070 - Al-Ma'aarij

 

 

 

  الْمَعَارِج

Al-Ma’aarij: 070

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

سَأَلَ سَائِلٌ بِعَذَابٍ وَاقِعٍ﴿١﴾

1. Muulizaji ameuliza kuhusu adhabu itakayotokea.

 

 

لِّلْكَافِرِينَ لَيْسَ لَهُ دَافِعٌ﴿٢﴾

2. Kwa makafiri, ambayo hakuna wa kuikinga.

 

 

مِّنَ اللَّـهِ ذِي الْمَعَارِجِ﴿٣﴾

3. Kutoka kwa Allaah Mwenye Kumiliki njia za kupandia.

 

 

تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ﴿٤﴾

4. Malaika na Ar-Ruwh (roho za viumbe au Jibriyl) wanapanda Kwake katika siku kadiri yake ni miaka khamsini elfu.

 

 

فَاصْبِرْ صَبْرًا جَمِيلًا﴿٥﴾

5. Basi subiri, subira njema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).

 

 

إِنَّهُمْ يَرَوْنَهُ بَعِيدًا﴿٦﴾

6. Hakika wao wanaiona (adhabu, Qiyaamah) iko mbali.

 

 

وَنَرَاهُ قَرِيبًا﴿٧﴾

7. Nasi Tunaiona  ikaribu.

 

 

يَوْمَ تَكُونُ السَّمَاءُ كَالْمُهْلِ﴿٨﴾

8. Siku mbingu itakapokuwa kama masazo ya zebaki nyeusi iliyoyeyushwa.

 

 

وَتَكُونُ الْجِبَالُ كَالْعِهْنِ﴿٩﴾

9. Na milima itakuwa kama sufi iliyochambuliwa.

 

 

وَلَا يَسْأَلُ حَمِيمٌ حَمِيمًا﴿١٠﴾

10.  Na wala rafiki wadhati hatomuuliza rafiki yake wa dhati. 

 

 

يُبَصَّرُونَهُمْ ۚ يَوَدُّ الْمُجْرِمُ لَوْ يَفْتَدِي مِنْ عَذَابِ يَوْمِئِذٍ بِبَنِيهِ﴿١١﴾

11. Watafanywa waonane. Mhalifu atatamani ajitolee fidia kutokana na adhabu ya Siku hiyo kwa watoto wake.

 

 

وَصَاحِبَتِهِ وَأَخِيهِ﴿١٢﴾

12. Na mkewe na nduguye.

 

 

وَفَصِيلَتِهِ الَّتِي تُؤْوِيهِ﴿١٣﴾

13. Na jamaa zake wa karibu ambao wanampa hifadhi na makazi.

 

 

وَمَن فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ يُنجِيهِ﴿١٤﴾

14. Na wale wote waliomo ardhini, kisha aokoke yeye.

 

 

كَلَّا ۖ إِنَّهَا لَظَىٰ﴿١٥﴾

15. Laa hasha! Hakika huo ni moto wenye mwako mkali.

 

 

نَزَّاعَةً لِّلشَّوَىٰ﴿١٦﴾

16. Unyofoao kwa nguvu na kuunguza kikamilifu ngozi ya kichwa na viungo vya mwili.

 

 

تَدْعُو مَنْ أَدْبَرَ وَتَوَلَّىٰ﴿١٧﴾

17. Utamwita yule aliyegeuza mgongo na akakengeuka.

 

 

وَجَمَعَ فَأَوْعَىٰ﴿١٨﴾

18. Na akakusanya (mali) kisha akayahifadhi katika makasha.

 

 

إِنَّ الْإِنسَانَ خُلِقَ هَلُوعًا﴿١٩﴾

19. Hakika binaadamu ameumbwa kuwa ni mwenye kukosa subira na mwingi wa pupa.

 

 

إِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ جَزُوعًا﴿٢٠﴾

20. Inapomgusa shari, anakuwa mwingi wa kusononeka, kupapatika na kuhuzunika.

 

وَإِذَا مَسَّهُ الْخَيْرُ مَنُوعًا﴿٢١﴾

21. Na inapomgusa kheri, anakuwa mwingi wa kuzuia (kwa uchoyo).

 

 

إِلَّا الْمُصَلِّينَ﴿٢٢﴾

22. Isipokuwa wenye kuswali.

 

 

الَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ دَائِمُونَ﴿٢٣﴾

23. Ambao wao katika Swalaah zao ni wenye kudumu.

 

 

وَالَّذِينَ فِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ مَّعْلُومٌ﴿٢٤﴾

24. Na ambao katika mali zao kuna haki maalumu.

 

 

لِّلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ﴿٢٥﴾

25. Kwa ajili ya muombaji na asiyeomba kwa kujistahi.

 

 

وَالَّذِينَ يُصَدِّقُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ﴿٢٦﴾

26. Na ambao wanasadikisha Siku ya Malipo.

 

 

وَالَّذِينَ هُم مِّنْ عَذَابِ رَبِّهِم مُّشْفِقُونَ﴿٢٧﴾

27. Na wale wanaoiogopa adhabu kutoka kwa Rabb wao.

 

 

إِنَّ عَذَابَ رَبِّهِمْ غَيْرُ مَأْمُونٍ﴿٢٨﴾

28. Hakika adhabu ya Rabb wao haina muamana kwa yeyote.

 

 

وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ﴿٢٩﴾

29. Na ambao wanahifadhi tupu zao.

 

 

إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ﴿٣٠﴾

30. Isipokuwa kwa wake zao, au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao si wenye kulaumiwa.

 

 

فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ﴿٣١﴾

31. Basi yeyote yule atakayetaka kinyume ya hayo, basi hao ndio warukao mipaka.

 

 

وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ﴿٣٢﴾

32. Na ambao amana zao na ahadi zao wanazichunga (na kuzitimiza).

 

 

وَالَّذِينَ هُم بِشَهَادَاتِهِمْ قَائِمُونَ﴿٣٣﴾

33. Na ambao wanatoa ushahidi wa haki na kweli.

 

 

وَالَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ﴿٣٤﴾

34. Na ambao Swalaah zao wao wanazihifadhi.

 

 

أُولَـٰئِكَ فِي جَنَّاتٍ مُّكْرَمُونَ﴿٣٥﴾

35. Hao watakuwa kwenye Jannah wakikirimiwa.

 

 

فَمَالِ الَّذِينَ كَفَرُوا قِبَلَكَ مُهْطِعِينَ﴿٣٦﴾

36. Basi wana nini waliokufuru wanaharakiza mbele yako wakinyosha shingo zao na kukukodolea macho (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)?

 

 

عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ عِزِينَ﴿٣٧﴾

37. (Kukukalia) makundi kwa makundi kuliani na kushotoni.

 

 

أَيَطْمَعُ كُلُّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُدْخَلَ جَنَّةَ نَعِيمٍ﴿٣٨﴾

38. Je, anatumai kila mtu miongoni mwao kwamba ataingizwa Jannah ya neema?

 

 

 

كَلَّا ۖ إِنَّا خَلَقْنَاهُم مِّمَّا يَعْلَمُونَ﴿٣٩﴾

39. Laa, hasha!  Hakika Sisi Tumewaumba kutokana na kile wanachokijua.

 

 

فَلَا أُقْسِمُ بِرَبِّ الْمَشَارِقِ وَالْمَغَارِبِ إِنَّا لَقَادِرُونَ﴿٤٠﴾

40. Basi Naapa kwa Rabb wa Mashariki na Magharibi, hakika Sisi bila shaka Ni Wenye uwezo.

 

 

عَلَىٰ أَن نُّبَدِّلَ خَيْرًا مِّنْهُمْ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ﴿٤١﴾

41. Wa kwamba Tuwabadili walio bora kuliko wao, Nasi Hatushindwi.

 

 

فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا وَيَلْعَبُوا حَتَّىٰ يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي يُوعَدُونَ﴿٤٢﴾

42. Basi waachilie mbali watumbukie katika porojo na upuuzi na wacheze, mpaka wakutane na Siku yao ambayo wanaahidiwa.

 

 

يَوْمَ يَخْرُجُونَ مِنَ الْأَجْدَاثِ سِرَاعًا كَأَنَّهُمْ إِلَىٰ نُصُبٍ يُوفِضُونَ﴿٤٣﴾

43. Siku watapotoka makaburini haraka haraka kama kwamba wanakimbilia viabudiwa vyao.

 

 

خَاشِعَةً أَبْصَارُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۚ ذَٰلِكَ الْيَوْمُ الَّذِي كَانُوا يُوعَدُونَ﴿٤٤﴾

44. Macho yao yatainama chini, udhalilifu utawafunika. Hiyo ndio ile siku waliyokuwa wakiahidiwa.

 

 

Share