049 - Al-Hujuraat
الْحُجُرَات
Al-Hujuraat: 049
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيِ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿١﴾
1. Enyi walioamini! Msikadimishe (lolote) mbele ya Allaah na Rasuli Wake. Na mcheni Allaah, hakika Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَرْفَعُوا أَصْوَاتَكُمْ فَوْقَ صَوْتِ النَّبِيِّ وَلَا تَجْهَرُوا لَهُ بِالْقَوْلِ كَجَهْرِ بَعْضِكُمْ لِبَعْضٍ أَن تَحْبَطَ أَعْمَالُكُمْ وَأَنتُمْ لَا تَشْعُرُونَ﴿٢﴾
2 Enyi walioamini! Msipandishe sauti zenu juu ya sauti ya Nabiy, na wala msiseme naye kwa sauti ya juu, kama mnavyosemezana wenyewe kwa wenyewe kwa sauti za juu, zisije zikaporomoka ‘amali zenu nanyi hamhisi.
إِنَّ الَّذِينَ يَغُضُّونَ أَصْوَاتَهُمْ عِندَ رَسُولِ اللَّـهِ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ امْتَحَنَ اللَّـهُ قُلُوبَهُمْ لِلتَّقْوَىٰ ۚ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ عَظِيمٌ﴿٣﴾
3. Hakika wale wanaoteremsha sauti zao mbele ya Rasuli wa Allaah, hao ndio ambao Allaah Amezichuja nyoyo zao kwa ajili ya taqwa. Watapata maghfirah na ujira adhimu.
إِنَّ الَّذِينَ يُنَادُونَكَ مِن وَرَاءِ الْحُجُرَاتِ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ﴿٤﴾
4. Hakika wale wanaokuita (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) nyuma ya vyumba, wengi wao hawatii akilini.
وَلَوْ أَنَّهُمْ صَبَرُوا حَتَّىٰ تَخْرُجَ إِلَيْهِمْ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٥﴾
5. Na lau kwamba wao wangelisubiri mpaka ukawatokea, bila shaka ingelikuwa ni kheri zaidi kwao. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَن تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَىٰ مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ﴿٦﴾
6. Enyi walioamini! Anapokujieni fasiki kwa habari yoyote, basi pelelezeni, msije mkawadhuru watu kwa ujahili, mkawa kuwa wenye kujuta juu ya ambayo mmeyafanya.
وَاعْلَمُوا أَنَّ فِيكُمْ رَسُولَ اللَّـهِ ۚ لَوْ يُطِيعُكُمْ فِي كَثِيرٍ مِّنَ الْأَمْرِ لَعَنِتُّمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ حَبَّبَ إِلَيْكُمُ الْإِيمَانَ وَزَيَّنَهُ فِي قُلُوبِكُمْ وَكَرَّهَ إِلَيْكُمُ الْكُفْرَ وَالْفُسُوقَ وَالْعِصْيَانَ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الرَّاشِدُونَ﴿٧﴾
7. Na jueni kwamba pamoja nanyi yuko Rasuli wa Allaah. Lau kama atakutiini katika mambo mengi bila shaka mngelitaabika, lakini Allaah Amekupendezesheeni Iymaan, na Akaipamba katika nyoyo zenu, na Akakuchukizisheni kufuru, na ufasiki na maasi. Hao ndio walioongoka sawasawa.
فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَنِعْمَةً ۚ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿٨﴾
8. Ni Fadhila kutoka kwa Allaah na Neema. Na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
وَإِن طَائِفَتَانِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ اقْتَتَلُوا فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا ۖ فَإِن بَغَتْ إِحْدَاهُمَا عَلَى الْأُخْرَىٰ فَقَاتِلُوا الَّتِي تَبْغِي حَتَّىٰ تَفِيءَ إِلَىٰ أَمْرِ اللَّـهِ ۚ فَإِن فَاءَتْ فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا بِالْعَدْلِ وَأَقْسِطُوا ۖ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ﴿٩﴾
9. Na ikiwa makundi mawili ya Waumini yatapigana, basi suluhisheni baina yao. Lakini mojawapo likikandamiza jengine, basi piganeni na ambalo linakandamiza mpaka lielemee kwenye Amri ya Allaah. Likishaelemea, basi suluhisheni baina yao kwa uadilifu, na tendeni haki. Hakika Allaah Anapenda wenye kutenda haki.
إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ﴿١٠﴾
10. Hakika Waumini ni ndugu, basi suluhisheni baina ya ndugu zenu. Na mcheni Allaah ili mpate kurehemewa.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَسْخَرْ قَوْمٌ مِّن قَوْمٍ عَسَىٰ أَن يَكُونُوا خَيْرًا مِّنْهُمْ وَلَا نِسَاءٌ مِّن نِّسَاءٍ عَسَىٰ أَن يَكُنَّ خَيْرًا مِّنْهُنَّ ۖ وَلَا تَلْمِزُوا أَنفُسَكُمْ وَلَا تَنَابَزُوا بِالْأَلْقَابِ ۖ بِئْسَ الِاسْمُ الْفُسُوقُ بَعْدَ الْإِيمَانِ ۚ وَمَن لَّمْ يَتُبْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ﴿١١﴾
11. Enyi walioamini! Wanaume wasiwafanyie dhihaka na kuwadharau wanaume wengineo asaa wakawa bora kuliko wao, wala wanawake kwa wanawake wengineo, asaa wakawa bora kuliko wao. Na wala msifedheheshane kwa kutukanana, na wala msiitane majina (mabaya) ya utani. Ubaya ulioje kuita jina la ufasiki baada ya Iymaan! Na yeyote asiyetubu, basi hao ndio madhalimu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اجْتَنِبُوا كَثِيرًا مِّنَ الظَّنِّ إِنَّ بَعْضَ الظَّنِّ إِثْمٌ ۖ وَلَا تَجَسَّسُوا وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا ۚ أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَن يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا فَكَرِهْتُمُوهُ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ تَوَّابٌ رَّحِيمٌ﴿١٢﴾
12. Enyi walioamini! Jiepusheni sana na dhana, kwani hakika baadhi ya dhana ni dhambi. Na wala msichunguzane, na wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je, anapenda mmoja wenu kwamba ale nyama ya nduguye aliyekufa? Basi mmelichukia hilo! Na mcheni Allaah! Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu.
يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَىٰ وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا ۚ إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّـهِ أَتْقَاكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ﴿١٣﴾
13. Enyi watu! Hakika Sisi Tumekuumbeni kutokana na mwanamme na mwanamke, na Tukakufanyeni mataifa na makabila ili mtambuane. Hakika aliye na hadhi zaidi miongoni mwenu mbele ya Allaah ni mwenye taqwa zaidi kati yenu. Hakika Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Khabari za dhahiri na siri.
قَالَتِ الْأَعْرَابُ آمَنَّا ۖ قُل لَّمْ تُؤْمِنُوا وَلَـٰكِن قُولُوا أَسْلَمْنَا وَلَمَّا يَدْخُلِ الْإِيمَانُ فِي قُلُوبِكُمْ ۖ وَإِن تُطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ لَا يَلِتْكُم مِّنْ أَعْمَالِكُمْ شَيْئًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١٤﴾
14. Mabedui walisema: Tumeamini! Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hamkuamini, lakini semeni: Tumesilimu. Kwani Iymaan haijaingia bado nyoyoni mwenu. Na mtakapomtii Allaah na Rasuli Wake, Hatokupunguzieni katika ‘amali zenu kitu chochote. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ لَمْ يَرْتَابُوا وَجَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ﴿١٥﴾
15. Hakika Waumini ni wale waliomwamini Allaah na Rasuli Wake, kisha wakawa si wenye shaka, na wakafanya Jihaad kwa mali zao na nafsi zao katika Njia ya Allaah. Hao ndio wakweli.
قُلْ أَتُعَلِّمُونَ اللَّـهَ بِدِينِكُمْ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ﴿١٦﴾
16. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Je, ati ndio mnamjulisha Allaah kuhusu Dini yenu, na hali Allaah Anajua yale yaliyomo mbinguni na yale yaliyomo ardhini? Na Allaah Ni Mjuzi wa kila kitu.
يَمُنُّونَ عَلَيْكَ أَنْ أَسْلَمُوا ۖ قُل لَّا تَمُنُّوا عَلَيَّ إِسْلَامَكُم ۖ بَلِ اللَّـهُ يَمُنُّ عَلَيْكُمْ أَنْ هَدَاكُمْ لِلْإِيمَانِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿١٧﴾
17. Wanadhani wamekufanyia fadhila kwamba wamesilimu? Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Msidhani mmenifanyia fadhila kusilimu kwenu. Bali Allaah Amekufanyieni Fadhila kwamba Amekuongozeni kwenye Iymaan mkiwa ni wakweli.
إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ غَيْبَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ﴿١٨﴾
18. Hakika Allaah Anajua ghaibu ya mbingu na ardhi, na Allaah ni Mwenye Kkuona myatendayo.
