072 - Al-Jinn

 

 

 

  الْجِنّ

Al-Jinn: 072

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا﴿١﴾

1. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Nimefunuliwa Wahy kwamba kundi miongoni mwa majini lilisikiliza, wakasema: Hakika sisi tumeisikia Qur-aan ya ajabu.

 

 

 

يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ ۖ وَلَن نُّشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا﴿٢﴾

2. Inaongoza kwenye uongofu, basi tukaiamini, na wala hatutomshirikisha Rabb   wetu na yeyote.

 

 

وَأَنَّهُ تَعَالَىٰ جَدُّ رَبِّنَا مَا اتَّخَذَ صَاحِبَةً وَلَا وَلَدًا﴿٣﴾

3. Na kwamba hakika umetukuka kabisa Ujalali wa Rabb wetu, Hakujifanyia mke wala mwana.

 

 

وَأَنَّهُ كَانَ يَقُولُ سَفِيهُنَا عَلَى اللَّـهِ شَطَطًا﴿٤﴾

4. Na kwamba safihi miongoni mwetu alikuwa akisema juu ya Allaah uongo uliopinduka mipaka.

 

 

وَأَنَّا ظَنَنَّا أَن لَّن تَقُولَ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا﴿٥﴾

5. Na hakika sisi tulidhania kuwa wanaadamu na majini hawatosema uongo juu ya Allaah.

 

 

وَأَنَّهُ كَانَ رِجَالٌ مِّنَ الْإِنسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالٍ مِّنَ الْجِنِّ فَزَادُوهُمْ رَهَقًا﴿٦﴾

6. Na kwamba wanaume miongoni mwa wanaadamu walikuwa wanajikinga na wanaume miongoni mwa majini, basi wakawazidishia madhambi, uvukaji mipaka ya kuasi na khofu.

 

 

وَأَنَّهُمْ ظَنُّوا كَمَا ظَنَنتُمْ أَن لَّن يَبْعَثَ اللَّـهُ أَحَدًا﴿٧﴾

7. Na kwamba wao walidhania kama mlivyodhani nyinyi kwamba Allaah Hatomfufua yeyote (au Hatomtuma Rasuli).

 

 

وَأَنَّا لَمَسْنَا السَّمَاءَ فَوَجَدْنَاهَا مُلِئَتْ حَرَسًا شَدِيدًا وَشُهُبًا﴿٨﴾

8. Na kwamba sisi tulitafuta kuzifikia mbingu, basi tukazikuta zimejaa walinzi wakali na vimondo.

 

 

وَأَنَّا كُنَّا نَقْعُدُ مِنْهَا مَقَاعِدَ لِلسَّمْعِ ۖ فَمَن يَسْتَمِعِ الْآنَ يَجِدْ لَهُ شِهَابًا رَّصَدًا﴿٩﴾

9. Na kwamba sisi tulikuwa tukikaa huko vikao kwa ajili ya kusikiliza, basi atakayetega sikio kusikiliza sasa atakuta kimondo kinamvizia.

 

 

وَأَنَّا لَا نَدْرِي أَشَرٌّ أُرِيدَ بِمَن فِي الْأَرْضِ أَمْ أَرَادَ بِهِمْ رَبُّهُمْ رَشَدًا﴿١٠﴾

10. Nasi hatujui kama wanatakiwa shari wale wanaokaa ardhini, au Rabb wao Anawatakia uongofu.

 

 

وَأَنَّا مِنَّا الصَّالِحُونَ وَمِنَّا دُونَ ذَٰلِكَ ۖ كُنَّا طَرَائِقَ قِدَدًا﴿١١﴾

11. Na kwamba miongoni mwetu wako walio wema, na miongoni mwetu wako walio kinyume chake, nasi tumekuwa makundi ya njia mbali mbali.

 

 

وَأَنَّا ظَنَنَّا أَن لَّن نُّعْجِزَ اللَّـهَ فِي الْأَرْضِ وَلَن نُّعْجِزَهُ هَرَبًا﴿١٢﴾

12. Na sisi tulikuwa na yakini kwamba hatutoweza kumshinda Allaah ardhini, na wala hatutoweza kumkwepa kutoroka.

 

 

وَأَنَّا لَمَّا سَمِعْنَا الْهُدَىٰ آمَنَّا بِهِ ۖ فَمَن يُؤْمِن بِرَبِّهِ فَلَا يَخَافُ بَخْسًا وَلَا رَهَقًا﴿١٣﴾

13. Na kwamba sisi tuliposikia mwongozo (hii Qur-aan) tuliuamini. Basi atakayemuamini Rabb wake, hatoogopa kupunjwa mazuri yake wala kuzidishiwa adhabu ya madhambi.

 

 

وَأَنَّا مِنَّا الْمُسْلِمُونَ وَمِنَّا الْقَاسِطُونَ ۖ فَمَنْ أَسْلَمَ فَأُولَـٰئِكَ تَحَرَّوْا رَشَدًا﴿١٤﴾

14. Na kwamba miongoni mwetu ni Waislamu, na miongoni mwetu ni wakengeukaji haki. Hivyo atakayesilimu, hao ndio waliofuata kidhati uongofu.

 

 

وَأَمَّا الْقَاسِطُونَ فَكَانُوا لِجَهَنَّمَ حَطَبًا﴿١٥﴾

15. Ama wakengeukaji haki, hao watakuwa kuni za Jahannam.

 

 

وَأَن لَّوِ اسْتَقَامُوا عَلَى الطَّرِيقَةِ لَأَسْقَيْنَاهُم مَّاءً غَدَقًا﴿١٦﴾

16. (Allaah Anasema):  Na kwamba lau wangelinyooka kwenye njia, bila shaka Tungeliwanywesha maji kwa wingi.

 

 

لِّنَفْتِنَهُمْ فِيهِ ۚ وَمَن يُعْرِضْ عَن ذِكْرِ رَبِّهِ يَسْلُكْهُ عَذَابًا صَعَدًا﴿١٧﴾

17. Ili Tuwatie katika jaribio kwayo. Na anayepuuza Ukumbusho wa Rabb wake, Atamsukuma kwenye adhabu ngumu ya kumlemea asiiweze.

 

 

وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا﴿١٨﴾

18. Na kwamba Misikiti ni kwa ajili ya Allaah tu, basi msiombe yeyote pamoja na Allaah.

 

 

وَأَنَّهُ لَمَّا قَامَ عَبْدُ اللَّـهِ يَدْعُوهُ كَادُوا يَكُونُونَ عَلَيْهِ لِبَدًا﴿١٩﴾

19. Na kwamba Mja wa Allaah (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) aliposimama kumwomba (Rabb wake), walikaribia kwa mlundikano wao kumzonga.

 

 

قُلْ إِنَّمَا أَدْعُو رَبِّي وَلَا أُشْرِكُ بِهِ أَحَدًا﴿٢٠﴾

20. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika mimi namuomba Rabb wangu na wala simshirikishi na yeyote.

 

 

قُلْ إِنِّي لَا أَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا رَشَدًا﴿٢١﴾

21. Sema: Hakika mimi sikumilikieni dhara wala uongofu.

 

 

قُلْ إِنِّي لَن يُجِيرَنِي مِنَ اللَّـهِ أَحَدٌ وَلَنْ أَجِدَ مِن دُونِهِ مُلْتَحَدًا﴿٢٢﴾

22. Sema: Hakika hakuna yeyote awezaye kunilinda na Allaah na wala sitoweza kupata mahali pa kukimbilia ila Kwake tu.

 

 

إِلَّا بَلَاغًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِسَالَاتِهِ ۚ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَإِنَّ لَهُ نَارَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا﴿٢٣﴾

23. Isipokuwa nibalighishe (haki) kutoka kwa Allaah na Ujumbe Wake. Na yeyote yule atakayemwasi Allaah na Rasuli Wake, basi hakika atapata Moto wa Jahannam, watadumu humo abadi.

 

 

حَتَّىٰ إِذَا رَأَوْا مَا يُوعَدُونَ فَسَيَعْلَمُونَ مَنْ أَضْعَفُ نَاصِرًا وَأَقَلُّ عَدَدًا﴿٢٤﴾

24. Mpaka watakapoona yale wanayoahidiwa sasa, basi watajua ni nani msaidizi dhaifu, na mchache zaidi kwa idadi.

 

 

قُلْ إِنْ أَدْرِي أَقَرِيبٌ مَّا تُوعَدُونَ أَمْ يَجْعَلُ لَهُ رَبِّي أَمَدًا﴿٢٥﴾

25. Sema: Mimi sijui kama yapo karibu hayo mnayoahidiwa, au Rabb wangu Atayaweka muda mrefu.

 

 

عَالِمُ الْغَيْبِ فَلَا يُظْهِرُ عَلَىٰ غَيْبِهِ أَحَدًا﴿٢٦﴾

26.  Mjuzi wa ghaibu, na wala Hamdhihirishii yeyote Ghaibu Yake.

 

 

إِلَّا مَنِ ارْتَضَىٰ مِن رَّسُولٍ فَإِنَّهُ يَسْلُكُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ رَصَدًا﴿٢٧﴾

27. Isipokuwa Rasuli ambaye Yeye Amemridhia. Basi hakika Yeye Anamwekea walinzi mbele yake na nyuma yake.

 

 

لِّيَعْلَمَ أَن قَدْ أَبْلَغُوا رِسَالَاتِ رَبِّهِمْ وَأَحَاطَ بِمَا لَدَيْهِمْ وَأَحْصَىٰ كُلَّ شَيْءٍ عَدَدًا﴿٢٨﴾

28. Ili Ajue kwamba wamekwishabalighisha   Ujumbe wa Rabb wao, na Ameyazunguka (kwa Ujuzi Wake) yale waliyo nayo, na Ametia hesabuni barabara idadi ya kila kitu.

 

 

 

Share