069 - Al-Haaqah
الْحآقَّة
Al-Haaqah: 069
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الْحَاقَّةُ﴿١﴾
1. Tukio la haki lisiloepukika!
مَا الْحَاقَّةُ﴿٢﴾
2. Ni nini tukio la haki lisiloepukika?
وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْحَاقَّةُ﴿٣﴾
3. Na nini kitakachokujulisha nini tukio la haki lisiloepukika?
كَذَّبَتْ ثَمُودُ وَعَادٌ بِالْقَارِعَةِ﴿٤﴾
4. Kina Thamuwd na ‘Aad walikadhibisha tukio lenye kugongagonga na kutia kiwewe nyoyo.
فَأَمَّا ثَمُودُ فَأُهْلِكُوا بِالطَّاغِيَةِ﴿٥﴾
5. Ama kina Thamuwd, wao waliangamizwa kwa ukelele mkali uliovuka mipaka.
وَأَمَّا عَادٌ فَأُهْلِكُوا بِرِيحٍ صَرْصَرٍ عَاتِيَةٍ﴿٦﴾
6. Na ama kina ‘Aad, hao waliangamizwa kwa upepo mbaya wa sauti na baridi kali, uvumao kwa nguvu.
سَخَّرَهَا عَلَيْهِمْ سَبْعَ لَيَالٍ وَثَمَانِيَةَ أَيَّامٍ حُسُومًا فَتَرَى الْقَوْمَ فِيهَا صَرْعَىٰ كَأَنَّهُمْ أَعْجَازُ نَخْلٍ خَاوِيَةٍ﴿٧﴾
7. Aliwalazimishia nyusiku saba na michana minane mfululizo, basi utaona watu humo wameanguka chini kama kwamba ni magogo ya mitende iliyo mitupu.
فَهَلْ تَرَىٰ لَهُم مِّن بَاقِيَةٍ﴿٨﴾
8. Basi je, unaona mabakio yao yoyote?
وَجَاءَ فِرْعَوْنُ وَمَن قَبْلَهُ وَالْمُؤْتَفِكَاتُ بِالْخَاطِئَةِ﴿٩﴾
9. Na akaja Firawni na wale walio kabla yake, na (watu wa) miji iliyopinduliwa chini juu kwa sababu ya hatia zao.
فَعَصَوْا رَسُولَ رَبِّهِمْ فَأَخَذَهُمْ أَخْذَةً رَّابِيَةً﴿١٠﴾
10. Basi wakamuasi Rasuli wa Rabb wao, Akawachukua mchukuo uliopindukia ukali.
إِنَّا لَمَّا طَغَى الْمَاءُ حَمَلْنَاكُمْ فِي الْجَارِيَةِ﴿١١﴾
11. Hakika Sisi, pale maji yalipopinduka mipaka, Tulikubebeni katika merikebu.
لِنَجْعَلَهَا لَكُمْ تَذْكِرَةً وَتَعِيَهَا أُذُنٌ وَاعِيَةٌ﴿١٢﴾
12. Ili Tuifanye kuwa ni ukumbusho kwenu, na ibakie kumbukumbu katika sikio linalobakisha kumbukumbu.
فَإِذَا نُفِخَ فِي الصُّورِ نَفْخَةٌ وَاحِدَةٌ﴿١٣﴾
13. Basi litakapopulizwa baragumu mpulizo mmoja.
وَحُمِلَتِ الْأَرْضُ وَالْجِبَالُ فَدُكَّتَا دَكَّةً وَاحِدَةً﴿١٤﴾
14. Na ardhi na milima ikaondolewa kisha ikapondwa mpondo mmoja.
فَيَوْمَئِذٍ وَقَعَتِ الْوَاقِعَةُ﴿١٥﴾
15. Basi siku hiyo ndio litatokea tukio la kutokea.
وَانشَقَّتِ السَّمَاءُ فَهِيَ يَوْمَئِذٍ وَاهِيَةٌ﴿١٦﴾
16. Na mbingu zitararuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu sana.
وَالْمَلَكُ عَلَىٰ أَرْجَائِهَا ۚ وَيَحْمِلُ عَرْشَ رَبِّكَ فَوْقَهُمْ يَوْمَئِذٍ ثَمَانِيَةٌ﴿١٧﴾
17. Na Malaika watakuwa pembezoni mwake, na watabeba ‘Arsh ya Rabb wako juu yao siku hiyo (Malaika) wanane.
يَوْمَئِذٍ تُعْرَضُونَ لَا تَخْفَىٰ مِنكُمْ خَافِيَةٌ﴿١٨﴾
18. Siku hiyo mtahudhurishwa, halitofichika tendo lenu lolote la siri.
فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ فَيَقُولُ هَاؤُمُ اقْرَءُوا كِتَابِيَهْ﴿١٩﴾
19. Basi ama yule atakayepewa kitabu chake kuliani mwake, atasema: Hebu chukueni someni kitabu changu!
إِنِّي ظَنَنتُ أَنِّي مُلَاقٍ حِسَابِيَهْ﴿٢٠﴾
20. Hakika mimi niliyakinisha kuwa hakiki mimi ni mwenye kukutana na hesabu yangu!
فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ﴿٢١﴾
21. Basi yeye atakuwa katika maisha ya kuridhisha.
فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٍ﴿٢٢﴾
22. Kwenye Jannah ya juu.
قُطُوفُهَا دَانِيَةٌ﴿٢٣﴾
23. Matunda yake ya kuchumwa yako karibu.
كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا أَسْلَفْتُمْ فِي الْأَيَّامِ الْخَالِيَةِ﴿٢٤﴾
24. (Wataambiwa): Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyoyatanguliza katika siku nyingi zilizopita.
وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِشِمَالِهِ فَيَقُولُ يَا لَيْتَنِي لَمْ أُوتَ كِتَابِيَهْ﴿٢٥﴾
25. Na ama yule atakayepewa kitabu chake kushotoni mwake, atasema: Ee! Laiti nisingelipewa kitabu changu!
وَلَمْ أَدْرِ مَا حِسَابِيَهْ﴿٢٦﴾
26. Na wala nisingelijua hesabu yangu!
يَا لَيْتَهَا كَانَتِ الْقَاضِيَةَ﴿٢٧﴾
27. Ee! Laiti yangelikuwa (mauti) ndio kumalizika kwangu.
مَا أَغْنَىٰ عَنِّي مَالِيَهْ ۜ﴿٢٨﴾
28. Haikunifaa mali yangu.
هَلَكَ عَنِّي سُلْطَانِيَهْ﴿٢٩﴾
29. Madaraka yangu yamenitoweka.
خُذُوهُ فَغُلُّوهُ﴿٣٠﴾
30. (Patasemwa): Mchukueni, na mfungeni pingu.
ثُمَّ الْجَحِيمَ صَلُّوهُ﴿٣١﴾
31. Kisha kwenye moto uwakao vikali mno muingizeni aungue.
ثُمَّ فِي سِلْسِلَةٍ ذَرْعُهَا سَبْعُونَ ذِرَاعًا فَاسْلُكُوهُ﴿٣٢﴾
32. Kisha mtieni pingu katika minyororo yenye urefu wa dhiraa sabini.
إِنَّهُ كَانَ لَا يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ الْعَظِيمِ﴿٣٣﴾
33. Hakika yeye alikuwa hamuamini Allaah Mwenye Taadhima.
وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ الْمِسْكِينِ﴿٣٤﴾
34. Na wala hahamasishi kulisha masikini.
فَلَيْسَ لَهُ الْيَوْمَ هَاهُنَا حَمِيمٌ﴿٣٥﴾
35. Basi leo hapa hatokuwa na rafiki wa dhati.
وَلَا طَعَامٌ إِلَّا مِنْ غِسْلِينٍ﴿٣٦﴾
36. Wala chakula isipokuwa usaha (wa walio motoni).
لَّا يَأْكُلُهُ إِلَّا الْخَاطِئُونَ﴿٣٧﴾
37. Hawakili chakula hicho isipokuwa wenye hatia.
فَلَا أُقْسِمُ بِمَا تُبْصِرُونَ﴿٣٨﴾
38. Basi Naapa kwa yale mnayoyaona.
وَمَا لَا تُبْصِرُونَ﴿٣٩﴾
39. Na kwa yale msiyoyaona.
إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ﴿٤٠﴾
40. Hakika hii (Qur-aan) bila shaka ni kauli ya Rasuli Mtukufu.
وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَاعِرٍ ۚ قَلِيلًا مَّا تُؤْمِنُونَ﴿٤١﴾
41. Na si kauli ya mshairi. Ni machache sana yale mnayoamini.
وَلَا بِقَوْلِ كَاهِنٍ ۚ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ﴿٤٢﴾
42. Na wala si kauli ya kahini. Ni machache sana yale mnayokumbuka.
تَنزِيلٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ﴿٤٣﴾
43. Ni uteremsho kutoka kwa Rabb wa walimwengu.
وَلَوْ تَقَوَّلَ عَلَيْنَا بَعْضَ الْأَقَاوِيلِ﴿٤٤﴾
44. Na lau kama (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) angetutungia baadhi ya kauli.
لَأَخَذْنَا مِنْهُ بِالْيَمِينِ﴿٤٥﴾
45. Bila shaka Tungelimchukua kwa Mkono wa kuume.
ثُمَّ لَقَطَعْنَا مِنْهُ الْوَتِينَ﴿٤٦﴾
46. Kisha bila shaka Tungelimkata mshipa mkubwa wa moyo wa uhai.
فَمَا مِنكُم مِّنْ أَحَدٍ عَنْهُ حَاجِزِينَ﴿٤٧﴾
47. Basi hakuna mmoja yeyote kati yenu angeliweza kutuzuia naye.
وَإِنَّهُ لَتَذْكِرَةٌ لِّلْمُتَّقِينَ﴿٤٨﴾
48. Na hakika hii (Qur-aan) bila shaka ni ukumbusho kwa wenye taqwa.
وَإِنَّا لَنَعْلَمُ أَنَّ مِنكُم مُّكَذِّبِينَ﴿٤٩﴾
49. Na hakika Sisi bila shaka Tunajua kwamba miongoni mwenu wako wenye kukadhibisha.
وَإِنَّهُ لَحَسْرَةٌ عَلَى الْكَافِرِينَ﴿٥٠﴾
50. Na hakika hii (Qur-aan) bila shaka itakuwa ni majuto makubwa juu ya makafiri.
وَإِنَّهُ لَحَقُّ الْيَقِينِ﴿٥١﴾
51. Na hakika hii (Qur-aan) ni haki ya yakini.
فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ﴿٥٢﴾
52. Basi sabbih kwa Jina la Rabb wako Adhimu.
