047 - Muhammad
مُحَمَّد
047-Muhammad
047-Muhammad: Utangulizi Wa Suwrah
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ أَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ﴿١﴾
1. Wale waliokufuru na wakazuia Njia ya Allaah, Atazipoteza ‘amali zao.
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَآمَنُوا بِمَا نُزِّلَ عَلَىٰ مُحَمَّدٍ وَهُوَ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ ۙ كَفَّرَ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَأَصْلَحَ بَالَهُمْ﴿٢﴾
2. Na wale walioamini na wakatenda mema na wakaamini yale aliyoteremshiwa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), nayo ni ya haki kutoka kwa Rabb wao, Atawafutia maovu yao na Atatengeneza hali zao.
ذَٰلِكَ بِأَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا اتَّبَعُوا الْبَاطِلَ وَأَنَّ الَّذِينَ آمَنُوا اتَّبَعُوا الْحَقَّ مِن رَّبِّهِمْ ۚ كَذَٰلِكَ يَضْرِبُ اللَّـهُ لِلنَّاسِ أَمْثَالَهُمْ﴿٣﴾
3. Hivyo kwa kuwa wale waliokufuru wamefuata ubatilifu, na kwamba wale walioamini wamefuata haki kutoka kwa Rabb wao. Hivyo ndivyo Allaah Anavyowapigia watu mifano yao.
فَإِذَا لَقِيتُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا فَضَرْبَ الرِّقَابِ حَتَّىٰ إِذَا أَثْخَنتُمُوهُمْ فَشُدُّوا الْوَثَاقَ فَإِمَّا مَنًّا بَعْدُ وَإِمَّا فِدَاءً حَتَّىٰ تَضَعَ الْحَرْبُ أَوْزَارَهَا ۚ ذَٰلِكَ وَلَوْ يَشَاءُ اللَّـهُ لَانتَصَرَ مِنْهُمْ وَلَـٰكِن لِّيَبْلُوَ بَعْضَكُم بِبَعْضٍ ۗ وَالَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَلَن يُضِلَّ أَعْمَالَهُمْ﴿٤﴾
4. Na mtakapokutana (vitani) na wale waliokufuru, basi wapigeni shingo zao, mpaka muwashinde kwa kuwajeruhi na kuwaua, na hapo wafungeni pingu barabara. Kisha ima (wafanyieni) ihsani baada ya hapo au wajifidie mpaka vita vitue mizigo yake. Ndio hivyo, na lau Allaah Angelitaka basi Angewalipiza kisasi Mwenyewe, lakini (Ameamrisha Jihaad) ili Akujaribuni nyinyi kwa nyinyi. Na wale waliouliwa katika Njia ya Allaah, basi Hatopoteza ‘amali zao.
سَيَهْدِيهِمْ وَيُصْلِحُ بَالَهُمْ﴿٥﴾
5. Atawaongoza na Atatengeneza hali zao.
وَيُدْخِلُهُمُ الْجَنَّةَ عَرَّفَهَا لَهُمْ﴿٦﴾
6. Na Atawaingiza Jannah Aliyoitambulisha kwao.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّـهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ﴿٧﴾
7. Enyi walioamini! Mkisaidia kunusuru Dini ya Allaah, (Allaah) Atakunusuruni na Ataithibitisha miguu yenu.
وَالَّذِينَ كَفَرُوا فَتَعْسًا لَّهُمْ وَأَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ﴿٨﴾
8. Na wale waliokufuru, basi ni maangamizo kwao, na Atapoteza amali zao.
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَرِهُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ﴿٩﴾
9. Hivyo ni kwa sababu wao wamekirihika na ambayo Allaah Ameyateremsha basi Amezibatilisha ‘amali zao.
أَفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ دَمَّرَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ ۖ وَلِلْكَافِرِينَ أَمْثَالُهَا﴿١٠﴾
10. Je, hawakutembea katika ardhi wakatazama vipi imekuwa hatima ya waliopita kabla yao? Allaah Amewadamirisha mbali, na kwa makafiri (itakuwa) mfano wa hayo.[1]
ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ مَوْلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَأَنَّ الْكَافِرِينَ لَا مَوْلَىٰ لَهُمْ﴿١١﴾
11. Hivyo ni kwa kuwa Allaah Ni Mlinzi wa wale walioamini na kwamba makafiri hawana mlinzi.
إِنَّ اللَّـهَ يُدْخِلُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا يَتَمَتَّعُونَ وَيَأْكُلُونَ كَمَا تَأْكُلُ الْأَنْعَامُ وَالنَّارُ مَثْوًى لَّهُمْ﴿١٢﴾
12. Hakika Allaah Atawaingiza wale walioamini na wakatenda mema Jannaat zipitazo chini yake mito. Na wale waliokufuru wanastarehe na wanakula kama walavyo wanyama wa mifugo, na moto ndio makazi yao.
وَكَأَيِّن مِّن قَرْيَةٍ هِيَ أَشَدُّ قُوَّةً مِّن قَرْيَتِكَ الَّتِي أَخْرَجَتْكَ أَهْلَكْنَاهُمْ فَلَا نَاصِرَ لَهُمْ﴿١٣﴾
13. Na miji mingapi iliyokuwa yenye nguvu zaidi kuliko mji wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ambao umekutoa? Tuliwaangamiza! Na hawakuwa na wa kuwanusuru.
أَفَمَن كَانَ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّهِ كَمَن زُيِّنَ لَهُ سُوءُ عَمَلِهِ وَاتَّبَعُوا أَهْوَاءَهُم﴿١٤﴾
14. Je, basi aliye kwenye hoja bayana kutoka kwa Rabb wake, ni sawa na ambaye amepambiwa uovu wa ‘amali zake na wakafuata hawaa zao?
مَّثَلُ الْجَنَّةِ الَّتِي وُعِدَ الْمُتَّقُونَ ۖ فِيهَا أَنْهَارٌ مِّن مَّاءٍ غَيْرِ آسِنٍ وَأَنْهَارٌ مِّن لَّبَنٍ لَّمْ يَتَغَيَّرْ طَعْمُهُ وَأَنْهَارٌ مِّنْ خَمْرٍ لَّذَّةٍ لِّلشَّارِبِينَ وَأَنْهَارٌ مِّنْ عَسَلٍ مُّصَفًّى ۖ وَلَهُمْ فِيهَا مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ وَمَغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ ۖ كَمَنْ هُوَ خَالِدٌ فِي النَّارِ وَسُقُوا مَاءً حَمِيمًا فَقَطَّعَ أَمْعَاءَهُمْ﴿١٥﴾
15. Mfano wa Jannah ambayo wameahidiwa wenye taqwa; humo mna mito ya maji yasiyovunda, na mito ya maziwa isiyotaghayari ladha yake, na mito ya mvinyo yenye burudisho kwa wanywaji, na mito ya asali iliyosafishwa. Tena watapata humo kila aina ya matunda, na pia Maghfirah kutoka kwa Rabb wao. (Je hao) ni kama yule mwenye kudumu motoni? Na watanyweshwa maji yachemkayo yakatekate machango yao?
وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُ إِلَيْكَ حَتَّىٰ إِذَا خَرَجُوا مِنْ عِندِكَ قَالُوا لِلَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ مَاذَا قَالَ آنِفًا ۚ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ طَبَعَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَاتَّبَعُوا أَهْوَاءَهُمْ﴿١٦﴾
16. Na wapo miongoni mwao ambao wanakusikiliza kwa makini, mpaka wanapotoka kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) huwaambia wale waliopewa ilimu: Amesema nini sasa hivi? Hao ndio ambao Allaah Amepiga chapa juu ya nyoyo zao, na wakafuata hawaa zao.
وَالَّذِينَ اهْتَدَوْا زَادَهُمْ هُدًى وَآتَاهُمْ تَقْوَاهُمْ﴿١٧﴾
17. Na wale waliohidika, Anawazidishia Hidaya na Huwajaza taqwa yao.
فَهَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا السَّاعَةَ أَن تَأْتِيَهُم بَغْتَةً ۖ فَقَدْ جَاءَ أَشْرَاطُهَا ۚ فَأَنَّىٰ لَهُمْ إِذَا جَاءَتْهُمْ ذِكْرَاهُمْ﴿١٨﴾
18. Je, basi wanangojea nini isipokuwa Saa iwafikie ghafla? Na kwa yakini zimekwishakuja ishara zake (Qiyamaah). Basi kutawafaa nini kukumbuka kwao itakapowajia (hiyo Saa)?[2]
فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مُتَقَلَّبَكُمْ وَمَثْوَاكُمْ﴿١٩﴾
19. Basi jua kwamba: hapana muabudiwa wa haki ila Allaah, na omba Maghfirah kwa dhambi zako na kwa ajili ya Waumini wa kiume na Waumini wa kike. Na Allaah Anajua harakati zenu huku na kule na pahala penu pa kupumzikia.
وَيَقُولُ الَّذِينَ آمَنُوا لَوْلَا نُزِّلَتْ سُورَةٌ ۖ فَإِذَا أُنزِلَتْ سُورَةٌ مُّحْكَمَةٌ وَذُكِرَ فِيهَا الْقِتَالُ ۙ رَأَيْتَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ يَنظُرُونَ إِلَيْكَ نَظَرَ الْمَغْشِيِّ عَلَيْهِ مِنَ الْمَوْتِ ۖ فَأَوْلَىٰ لَهُمْ﴿٢٠﴾
20. Na wanasema wale walioamini: Kwa nini isiteremshwe Suwrah? Inapoteremshwa Suwrah iliyo wazi na ikatajwa humo kupigana vita, utawaona wale ambao katika nyoyo zao mna maradhi[3] wanakutazama mtazamo wa mwenye kughumiwa na mauti. Basi ni awla kwao (kumtii Allaah).
طَاعَةٌ وَقَوْلٌ مَّعْرُوفٌ ۚ فَإِذَا عَزَمَ الْأَمْرُ فَلَوْ صَدَقُوا اللَّـهَ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ﴿٢١﴾
21. Utiifu na kauli njema. Na likiazimiwa jambo (la kupigana), basi kama wangekuwa wakweli kwa Allaah, bila shaka ingalikuwa kheri kwao.
فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِن تَوَلَّيْتُمْ أَن تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ﴿٢٢﴾
22. Basi lipi zaidi litarajiwalo kwenu mkigeuka isipokuwa kufanya ufisadi katika ardhi na kuwakata jamaa zenu wa damu?[4]
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَىٰ أَبْصَارَهُمْ﴿٢٣﴾
23. Hao ndio ambao Allaah Amewalaani, Akawafanya viziwi na Akawapofua macho yao.
أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ أَمْ عَلَىٰ قُلُوبٍ أَقْفَالُهَا﴿٢٤﴾
24. Je, hawaizingatii Qur-aan! Au nyoyoni (mwao) mna kufuli?
إِنَّ الَّذِينَ ارْتَدُّوا عَلَىٰ أَدْبَارِهِم مِّن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ الْهُدَى ۙ الشَّيْطَانُ سَوَّلَ لَهُمْ وَأَمْلَىٰ لَهُمْ﴿٢٥﴾
25. Hakika wale walioritadi kurudi nyuma baada ya kuwa Hidaya imewabainikia, hao shaytwaan amewarubuni na akawarefushia matumaini ya uongo.
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لِلَّذِينَ كَرِهُوا مَا نَزَّلَ اللَّـهُ سَنُطِيعُكُمْ فِي بَعْضِ الْأَمْرِ ۖ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ إِسْرَارَهُمْ﴿٢٦﴾
26. Hivyo ni kwa sababu wao wamewaambia wale waliokirihika na yale Aliyoyateremsha Allaah: Tutakutiini katika baadhi ya mambo. Na Allaah Anajua siri zao.
فَكَيْفَ إِذَا تَوَفَّتْهُمُ الْمَلَائِكَةُ يَضْرِبُونَ وُجُوهَهُمْ وَأَدْبَارَهُمْ﴿٢٧﴾
27. Basi itakuwa vipi pale Malaika watakapowafisha wakiwapiga nyuso zao na migongo yao?
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ اتَّبَعُوا مَا أَسْخَطَ اللَّـهَ وَكَرِهُوا رِضْوَانَهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ﴿٢٨﴾
28. Hivyo ni kwa sababu wao wamefuata yaliyomghadhibisha Allaah, na wakachukia yanayomfurahisha, basi Akaziporomosha ‘amali zao.
أَمْ حَسِبَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ أَن لَّن يُخْرِجَ اللَّـهُ أَضْغَانَهُمْ﴿٢٩﴾
29. Je, wanadhania wale ambao nyoyoni mwao mna maradhi[5] kwamba Allaah Hatafichua kamwe vinyongo vyao vya chuki na niya mbaya?
وَلَوْ نَشَاءُ لَأَرَيْنَاكَهُمْ فَلَعَرَفْتَهُم بِسِيمَاهُمْ ۚ وَلَتَعْرِفَنَّهُمْ فِي لَحْنِ الْقَوْلِ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ أَعْمَالَكُمْ﴿٣٠﴾
30. Na lau Tungelitaka, Tungelikuonyesha hao, ukawatambua kwa alama zao dhahiri. Na bila shaka utawatambua kwa kwa jinsi wanavyoyafumbia maneno (yao). Na Allaah Anajua ‘amali zenu.
وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ حَتَّىٰ نَعْلَمَ الْمُجَاهِدِينَ مِنكُمْ وَالصَّابِرِينَ وَنَبْلُوَ أَخْبَارَكُمْ﴿٣١﴾
31. Na bila shaka Tutakujaribuni mpaka Tuwadhihirishe wenye kufanya Jihaad miongoni mwenu na wenye kuvuta subira, na Tutazibainisha khabari zenu.
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَشَاقُّوا الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ الْهُدَىٰ لَن يَضُرُّوا اللَّـهَ شَيْئًا وَسَيُحْبِطُ أَعْمَالَهُمْ﴿٣٢﴾
32. Hakika wale waliokufuru na wakazuia Njia ya Allaah, na wakampinga kwa uadui Rasuli baada ya kuwabainikia Hidaya hawatoweza kumdhuru Allaah kwa chochote, na Ataziporomosha ‘amali zao.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَلَا تُبْطِلُوا أَعْمَالَكُمْ﴿٣٣﴾
33. Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Rasuli, na wala msitengue ‘amali zenu.
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ثُمَّ مَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَن يَغْفِرَ اللَّـهُ لَهُمْ﴿٣٤﴾
34. Hakika wale waliokufuru na wakazuia Njia ya Allaah, kisha wakafa hali ya kuwa ni makafiri, Allaah Hatowaghufuria kamwe.
فَلَا تَهِنُوا وَتَدْعُوا إِلَى السَّلْمِ وَأَنتُمُ الْأَعْلَوْنَ وَاللَّـهُ مَعَكُمْ وَلَن يَتِرَكُمْ أَعْمَالَكُمْ﴿٣٥﴾
35. Basi msinyong’onyee mkataka suluhu, kwani nyinyi ndio mko juu. Na Allaah Yu pamoja nanyi, na Hatawapunguzieni (thawabu za) ‘amali zenu.
إِنَّمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا لَعِبٌ وَلَهْوٌ ۚ وَإِن تُؤْمِنُوا وَتَتَّقُوا يُؤْتِكُمْ أُجُورَكُمْ وَلَا يَسْأَلْكُمْ أَمْوَالَكُمْ﴿٣٦﴾
36. Hakika uhai wa dunia ni mchezo na pumbao. Lakini mkiamini na mkawa na taqwa, (Allaah) Atakupeni ujira wenu na wala Hatokutakeni mtoe mali zenu.
إِن يَسْأَلْكُمُوهَا فَيُحْفِكُمْ تَبْخَلُوا وَيُخْرِجْ أَضْغَانَكُمْ﴿٣٧﴾
37. Akikutakeni hayo Akakukazanieni mtafanya ubakhili, na Atatoa vinyongo vyenu vya kukirihika na niyyah mbaya.
هَا أَنتُمْ هَـٰؤُلَاءِ تُدْعَوْنَ لِتُنفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَمِنكُم مَّن يَبْخَلُ ۖ وَمَن يَبْخَلْ فَإِنَّمَا يَبْخَلُ عَن نَّفْسِهِ ۚ وَاللَّـهُ الْغَنِيُّ وَأَنتُمُ الْفُقَرَاءُ ۚ وَإِن تَتَوَلَّوْا يَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُونُوا أَمْثَالَكُم﴿٣٨﴾
38. Ha! Nyinyi ndio hawa mnaoitwa ili mtoe katika Njia ya Allaah. Basi yuko miongoni mwenu ambaye anafanya ubakhili, na afanyaye ubakhili, basi hakika hapana ila anafanya ubakhili dhidi ya nafsi yake. Na Allaah Ni Mkwasi, nanyi ni mafakiri. Na mkikengeuka Atabadilisha watu ghairi yenu kisha hawatokuwa mfano wenu.[6]
