَّةَ حَمِيَّةَ الْجَاهِلِيَّةِ فَأَنزَلَ اللَّـهُ سَكِينَتَهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ وَعَلَى الْمُؤْمِنِينَ وَأَلْزَمَهُمْ كَلِمَةَ التَّقْوَىٰ وَكَانُوا أَحَقَّ بِهَا وَأَهْلَهَا ۚ وَكَانَ اللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا﴿٢٦﴾

26. Pale waliokufuru walipotia katika nyoyo zao ghadhabu na kiburi; ghadhabu na kiburi za ujahili, na Allaah Akateremsha utulivu Wake juu ya Rasuli Wake na juu ya Waumini, na Akawalazimisha neno la taqwa (laa ilaaha illa-Allaah), na wakawa ndio wenye haki zaidi kwalo na wenye kustahiki. Na Allaah daima Ni Mjuzi wa kila kitu.

 

 

لَّقَدْ صَدَقَ اللَّـهُ رَسُولَهُ الرُّؤْيَا بِالْحَقِّ ۖ لَتَدْخُلُنَّ الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ إِن شَاءَ اللَّـهُ آمِنِينَ مُحَلِّقِينَ رُءُوسَكُمْ وَمُقَصِّرِينَ لَا تَخَافُونَ ۖ فَعَلِمَ مَا لَمْ تَعْلَمُوا فَجَعَلَ مِن دُونِ ذَٰلِكَ فَتْحًا قَرِيبًا﴿٢٧﴾

27. Kwa yakini Allaah Amemsadikisha Rasuli Wake ndoto kwa haki. Bila shaka mtaingia Al-Masjidul-Haraam In Shaa Allaah mkiwa katika amani, wenye kunyoa vichwa vyenu na wenye kupunguza, hamtakuwa na khofu.  Ameyajua ambayo hamkuyajua, Akajaalia kabla ya hayo ushindi wa karibu.  

 

 

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا﴿٢٨﴾

28. Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)  kwa mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote. Na Allaah Anatosha kuwa Ni Shahidi.

 

 

 

مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖ تَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا ۖ سِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِم مِّنْ أَثَرِ السُّجُودِ ۚ ذَٰلِكَ مَثَلُهُمْ فِي التَّوْرَاةِ ۚ وَمَثَلُهُمْ فِي الْإِنجِيلِ كَزَرْعٍ أَخْرَجَ شَطْأَهُ فَآزَرَهُ فَاسْتَغْلَظَ فَاسْتَوَىٰ عَلَىٰ سُوقِهِ يُعْجِبُ الزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ ۗ وَعَدَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنْهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا﴿٢٩﴾

29. Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Rasuli wa Allaah. Na wale walio pamoja naye ni wakali zaidi dhidi ya makafiri wanahurumiana baina yao. Utawaona wakirukuu na wakisujudu wakitafuta fadhila na radhi kutoka kwa Allaah. Alama zao dhahiri zi katika nyuso zao kutokana na athari za sujudu. Huo ni mfano wao katika Tawraat na mfano wao katika Injiyl. Ni kama mmea umetoa chipukizi lake, likautia nguvu kisha likawa nene, kisha likasimama sawasawa juu ya shina lake, linawapendeza wakulima, ili liwatie ghaidhi makafiri. Allaah Amewaahidi wale walioamini na wakatenda mema miongoni mwao Maghfirah na ujira adhimu.

 

 

Share