071 - Nuwh

 

نُوح

 

071-Nuwh

 

071-Nuwh: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com 

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

 

إِنَّا أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ أَنْ أَنذِرْ قَوْمَكَ مِن قَبْلِ أَن يَأْتِيَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿١﴾

1. Hakika Sisi Tumemtuma Nuwh kwa kaumu yake kwamba: Waonye watu wako kabla haijawafikia adhabu iumizayo.[1]

 

 

 

 

قَالَ يَا قَوْمِ إِنِّي لَكُمْ نَذِيرٌ مُّبِينٌ﴿٢﴾

2. (Nuwh) akasema: Enyi kaumu yangu! Hakika mimi kwenu ni mwonyaji aliye bayana.

 

 

 

 

أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاتَّقُوهُ وَأَطِيعُونِ﴿٣﴾

3. Kwamba muabuduni Allaah, na mcheni, na mnitii.

 

 

 

 

 

يَغْفِرْ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُؤَخِّرْكُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ إِنَّ أَجَلَ اللَّـهِ إِذَا جَاءَ لَا يُؤَخَّرُ ۖ لَوْ كُنتُمْ تَعْلَمُونَ﴿٤﴾

4. (Allaah) Atakughufurieni madhambi yenu, na Atakuakhirisheni mpaka muda maalumu uliokadiriwa. Hakika muda uliokadiriwa na Allaah utakapokuja hautoakhirishwa, lau kama mtakuwa mnajua.

 

 

 

 

 

قَالَ رَبِّ إِنِّي دَعَوْتُ قَوْمِي لَيْلًا وَنَهَارًا﴿٥﴾

5. (Nuwh) akasema: Rabb wangu! Hakika mimi nimewalingania watu wangu usiku na mchana.

 

 

 

 

فَلَمْ يَزِدْهُمْ دُعَائِي إِلَّا فِرَارًا﴿٦﴾

6. Lakini wito wangu haukuwazidishia isipokuwa kukimbia. 

 

 

 

 

 

وَإِنِّي كُلَّمَا دَعَوْتُهُمْ لِتَغْفِرَ لَهُمْ جَعَلُوا أَصَابِعَهُمْ فِي آذَانِهِمْ وَاسْتَغْشَوْا ثِيَابَهُمْ وَأَصَرُّوا وَاسْتَكْبَرُوا اسْتِكْبَارًا﴿٧﴾

7. Na hakika mimi kila nilipowaita ili Uwaghufurie, waliweka vidole vyao masikioni mwao, na wakajigubika nguo zao[2], na wakashikilia (kukanusha) na wakatakabari kwa majivuno makubwa.

 

 

 

 

ثُمَّ إِنِّي دَعَوْتُهُمْ جِهَارًا﴿٨﴾

8. Kisha hakika mimi niliwalingania kwa waziwazi.

 

 

 

 

ثُمَّ إِنِّي أَعْلَنتُ لَهُمْ وَأَسْرَرْتُ لَهُمْ إِسْرَارًا﴿٩﴾

9. Kisha hakika mimi niliwatangazia, na nikawasemesha kwa siri sana.

 

 

 

 

فَقُلْتُ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ إِنَّهُ كَانَ غَفَّارًا﴿١٠﴾

10. Nikasema: Ombeni maghfirah kwa Rabb wenu, hakika Yeye Ni Mwingi mno wa Kughufuria.[3]

 

 

 

يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا﴿١١﴾

11. Atakutumieni mvua tele ya kuendelea.

 

 

 

 

وَيُمْدِدْكُم بِأَمْوَالٍ وَبَنِينَ وَيَجْعَل لَّكُمْ جَنَّاتٍ وَيَجْعَل لَّكُمْ أَنْهَارًا﴿١٢﴾

12. Na Atakuongezeeni mali na wana, na Atakupeni mabustani na Atakupeni mito.

 

 

 

مَّا لَكُمْ لَا تَرْجُونَ لِلَّـهِ وَقَارًا﴿١٣﴾

13. Mna nini? Hamtaraji na hamkhofu Taadhima ya Allaah? 

 

 

 

 

وَقَدْ خَلَقَكُمْ أَطْوَارًا﴿١٤﴾

14. Na hali Amekuumbeni hatua baada ya hatua?

 

 

 

 

أَلَمْ تَرَوْا كَيْفَ خَلَقَ اللَّـهُ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ طِبَاقًا﴿١٥﴾

15. Je, hamuoni vipi Allaah Ameumba mbingu saba tabaka tabaka?

 

 

 

 

وَجَعَلَ الْقَمَرَ فِيهِنَّ نُورًا وَجَعَلَ الشَّمْسَ سِرَاجًا﴿١٦﴾

16. Na Akaufanya mwezi ndani yake uwe nuru, na Akalifanya jua ni taa ya mwanga mkali.

 

 

 

وَاللَّـهُ أَنبَتَكُم مِّنَ الْأَرْضِ نَبَاتًا﴿١٧﴾

17. Na Allaah Amekuanzisheni asili yenu kutokana na (udongo wa) ardhi.

 

 

 

ثُمَّ يُعِيدُكُمْ فِيهَا وَيُخْرِجُكُمْ إِخْرَاجًا﴿١٨﴾

18. Kisha Atakurudisheni humo, na Atakutoeni tena mtoke (kuwa hai).

 

 

 

 

وَاللَّـهُ جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ بِسَاطًا﴿١٩﴾

19. Na Allaah Amekufanyieni ardhi kuwa (kama) busati.

 

 

 

لِّتَسْلُكُوا مِنْهَا سُبُلًا فِجَاجًا﴿٢٠﴾

20. Ili mpite humo njia zilizo pana.

 

 

 

 

قَالَ نُوحٌ رَّبِّ إِنَّهُمْ عَصَوْنِي وَاتَّبَعُوا مَن لَّمْ يَزِدْهُ مَالُهُ وَوَلَدُهُ إِلَّا خَسَارًا﴿٢١﴾

21. Nuwh akasema: Rabb wangu! Hakika wao wameniasi, na wakamfuata yule ambaye hayakumzidishia mali yake na watoto wake isipokuwa khasara.

 

 

 

وَمَكَرُوا مَكْرًا كُبَّارًا﴿٢٢﴾

22. Na wakapanga njama kubwa mno.

 

 

 

 

وَقَالُوا لَا تَذَرُنَّ آلِهَتَكُمْ وَلَا تَذَرُنَّ وَدًّا وَلَا سُوَاعًا وَلَا يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسْرًا﴿٢٣﴾

23. Wakasema: Msiwaache katu waabudiwa wenu. Na wala msimwache abadani Waddaa, wala Suwaa’aa, wala Yaghuwtha, na Ya’uwqa, na Nasraa.[4]

 

 

 

وَقَدْ أَضَلُّوا كَثِيرًا ۖ وَلَا تَزِدِ الظَّالِمِينَ إِلَّا ضَلَالًا﴿٢٤﴾

24. Na kwa hakika wamekwishawapoteza wengi. Na wala Usiwazidishie madhalimu isipokuwa upotofu.

 

 

 

مِّمَّا خَطِيئَاتِهِمْ أُغْرِقُوا فَأُدْخِلُوا نَارًا فَلَمْ يَجِدُوا لَهُم مِّن دُونِ اللَّـهِ أَنصَارًا﴿٢٥﴾

25. Kutokana na hatia zao walizamishwa, kisha wakaingizwa motoni. Basi hawakupata wowote wa kuwanusuru badala ya Allaah.

 

 

 

وَقَالَ نُوحٌ رَّبِّ لَا تَذَرْ عَلَى الْأَرْضِ مِنَ الْكَافِرِينَ دَيَّارًا﴿٢٦﴾

26. Na Nuwh akasema tena: Rabb wangu! Usimwache juu ya ardhi mkaazi yeyote yule kati ya makafiri.

 

 

 

إِنَّكَ إِن تَذَرْهُمْ يُضِلُّوا عِبَادَكَ وَلَا يَلِدُوا إِلَّا فَاجِرًا كَفَّارًا﴿٢٧﴾

27. Hakika Wewe Ukiwaacha, watawapoteza Waja Wako, na wala hawatozaa isipokuwa mtendaji dhambi, kafiri mkanushaji mno.

 

 

 

رَّبِّ اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِمَن دَخَلَ بَيْتِيَ مُؤْمِنًا وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَلَا تَزِدِ الظَّالِمِينَ إِلَّا تَبَارًا﴿٢٨﴾

28. Rabb wangu! Nighufurie mimi, na wazazi wangu wawili, na kila aliyeingia nyumbani mwangu akiwa Muumini na Waumini wa kiume na Waumini wa kike, na wala Usiwazidishie madhalimu isipokuwa kuteketea kabisa.

 

 

 

[1] Nuwh (عليه السّلام) Ni Rasuli Wa Kwanza Ardhini Na Ni Baba Wa Pili Wa Wanaadam Baada Ya Nabiy Aadam (عليه السّلام):

 

Katika Hadiyth ndefu ya Ash-Shafaa’ah Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amethibitisha kuwa Nuwh (عليه السّلام) ni Rasuli wa kwanza ardhini kama ifuatavyo:

 

ائْتُوا نُوحًا فَإِنَّهُ أَوَّلُ رَسُولٍ بَعَثَهُ اللَّهُ إِلَى أَهْلِ الْأَرْضِ،   فَيَأْتُونَهُ فَيَقُولُ لَسْتُ هُنَاكُمْ وَيَذْكُرُ سُؤَالَهُ رَبَّهُ مَا لَيْسَ لَهُ بِهِ عِلْمٌ  فَيَسْتَحِي

 

“Mfuateni Nuwh, hakika yeye ndiye Rasuli wa kwanza Aliyemtuma Allaah kwa watu ardhini. Watamfuata. Naye atasema: Siwezi kufanya mnaloomba! Na atakumbuka kumuomba kwake Allaah kwa jambo asilokuwa na ujuzi nalo.  Naye ataona hayaa.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hivyo, ni kwa vile makafiri wote waliokuwa hawakupanda jahazini, waligharakishwa wakabaki wale waliopanda pamoja na Nabiy Nuwh (عليه السّلام) jahazini, ambao ni wachache katika walioamini, kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika kisa cha Nabiy Nuwh (عليه السّلام) kwenye Suwrah ya Huwd (11:25-48) na katika humo ni Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَمْرُنَا وَفَارَ التَّنُّورُ قُلْنَا احْمِلْ فِيهَا مِن كُلٍّ زَوْجَيْنِ اثْنَيْنِ وَأَهْلَكَ إِلَّا مَن سَبَقَ عَلَيْهِ الْقَوْلُ وَمَنْ آمَنَ ۚ وَمَا آمَنَ مَعَهُ إِلَّا قَلِيلٌ﴿٤٠﴾

“Mpaka ilipokuja Amri Yetu na tanuri likafoka, Tukasema: Beba humo (jahazini) wawili wawili kutoka kila aina; dume na jike na ahli zako, isipokuwa (kafiri) ambaye imemtangulia kauli ya hukmu na (beba humo) wale walioamini. Na hawakuamini pamoja naye isipokuwa wachache.” [Huwd (11:40)]

 

Rejea huko kupata faida nyenginezo.

 

[2] Ada Ya Makafiri Kuweka Vidole Masikioni Mwao Na Kujigubika Nguo Wasisikie Risala Wala Wasiwaona Rusuli Wanaowalingania.

 

Rejea An-Nisaa (4:110), Huwd (11:3) kwenye maelezo bayan na rejea mbalimbali. Pia At-Tahriym (66:8), Adh-Dhaariyaat (51:18).

 

[3] Fadhila Za Istighfaar (Kuomba Maghfirah )Na Tawbah (Kutubia):

 

Baadhi ya fadhila za Istighfaar (kuomba maghfirah) zimetajwa katika Aayah hizi (11-12), nazo ni kuteremshiwa kwa wingi, kupanuliwa mali na kuzidishiwa kizazi,  kujaaliwa mashamba na mito. Fadhila nyenginezo zinapatikana katika kiungo kifuatacho pamoja na maudhui nzima ya kuomba maghfirah na kutubia:

 

Tawbah: Hukmu Na Fadhila Zake

 

Rejea pia At-Tahriym (66:8) kwenye sharti za kuomba tawbah, pamoja na viungo kadhaa vya maudhui hii pamoja na faida nyenginezo na rejea mbalimbali.

 

Rejea pia An-Nisaa (4:110), Huwd (11:3) At-Tahriym (66:8).

 

[4] Waddaa, Suwaa’aa, Yaghuwtha, Ya’uwqa, Nasraa:

 

Ni majina ya waja wema ambao baada ya kufariki kwao, watu walichora sura zao wakawa wanawaabudu. Mwishowe wakachonga masanamu waliyokuwa wakiyaabudu watu wa Nabiy Nuwh (عليه السلام)  kama inavyoelezewa katika Tafsiyr ifuatayo:

 

Na wakawaambia: “Msiache kuwaabudu waungu wenu mkaelekea kwenye kumuabudu Allaah Peke Yake Ambaye Nuwh (عليه السّلام)  anawalingania nyinyi mumuabudu, na msimuache Waddaa, Suwaa’aa, Yaghuwth, Ya’uwq wala Nasraa.”  Na haya ni majina ya masanamu yao ambayo walikuwa wakiyaabudu badala ya Allaah. Na yalikuwa ni majina ya watu wema. Walipokufa, shaytwaan alitia kwenye mawazo ya watu wao kwamba wawasimamishie masanamu na picha ili wapate moyo, kama wanavyodai, wa kuwa watiifu wanapoyaona. Walipoondoka hao waliosimamisha masanamu na muda mrefu ukapita, wakaja watu wasiokuwa wao, shaytwaan aliwatia tashwishi kwamba wakale wao waliopita walikuwa wakiyaabudu haya masanamu na picha na kutawassal nayo. Hii ndio hekima ya kuharamishwa masanamu na kuharamishwa ujengaji wa makuba juu ya makaburi. Kwa kuwa hayo kwa kupitiwa na muda yanakuwa ni yenye kuabudiwa na wajinga. [Tafsiyr Al-Muyassar]

 

 

Share